MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA KUMI NA MOJA-11 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, January 16, 2020

MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA KUMI NA MOJA-11




MREMBO WA WA KIJIJI


         SEHEMU YA KUMI NA MOJA-11

Bibi Pili alishtuka kusikia maneno hayo yaliyoongeleka kwa kujiamini, aliyasema maneno hayo hakuwa mtu mwingine ni mzee Bidobido mdogo wake mzee J ambaye kwa upande wa Chitemo ni baba yake mdogo.

 "Wewe unaongea hayo ni kama nani?.." Aliuliza bibi Pili. Bidobido akaangua kicheko kisha akajibu "Hupaswi kujua, sema kama upo tayari" Maneno hayo ya Bidobido yalimshangaza sana bibi Pili, ndipo alipoona hakuna haja ya kumkimbia mzee huyo. Alipiga kiganja chake chini, ikatimka vumbi ya ajabu halafu akarusha kombora la kichawi. Bidobido akapotea akaibukia upande wa pili, makombora hayo ya bibi Pili yakawa yamepotelea sehemu isiyojulikana.

"Aha hahahahah hahahah!.." Alicheka mzee Bidobido wakati huo huo bibi Pili akarudia kuachia makombora mfululizo, bado Bidobido alionyesha umahili wake wa kuyakwepa lakini licha ya kujitahidi  moja lilimpata, mzee huyo akawa ameanguka chini kama mzigo wa kuni uangukapo kutoka kichwani.  Alisafa  akiwa chini. Baada ya muda mchache alinyanyuka akajikung'uta vumbi kisha naye akajibu mashambulizi ambapo alimrushia bibi Pili visu vya kichawi vilivyo sheheni sumu, bibi Pili akapotea mahali hapo, vumbi kibao ikatimka vilivyo. Na punde si punde akaibukia nyuma ya mzee Bidobido bila kupoteza muda akamtupia kombora lakini uzuri halikumpata mzee huyo kwani alishtuka akageuka nyuma na kisha akaliyeyusa kombora hilo likawa maji. Hapo sasa patashika nguo kuchanika, ugomvi mzito ulitawala wakati huo kijana Chitemo akiwa kando akishuhudia balaa la bibi Pili na baba yake mdogo.

   Upande wa pili, mzee J alionekana kupagawa. Akatoka chumbani kwa mwanae huku akichechemea akarudia chumbani kwake, kwa sauti kuu akamuuliza mkewe "Mama Chitemo, kwani kuna mahala umetuma Chitemo?.."

"Hapana, umemkosa chumbani kwake?.." Alijibu mama Chitemo huku akiacha na Swali. Mzee J alishusha pumzi kwanza halafu akajibu "Ndio ila sijamkuta"

"Mmmh au kuna mahali kadamkia? Lakini kama kuna mahali kaenda si angesema?.." Aliongeza kusema mama Chitemo. Mzee J hakusema jambo hapo, alikaa kimya huku akaonekana kufikiria kitu fulani. Akakumbuka zaruba la jana alilokumbana nalo, akakumbuka pia na sauti ile ya treni. Hapo J akapata taswila fulani, hivyo alizama uvungini mwa kitanda chake haraka sana. Punde si punde akatoka na jungu kuu jeusi lililojaa mazaga zaga ya kichawi.

"Baba Chitemo unataka kufanya nini sasa?.." Aliuliza mama Chitemo. J hakujibu aliendelea na mkakati wake, lakini bado mama Chitemo alihitaji kujua ni kitu gani anachotaka kukifanya mume wake hivyo alirudia kumuuliza. Safari hiyo mzee alimkunjia sura kisha akamjibu
" Wewe mwanamke wewe, kaa kimya mbona unakiherere sana? Nitakufanya kitu kibayaa? Ooonhoo sio kila kitu lazima ukijue, nimekuuliza mtoto yuko wapi, umenijibu majibu ya kipuuzi tu yasiyokuwa na mbele wala nyuma. Basi utulie ili nifanye mambo yangu ili nijue wapi alipo, unakazi kuniuliza tu. Hebu niache"

" Mmmh kwa hiyo baba Chitemo nimekosea kuuliza?.. " Alihoji mama Chitemo ila kabla mzee J hajamjibu mara ghafla nje ilisikika sauti ikisema" Bwana mkubwa! Bwana mkubwa!.. " Mzee J aliposikia sauti hiyo alitulia huku akiisikiliza kwa umakini alipojua ni sauti ya mdogo wake alikisukuma uvunguni chungu chake hicho kilichojaa mazaga ya kichawi kisha akainuka akajikokota mpaka nje. Alipofika nje alipigwa na butwaa baada kumkuta mdogo wake akiwa amempakata Chitemo.

Chitemo alikuwa amepoteza fahamu wakati huo mwenyewe mdogo wake akivujwa damu sehemu baadhi ya mwili wake  "Nani kafanya hayo?.." Aliuliza mzee J kwa hasira. Mzee Bidobido akamshusha Chitemo chini kisha akajibu "Kaka nimemkuta mtoto huyu yupo na bibi mmoja hivi, na kama nisingefika mapema basi leo Chitemo tungemzika"

"bibi huyo yupoje, unaweza kuniambia?.." Alirudia kuuliza mzee J kwa hamaki kubwa. Bidobido akashusha pumzi ndefu kisha akajibu "Abadani siwezi kumfahamu ila nafikiri baadaye kijana akizunduka ataweza kutuambia, hakika ni moto wa kuotea mbali mzee mwenzangu" Alijibu mzee Bidobido wakati huo huo mama Chitemo alifika, alijikuta akiangua kilio baada kumuona shemeji yake na mwanaye wapo hali mbaya hali ya kuwa Chitemo akiwa kazimia.

Hayo yalipokuwa yakiendelea nyumbani kwa mzee J, kwingineko bibi Pili alitokea nyumbani kwake. Naye alikuwa hoi. Alikaa chini ya mti wa mwembe ulikokuwa karibu na nyumba yake halafu akamuita mjukuu wake wakuitwa Pili.

"Abee bibi" Aliitika Pili na punde si punde akatii wito, alipomkaribia bibi yake akatabasamu halafu akasema "Umekuja saa ngapi bibi?.." bibi Pili aliangua kicheko kisha akajibu "Ndio nimefika mjukuu wangu wewe siulikuwa ndani? Utanionaje sasa"

"Sawa. Eenh! Vazi tayari vimeiva ila karanga bado. Vipi nikuletaa hivyo hivyo ili upoze njaa?" Aliongeza kusema Pili.

 "Aah hapana ngoja nipumzike kwanza, wakati huo wewe unaziandaa na hizo karanga" Alijibu bibi Pili. Hapo pili akasimama akazipiga hatua kuelekea ndani kuendelea na mapishi lakini kabla hajaingia ndani bibi yake akamuita kwa mara nyingine tena. Pili akatii wito ambapo bibi yake akamtazama usoni kisha akamuuliza "Hivi ni kweli unamtaka Chitemo?.." Swali hilo lilimfanya Pili kuonyesha tabasamu pana, baada ya tabasamu hilo akajibu "Ndio"

"Aanhaaa basi usijali utapata tu kwa vyovyote vile liwake jua inyeshe mvua. Akikukataa nitamfanya kitu kibaya sana mpaka ajutie maamuzi yake ya kukuacha"

"Wewe sio uwanja wa mazoezi Pili, kama aliweza kukurubuni ukampa bikira yako, basi kwa vyovyote vile atakuoa" Aliongeza kusema bibi Pili, kwa msisitizo. Wakati bibi huyo anasema hayo, upande wa mwingine mzee J alionekana kusikitishwa na jambo hilo alilofanyiwa kijana wake pamoja na mdogo wake.

"Bwana mdogo hebu muingize ndani kijana wetu, bila shaka watu wa kijiji hiki wanatafuta balaa. Wao siwanaunda treni zao zinazotembea pasipo na reli? Sasa mimi nitawageuza wote vyura. Ili wajue kuwa mimi J sijaribiwi"

"Mambo sasa yamekuwa makubwa, acha moto uwake Ndaulaike" Aliongeza kusema mzee J kwa hasira na ghadhabu punde mboni za macho yake zikabadilika rangi zikiwa za kijani kwa sekunde kadhaa kisha zikarejea kwenye hali yake. Balaa.

JE, MZEE J ATAWEZA KUFUA DAFU? Mambo yamekuwa makubwa.
    >>Kundi la Bibi Pili kikwazo 😎
      SHEA MARA NYINGI ILI kisha NJOO INBOX NIKUTUMIE SEHEMU YA 12..ofa hiyo.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa