RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA 21 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, January 25, 2020

RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA 21



ENDELEA.......
.......Mlango unafunguliwa na kuingia Vijana kama watatu ambao sikuwa nawafahamu kwa sura, bali kwa idadi kutokana na wao walikuwa wakinimulika tochi usoni na kufanya nikose nuru.
"Eheee! Kwa hiyo bwana Paul hakuona vijana wa kufanya nao kazi hatari kama hii na wakakutumia wewe?".
Mmoja wao aliongea aliyeonekana kuwa kama mkubwa kati ya wale watatu. Lile swali halikunifanya nijibu kwa haraka kama vile ambavyo wao walihitaji nijibu bali nilibaki kuwa kimya. Hii yote kutokana na kichwa changu kupokea maumivu makali ambayo yalisababishwa na purukushani za kutwa nzima hadi nyakati zile.
"Kijana! Sisi hatuna shida na wewe kabisa, tunachohitaji ni kujua unaeje huyu bwana Paul?"
"Mimi sijui chochote".
Nilimjibu.
Lakini ilionyesha wazi kuwa jibu langu hakulizika nalo maana alisimama kisha akainama tena na kuniangalia
"Unasemaje?"
Aliniuliza swali lilelile
"Mimi sijui chochote"
Alinizaba kibao cha maana, kilichonipeperusha kama mzoga hadi ukutani na kujikuta napata maumivu ya zaidi.
"Aiseee! Muite mzee mara moja nitamuua huyu".
Ndipo yule kijana mwingine kati ya wale wawili waliobakia alitoka na kuelekea nje ya chumba tofauti na pale.
"Kijana, nakuambia hivi huyu anaekuja ni mkatili sana sasa mjibu upuuzi wako alafu utajua nini atakufanya nyang'ao nyoooooooh!".
Dawa ya mjuaji au baunsa ni kukaa kimya tu wala usijibujibu ovyo.
Punde tu wanaingia wawili. Taa iliwashwa na kunipa mimi nafasi ya kuwaona wote wa mule ndani. Huyu aliyeongezeka nadhani ndie alikuwa mkuu au mzee wao ambao walikuwa wanamzungumzia.
Yule jamaa aliwaomba wale waondoke kwanza, baada ya kuondoka ndipo akachuchumaa na kunitazama kwa makini.
"Kijana unaitwa nani?"
"Naitwa Mnali"
Nilimjibu
"Ooooh! Wewe kijana sio mgeni kwa hilo jina lako, bwana Paul ni mtu mdogo sana kwenye biashara, sasa alinipa taarifa zako juu ya wewe kuwa ukimsumbua sana".
"Lakini sio kesi, nahitaji unifanyie kazi yangu tofauti na hapo nakuua"
Nilishtuka sana kiukweli,
"Kazi gani hiyo".
Alikuwa anacheka.
"Hahaaaah! Hahaaaa! Aaaaah"
Nilibaki kumtazama tu huku nikitafakari ile kauli yake.
"Wewe ni mvuvi hodari si ndioo!"
"Ndio ndio kazi yangu hiyoo"
"Sawa! Kuanzia sasa acha kufanya kazi na Paul. Mimi nina kazi yangu ya kuuza madawa ya kulevya, sasa nitakutumia wewe kuuza".
"Hapana kiukweli siwezi kufanya hiyo kazi mimi, na pia naomba uniachie tu maana mimi ni mtu duni sana sina cha kukulipa au kukupa zaidi utanionea bure".
"Hapana wewe ni muhimu kwetu na kama utasumbua tunakuua".
Tulichukua kama dakika kama kumi tukizozana ndipo mzee akapandwa na hasira akamuita kijana mmoja aliyepo nje.
"Nataka huyu usiku huu.."
Akiwa anaangalia saa
"Saa! Saba...mpatieni Adhabu si hapa! Pelekeni kokote kule piga mpaka afe! Pumbavu hatutaki ushahidi..akiachwa huyu polisi watatusumbua uaaaaa!".
Hilo ndilo lilikuwa tamko la huyu jamaa kuwa niuliwe lakini si pale kwake.
Nikiwa nasubiri kinachoendelea, ghafla kwa nje nilisikia gari likinguruma. Ndipo nikajua maandalizi ya mimi kwenda kuuliwayalikuwa tayari.
Mlango ulifunguliwa na mimi nikachukuliwa mkukumkuku hadi kwenye gari.
Vijana wapatao sita sasa walinizoa moja kwa moja njia kuu kuelekea huko ambako walitaka kuelekea kutimiza azma yao.
Njiani nikiwa naomba mungu anisaidie kikombe kile kisinikute, nilijikuta nakumbuka mambo mengi ya nyuma ambayo yalinipandisha hasira sana. Nilishindwa kufanya chochote.
Walizidi kusonga mbele zaidi majira ya usiku, mimi nikiwa nawasikiliza sina uwezo kwani hata nikipiga kelele hakuna ambae anaweza sikia.
Kwa mbali sauti ya maji yakinguruma kutokana na mawimbi ya bahari, ndipo nikajua kuwa napelekwa baharini, baharini wakiniua kwao ni rahisi kunitupa humo.
Nikakumbuka kifo cha Kibona alivyokufa, alifia mule baharini tena kwa hila za hawa watu hasa za bwana Paul. Bwana Paul anafanya kazi, anamiliki hotel nyingi, lakini pia anafanya kazi za uuzaji wa madawa ya kulevya, akishirikiana na huyu jamaa ambae simfahamu kabisa.
Safari ilifika mwisho hadi kwenye ufukwe wa bahari ambako kulikuwa kimya kabisa, kwa kuwa ni usiku mnene. Walinitoa mkuku mkuku na kunitupa kwenye mchanga.
"Moris!..."
"Naaam!"
"Tunafanya lipi, kupiga kwanza na kumtupa au tunamtupa moja kwa moja".
Nilimsikia mmoja akiwa anaongea hivyo.
"Hapana! Hawezi kutupwa hivihivi, huyu ni mvuvi pia anajua kuogelea! Tupige tuvunje nguvu kisha tunamaliza kilain".
Nikiwa pale chini, nilihisi kama wale viumbe ambao nilikutana nao kule kisiwani, wananiangalia kwa huruma sana, pia niliona kama yule rafiki niliyekutana nae kule kama namuona kwenye macho yangu yenye kutoa chozi la hasira.
Kama unafahamu kuwa baharini kuna hali ambayo inaonyesha harufu ya samaki. Ile harufu yake nilipata kuivuta kwenye pua zangu na kuanza kuhisi msisimko.
Wakati najikongoja kuondokana na ile hali ndipo nashindiliwa teke, nikaanguka tena chini, akaja mwingine akanipiga nondo ya mguuni 😢😢 nikashtuka na mguu nikahisi umevunjika kwa maumivu wakati wanavuta bangi zao na wengine wakivuta kupitia viganja na pua zao, walianza kunicheka kwa dharau..
"Haaaaa! Haaaaa! Lazima ukasalimie kuzimu mbaaaaafu!"
Nilijaribu kuomba msamaha kwao ili wasiendelee kunidhuru lakini majibu yao yalinikata maini.
"Jamanii mimi masikini, nisietaka shari na mtu, nimetoka kwenye matatizo na mpaka leo hii nahangaika nipate kumsomesha mwanangu naomba mnisameheee"
"Haaaa! Una mtoto wewe! Ina maana una mwanamke! Huyo mwanamke unampa nini...anaitwa nani huyo demu maana wewe unakufa yeye tunaenda kumhudumia sisi.."
"Jamani kuweni na huruma! Familia yangu inaishi kwa mwingine..mwanangu anaitwa Asantee.."
"Oooh!!! Haijarishi kwetu hilo kukuua wewe sisi tunapata pesa ndefu...."
Wakaanza kunivutavuta pale kama mpira wa kona. Hapo sasa mwili unachachamaa kubadilika baada ya kupata harufu ya nyama ile ya samaki. Nilijikuta nikipiga keleleee.
"Kimbieniiiiiiii....msije karibu yanguuuu".
Walinicheka na hapo wakiwa na nia ya kuja kunimaliza kabisa waondoke.
Aiseee! Nguvu na shauku ya kila kiungo cha mwili wangu kufanya kazi ilikuja, sielewi hata ilikuwaje maana nilikuja kujitambua Karibu alfajiri hivi kidogo gari kwa mbali nilizisikia.
Niliamka na kuangalia pale chini yote mizoga na wengine hawana viungo kama mkono pamoja na uso hautamaniki.
Ghaaa! Nilistaajabu baada ya kuona lile tukio la ghafla na hatari kwangu.
Gari naliona wale watu walikuwa sita. Pale chini wako tano hata sikuwa naelewa kwa lile tukio kwa kuwa sifahamu. Niliona vyema nijifiche kwanza, niliiba mtumbwi wa karibu yangu kisha nikaingia ndani ya maji na kukaa kwa mbali hivi nione nani ambae alifanya lile tukio au ilikuwaje...

TUKUTANE TOLEO LIJALO.....



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa