JE HAYA NI MAPENZI!! 38: - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Monday, February 17, 2020

JE HAYA NI MAPENZI!! 38:





Sabrina alijikuta akipatwa na mshtuko wa gafla
na kuanguka.
Joy akaanza kumpa huduma ya kwanza binti yake kwani alianguka vibaya, alitoka pale kwenye kochi hadi kwenye sakafu na kutulia tuli.
Joy akampepea pale binti yake na kummwagia maji mpaka pale Sabrina alipozinduka na kumuuliza tena
"Kwani kuna nini mama?"
"Hakuna kitu mwanangu"
Sabrina akatulia kidogo na kuwa kama anavuta kumbukumbu pale.
Joy akaamua kumkatisha kwanza ili asiwaze sana waliyozungumza.
"Sabrina mwanangu, unaonaje tukaenda nyumbani!"
"Mmh mama, na wewe mara moja moja ukae hapa kwangu"
"Hilo sio tatizo, ila twende nyumbani ukamuone wifi yako"
"Basi sawa, ngoja nikachukue mkoba wangu chumbani"
Sabrina akainuka na kwenda chumbani, alipoingia akatazama mandhari ya chumba chake na kuliona lile shuka pembeni na kukumbuka kila kitu kumuhusu Jeff kisha moyo nao kuanza kumuuma upya kabisa, tena ukamuuma zaidi baada ya kukumbuka kuwa ameambiwa kwamba Jeff kapata ajali, kisha  akatoka kule chumbani kwake na kurudi tena sebleni, mama yake akamwambia
"Twende basi Sabrina"
"Hapana mama, niache nimuombee Jeff apone"
Joy akamuangalia mwanae na kujua kuwa kumbukumbu zimemrudia, kisha akamwambia tena
"Twende basi huko hospitali ukamuone"
"Usijali mama, nimekwambia niache kwanza nimuombee sababu najua nini chanzo"
"Mmh makubwa haya, leo hadi mwanangu Sabrina naye anajua kuombea!"
Basi Joy akaona ni vyema yeye awasiliane na huyo Sam aliyewapa taarifa ili aende kumuona Jeff na kumfariji Sakina, kisha akamwambia mwanae
"Basi badae kidogo nitakuja kukupitia tena kidogo ili angalau Sakina akuone na wewe kidogo"
Kisha akamuaga na kuondoka, kwahiyo sasa mawazo yote yalikuwa juu ya ajali aliyoipata Jeff na si vinginevyo.

Sabrina alibaki pale ndani kwake mwenyewe akitafakari, akayakumbuka maisha yake ya zamani.
Maisha yale yaliyomfanya kuwa na kila mwanaume aliyemtamkia nakupenda, maisha yale yaliyomfanya aende rumande sababu ya mapenzi, yaliyofanya wanaume wale wale waliosema wanampenda na kuanza kumchukia, ila kati ya wote alibaki mtoto mdogo Jeff aliyemuombea mema muda wote, mtoto ambaye hakupenda kumuona Sabrina akiangamia, mtoto ambaye alimtahadharisha Sabrina kwenye kila aina ya majanga kwani aliweza hata kumng'ang'ania Sabrina alipokuwa shuleni na kumfanya achelewe ndege aliyotakiwa kupanda na kuponyeka na ajali iliyopangwa dhidi yake.
Ila leo mtoto huyo huyo kapata ajali sababu ya kitu kimoja tu, Sabrina akawaza na kusema,
"Tamaa na balehe ndio vimemchochea Jeff kufanya hivi na kumfanya aingie kwenye mlolongo wa matatizo yangu"
Sabrina akakumbuka ile kamba aliyofungwa kipindi kile kwenye kiuno chake, akakumbuka masharti aliyopewa mara ya mwisho kuwa haruhusiwi kuingiliwa kimwili na mwanaume yeyote yule. Na kama ikitokea kaingiliwa kimwili basi huyo mwanaume atakufa.
Sabrina aliinu a mikono yake juu na kushika kichwa chake huku akihofia maisha ya Jeff.
Muda huu Sabrina aliamua kupiga magoti chini na kuanza kumuombea Jeff.

Joy alimkuta Sakina akiwa pale nje ya hospitali huku machozi yakimtoka tu sababu ya hali mbaya aliyokuwa nayo mtoto wake.
Sakina akamkumbatia Joy kwa uchungu sana huku akilia,
"Sijui mwanangu atapona, mtoto mwenyewe huyo huyo mmoja kama jicho jamani. Mwanangu Jeff, uwiii sijui mimi jamani!"
Joy akajitahidi kumbembeleza Sakina kuwa wazidi kumuomba Mungu ili Jeff aweze kupona.

Sam ndiye aliyekuwa akishughulika na kila kitu kuhusu Jeff, ndiye aliyekuwa akihakikisha kuwa Jeff anapatiwa matibabu sahihi ili arudi katika hali yake ya kawaida.
Ingawa Sam naye hakuelewa mlolongo wa haya matukio kabisa.
Akakumbuka usiku alipokwenda kwa Sabrina na kujibiwa na Jeff kuwa Sabrina ametoka, akakumbuka asubuhi alipoenda tena na kugonga bila kufunguliwa, akakumbuka alipoenda  tena mchana na kugonga ila akasikia majibishano kati ya Jeff na Sabrina na kisha pale Sabrina alipomfukuza Jeff.
Hakuelewa kwanini Jeff alifukuzwa, na pia hakutambua kuwa imekuwaje hadi Jeff akapata ajali ingawa yeye alikuwa wa kwanza kumshuhudia Jeff akivuja damu pale chini baada ya ajali.
"Hata sielewi kwakweli, sielewi kabisa kabisa kuwa kwanini inakuwa hivi"
Alitulia na kwenda kuwapa majibu ya daktari ndugu wa Jeff waliokuwepo pale hospitali.

Sam alikaa nao pale na kuzungumza nao kuhusu Jeff,
"Vipi lakini atapona?"
"Tumuombe Mungu jamani ili ainusuru hii hali"
Sakina alihisi kuchanganyikiwa muda wote na kujiona kama vile ni mtu asiyejielewa.
Muda kidogo, daktari naye akawafata na kufanya wote washtuke huku kila mmoja akifikiria yake kuhusu Jeff.
Daktari akawauliza,
"Jamani Samahanini, kuna yeyote anayeitwa Sabrina hapo kati yenu?"
Wakatazamani wote, kisha Sakina akajibu,
"Sabrina bado hajafika, kwani imekuwaje jamani! Sabrina wa nini?"
"Basi mwambieni huyo Sabrina aje, kwani tangu mwanzo huyu kijana amekuwa akimtaja sana, sasa kama madaktari tumeshauriana kuwa itakuwa vyema kama huyo Sabrina akija karibu."
Ikabidi Sam aamue kwenda kumfata Sabrina nyumbani kwake.

Sam alienda kwa Sabrina na kugonga, ila alipojaribu kufungua mlango aliukuta upo wazi na Sabrina akiwa bado amepiga magoti huku akiendelea na maombi yake.
Sam alikaa kwenye kochi huku akimsubiri Sabrina amalize maombi yake.
Baada ya muda kidogo, Sabrina akainuka na kukaa kwenye kochi kisha Sam akamueleza Sabrina yaliyojiri naye akakubali kwenda hospitali kumuona huyo Jeff ambaye muda wote alikuwa akimtaja Sabrina tu.

Sabrina alipofika hospitali, moja kwa moja Jeff akamuongoza kwenye chumba cha daktari
"Tuliona ni vyema tumchome sindano ya usingizi kwahiyo sahivi yupo kwenye usingizi wa sindano"
"Basi naomba hata nikamchungulie tu"
Daktari hakukataa zaidi ya kwenda na Sabrina kwenye chumba walichomlaza Jeff.
Sabrina alimwangalia Jeff na kumuhurumia sana hata akasahau yote yale ambayo Jeff alimtendea.

Sabrina alipotoka kwenye kile chumba, akaenda kwa ndugu wa Jeff kuwasalimia na hapo akakutana na Sakina ambaye alikuwa na majonzi tu na kumkumbatia Sabrina.
"Sabrina mtoto wetu jamani, sijui kama atapona"
"Usijali dada, Jeff atapona tu."
Sabrina akajitahidi kumpa moyo Sakina pale kwavile alionekana kukata tamaa kabisa.
Kisha Sakina akamuuliza Sabrina,
"Kwani alikuaga anaenda wapi leo?"
Sabrina akakaa kimya kwa muda na kumwambia Sakina,
"Tuachane na hizo khabari kwanza za kuaga au kutokuaga. Tuangalie kwanza hali ya Jeff"
"Nimekuuliza hivyo nikiwa na maana kabisa Sabrina, sababu nilimnenea mwanangu vibaya"
"Ulimnenea nini?"
"Jana usiku nilimnenea mwanangu hivi, akienda kwa huyo sugar mamy wake basi apatwe na majanga yeye pamoja na huyo mmama, sasa leo napewa taarifa kuwa mwanangu amepatwa na ajali kwakweli nimechanganyikiwa sana hata najuta kunena maneno ya ajabu kiasi kile. Ndiomana nikakuuliza kuwa alikuaga anaenda wapi? Namuomba Mola amnusuru mwanangu jamani"
"Pole sana dada, ila siku nyingine usimnenee mambo hayo mtoto wako, si unaona tabu tunayoipata? Maneno yako huwezi jua kuwa yatawaponza wangapi."
"Nimekoma mdogo wangu, yani sirudii tena mimi jamani. Mwanangu apone tu jamani, mtoto mwenyewe ndio huyo huyo kama jicho."
Sabrina alijitahidi pale kumfariji Sakina na kumpa moyo kuwa Jeff atapona tu.

Usiku nao uliwakutia pale pale hospitali, ila kwavile Jeff alikuwa bado hajazinduka ikabidi warudi nyumbani kupumzika ili waende kesho yake.
Ila Sakina bado aliendelea kulalamika na kujiona kuwa yeye ndiye chanzo cha mambo yote yale.
"Bora ningemnenea yule jimama tu kuliko kumnenea na mwanangu"
"Acha maneno hayo dada, utapata laana kwa Mungu."
"Roho inaniuma Sabrina yani inaniuma sana, hata sijui nifanyeje!"
"Muombe Mungu akupe subira na uvumilivu na tuendelee kumuombea Jeff apone"
Basi sam alimpeleka Sakina hadi nyumbani kwake na kumuacha hapo kisha akampeleka Sabrina nyumbani kwake.
"Utaweza kulala mwenyewe nyumba yote mpenzi?"
"Usijali naweza"
"Nilitaka nibaki hapa nikupe kampani ya kulala pamoja"
"Hata usijali Sam"
Basi Sam akamuaga Sabrina na kuondoka, kisha Sabrina akaanza kufanya usafi wa nyumba yake usiku ule ule kwa kuyaloweka yale mashuka na usafi mwingine, alipomaliza ndio akalala.

Asubuhi na mapema, Sam akampitia Sabrina ili waende kazini ila Sabrina akamuomba Sam wapite kwanza hospitali.
Sam hakupinga na wakaenda hospitali kwanza.
Walipofika, walimkuta Jeff amefumbua macho na anaweza kuongea kwa mbali kidogo.
"Pole sana Jeff utapona"
"Asante mamdogo, ila nakuomba kitu kimoja"
Sabrina akashtuka na kumuuliza Jeff kwa sauti  ya chini.
"Kitu gani?"
"Nakuomba usitembee peke yako"
Sam akadakia,
"Hilo halina shaka Jeff, yupo na mimi. Kwahiyo usijali"
Jeff akatikisa kichwa tu, kisha wakamuaga na kwenda kazini.

Sabrina alijifikiria sana alipokuwa kazini kuwa kwanini Jeff amemwambia kuwa asitembee peke yake,
"Au anahofia nitabakwa tena kama alivyonibaka yeye!"
Hapo akasita kidogo kwani moyo ulimuuma sana na kujiona kuwa atakuwa mjinga kuendelea kusikiliza maneno ya Jeff,
"Itabidi badae niende mwenyewe nikamuulize kuwa ana maana gani kuniambia mimi vile. Asiniletee ujinga wake kabisa."
Mara Sam akapita karibu na meza ya Sabrina na kumuona akinung'unika peke yake, kisha akamfata na kumuuliza kama kuna tatizo,
"Hakuna tatizo kwakweli"
"Basi mimi natoka kidogo, kuna watu wa kodo naenda kuzungumza nao ila nitawahi kurudi"
"Sawa boss"
Sam akatabasamu na kumuangalia Sabrina kisha akaondoka zake.
Sabrina aliendelea kufanya kazi yake ila mawazo yote ni kutaka kujua kuwa Jeff alikuwa na maana gani, hivyo akaona ni vyema aombe ruhusa hata ya saa moja akamuangalie Jeff hospitali na kujua kuwa alikuwa na maana gani.

Sakina alikuwa hospitali na mtoto wake, na alifurahi baada ya kuona hali ya mwanae ikiendelea vizuri leo.
Alizungumza na mwanae huku akimpa pole na kujutia maneno yake aliyotamka hapo kabla.
"Nisamehe sana mwanangu"
"Usijali mama"
"Ila hilo lijanamke hilo limama lililoitawala akili yako mwanangu, nataka mabaya yako yote yamfike yeye popote pale alipo"
"Jamani mama usiseme hivyo, au unataka mimi nife?"
"Hapana mwanangu, siwezi kutaka wewe ufe"
"Basi usiseme tena hayo maneno yako, utawaingiza hatiani watu wasio na hatia mama. Mimi sina mwanamke yeyote unayemsema wewe, mwisho wa siku hata watu wasiohusika nao utawaingiza humo. Mimi nipo kitandani hapa naumwa, wewe badala ya kunihurumia unaniambia maneno ya ajabu tu. Bora uende kama umechoka kuniona"
Sakina akajua wazi kuwa mtoto wake amechukizwa na yale maneno aliyokuwa akiyazungumza na kumlazimu kubadilisha ile mada yake ila Jeff alikuwa tayari ameshachukizwa na kumfanya asimsikilize tena mama yake.
"Jamani Jeff nisamehe mwanangu"
"Futa kwanza ile kauli yako"
"Naifuta mwanangu, huyo mwanamke asipatwe na baya lolote lile sababu ndio kipenzi cha mwanangu. Vipi sasa umenisamehe?"
Jeff akatikisa kichwa tu kama ishara ya kukubali ule msamaha.

Sabrina alitoka pale ofisini na kuianza safari ya kwenda hospitali ili akazungumze na Jeff.
Alipokuwa anatoka ofisini akakutana na Fredy, ambaye alimshtua na kupanda kwenye ile piki piki ya Fredy.
Muda huo huo Sam nae aliwasili pale ofisini na kumuona Sabrina akiishia na ile pikipiki.
Sam akachukia sana, kisha akaenda kuweka mafaili yake ofisini na kwenda kupanda gari lake ili aweze kufatilia Sabrina anapoenda.

Wakati Sam yupo njiani, akakuta ku na foleni ya gafla.
Ikabidi ashuke na kwenda kuulizia,
"Kwani kuna nini hapo mbele?"
"Kuna ajali, bodaboda mbili zimegongana na abiria mmoja mwanamke kafa pale pale"
Sam alihisi kuchanganyikiwa kabisa ukizingatia alimuona Sabrina akiondoka kwa bodaboda.

Itaendelea



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa