Ilipoishia jana…
.Unajua jinsi ya kumlegeza mtu kwa maneno na kumfanya ajisikie mwenye hekima. Kama si tabia za ajabu tulizonazo sisi,ningekuomba umuoe Tuse,lakini haiwezekani,sisi ni kama Mashetani wadogo.
Songa nayo sasa..
“Najisikia aibu sana kukaa na wewe hivi nikiwa uchi,lakini nitafanya nini na hii ndiyo kazi yangu? Nitafanya nini na wakati nahitaji mambo yatakayonifanya nipumzike kuranda na wanaume kila kukicha.Nitafanya nini na wakati watoto wanahitaji kwenda shule na kula?
Prince,usinifikirie vibaya. Na usinichukulie mimi kama ndugu yako yoyote wa kike,bali niangalie mimi kama wanawake wengine wa mtaani”.
Mama Tuse hadi anamaliza kuongea hayo,alikuwa tayari kishaiva uso vya kutosha.Alikuwa mwekundu sana,na ule mkorogo anaoutumia,basi ndiyo mama wee,unaweza kusema ni andazi.
“Lakini Mama Tuse,wewe si una mume? Licha ya hayo,mimi nishatembea na mtoto wako,huoni aibu? Huoni aibu mimi kufanya mapenzi na mtoto wako na wewe unata……”.
Sikumalizia sentensi niliyokusudia,Mama Tuse akawa kadakia maongezi yale niliyokuwa nayaongea.
”Tuse si mwanangu,na yule si mume wangu. Ngoja nikutoe gizani sasa,lakini ndio iwe siri yako. Tumeamua kukwambia haya yote karibu kabisa na kaka yako kuja ili akija wewe uondoke uende popote,kwa sababu hatuwezi kuvumilia kuendelea kumuangalia mtu anayejua siri zetu.
Hapo nyuma,yule aliyegundua siri zetu,tulimfutilia mbali,ila wewe tunakuomba uondoke baada ya kujua haya”.
Mama yule aliongea kwa uchungu sana hadi nikajihisi kitu fulani kama huruma kikinikaba kwenye koo. Akaendelea kueleza.
“Baada ya maisha ya Mbeya kuwa magumu kwangu,niliamua kujiingiza kwenye biashara ya kuuza mwili,huko nilikutana na marika mbali-mbali ya watu wenye kazi kama mimi niliyokusudia kwenda kuianza.
Nilijitahidi sana ili hawa watoto wawili ambao ni Yesaya na Tumpare wapate chakula hasa huyu Tumpare aliyekuwa na miezi kama sita hivi.
Tumpare na Yesaya.Hawa ni watoto wa dada yangu aliyefariki wakati anajifungua huyu Tumpare. Alipoteza damu nyingi sana,na kwa kuwa tulikuwa tunaishi maisha ya kubangaiza,tulikosa hata hela ya kununulia damu hiyo,hivyo dada yangu aliaga dunia kihivyo. Nikaachwa na hawa watoto.
Nikawalea hivyo-hivyo huku maisha yangu yakiwa ya tabu sana tena sana. Huyu Tumpare muone hivi-hivi,kapita kwenye mabonde ambayo wewe hutokuja kuyapitia. Akiwa na mwezi mmoja tu! Alishazijua shida kama mtu mzima. Maji yasiyochemshwa huyu mtoto kabwia kama hana akili nzuri,hiyo ni sababu mimi sikuwa na maziwa wala hela ya kuyanunua.
Huyu Yesaya,na miaka yake minne,nilikuwa namtuma aende kutungua maembe au maparachichi ili tuje kula kama chakula cha mchana. Hakuna ajuaye sababu za sisi kufanya miili yetu maduka,bali yule muelewa pekee anaweza akakuelewa nini usemacho”.Mama Tuse japo aliongea kwa uchungu sana,lakini kamwe hakujaribu kutoa chozi.
“Prince. Mimi baada ya kuona watoto hawa watanishinda,ndio nikaamua kuingia kwenye biashara hii ya kuuza mwili,na baada ya kuingia tu!. Ni kama soko lilikuwa linanisubiri,haikuwa taabu kwangu kulala na wanaume wawili au watatu kwa siku moja. Na saa nyingine nililala na wanaume watatu kwa wakati mmoja.
Nilichokumbuka cha msingi,ni kwenda kutoa kizazi changu ili nisipate mimba zisizotarajika na wakati bado na watoto wengine,na ndiyo maana siku ile uliposema unajilinda kwa dhana ili mzuie mimba,nilikuona mtu mmoja makini sana”.Bado Mama yule aliendelea kunipa hadithi maisha yake.
“Kazi ilinilipa sana tu! Watoto sasa wakawa wanakula na kulala mahala panapoeleweka. Mavazi pia yakawa mazuri kwao.
Mwaka mmoja ukapita na maisha kwangu yakawa mazuri tu!. Katika mwaka huo,ndio nikakutana na huyu Tuse ambaye yeye alipenda kujiita Suzy,lakini mimi nilimuita Tuse ili aendane na hali ya kule Mbeya. Huyu na yeye ana historia yake binafsi ya kwa nini aliingia kwenye shughuli hii,sintomsemea moyo.
Camp ikaongezeka baada ya ujio wa huyu,na hela zikawa zinaingia haswa. Hapo ndipo tulipata wazo la kuhamia Dar kwa sababu kule kuna soko zuri kuliko Mbeya.
Tulipofika Dar,tukasaka nyumba moja kubwa,na kuanza maisha yetu kwa kazi ile-ile. Hapo sasa,ndiyo kama uchangudoa ukafika mahala pake.Kwani Tumpare akawa kidogo anaanza kutembea na kuongea,huyu Yesaya ikabidi tumpeleke shule za bweni maana tayari alishaanza kuelewa baya na zuri kwa umri wake wa miaka mitano.
Kazi ilipokuwa inazidi kunoga,ndipo tukakutana na huyu baba. Najua huwezi kuamini kwa muonekano wake,waweza kuhisi ni jambazi au mtu fulani mwizi. Lakini naye ana historia yake binafsi ya kuwa vile”.
Akanyamaza kidogo na kumuangalia tena Tuse ambaye alikuwa kimya wakati wote Mama yule anasimulia.
Baada ya kumuangalia sana Tuse. Nikaona Tuse akinyanyua mgongo wake pale alipokuwa kakaa na kuanza kuongea.
“Prince tunakwambia haya kwa sababu unaonekana huna mambo ya ajabu wala nini. Na kwa kuwa una-idea ya muziki na sanaa nyingine,tunaomba haya uyafikishe katika jamii. Baada ya mama kukwambia historia yake,na mimi nitakutafuta nikupe historia yangu na ya baba pia. Tunataka ujumbe ufike kwa kila mtu,ila tunaomba uondoke baada ya kujua haya. Nenda huko mbali kabisa,ndiyo katuelezee tulichokifanya. Hatukupenda hata kidogo,ni maisha tu! Mama endelea”.
Tuse aliongea na kumpa mama yake ruhusa ya kuendeleza gurudumu la hadithi aliyoianza.
“Huyu baba ni shoga, Prince”.Mama Tuse aliongea na kuangalia chini kwa aibu kubwa,na wakati huo mimi nilibaki kinywa wazi nisijue ni nini niulize au kujibu.
“Mwili wote wote ule,maguvu yote yale na mikwara kibao,kumbe si ridhiki? Daah! Kweli dunia ni tambara bovu”.
Nilijiwazia kichwani na kushindwa kuvumilia kabisa kwa nilichokisikia.
“Sasa kwa nini kawa vile?”.Niliwauliza.
“Hiyo ni historia nyingine ndefu sana aliyoipitia baba. Wala usijali,kabla ya kuondoka utakuwa umeipata”.Alijibu Tuse na kuniacha bila swali.
“Ndiyo hivyo Prince. Na yeye nilikutana naye katika harakati hizi hizi za kutafuta maisha. Tena yeye naweza kusema ana bahati japo afanyacho si chema. Watu wake ni watu wakubwa na wenye fedha sana. Hawa wazungu na watu wa nchi za nje,ndiyo wanaomweka mjini”.Mama Tuse aliongea huku bado akiwa ameangalia chini.
“Kitu pekee ambacho nakifanya katika maisha yangu,ni kuwawekea watoto wa dada yangu amana ya fedha ambazo zitawasomesha hadi watakaporidhika. Na najua watasoma sana baada ya kujua mama yao mdogo nahangaika kwa kujiuza ili wao wasome. Sina kingine cha kuwapa zaidi ya elimu,na nina amini,ipo siku watasema asante mama kwa msaada wako hata kama nikiwa kaburini.
Hata baada ya kufanikiwa kwao,labda mmoja akawa Rais,basi mimi nitamuita Rais aliyesoma kwa fedha za kujiuza mwili. Au shujaa wa changudoa. Nawapenda sana wanangu”.Alimaliza mama yule kwa kachozi kadogo kaliko mtiririka bila yeye kujijua.
***EPOSODE YA 11 Inaendelea*****
No comments:
Post a Comment