RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU 23 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, January 25, 2020

RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU 23




ENDELEA........
.................

.................
................
................Baada ya kuhakikisha kuwa nilikuwa kwenye njozi nilikaa kitako lakini bado harufu kali ilizidi kunibana puani mwangu.
Siku na hata la kufanya kwani mwanga ule wa mwanzo sikuupata tena zaidi ya kiza kinene kutanda.
Hata njia ile ya mwanzo niliyoingilia sikuweza kuiona tena, hapo ndipo nilipojua kuwa sasa nakwenda kuangamia. Nyakati hizo nilijishangaa ule unyamaunyama ulishaniisha kabisa na nikabaki kuwa wa kawaida sana. Nilisimama kisha nikaanza kuchunguza mazingira ambayo ningeweza kutoka mule pangoni.
Kwa kweli nilijiona nakwenda kufa kwani hewa yote ya oxygen ilikuwa imepotea. Nilijipa moyo kwa kutembea kwenye miili ya wanyama waliokufa.
Nilipata wakati mgumu kupitia ile ndoto kuwa lile sanduku ndio maisha yangu na nahitajika nifanye harakati zote kulipata, lakini hawa wasifahamu kuwa natoka.
Niliendelea kuzunguka mpaka pale nilipoishiwa nguvu za kutembea kutokana na harufu chafu ya mizoga. Sikuwa nafahamu vyema ni aina gani ya mizoga ilikuwemo humo japo ni ya wanyama lakini wanyama wa aina gani, hii ilitokana na giza nene.
Nikiwa kwenye moja ya kona ndipo niliona kama mstari hivi unajichora kumbe ni mwanga uliojitokeza kutoka kule kwenye mlango wa kuingilia ndani.
Ule mwanga ulinipa mashaka kwa kiasi fulani, ndipo moyo ukaanza kudunda ghafla ndege waliokurupuka kutoka kule kwenye mwanga walikuja hadi lile eneo ambalo mimi nipo. Ndege hao aina ya popo walinipipa bishara kuwa mlango umefunguliwa kwani walionekana kutokea nje.
Niliona ni wakati tosha sasa niweze kunyatia kupita pale ili nitokee kule ufukweni. Kwa mshituko wa hali ya juu nilishangaa baada ya kusikia sauti ya mingurumo ya wanyama fulani ambao sikuweza kuwafahamu vyema.
'Mh! Hili eneo ni hatari, hapa nikichelewa naweza kuwa maiti muda si mrefu'.
Niliweza kutafakari mimi mwenyewe baada ya kuhisi hatari kubwa mbele yangu.
Niliamua kuingia ndani zaidi ya pango kisha nikafika mwisho wa safari yangu.
'Hakika mbio za sakafuni huishia ukingoni! Leo yamenikuta'.
Tumbo langu lina njaa kali sana, lakini hakuna hata chakula pale nilipo, hata kama kingekuwepo nisingeweza kula kutokana na hali ya hofu niliyonayo.
Kwa mbali nilisikia kama ukuta unapigwa na wimbi la maji kutoka baharini,
'Khaaa! Ina maana nakaribia kutoka'.
Nilipata wazo niweze kubomoa sehemu ya ukuta ili niweze kupita na kutokomea kabisa maeneo yale yenye hatari. Nilifanikiwa kuvunja hadi nikaona tundu kubwa limepatikana na ndipo nikalazimisha kichwa kupita. Kama unavyofahamu sehemu yeyote kichwa kikipita basi mwili nao utapita.
Nilipata nafasi hiyo na kutokeza hadi nje na mimi kujiona mshindi wa lile shindano ambalo bado sijui mwisho wake uko wapi😂😂😂. Sikuwa na jambo lingine zaidi ni kuanza kutokomea pale. Ndipo nashangaa kuona wanyama wale vibwengo wakipita nao pale kwenye tundu na kushuka chini huku wakionekana kuwa na hasira kubwa sana. Nilipatwa na mshtuko mkubwa sana, nilikumbuka ile ndoto kipindi nipo pangoni ikinisihi niondoke mule lakini bila wale viumbe kuniona.
Itakuwa walikuwa wananitafuta mule pangoni na hatimae wakafanikiwa kuniona. Niliwafahamu kuwa hawa viumbe hawana uwezo wa kuingia ndani ya maji kwa hiyo wataendelea kubaki palepale wakitapatapa na ndimi zao ndefu kunitamani mimi.
Niliamua kuwakatisha tamaa baada ya kuingia ndani ya bahari na kusogea eneo mpaka kule nilikokuwa awamu ya kwanza.
Nakumbuka kipindi nipo na yule jamaa aliyenisaidiaga kipindi kile baada ya kudhuriwa na hawa viumbe kisha yeye akatokomea ndani ya maji baada ya kunisaidia kupata sanduku.
Mitumbwi kwenye fukwe yeyote hata kisiwa huwa haikosekani.
Niliupata mmoja kisha nikajipanga kurudi kuelekea mjini kwa ajili ya kuchukua lile sanduku.
Safari yangu kama kawaida niliisubiri hadi usiku ndipo nikaingia nchi kavu ya ule mji wangu ninaoishi. Kama kawaida nilifika nyumbani sehemu ambayo imekuwa kama gofu kwa sasa nikapata shati na suruali nikabadili japo zilikuwa chafu sana. Usiku uleule nilitimua mbio kuelekea kwa yule binti anaejulikana kwa jina la Salha.
Sikufahamu yalikuwa majira gani lakini nilichojua ni kufika tu kwenye ile nyumba basi. Hatimae nilitumia muda mwingi kutokana na umbali wa lile eneo hivyo nilichoka sana. Nilipofika getini sikutaka kuingia kwa njia ya geti kutokana na shauku niliyonayo ya kutaka lile sanduku.
Sikujali kama nitakutana na afande kolokoloni pale, nilitafuta eneo zuri ambalo ninaweza kupitia. Nilirukia ukutani na kwa jinsi nilivyouparamia nadhani hata kama mlinzi alikuwa kalala basi aliamka.
Nilijinyonga vyema kutokana na wepesi wangu wa kupita maeneo kama yale. Sasa na mimi nilikuwa kama kibwengo wa kule kisiwani maana mambo yangu hata sikuwa nayaelewa. Nilipotua chini nakutana na mlinzi ambae alishawasha taa na kuukoki mgobole wake (Bunduki) ili akabiliane na adui.
Nilimuangalia kisha nikataka kuwa mpole baada ya kuhisi kuwa kaniona, lakini ajabu ananisogelea na kunipita kana kwamba hanioni, nilipiga hatua mbele napo hakustuka.
'Ina maana hanioni?, mimi ni nani safari hii'. Nilijiuliza swali hilo huku nikimuona mlinzi huyo akielekea eneo lake la kupumzika na kuupiga usingizi.
Nilipata fununu kuwa labda mlinzi alikuwa na mchoko wa usingizi ndio maana hakuweza kunizingatia. Taratiibu naelekea hadi kwenye mlango wa mbele ambao huwa wanaingilia. Nilishika kitasa ghafla nikasikia kitchie!!!. Alafu mlango unajifungua.
Huwezi kuamini geti lilikuwa kama buwa kuligusa tu napita. Nilijishangaa, lengo ni kupata boksi langu. Nilitembea kidogokidogo kuelekea chumbani kwa Salha ambako nilipafahamu mwanzo kabisa. Nilifanikiwa kuingia hadi chumbani kwake ndipo nilimkuta akiwa kalala kama alivyozaliwa. Tamaa ya mwili kama mwanadamu ilinifanya nijikute namuingilia binti yule bila hata yeye kujifahamu. Nilikuwa kama shetani aliyekimbia kuzimu.
Lakini kwangu ndio lilikuwa kosa kubwa sana kwani nilishtuka asubuhi baada ya kelele za Salha.
"Heeee! Nini"
"Wewe nani? Na umewezaje kuingia humu ndani".
Niliona ni muda wa kutumia nguvu sasa.
"Samahani ila, hata nikakuambia huwezi nielewa, unanikumbuka mimi ni yule ambae ulinisaidia kile kipindi nimekamatwa na polisi kupelekwa hadi hospitali.. na wewe ukanisaidia hadi hapa".
"Sawa...nakumbuka umeingiaje humu....?"
Tulizozana sana hadi nilipotumia nguvu ya kumkalisha kimya.
"Wewe mwanamke! Niambie sanduku langu umeliweka wapi...?"
"Hapana mimi sifahamu tangu wazoa taka waje hapa kuchukua ile siku nadhani walilibebelea..."
"Sikia lile sanduku ndio maisha yangu mimi mpaka sasa.....nakutaka unipe taarifa kamili kuhusiana na hao wazoa taka niwafahamu...boksi kama lile likionekana lazima likamatwe hakuna anaeweza kuliacha hivhivi.".
Salha alinielewa kwa kuwa hata mwanzo nilikuwa pale.
Tulianza kupanga mishen nzima ili kupata lile sanduku.
"Sasa...mnali unatakiwa kujificha humu chumbani....utakuwa unatoka usiku tu huo ndio msaada wangu uliobaki".
Nilikubaliana na yeye ila nilimuomba anipe taarifa kuhusiana na hao watu wanaohusika na mambo ya uchukuaji taka majumbani. Siku kama tatu nikawa nimefanikiwa kuwajua hadi eneo ambalo wanaishi wale wazoa taka na mimi nikajiandaa kwa ajili ya kuelekea huko.
"Mnali... unajua sikuelewi siku ya pili hii unachokula sikifahamu haya leo unakula nini?".
Nilishindwa kumueleza ukweli kuwa chakula cha kawaida kwangu hakipandi zaidi ya nyama mbichi.
"Salha! Ngoja nikuhadithie historia yangu ili unielewe..."
"Haya nakusikiliza..."
Nilimhadithia kila kitu.
"Daaah! Jamani sikudhani kamaa kuna watu wanaishi hivyo kama wewe...kwa hiyo nyama mbichi tu basi".
"Yani ndio hivyo ndio inanipa nguvu hata kufanya vitu vingine ambavyo mwanadamu wa kawaida hafanyi..."
"Mh! Kwa nini"
"🤣🤣🤣🤣🤣 teh teh"
Nilibaki kucheka tu.
"Unataka ufahamu?"
"Ndio..."
"Basi niletee nyama mbichi alafu kabla sijaenda kuwafuata wale watu nitakuonyesha wewe kwanza hapahapa chumbani...."
Salha alizidi kuchoka kwa kila hatua ninayomueleza.

TUKUTANE TOLEO LIJALO



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa