RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI 22 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, January 25, 2020

RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI 22





ENDELEA......
.................Nilikaa kwa takribani dakika kadhaa, jua likapambazuka na asubuhi ndio inaingia. Watu walianza kuingia maeneo yale ya ufukwe ndipo wakaanza kuzunguka lile eneo huku wengine wakawa wanakimbia ovyo.
Akili yangu ilirejea sasa kwa kile kilichotokea kuwa mimi ndio sababu kubwa.
Niliwaza baada ya kuwa na akili ya kawaida sasa ya kibinaadamu na kujua kuwa yale niliyoyafanya si mazuri kabisa. Ila tatizo nilishindwa kurudi pale kuwa watanifikiria vipi. Nilisukuma lile jahazi langu taratiibu kuelekea pale ufukweni.
Nikiwa na bukta yangu, nilikaribia fukwe ndipo watu wakaanza kugeuka na kunitizama mimi pale. Tukawa sasa tunashangaana. Lile eneo wengi walikuwepo akiwa na yule mzee mashuhuri kwa mambo ya uvuvi, yeye alikuwa ananifahamu fika kutokana na kuujua mkasa wangu kidogo.
Mimi pia macho yangu yaligota kwenye viini vya macho ya yule mzee na kufanya tutizamane kwa sekunde kadhaa. Palepale lilisikika gari lenye mlio wa king'ola kuhashiria ujio wa polisi ambao waliitwa kushuhudia yaliyojiri pale.
Yule mzee nilimuona kama kapandwa na jazba uliojawa na mshangao mkubwa, aliendelea kunikazia macho na mimi nikaanza kurudi nyumanyuma baada ya kuhisi jambo la hatari mbele yangu likikaribia kupitia yule mzee. Ndipo alipoanza kusema na kuwafanya wale wengine kushiriki kile akisemacho.
"Jamanii! Huyu mnamfahamu huyuu?"
Wengine walishindwa kuitikia kwa kuwa hawakunifahamu ila wengi hasa akina mama waliitikia.
"Ndio huyu si Mnalihuyu, alikuwa anatuuzia samaki".
"Sasa naomba mnisikilize! Huyu sio mtu kwa sasa"
"Sio mtuuuu...kivipi?"
"Hizi maiti huyu ndio mhusika na ndie alimuua Kibona ndugu yetu hapaswi kumuacha hai".
Aliendelea kuongea huku akilazimisha kuendesha hisia za watu na kuziteka kwa kuziamisha kuwa mimi mbaya.
Ni kweli ila yeye alizidi kuliongea lile kwa hasira ya kutaka kunimaliza. Palepale Polisi nao walifika mimi nikiwa kwa mbali hivi nazidi kuyoyoma.
Huku ufukweni zilibaki kelele za kunipigia mimi wakiwa hawafahamu kuwa wanampiga teke chura kwenye maji.
"Huyooo muuaji huyoooo".
"Mkamateniiiiiii".
Nashangaa nilipata nguvu za kupiga kasia na kukiondoa chombo pale. Punde kauli ya mapolisi ambayo iliniamuru mimi kusimama ilisikika.
"Kijana kwa usalama wako simama kabla hata hatujatuma vyombo kuja kukukamata kwa nguvu ya sheria".
Nikiwa najisemea mwenyewe kuwa.
'Bora hata kwenda kuishi kule kisiwani kuliko kunikamata nyinyi'.
Hapo ndipo kasi ilizidi kuongezeka zaidi ya kupiga kasia. Niligeuka nyuma kwa mbali naona boti zenye kutumia mashine zikipiga mwanga kuelekea kwangu. Tayari kila mmoja ana uchungu na mimi na ana hamu na mimi kukamatwa na kufanyiwa haki ambayo ingepaswa kufanyiwa.
Kutokana na upepo kuvuma sana maji yakiwa yanakupwa. Kutoka ufukweni kwenda mbali upepo uliovuma kutoka nchi kavu kuingia baharini. Ulifanya chombo changu kusonga haraka sana.
Sikuwa nafahamu wapi naelekea lakini niliwaza kuwa lazima nifike kule kisiwani hata kwa nguvu yeyote ile.
Kutokana na hofu kubwa niliyonayo, pamoja na mashaka ya kukamatwa na mapolisi walioungana na wavuvi kadhaa ilinifanya hali yangu kubadilika sasa.
Mikono yangu ilikakamaa na kufanya misuli itune. Hali hiyo ilipelekea damu nyingi sana kuelekea kwenye mikono na hatimae kuwa na nguvu maradufu.
Lakini damu ni ngumu kushindana na mashine, Wale polisi walinikaribia na kunizingira huku wakitaka nirejeshe chombo nyuma yaani nirudi nchi kavu.
Taratiibu hawa wanasogea kadhaa wakinionyeshea bunduki, nilifikilia kuwa nikikamatwa nitakufa dhalili mbele yao kwa sababu sitokubali kuteswa kwani hata hali yangu tangu inianze haitajiki nisumbuliwe hivyo nitasababisha madhara tu. Lakini pia nikikamatwa nitafanywa kama jumba la makumbusho kila mmoja kuja kunitizama ninavyobadilika pia najua hata mke wangu na mwanangu wakisikia hawatokuwa na amani.
Hili tatizo limetokea kisiwani kule inabidi nirudi kulekule kutafuta tiba yake, siwezi kukubali nikamatwe kizembe hapa.
Niliamua kujitupa kwenye maji na kuwaacha wakizubaa kwenye vyombo vyao.
"Hakikisheni mnamkamata huyo".
Nilijaaliwa kuwa na uwezo wa kutopumua kwa sekunde za kutosha ambazo pia nilizitumia kwa umbali mrefu.
Niliibuka mbali na wao, waliponiona nikazama kwa hiyo mchezo ukawa huo mpaka tulipopotezana.
Nguvu ziliniishia kabisa ndipo nikabaki nahemea juu juu kama mwizi aliyepigwa na kusubiri hukumu ya kifo tu.
Maji yalinipeleka nikiwa kwenye usingizi mzito ambao ulitokana na kupoteza fahamu.
Nilishtuka baada ya kuanza kutema maji kwa wingi. Kama mara sita hivi nilitapika maji tu, nilishtuka nipo fukweni tofauti na pale ambapo napafahamu.
Niliinuka taratiibu huku nikipiga mahesabu kuwa haya ni maeneo gani. Baada ya muda kadhaa jua lilikuwa kali sana na mimi nikiwa ndani ya hiko kisiwa nisichokifahamu.
Nilijichimbia ndani huku nikiwa makini nisije kukutana na vile viumbe tena.
Lakini ghafla nilikutana nao kama watatu. Nilishtuka, nikataka kurudi nyuma, nikapiga hatua moja nyuma.
"Ng'raaaiiiii...iiiiiiieeeiii".
Sauti ya wale viumbe nyuma yangu ilikuwa inasikika. Hapo ndipo nikajua maisha yangu yamekuwa mwisho sasa.
Niligeuka kweli nilikutana nae mmoja na mbele yangu wakiwa watatu sasa. Walinikaribia na kuanza kuninusanusa mara kadhaa huku wakinizunguka.
Niliwaza nikimbie maana hofu ilinitanda mpaka miguu ikaishiwa nguvu na haja ndogo ikigonga zipu.
Asikwambie mtu jasho lilitoka japo kulikuwa na ubaridi wa aina yake. Sasa wote walikaa upande mmoja yani wale watatu waliama mbele yangu na kukaa kwa yule mmoja huku wakinirukiarukia kama kunilazimisha kutembea.
Nililiwaza hilo nikapiga hatua moja na nyingine wakawa wanafuata kwa nyuma. Ndipo nilipotembea huku nikiwaangalia wale. Mmoja akasonga mbele kwamba nimfuate. Nilitembea hivohivo hadi eneo fulani hivi ambalo nilikuta mifupa mingi ya wanyama na mafuvu ya wanadamu kadhaa.
Nilizidi kuchanganyikiwa pale, nilishindwa kuwaelewa wale wanyama aina ya vibwengo vina nia gani na mimi. Ndipo mmoja akawahi kwa mbele na kupita kwenye kipango hivi, kazi huku nyuma hawa wengine waliokuwa wakikoroma na minjino yao ya ajabu. Sasa kila hatua niliyokuwa napiga pale nakanyaga fupa au fuvu la kichwa cha mnyama au binadamu.
'Daaah! Sasa kama hawa wameliwa mimi nitabaki kweli au ndio naenda kuliwa'.
Nilizidi kuwaza zaidi huku nikiomba mungu japo nilitaka mwenyewe kuja kisiwani.
Tulipofika pale kwenye lile pango mmoja akaingia na kutoka huku wakikoroma kwa nyuma yangu kama kunilazimisha na mimi niingie.
Niliinama na kujilazimisha kupita kwenye lile pango hadi nilipofanikiwa kuingia ndani. Aisee huko ndani hakusemeki kiza kinene, taa zilizokuwa zinaonekana ni macho yao tu. Ghafla ule mlango wa kuingilia ulifungwa "Mbaaa".
Mamaa yangu!.
Nilijisemea mwenyewe.
Nilitembea mule ndani hadi mahali fulani ambako kuna ukuta hivi, ule ukuta katikati yake kulikuwa na kama tundu ambalo lilikuwa linatoa mwanga mkali, niliusogelea ule mwanga hadi karibu na kuangalia lile tundu lipo la aina flani hivi limechongwa. Sikuwa naelewa hata mara moja.
Nilipata wazo kurudi maana pumzi ziliniishia kutokana na harufu kali ya mizoga. Kila utakapokanyaga basi mwili wa mnyama uliooza.
Hatimae na mimi nikashindwa kuvumilia na kudondoka palepale.
"...kijana! Unakumbuka mzigo gani ulikabidhiwa!..jitahidi sana ile almasi nilikuambia itakusaidia kwenye maisha yako nyakati zinyewe ndio hizi..na hapo ndio mahali penyewe...ulipouona uo mwanga...hao viumbe wamekulazimisha ufike hapo kwa sababu hiyo..wameshindwa kukuua kwa sababu una asili yao kutokana na kkuathiriwa baada ya kung'atwa....fanya hima upate lile sanduku ndio maisha yako...pia hao wanaamini kuwa wewe ndio mwenye uwezo wa kuwasaidia..hao...hawawezi kukuacha hapo...sasa fanya jitihada kuwatoka pia fanya jitihada kurudi kwenu kuchukua lile sanduku kwa maisha yako....".
Nilishtuka toka ndotoni. Maneno ambayo niliyapata kutoka kwa mtu nisiyemfahamu sasa kibarua kizito...

Je?...nini kitajiri



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa