JE HAYA NI MAPENZI!! 53: - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Tuesday, February 18, 2020

JE HAYA NI MAPENZI!! 53:





Sam alifika kwenye nyumba ya Sabrina kwenye
mida ya saa tano usiku, kwavile alikuwa na funguo
za geti akafungua bila ya kugonga.
Alipoingia, moyo wake ukamtuma kuwa
akachungulie kwanza dirishani kwenye chumba cha
Sabrina.
Ila aliposogea madirisha yote yalikuwa yamefungwa
vizuri, ila aliposogeza sikio akasikia kuna miguno ya
kimahaba kutoka kwenye kile chumba.
Sam akapatwa na wasiwasi juu ya kitu kinachoendelea ndani ya chumba cha Sabrina.
Akaenda kufungua mlango, akaona ni wazi umefungwa kwa ndani kwani hata haukufunguka.
Akaanza kujiuliza kuwa Sabrina yupo na nani, akajaribu kuipiga simu ya Sabrina ila iliita tu bila ya kupokelewa.
Sam akaona hapa sasa mambo yanakuwa magumu kwake.
Akaamua tena kwenda mlangoni huku akibamiza mlango huku akiita kwa nguvu jina la Sabrina.
"Sabrina, Sabrina"
Sabrina alishtuka baada ya kusikia jina lake likitajwa sana tena kwa nguvu na moja kwa moja akaigundua ile sauti kuwa ni ya Sam.

Jeff akainuka na kwenda kumfungulia Sam mlango huku akifikicha fikicha macho yake kuonyesha kuwa ametoka usingizini, ambapo pale pale mlangoni alikula ngumi ya sura hadi chini, kisha Sam akamkwida Jeff na kuanza kumuuliza,
"Niambie ukweli sasa, mamako mdogo yupo na nani chumbani kwake?"
"Mi sijui"
Sam akampiga tena Jeff   ngumi ya sura na kuzidi kumkunja huku akitaka amwambie ukweli wa mambo,
"Unanionea kaka, sijui chochote hapa unanionea tu"
"Nakuonea kitu gani wakati wewe ndio unaishi na Sabrina humu ndani"
"Ndio, ila sijui chochote. Mi nimetoka kulala, hata sijui nikwambie ukweli upi"
Sam akazidi kumsukumia Jeff chini kwa hasira, kisha akamuacha pale chini na yeye kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha Sabrina.

Alipoufungua mlango wa Sabrina, ulifunguka bila ya tatizo lolote kwamaana kwamba hakuufunga kwa funguo ndani.
Sam alimuona Sabrina akiwa amelala huku akiweweseka kimahaba na kumshangaa kwani sauti aliyoitoa ilikuwa kamavile yupo na mwanaume.
Ikabidi amsogelee karibu zaidi na kumshtua kwa kumuamsha ambapo Sabrina alishtuka kamavile mtu aliyetoka kwenye usingizi mzito sana na kumfanya awe kama amepatwa na mshangao kwa kumuona Sam muda huo kwenye chumba chake.
Sam nae alikuwa akimshangaa tu kisha akamuuliza,
"Kwani una matatizo gani Sabrina?"
"Matatizo? Kivipi?"
Huku akijifikicha fikicha macho na kumfanya Sam aone aibu kumueleza kile alichomuhisi na alichokisikia.
Akaamua kumuuliza swali jingine,
"Mbona leo hukufunga mlango wakati umelala?"
"Kumbe sikufunga mlango? Hapa ndio nilitaka kukuuliza kuwa umeingiaje bila kugonga!"
Huku akipiga miyayo ya usingizi na kufanya Sam ampe pole sasa,
"Pole sana mpenzi kwa kushtua usingizini ila sijui nimekushtua wakati unaota!"
"Wakati naota? Kwanini unasema wakati naota?"
"Nimekuona ukiweweseka hapa"
"Mmh Sam jamani, mbona mi sikumbuki huko kuota! Umenikuta nikiweweseka kweli?"
"Ndio, tena hadi ulikuwa ukiongea peke yako"
"Mmh uongo huo Sam, maneno gani hayo nimeongea?"
"Mmh tuachane na hayo basi, hebu tuzungumze mengine au nikuache uendelee kupumzika na samahani kwa kukushtua"
Sabrina alimuangalia tu Sam akifululiza na maneno yake kisha akavuta shuka kuonyesha kwamba swala la kumuacha yeye apumzike ni la muhimu zaidi.
Sam nae alipoona vile akainuka na kuanza kutoka.
Ila kabla hajatoka akamwambia Sabrina,
"Ukumbuke kufunga mlango wako"
"Sawa hakuna tatizo"
Kisha Sam akatoka.

Alipofika sebleni alimkuta Jeff akiwa kakaa huku amejiinamia kwa mawazo.
Akamuinua kichwa na kumwambia,
"Samahani dogo"
Kisha akatoka nje na kuondoka.
Jeff akainuka na kufunga mlango, kisha akarudi kukaa pale kwenye kochi huku akitabasamu.
Baada ya muda mfupi, Sabrina alitoka chumbani kwake na kumfata Jeff pale sebleni,
"Uwii ndio amekuumiza hivyo?"
Jeff akatikisa kichwa kuitikia,
"Pole jamani, hatukuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya hii"
Jeff akawa anatabasamu na kucheka, na kumfanya Sabrina amuulize,
"Unacheka nini sasa"
"Nimefurahi tu, yani siamini kama hili jambo limepita kwa amani kiasi hiki"
"Muone vile, yani leo dah sijui hata ingekuwaje jamani! Ila Jeff una akili sana, ngoja tukalale halafu asubuhi tujue nini kinaendelea"
Wakainuka na kwenda kulala.

Kulipokucha, Sam alifika tena nyumbani kwa Sabrina asubuhi na mapema na kwa muda huo alimkuta Sabrina akiwa bafuni kuoga.
Sam akaingia chumbani kwa Sabrina na kukaa kwenye kitanda.
Katika kuangaza angaza macho yake kwenye kile chumba, akaona shati ambalo huwa anamuona Jeff amevaa.
Akajiuliza maswali bila majibu huku akimngoja Sabrina atoke bafuni.
Sabrina alipotoka bafuni alishangaa kumuona Sam akiwa ameshikilia lile shati la Jeff, moja kwa moja akajiandaa kumpa majibu.
Na Sam alipomuona Sabrina moja kwa moja akamuuliza,
"Hii shati inafanya nini humu chumbani kwako?"
"Ooh ni shati ya Jeff hiyo, wakati naanua nguo nikasahau nayo nikaingiza ndani kwangu. Maskini Jeff najua hata nae hajui kama shati yake ipo humu"
Kisha Sabrina akaichukua ile shati toka mikononi mwa Sam na kumwambia,
"Ngoja nimpelekee huyo Jeff"
Sam hakusema kitu zaidi tu ya kumtazama tu na kumuangalia kile anachofanya.
Sabrina alitoka sebleni huku akiongea sauti kubwa ili Sam asikie,
"Wee Jeff shati lako hili, nilijisahau na kuingia nalo kwangu baada ya kulianua"
"Sawa asante"
Kisha Sabrina akarudi tena chumbani kwake, ambapo Sam alitoka na kumpisha Sabrina ili avae.
Sabrina alizidi kupatwa na mashaka juu ya tabia ya Sam.

Joy na James walijipanga sasa kwaajili ya kukutanisha familia zao ili kufanikisha ndoa yao.
Joy alianza kumwambia James kuhusu Sam,
"Unajua familia imefurahi sana kuona Sam amepata mwanamke na kumpa mimba"
"Inamaana Sam hajawahi kuwa na mwanamke?"
"Yani hatujawahi kumuona akiwa makini na mwanamke kiasi hiki, sijui Sabrina kampa nini Sam kwakweli"
James akatabasamu tu huku wakiwaza siku yao itakavyokuwa.

Baada ya Sabrina kumaliza kujiandaa, akatoka sebleni na kumkuta Jeff na Sam kamavile wakijadiliana kitu fulani ambacho yeye   hakukifahamu kwa wakati huo ila hakuwa na mashaka kwani alijua wazi kuwa badae Jeff atamweleza kila kitu walichokuwa wakizungumza.
Kisha akamsogelea Sam ili kumuonyesha kwamba ameshajiandaa,
"Haya twende sasa"
"Ila hujaniambia kama tunaenda wapi Sam"
"Hata usijali, utaenda kupaona huko huko"
Wakaondoka pale nyumbani na kuelekea mahali ambako Sabrina hakupajua kwa wakati huo.

Walifika mahali Sam akasimamisha gari na kuingia kwenye eneo hilo.
"Sabrina, tunaenda hapo kuchagua nguo za harusi"
Sabrina alifurahi sana na kuona sasa ndoto yake ya kuolewa inatimia, tena ile ndoto ya kuolewa na mwanaume tajiri kama Sam.
"Yani Sam, hata siamini jamani"
"Ndio uamini sasa, harusi yetu tayari inanukia. Nataka mtoto wetu tumlee ndani ya ndoa"
Kwakweli moyo wa Sabrina ulimwambia wazi kuwa katika ulimwengu hakuna tena mwanaume kama Sam, mwanaume anayeweza kukubali mimba isiyoeleweka na kutaka kuharakisha ndoa ili mtoto ambaye ni haramu kwake azaliwe ndani ya ndoa na awe mtoto halali.
Sabrina hakujua cha kumwambia Sam zaidi ya kuonyesha tabasamu tu ili kudhihirisha kwamba amefurahi sana.

Waliingia kwenye hilo duka na kuanza kuchagua nguo zao za harusi.
Walichagua ngo na kujaribisha kisha wakazipenda na kuamua kwenda kuzilipia ili waondoke nazo.
Sabrina alipoangalia upande wa malipo wa duka hilo, alimuona mpokea pesa ambaye alikuwa ni rafiki yake mkubwa hapo kabla ila urafiki wao ukavunjika kwa mambo ambayo alifanyiwa.
Huyu si mwingine bali alikuwa Sia.
Sabrina alihisi moyo wake kujawa na ukungu kwa muda huo kwani hakutegemea kumuona huyo Sia mahali hapo.
Kisha akamgeukia Sam na kumwambia,
"Naomba tuondoke"
"Kwanini Sabrina?"
"Nguo za hapa sijazipenda"
"Jamani Sabrina, si ndio umesema mwenyewe kuwa umezipenda hizi tukazilipie!"
"Naomba unisikilize Sam, kama nilikwambia nimezipenda basi mimi mwenyewe nakwambia tena kuwa sijazipenda. Naomba tuondoke Sam"
Muhudumu wa lile duka kuona wanabishana, akaona ni vyema akamwambie yule mkubwa wake ili awabembeleze naye wapate kuchukua zile nguo.
Sia alipoambiwa, akasogea hadi eneo walilokuwepo wakina Sabrina ila alipomuona ni Sabrina akashindwa hata jinsi ya kumwambia na kujikuta akimuangalia tu huku akitamani hata kumuomba msamaha, ila muda huo Sam na Sabrina walishafikia muafaka na kuondoka kwenye duka lile.
Ambapo walienda kwenye duka lingine na kununua zile nguo.
Sia aliwaangalia na kurudi kwa yule muhudumu wake kisha akamwambia,
"Unajua, unaweza kufanya kitu leo ila madhara yake yakaja badae kabisa ingawa wakati unakifanya ulijua hakina madhara"
"Kwanini unasema hivyo?"
"Sasa najutia kosa nililolifanya miaka mingi iliyopita. Ila ndio hivyo tena. Ipo siku atanisamehe"
Kisha akarudi eneo lake na kuendelea na kazi.

Sam na Sabrina walipomaliza kununua mahitaji yao binafsi ya  harusi wakarudi nyumbani sasa.
Kisha Sabrina akamuuliza swali Sam kama kumtega hivi,
"Vipi Sam, leo nikalale nyumbani kwako basi"
"Bado Sabrina, haraka ya nini mama! Pale ni kwako, utalala hadi kupachoka hata usiwe na wasiwasi mke wangu mtarajiwa"
Sabrina hakutaka kuhoji zaidi kwani aliona wazi kuwa hata akihoji ni kazi bure tu.
Muda kidogo Sam akaaga na kuondoka zake.
Kisha Sabrina akamuita Jeff ili apate kujua kuwa walikuwa wanajadili kitu gani muda ambao yeye alikuwa akijiandaa.
"Eeh niambie Sam alikuwa akikwambia vitu gani?"
Jeff akacheka kwanza na kuanza kuzungumza,
"Aaaah alikuwa ananiambia tu kuwa nikulinde eti asikusogelee mwanaume yeyote"
Halafu Jeff akacheka tena na kusema,
"Wakati fisi nipo hapa hapa"
"Lione vile, nitakufukuza"
"Mmh hutaniwi jamani! Usichukie, mi nilikuwa nakutania tu"
"Haya, ila kesho kuna kazi nataka nikupe"
"Sawa hakuna tatizo mamy"
Jeff aliitikia bila ya pingamizi la aina  yoyote ile.

Sabrina akiwa anajiandaa kulala, akapigiwa simu na mama yake huku akipewa taarifa za harusi ya kaka yake.
"Wiki ijayo kabla ya harusi yenu tutaenda kulipa mahali kwa mke wa kaka yako kwahiyo na wewe unatakiwa kuwepo sawa"
"Hakuna tatizo mama nitakuwepo tu"
"Ndiomana nimeona nikupe taarifa mapema sababu wewe ni msumbufu na mbishi"
Sabrina alijikuta akicheka tu kwa maneno ya mama yake kisha akamuaga na kulala.

Kulipopambazaka, asubuhi na mapema Sabrina akatoka chumbani kwake na kwenda sebleni huku akitaka kumuita Jeff ila kabla hajamuita Jeff alisikia mtu akigonga mlango na kufanya ajiulize kuwa ni nani huyo kwa muda huo kwani angekuwa ni Sam basi angeita jina la Sabrina ili apate kufunguliwa.
Sabrina akajaribu kumuuliza yule mgongaji kuwa ni nani ila yule mgongaji hakujibu chochote na kumfanya Sabrina awe na wasiwasi na kumuita Jeff ambaye alitoka chumbani kwake na kwenda pale sebleni,
  "Kuna mtu anagonga, nimejaribu kumuuliza kuwa ni nani hajatoa jibu. Labda ukamuangalie kuwa ni nani"
Jeff akaenda na kufungua mlango ila hakumuona mtu yeyote pale nje.
"Hakuna mtu, au umesikia vibaya?"
"Hapana bhana, nimesikia vizuri mtu akigonga labda kama ameamua kuondoka"
Kisha wakafunga milango na kuendelea na mambo mengine kama kawaida.

Mchana wa siku hiyo, Sabrina akapigiwa simu na Joy ambaye ni wifi yake kwa upande wa kaka yake James na kwa upande wa mchumba wake Sam,
"Sabrina, kuwa makini kuna ndoto mbaya nimeota kuhusu wewe"
"Ndoto gani hiyo? Na niwe makini kivipi?"
"Yani ninachokuomba ni uwe makini tu. Kwakweli nimeota ndoto mbaya, siku nikipata muda nitakuelezea nilivyoota ila tu kuwa makini"
"Sawa, nimekuelewa"
Wakaongea na mawili matatu kisha simu ikakatika na kila mmoja kuendelea na mambo yake.

Ilipofika jioni Jeff akamuaga Sabrina kuwa anaenda kwao kwavile mama yake alimwambia aende.
  Kwahiyo Jeff akaondoka zake.
Muda kidogo simu ya Sabrina ikaita, akaipokea na mpigaji alikuwa ni Jeff,
"Nimesahau funguo za chumba changu cha nyumbani huko kwahiyo nitarudi kuzichukua"
"Na wewe kwa taarifa loh! Kama unarudi wewe rudi tu"
Kisha akakata simu na kuendelea na mambo mengine, akasikia mtu akigonga mlango, moja kwa moja akajua kuwa ni Jeff.
"Yani kasumbufu haka katoto"
Akawa anajisemea mwenyewe huku akienda kufungua mlango, na alipofungua tu waliingia watu wawili wakiwa wamevaa vitambaa vyeusi usoni na mmoja akakimbilia kumkaba Sabrina.

Itaendelea



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa