MREMBO WA WA KIJIJI
SEHEMU YA KUMI NA MBILI-12
"Ni kweli kaka usikubali kujaribiwa bwana, inatakiwa kijiji chote kikuogope maana la sivyo utachezewa sana wewe na familia yako. Leo sikachezewa mwanao? Kesho huwenda akachezewa mkeo keshokutwa utachezewa wewe. Kwahiyo jihadhali kabla ya ajari unajua kinga bora kuliko tiba "alisema mzee Bidobido akimuasa kaka yake.
Upande mwingine mzee Nhomo alikuwa akizipiga hatua kurudi nyumbani, usiku wa jana alilala shambani baada kuanguka wakati alipokuwa kwenye haraki za kwenda nyumbani kwa mzee J kwa nia ya kupambana lakini safari hiyo ikawa imeishia njiani baada kutunguliwa na makombora ya kichawi kutoka kwa timu aliyomo bibi Pili. Mzee Nhomo alipoanguka usiku huo hakutaka kurudi nyumbani, alipita shambani ambapo huko alilala kibandani mpaka asubuhi. Alionekana akitembea kwa kuchechemea, ni dhahili shahili makombora yale yakina bibi Pili yalimchafua vilivyo. Alipofika nyumbani kwake alimwambia mkewe amchemshie maji ili ajikande, alijihisi maumivu makali mwili mzima. Jambo hilo lilimshtua mkewe ambapo alikata kauli na kisha kumuuliza kipi kilicho mkuta "Mume wangu kwani umetoka wapi asubuhi yote hii? Ina maana ulishindwa kurudi nyumbani mapema?.."
Mzee Nhomo aliposikia swali hilo la mkewe aligugumia maumivu kidogo halafu akajibu "Mama Chaudele, ujue jana wakati naenda kwa mzee J ili nimuadabishe ghafla nikakumbana na makombora mkali mno. Yalinishambulia mfululizo, nikajitahidi kuyadhibiti ila yakanishinda nguvu nikadondoka chini. Maumivu haya ni yakishindo cha mueleka nilioanguka mke wangu" Alisema mzee Nhomo kisha akanyamanza kidogo. Baada ya kimya hicho akaendelea kusema "Sikuona haja ya kurudi nyumbani moja kwa moja, kwahiyo nikapita shambani niakalala huko kibandani sababu muda ule sikuwa na nguvu ya kichawi tena eti kwamba nirudi kwa mazingala. Lakini yote kwa yote nitajua cha kufanya"
Mama Chaudele aliposikia maneno hayo ya mumewe alishusha pumzi ndefu kisha akasema "Pole sana mume wangu, lakini inaonyesha mzee J yupo vizuri sana kwahiyo unatakiwa ujipange kikamilivu la sivyo atakuumbua jua la mchana"
"Ahahaha hahaha" Mzee Nhomo aliangua kicheko, alipokatisha cheko lake akasema "Hilo ni jambo lisilo wezekana mke wangu, na ndio maana nimekwambia najua cha kufanya"
"Sawa mume wangu mimi nakutakia ushindi mwema" Akikata kauli mama Chaudele kisha akanyanyuka akatoka ndani akaelekea nje kuchochea moto ili ampashie maji ajikande maumivu.
Kwingeneko nyumbani kwa mzee Mligo, Saidon aliamka huku akilalama kuchoka mwili mzima. Babu yake aliposikia malalamishi hayo alicheka kimoyo moyo kwani alijua chanzo cha Saidon kuchoka. Baada ya kuhitimisha kicheko chake akasema "Usijali mjukuu wangu, unajua umezoea kulalia godoro kwahiyo ukilalua kilago lazima ujihisi kuchoka. Ila utazoea tu na hii hali"
"Kweli babu?.." Saidon aliuliza.
Mzee Mligo akakaa kimya kidogo kisha akajibu "Ndio lazima uzoee kwa sababu siku zote hali ya mwili hubadirika kulingana na mazingira"
"Hahahaha hahaha!.." Alicheka Saidon pindi aliposikia maneno hayo ya babu yake. Na mara baada ya kicheko hicho akaongeza kusema "Ni kweli kabisa babu, daah unaonekana ulikuwa vizuri sana darasani"
"Haswaa hujakosea, istoshe sisi enzi hizo hayakuwepo mambo ya uashirati. Sio Kipindi chenu nyinyi utakuta mwanafunzi anamchumba, kichwa kina jaza mambo mawili tofauti mapenzi na elimu"
"Mmmh" Aliguna Saidon. Hapo babu yake akamgeukia halafu akamwambia "Ndio kwani uongo? Hahahah! Tuachane na hayo mjukuu wangu, leo sijachemsha mihogo ila kuna nyama zimebaki jana usiku kwahiyo songa ugali kula. Mimi muda huu naelekea kijiji cha pili kuna mambo leo tunaenda kuyaweka Sawa, sababu kesho kutwa hapa kijijini kutakuwa na mechi. Hivyo Mimi kama katibu wa michezo lazima niweke mipango sawa " Alisema mzee Mligo.
" Sawa babu kila laheri "Alijibu Saidon.
Baada mzee Mligo kuondoka zake, punde si punde akaonekana kijana Maige akaiendesha baiskeli kwa kasi kuja nyumbani kwa mzee Mligo. Maige alikuja kwa niaba ya kumsabahi rafiki yake ambaye ni Saidon. Hivyo alipofika nyumba hapo alipiga msele kwa style ya kuizungusha baiskeli yake kisha akasimama akapiga kengere. Saidon aliposikia sauti ya kengere alitoka ndani, akamkuta ni swahiba wake ndiye aliyepiga kengere. Akatabasamu halafu akasema "Ndio rafiki yangu, karibu sana. Halafu mimi nifikiri wewe umezaliwa wakati wa shibe, maana umekuta tayari nimeinjika maji ya ugali jikoni" Alitania Saidoni.
" Ahahahahaha" Alicheka Maige baada kusikia masihara hayo ya Saidon. Na mara baada ya kukatisha kicheko hicho alipaki baiskeli yake kisha akazipiga hatua kuingia ndani. Alipofika ndani alichukuwa kigido akaketi, hapo alishusha pumzi kwanza halafu akasema "Unajua Saidon mabinti wa kijiji hiki walishaanza kukuzungumzia"
"Mmmh kweli?.." Alitaharuki Saidon.
"Ndio nikudanganye ili iweje sasa?.." Aliongeza kusema Maige. Hapo Saidon alicheka kidogo halafu akasema "Sawa hakuna tatizo bwana, ila Maige mimi nimemkubali yule binti bwana yuleee"
"Nani Chaudele?.."
"Mmh sijui ndio huyo? Yule niliyemuona kwa yule mzee tuliyenunua nyama kwake"
"Nndio huyo anaitwa Chaudele ama ukipenda muite mrembo wa kijiji. Kwa sababu kijiji kizima hakuna kama Chaudele. Lakini ndugu yangu, rafiki yangu bwana Saidon. Mrembo yule Chaudele anafuatiliwa na mwamba mmoja hivi anaitwa Chitemo. Huyu jamaa kashatangaza vita kwa kijana yoyote atakaye mtongoza, ujue kwanini?.. "
"Hapana sijui " Alijibu Saidon huku akionyesha utulivu wa hali ya juu wa kuyasikiliiza maneno ya Maige. Maige akaongeza kusema "Kwa sababu karibia ndugu zake woote ni wachawi, kwahiyo ukijifanya mbishi tunakukosa" Hapo kijana Saidon akashusha pumzi kwa nguvu, akatulia kidogo akiyatafakari maneno hayo aliyomwambia Maige. Baadae kidogo alivunja ukimya huo akasema "Poa tu, siku zote uchawi haufanyi kazi kwa mentali. Unajua Maige mimi sio mzawa wa kijiji hiki ila nataka niletee mapinduzi kwa huyo mnayemuita mwamba. Apende asipende atake asitake Chaudele lazima awe mpenzi wangu"
"Binti mrembo kama yule hawezi kumilikiwa na shamba Boy ikiwa sisi wajanja tunamuangalia tu, siogopi uchawi wao bro, maadam wameanza kunizungumzia basi ujue nyota imeweka" Aliongeza kusema Saidoni huku akijiamini kabisa, kitendo hicho kilimshangaza sana Maige ambapo ndani ya nafsi yake alijiuliza ni nini anacho jiamini kijana huyo. Lakini kabla hajapata jawabu la swali lake, ghafla nje wakasikia kicheko "Ahahahah hahahaha hahahaha" Cheko hilo lilimstua Saidoni, punde akamtazama Maige kwa jicho ngebe wakati huo huo Maige naye akionekana kupigwa na bumbuwazi..
JE, NI NANI HUYO ALIYEANGUA KICHEKO? USIKOSE SEHEMU IJAYO ILI KUJUA KILICHO ENDELEA.
SHEA MARA NYINGI ILI USIPITWE NA KIGONGO HIKI CHA KUSISIMUA.. VITA VITANI mzee baba Saidoni kuwa makini hapo ni Ndaulaike sio Tandale kwa tumbo 😂 ona sasa balaa.
No comments:
Post a Comment