ENDELEA.....................
.................
...24.........
Salha alitulia kisha akaniuliza tena,
"Mnali, unajua sijakuelewa japo umenieleza kila kitu kinachokuhusu, sasa inawezekana vipi usile chakula cha kawaida alafu badala yake ukapenda nyama mbichi?".
Swali lake lilikuwa lina maana kubwa sana kwangu lakini sikuwa na namna zaidi ya kuwa muwazi mbele yake.
"Salha! Nisikilize kwa makini tena kwa umakini mkubwa sana"
"Ndio nakusikiliza".
Niliinuka kisha nikauelekea mlango nikautikisa ili kujua kama umefungwa na kweli ulikuwa umefungwa.
"Vipi! Hakuna mtu tofauti na mimi na yule mlinzi"
"Kwa nini uishi peke yako"
"Basi tu haya tuendeleee"
"Sawa Salha! Kama nilivyokuelekeza natafutwa na makundi mawili mpaka sasa tena matatu..hapa ninapokuambia polisi nao wananitafuta, maisha yangu ni ya ajabu sana na yameibuka kutoka hivyo na tatizo ni Uvuvi wangu".
"Uvuvi wako? Kivipi tena".
Aliuliza
"Maisha ya Uvuvi ndio chanzo cha haya yote. Kama mke wangu asingekuwa analazimisha kutaka maisha mazuri ya kifahari mimi nisingejiingiza katika hali hii".
Tulitumia muda wa masaa kadhaa mimi na Salha kuongelea maisha yangu kiujumla. Historia iliyomuacha hoi na kumtoa chozi binti wa watu.
Wakati huo nina nia ya usiku kuwafuata wale majamaa kufuatilia lile swala la Sanduku ambalo ndio maisha yangu kwa sasa.
Ilikuwa majira ya Saa kumi na mbili jioni jua kuzama nikiwa kwenye foronya moja wapo mule ndani. Tangu niweze kuathirika na wale wanyama sikuwa na akili zangu za kawaida kwanza nilikuwa Mcheshi nisieogopa chochote kile, sikuwa muoga tena wala mwenye aibu kama mara ya kwanza pia ni historia yangu tu inayonihusu ndicho ambacho nilikuwa nakikumbuka kichwani kwangu.
Salha alinyanyuka na kwenda kuandaa chakula huku akiniacha peke yangu mule chumbani. Kama nilivyokuambia sikuwa na hofu kabisa alafu nilikuja kujiamini sana.
Wakati yeye Salha yuko Jikoni mimi nilijiegemea kwenye kochi na kufumba macho kidogo huku nikitafakari juu ya mustakabari wa maisha yangu jinsi unavyokwenda.
...."Sikia! Usalama wako ni pale tu utakapofanikisha kufikisha sanduku sehemu husika...".
Nilikuja kushtuka kumbe nilikuwa dotoni. Kuna kitu kama kinanikumbusha wajibu wangu wa kufanya ila bado sijatambua ni nani au anahusika vipi huyu na maisha yangu mimi kiujumla.
Hapo ndipo Salha alikuja na Sahani mbili zilizofunikwa.
"Haya! Ila bado siamini kuwa ukila nyma mbichi unakuwa wa tofauti".
Kweli zililetwa Nyama kama vipande vitano hivi na yeye akawa anakula chipsi yai pamoja na nyama za kukaanga. Alianza kula na mimi nikaanza kuzitazama zile nyama ndipo mwili ukaanza kusisimka mate yakaanza kujaa pale ghafla napata hamasa ya kuvamia vile vipande na kuvitafuna dakika zisizozidi mbili tayari nilikwishamaliza na kumuacha Salha akiwa anaduwaa.
"Mamaaaa yanguuuu weeeee!"
Salha hakuweza kuamini kama kweli naweza kufanya vile.
"Salha! Unashangaa nini bado ngoja kama unakumbuka awamu ya kwanza ulishangaa nyama jikoni zinaisha hukuwa unafahamu alikuwa mimi yule.."
Palepale mwili ulichangamka damu zilikwenda kwa kasi ya ajabu mwilini. Mikono yangu ilikakamaa nilitokwa na jasho jingi, Salha aliniogopa kwa kweli.
Binafsi sikuwa nafahamu nini nafanya kwa kuwa hata akili iliruka. Kila nilichotaka kufanya niliona sawa tu. Nilisimama ndipo nikamtia hofu zaidi Salha aliyetaka kukimbia mule chumbani.
Muda wa mchache tayari nilishamkamata na kujikuta tunaingiliana kimwili, katika hali isiyofahamika Salha alilia kwa uchungu wa ukweli kuwa anapata maumivu sana. Mpaka tunamaliza hakuna ambae aliweza kumuangalia mwenzake.
Mimi tayari nguvu zote ziliniishia kwa kuwa nilitumia hadi nguvu zangu za ziada. Nakuja kushtuka saa nane usiku siwezi hata kuinuka kitandani. Asubuhi na mapema najilaumu kwa nini nilifanya lile tukio.
"Mnali sijawahi fikilia swala kama hili, kuanzia sasa naomba niwe wako sitaki nikose mapenzi yako kabisa".
"Hapana hata hivyo najilaumu kwa jambo kama hili ila siwezi kuwa na wewe kwa sababu nina mke na mtoto naamini mke wangu ananipenda bado sitaki ijirudie tena".
Nilijikuta namlaumu sana Salha, amenifanya hata kuchelewa katika lile dili langu.
"Khaaa! Unadhani ni mwanamke gani ambae anaweza kuacha radha hii au ni mwanamke gani anaweza kukuvulia nguo alafu umchezee umuache eti nilikuwa sijielewi, sasa sikia ukisumbua hutotoka humu ndani."
"Kwa nini Salha unifanyie hivyo"
"Au laaah! Utalikosa hilo sanduku."
"Hapana nakuomba uniache kwa sasa nikifanikiwa nitarejea kwa ajili yako. Nakuahidi.."
"Mnali mimi sio mtoto mdogo unaelewa. Chagua moja"
"Eeeeeh!"
"Husikiiii! Chagua moja kukosa Sanduku lako au kuwa na mimi ili ulipate hilo Sanduku kwa muda tutakaoishi kama wapenzi".
Hapo aliniacha nikiwa na mawazo mazito asubuhi hiyo, mpaka nikajilaumu kwa nini nimefika hapa, pia hali yangu.
Najua Salha niko mikononi mwake hadi sasa inanibidi nikubaliane na lile alitakalo ili nifanikishe azma yangu.
"Salha sawa nimekubali kuwa na wewe kama unavyohitaji ili niweze kupata sanduku langu."
"🤣😂🤣🤣"
Salha alicheka sana kwa kuwa anafahamu sina ujanja mwingine zaidi wa pale. Salha aliendelea kunipa maneno ya kimapenzi pale na ndipo akanikamata sana kimawazo. Kila mmoja alienda kuoga kwa muda wake. Wote tulikaa pale kitandani huku mimi nikiwa nawaza vitu vyangu kabisa.
Siku hiyo ilipita kimawengemawenge, mpaka ilipofika jioni ndipo nikajipanga vyema sasa kuelekea katika kampuni moja ya uzoaji wa takataka. Nilikuwa na Salha, tukiwa kwenye gari Salha aliniomba nibaki kwenye gari alafu yeye aelekee akaangalie humo ndani mkoje kisha atakuja kuniambia.
Njia ambayo aliniambia kuwa ataingia kwa njia ya kusema anaenda kulipia bili ya ukusanyaji wa takataka tena. Hapo sikuwa na ubishi. Nikiwa kwenye gari katika kuangalia angalia nilikutana na Simu ya Salha, niliigundua baada ya kuwaka mwanga.
Nilipoangalia niliona Meseji kutoka kwa mtu mmoja anaitwa (Mr. Poooo).
Mh! Sikuweza kuangalia nini kimeandikwa kwa sababu kulikuwa na pass word. Ila jina lilinitikisa akili kidogo si kwamba nilijua ni yule mzee Paul ila nilimkumbuka yule mzee. Ghafla Salha anarejea.
"Sasa! Sikia tayari nimeingia ndani nimeongea nao kuwa kuna mzigo walikuja kuuchukua kule nyumbani kimakosa...ila wanasema hawaufahamu..."
"Daaah! Sasa inakuaje tena!"
"Mh! Ngoja kwanza naomba simu yangu hapo kwenye kiti".
Niliichukua na kumpatia.
"Sawa nashukuru sana! Ngoja nakuja acha nikaongee nao tena".
Basi nilitulia kwa kuwa sina Uhakika sanduku liko wapi. Ghafla anakuja jamaa mmoja aliyeonekana kama msimamizi hivi wa mule kwenye kampuni.
"Mambo vipi mheshimiwa"
Jamaa aliniuliza
"Poa kabisa"
"Ok! Vipi mwenye hili gari yuko wapi yani yule dada ambae ulikuwa nae humu".
Kwa kuwa nilivaa jaketi lenye kofia hakuweza kuniona vyema.
"Aaah! Huyu dada yuko humo ndani anafanya mazungumzo na wahusika humo ndani".
Ajabu akanza kuniinamia kupitia pale dirishani, pia na mimi nilifunika zaidi Sura yangu ili asinione.
"Sikia! Unamjua vyema huyu dada...."
"Mh! Kwa nini unauliza hivyo.."
Nilishangaa sana yeye kuniuliza swali lile. Lakini alikuwa ananicheka sana kisha akasema
"Kijana Be care..".
Mh! Alinitisha sana sikujua anamaana gani kwa sababu hii lugha siifahamu kabisa kiingeleza.
Ndipo Salha anakuja anapishana na yule jamaa. "Mnali, ulikuwa unaongea nini na huyu!"
"Hapana alinishangaa tu kwa nn tupo hapa kwa muda sana".
"Mnali, Be care".
Hapo nilishtuka sana "Salha! Hilo neno lina maana gani?"
"🤣🤣🤣🤣🤣 maana yake Kuwa Makini na hawa watu"
Ahaaaa na mimi nikajua kuwa yule jamaa aliniambia niwe makini na Salhaaaa. Kwa nini niwe makini na Salha, ana nini Salha.
TUKUTANE TOLEO LIJALO




No comments:
Post a Comment