JE HAYA NI MAPENZI!! 39: - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Monday, February 17, 2020

JE HAYA NI MAPENZI!! 39:






abiria mmoja mwanamke kafa pale pale"
Sam alihisi kuchanganyikiwa kabisa ukizingatia
alimuona Sabrina akiondoka kwa bodaboda.
Sam akaamua kusogea kabisa kwenye eneo lile la tukio ili aweze kushuhudia kwa macho yake mwenyewe bila ya kusimuliwa.
Akawapita watu wengi waliozingira eneo lile, akaona kuna mwanamke amefunikwa khanga huku damu nyingi zikiwa zimetapakaa eneo lile.
Akaona pikipiki mbili zikiwa pembeni, pikipiki moja wapo ilikuwa haitamaniki kabisa hata kuitazama na ilikuwa ni pikipiki ile ile aliyomuona Sabrina amepanda.
Muda huu Sam alihisi kurukwa na akili kabisa na kusogelea pale alipolala yule marehemu kwa lengo la kumfunua ili ahakikishe kuwa ni nani.
Ila askari nao, na wale wa gari la kubeba wagonjwa walikuwa wamewasili eneo lile na kumkataza Sam kumfunua yule mwanamke, kitendo ambacho kilizidi kumpa uchizi Sam.
"Tafadharini jamani, naomba nimuone kama ni yeye"
"Ameumia vibaya sana, hatuwezi kuruhusu afunuliwe"
Ila Sam aling'ang'aniza na kuwafanya wamfunulie yule mtu ili amuone.
Ila kabla hajamuangalia, kuna mtu alikuja na kumshika bega Sam na kumfanya ashtuke sana.
Alipogeuka alikuwa ni Sabrina ambaye alikuwa anatetemeka sana.
Sam hakujielewa kabisa, wale manesi walipoona kuwa mtu mwenyewe haeleweki wakaamua kumpakiza yule marehemu kwenye gari yao na kuondoka naye.

Sam aliganda kama barafu huku akihisi ubaridi ukipita kwenye mwili wake, akamshika mabega Sabrina na kumuuliza,
"Ni wewe kweli Sabrina?"
Sabrina akatikisa kichwa kama ishara ya kuitikia kuwa ni yeye.
Sam akaishika sura ya Sabrina, akamuangalia kwa makini na kumkumbatia kwa nguvu.
Sabrina akamwambia Sam,
"Ila mwenzangu ameumia"
"Nani huyo?"
"Fredy aliyekuwa amenibeba kwenye pikipiki"
"Yuko wapi?"
Sabrina akamshika Sam mkono na kumpeleka kwenye mtaro wa pembezoni mwa barabara, ambapo Sam akasaidiana na baadhi ya watu kumtoa Fredy kwenye mtaro na kumpakiza kwenye gari ili kumuwaisha hospitali.

Sam ingawa alikuwa na Sabrina pemb eni ila bado alikuwa hajiamini kabisa, na Sabrina nae muda wote alikuwa akitetemeka, Sam alimuangalia tena Sabrina na kumuuliza,
"Sabrina, ni wewe kweli?"
"Ndio ni mimi Sam, yani hata mimi mwenyewe sijiamini kama kweli nimepona. Siamini kabisa, mwili wote umejawa na uoga hapa yani siamini"
"Kwani ilikuwaje Sabrina?"
Sabrina hata hakuelewa ni wapi aanzie kuelezea na wapi aishie,
"Niambie tu Sabrina tafadhari"
"Yani ilikuwa hivi, nilipotoka pale ofisini nikakutana na Fredy na kumuomba anipeleke kumuona Jeff. Na kweli tumeondoka vizuri tu hapo, kufika mbele kidogo Fredy akasimamisha ile pikipiki yake kisha akaniambia kuwa nishuke, nikamuuliza kwanini akasema nishuke tu atanipa sababu. Basi mimi nikashuka, nilipomaliza tu kushuka. Uuh Mungu wangu hata ilipotokea ile pikipiki nyingine sijui, kwani ilikuja na kugonga ile pikipiki ya Fredy kisha nikamuona Fredy akiangukia mtaroni halafu ile pikipiki yake iliinu ka juu kabisa na kuja kuponda mtu wa nyuma ya ile pikipiki ambaye alikuwa ni mwanamke, yani kilikuwa ni kitendo cha sekunde tu. Masikini yule dada alipiga yowe moja tu na kuwa kimya pale pale. Kwakweli nguvu ziliniisha na kujiona kama vile nipo kwenye ndoto. Hadi muda huu sijielewi, yani sielewi kabisa sielewi"
Sam akamsogeza Sabrina karibu yake na kumkumbatia kwaajili ya kumtoa uoga alionao,
"Pole sana Sabrina, ila tumshukuru Mungu kwa kukuponya jamani yani hadi mimi mwenyewe siamini mpaka muda huu jamani."
Walitulia kwa muda wakingoja majibu ya daktari kuhusiana na hali ya Fredy.
Huku Sam akijiuliza kuwa inamaana Fredy alijua kuwa kuna ajali itatokea? Na kama alijua mbona yeye hakujiepusha? Alikosa jibu ila alitambua wazi kuwa majibu yote anayo muhusika ambaye ni Fredy.

Hali ya Fredy iliendelea vizuri, hata muda ambao Sam na Sabrina wanaondoka pale hospitali, Fredy alikuwa akiendelea vizuri.
Sam alimru disha Sabrina nyumbani kwao kwani akaona kwamba itakuwa salama zaidi kumuepusha na mawazo ya siku hiyo.
Kisha Sam akaondoka zake.
Sabrina akamsimulia mama yake kila kitu ambacho kilimtokea kwa siku hiyo na kumfanya mama yake naye ashangae sana.
"Ndiomana hukuja tena hospitali kumuona Jeff"
"Ndio majanga hayo mama ndiomana nikashindwa"
"Basi kuna kitu kati yako wewe na Jeff kimewaunganisha"
Sabrina akashtuka sana na kumuuliza mama yake kwa mshangao ulioambatana na uoga.
"Kwanini mama?"
"Unajua leo wakati tupo pale hospitali, kuna muda Jeff alishtuka sana na kupiga kelele akisema, 'Sabrina no usipande' kiukweli hakuna aliyemuelewa kabisa. Mara akasema, 'Eeh Mungu mnusuru Sabrina' mi nikajiuliza kuwa anamuongelea Sabrina yupi hata sikupata jibu ila tangia hapo Jeff hakutaka tena kuongea na mtu yeyote yule halafu akalala. Mi nikajaribu kumpigia simu Sam na kumuuliza mnaendeleaje sababu simu yako haikupa tikana ila akanijibu kuwa mnaendelea vizuri kumbe hakutaka kuniambia ukweli wa hayo mambo"
Sabrina akapumua kiasi na kumuangalia mama yake huku akijaribu kumsoma kama kuna chochote amegundua baina yake na Jeff, ila alijua wazi kuwa mama yake hajagundua chochote kile.
Kisha Joy akaendelea kumwambia mwanae,
"Nashukuru Mungu amekulinda mwanangu, nadhani maombi ya Jeff yamesaidia kwakweli"
"Ndio mama"
Kisha wakaenda kulala ili waweze kuwahi kesho kwenda kuendelea na mambo mengine.

Kulipokucha, kama kawaida Sam alimfata Sabrina kwao na safari ya kwanza ilikuwa kwenda kumuona Jeff na kisha kumuona Fredy.

Jeff leo alikuwa vizuri na aliweza hata kukaa na alifurahi sana kumuona Sabrina.
"Siamini kama nakuona tena mamy"
"Usijali nilipona"
Sabrina hakutaka Jeff azungumze zaidi kwa kuhofia kuwa atasema mengi na kumuharibia kwa Sam.
Kwahiyo wakaongea nae kidogo tu kisha wakamuaga na kuondoka.

Walipofika kwa Fredy hali yake ilikuwa ni nzuri pia.
"Leo wanaweza kuniruhusu nirudi nyumbani"
"Pole sana Fredy"
"Asante Sabrina"
"Najua umeumia kwa kuniokoa mimi Fredy"
"Usijali hilo Sabrina, cha muhimu ni kuwa hata mimi nimepona."
Wakaongea pale mawili matatu kisha Sabrina na Sam wakarudi ofisini.

Walipokuwa ofisini, Sam alimuita Sabrina kwenye ofisi yake na kumwambia,
"Kuanzia leo Sabrina, huruhusiwi kutoka kwenda sehemu yoyote bila ruhusa yangu. Ukitoka bila ruhusa usije ukanilaumu kwa nitakachokufanyia. Na hilo sio ombi bali ni amri Sabrina. Nimemaliza, nenda ukaendelee na kazi"
Sabrina alirudi kwenye ofisi yake akiwa kanyong'onyea huku akijilaumu kuwa yote ameyasababisha yeye mwenyewe maana kila akionywa huwa anajifanya asikii.

Zikapita wiki mbili, Jeff alikuwa kapona kabisa na alirudi nyumbani kwao. Hata Fredy nae alikuwa ni mzima kabisa hata aliweza yeye mwenyewe kwenda kwa kina Sabrina,
"Unajua Fredy, mi hadi leo huwa nakosa majibu ya ile ajali. Hivi ulijuaje kama kutatokea ajali hadi kuniambia kuwa nishuke.?"
"Kiukweli hata sikujua kama itatokea ajali, ila wakati nakuendesha gafla moyo wangu ukawa mzito, nikahisi kuna kitu kibaya kinataka kutokea ila sikujua kama ni ajali. Ndiomana nikakwambia ushuke Sabrina"
"Mmh basi ni khatari"
"Yote sababu nakupenda Sabrina ila wewe hujui tu, laiti kama ungeingia kwenye moyo wangu basi ungegundua kuwa mimi ndio mwanaume wa pekee unayepaswa kuwa naye. Jaribu wewe mwenyewe kuangalia, ni mambo mangapi mabaya yananipata mimi kwaajili yako? Kumbuka nishawahi kuwa kipofu mimi kwaajili yako Sabrina. Hivi nifanye kitu gani ili uelewe upendo uliopo ndani yangu juu yako Sabrina? Niambie tafadhari."
Sabrina alikuwa kimya tu akimsikiliza Fredy ila hata yeye hakujua la kumwambia kwavile alishakubaliana na Sam tayari.
"Ni kweli unanipenda Fredy, hata moyo wangu unatambua hilo. Ila siwezi kuwa nawe sababu nina mwingine tayari"
Fredy aliumia ila akamjibu Sabrina,
"Hakuna shaka, nitasubiri hadi siku utakayokubali kuwa wangu"
Sabrina aliona ni vyema kubadilisha mada ili kuweza kumkatisha Fredy na mwisho wa siku Fredy akaaga na kuondoka.

Sam alikaa na Sabrina na kuamua kupanga naye maswala muhimu,
"Sabrina, nataka kukuoa"
"Mmh Sam, ya kweli hayo?"
"Ndio ni kweli, kwanini nikuongopee mpenzi? Sitaki kukuharibia maisha mpenzi wangu, ndiomana nahitaji tufunge ndoa ili mambo mengine yote tufanye tukiwa ndani ya ndoa"
Sabrina akafurahi sana na kujilaumu kwa kuchelewa kumkubali mwanaume wa muhimu kama Sam, mwanaume anayejua thamani ya mwanamke, mwanaume ambaye haitaji ngono tu bali mapenzi ya dhati ndiomana yuko tayari kumuoa kwanza kabla ya mambo yote.
Moyo wa Sabrina ukamwambia kuwa huyu ndiye mwanaume ambaye amekuwa akimuhitaji siku zote za maisha yake, huyu ndiye mwanaume sahihi kwake.
Sabrina  akainuka na kumkumbatia Sam kwa furaha ya hali ya juu kisha akamwambia,
"Nipo tayari kuolewa na wewe Sam, nakupenda kwakweli"
Sam naye akafurahi baada ya kuona kuwa Sabrina ameridhia ombi lake.

Sam alimzungusha Sabrina kwa ndugu zake wote ili wamtambue, na wote hawakuwa na pingamizi lolote kwani walimuona Sabrina ni mtu muelewa na mzuri pia.

Miezi miwili kupita hali ya Sabrina ilikuwa haieleweki kwani mara nyingi alikuwa mgonjwa na mara nyingine alijikuta akiwachukia watu bila sababu za msingi na kufanya wengi wamshangao na wao kuanza kumchukia pia.
Ila yeye aliona kuwa ile hali ni ya kawaida tu na wala haikumshtua na kitu chochote kile.

Siku moja walisafiri na kwenda Arusha kumsalimia mama wa Sam, ambapo alimuita mwanae pembeni na kumuuliza,
"Vipi mwanangu tayari nini?"
"Tayari nini mama?"
"Si huyo binti, tayari namaanisha ana mimba?"
Sam akamcheka mama yake,
"Ndivyo alivyo bhana mama, hana mimba wala nini"
"Mmh mwanangu  hadi mimi mama yako unanificha?"
"Sikufichi mama, ila huo ndio ukweli"
"Haya, ila ile kitu huwa inaenda mbele hairudi nyuma basi tutaona tu"
Sam akataniana pale na mama yake na kumaliza maongezi yao kisha wakarudi alipo Sabrina na kuendelea na mazungumzo mengine ambapo mama wa Sam alimkaribisha sana Sabrina kwenye ukoo wao.
Sabrina na Sam wakafurahi sana kuwa pale Arusha,
"Yani huku Arusha pananikumbusha mbali sana Sam"
"Kwanini?"
"Nakumbuka ile siku ya kwanza mimi nafahamiana na wewe, mmh isingekuwa mimi kuja Arusha basi tusingefahamiana jamani"
"Sabrina, kila kitu hupangwa na Mungu kwahiyo labda tungekutana sehemu nyingine"
"Ila saivi naelewa ule usemi usemao kuwa kila jambo hutokea kwasababu"
Sabrina aliyafurahia sana mapenzi yake na Sam huku akingojea ndoa yake kwa hamu kubwa sana.
Muda wa kulala ulipofika, Sam alimpeleka Sabrina kwenye chumba cha kulala kisha na yeye akalala kwenye chumba kingine.

Kulipokucha wakafunga safari na kurudi jijini ili kuendelea na taratibu zao za kazi.
Walipokaribia mjini, Sabrina akamuona Jeff akikatisha njiani na kumwambia Sam,
"Si Jeff yule? Hebu simamisha"
Sam akasimamisha, kisha Sabrina akashuka na kumuita Jeff ambapo Jeff aliitika na kusogea alipo Sabrina,
"Unaenda wapi?"
"Kuna mdada fulani hivi mama kanituma nikamchukulie mzigo wake"
Sabrina alijikuta akimuangalia Jeff kwa hasira iliyotawaliwa na chuki, kisha akamwambia.
"Panda kwenye gari tukupeleke"
"Hapana, nimeshafika ni hapo tu"
"Unanisikiliza au hunisikilizi?"
"Nakusikiliza"
"Haya panda kwenye gari"
Ikabidi Jeff apande kwenye lile gari kisha Sabrina nae akapanda kwenye gari na kumwambia Sam,
"Haya sasa tuendelee na safari yetu"
Sam akawasha gari na kuendelea, Jeff akamuuliza Sabrina
"Inakuwaje na mimi safari yangu?"
"Huendi popote, nakurudisha kwenu. Kwa huyo mdada ataenda mwenyewe mama yako"
"Jamani mamdogo!"
"Tena usinilalamikie ng'ombe wewe"
Hata Sam akamshangaa Sabrina kuwa kwanini amekuwa na hasira kiasi kile.
Walimpeleka Jeff hadi kwao na kumshusha kisha Sam akampeleka Sabrina nyumbani kwake ili atulize akili.

Kesho yake, Sam kama kawaida alimfata Sabrina na kwenda naye kazini ila Sabrina alikuwa akijisikia vibaya na muda wote alikuwa akilalamika tu.

Walipokuwa ofisini, Sabrina akaona vyema kwenda kumuomba ruhusa Sam ili akaangalie afya yake.
"Najihisi vibaya kwakweli, nadhani nina malaria au typhodi"
"Basi ukapime ila uniletee majibu na mimi hapa"
Sabrina akakubaliana na Sam kisha Sam akampa Sabrina dereva wake ili ampeleke hospitali.

Alipofika hospitali, alipimwa vipimo vyote kisha daktari akamletea majibu.
"Hongera sana dada"
"Hongera ya nini?"
"Una ujauzito"
"Mungu wangu"
Sabrina alijishika kichwa na kuanguka chini.

Itaendelea



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa