MREMBO WA WA KIJIJI
SEHEMU YA YA KUMI-10
Kipindi mzee J yupo angani na jopo lake la wachawi, upande wa pili timu ya bibi Pili nayo ilikuwa imeshatua nyumbani kwa huyo. Hapo ndelemo na vificho vilifuatia, zoezi hilo lilichukuawa muda mfupi na ndipo wakafanya kile kilicho waleta hapo kwenye imaya ya mzee J.
"Nafikiri hakuna cha kupoteza muda, Zauro na Tedi vijana wa kazi ingieni ndani mkamchukue Chitemo mumleta hapa" Alisema mkuu huyo, akiwataka vijana wake waingie ndani ya nyumba ya mzee J. Vijana hao bila kupoteza muda, wakizipiga hatua kuzisogelea kona za nyumba. Hatua hizo wakizipiga kwa style ya kurudi nyuma huku wakitazama mbele. Walipozikarubia kona hizo wakanuia baadhi ya maneno na punde wakajikuta wamo chumbani kwa Chitemo.
Huku nje, upepo mkali ulisikika ukivuma, upepo huo ukamshtua kiongizi wa wachwani yeye na kundi lake ambalo yumo bibi Pili.
"Mkuuu nini hiyo?.." Aliuliza mchawi mmoja. Mkuu wake hakunijibu, zaidi alitikisa kichwa kama ishara ya kukubali jambo fulani. Baada ya hapo alichukuwa pembe la Ng'ombe ambalo aliendelea kutembea nalo, pembe hilo alilikamata vizuri akalitwaa mdomoni mwake halafu akaanza kulipuliza mfano wa vuvuzela ama mbiyu kuelekea juu. Ndani ya pembe hilo yalitoka makombora saba ya kichawi, makombora hayo yaliruka kuelekea kule ulikokuwa ukisikika upepo wa ajabu.
"Ahahahahah anhaaa" Aliangua kicheko mkuu huyo aliyerusha makombora iliahali upande mwingine mzee Nhomo alijikuta akipata wakati mgumu wa kuyatoka makombora hayo ambayo yalirusha mfululizo. Lakini licha ya kujitahidi kadiri alivyojaribu ila moja lilimpata, kombora hilo lilikuwa la MOTO sana kiasi kwamba lilipompiga mzee Nhomo aliangua chini na safari yake ikawa imeishia hapo kwani alikuwa akisafa huku akijitahidi kuamka lakini mwishowe jitihada zake zikiishia kwenda kombo, kibaya zaidi ungo wake uliteketezwa na moto ule.
Mzee Nhomo alilaani sana jambo hilo, kimoyo moyo akajisemea "Mshenzi huyu, nilitaka leo nikamuonyeshe utofauti wa mimba na ujauzito. Ila kwa kuwa kaniwahi acha nikajipange upya, wallah sikubali"
Na wakati Nhomo anajisemea hayo, upande wa pili bado upepo ulivuma. Mkuu yule wa kundi lakina bibi Pili akarusha makombora kwa mara nyingine tena. Safari hiyo aliongeza badala ya kuwa saba alirusha kumi na mbili. Hapo sasa mzee J na kundi lake wakajikuta wakidondoka chini mithili ya kinyeshi cha kunguru, jambo ambalo lilimshangaza sana J na kumtia mashaka.
"Nani huyu anayetumia uchawi huu?" Kwa taharuki kubwa alijiuliza mzee J huku akiteteleka angani. Balaa lilikuwa nzito ikiwa nyumbani kwake tayari Zauro na Tedi walimtoa nje Chitemo. Vicheko vilisikika kisha mkuu wao akatoa mnyororo wa baiskeli kwenye moja ya mazagazaga aliyokuwa nayo. Mnyororo huo akauweka chini, akawambia watu wake wasogee mbali kidogo sababu kuna kitu anataka kukifanya. Wananzengo hao walitii matakwa ya mkuu wao, kufumba na kufumba mnyororo ule ukageuka treni. Kwa mara nyingine shangwe zilizuka, kila mmoja akimshangaa mkuu wao kwani hata mara moja haijawahi kutokea kitendo kile.
"Khee ni maajabu" Alisema mchawi mmoja, muda huo huo walipanda na Chitemo ndani ya treni hiyo kisha wakaondoka naye. Muda mfupi baadaye mzee J naye alitua nyumbani kwake akiwa hoi bin'taabani baada kuchoshwa na shughuli ya kupangua mabomu ya kichawi.
"Mmmmh mbona nasikia kama mlio wa treni, na wakati hapa kijijini kwetu hakuna reli?" Alijiuliza mzee J baada kusikia mlio wa treni ile ya kichawi waliyopanda bibi Pili pamoja na wenzake. Sintofahamu ikamjaa kuhusu trein ile. Mbali na mzee J kupigwa na butwaa, vile vile mzee Nhomo alipokuwa anatembea kurudi nyumbani kwake baada zoezi lake kuota mbawa, ghafla naye alisikia mlio wa treni. Alishtuka ilibidi asimame ili asikilize vizuri kwani alihisi kuwa huwenda masikio yake yanamdanganya. Alipoona chuma inatembea pasipo kuwa na leri hatimaye aliamini kuwa ni treni na kibaya zaidi treni hiyo ilikuwa ikija mahali alipo yeye, hivyo baada kuona ikimkaribia alichutama pembeni kwenye moja ya kichaka. Kwa macho yake akawa ameshuhudia treni ikipita kasi huku ndani zikisikika shangwe na nyimbo mbali mbali.
Nhomo alichoka "Loh ama kweli unaweza kujiona bora kumbe kuna bora zaidi yako. Sasa hawa nao hata sijui hii treni wameipataje.." Alisema mzee Nhomo kisha akainuka kutoka kichakani akaendelea na safari, safari hiyo alikwenda moja kwa moja mpaka shambani kwake. Huko kulikuwa na kibanda kidogo cha miti na tope ilihali jukuu kikiezekwa na nyasi. Alilala huko huko ikiwa kwingineko mzee Mligo alifanya makeke nyumba yake ikarejea kama kawaida. Hapo aliangua kicheko kisha akasema "Wajinga nyinyi mkajua mimi mchuzi wa pweza? Na mkome" Maneno hayo mzee Mligo aliyasema akiwa amesimama nje.
"kulikoni jirani mbona alfajiri yote hii unabwatuka?.." Aliuliza mzee mmoja ambaye ni jirani yake mzee Mligo. Mzee huyo alimsikia Mligo akibwatuka wakati huo yeye akiwa ametoka chooni kujisaidia, hivyo ikabidi amuulize kisa na mkasa kinacho mpelekea Mligo kulalama.
" Aah unajua bwana jirani kijiji hiki ukikitazama unaweza kudhania kuwa ni kizuri hakina matatizo yoyote ila sasa mambo haliyomo humu. Mmmh Mungu tu ndio anajua" Alijibu mzee Mligo.
"Loh! Kijiji hiki kimechafukwa mzee mwenzangu, yani badala ya kuwaza maendeleo watu wanawaza kulogana tu"
"Mmmh ni kweli kabisa, basi baadae asubuhi tutazungumza vizuri jirani yangu. Acha nikamalizie lepe langu la usingizi"
"Sawa"
*************
Upande mwingine treni ile ya kichawi ilifika mahala ikasimama kisha akashuka mkuu ambapo alifanya makeke yake na punde si punde ikatoweka. Wachawi wote waliokuwemo mle ndani walidondoka chini.
"Bibi Pili, nimeamuwa kufanya jambo hili kwa ajili yako. Hata mara moja sijawahi kufanya muujiza wa namna hii, hivyo basi yote ni kwa sababu upo makini na kile tunacho kutuma. Na sio wewe hata nyinyi wengine endapo mtafanya kile ninachokipenda Mimi kwa muda muafaka, hakika nawaambieni naweza kuitembeza meli nchi kavu kama nilivyofanya kuitembeza treni pasipo na reli" Alisema mkuu huyo wa kundi la kina bibi Pili. Baada ya hapo kila mmoja alipotea wakamuachia majukumu bibi Pili amfanye Chitemo kile anachoona kina mfaa.
Bibi huyo alimchukuwa Chitemo akamtundika juu kwenye mti kisha akaondoka zake, asubuhi mzee J anaingia chumbani kwa Chitemo ili amtume dawa ajitibu mahali alipokuwa ameumia alishtuka baada kutomkuta.
"Kadamkia wapi huyu mtoto?" Alijiuliza mzee kwa hasira, wakati huo kule alipotundikwa Chitemo alipotaka kujigeuza upande wa pili lakini alianguka chini, ilidhani yupo kitandani, kwa woga na hofu alipiga mayowe ya kuomba msaada punde si punde bibi Pili akatokea, kwa hasira akasema "Huu ni mwanzo tu, usipo muoa mjukuu wangu nitakulisha mpa kinyesi chako" Alishtuka Chitemo. Lakini muda huo huo sauti nyingine ikasikika ikisema "wewe ni mwanamke, umeumbwa kukojoa ukiwa umechuchumaa. Kwa kipi hasa ulicho nacho mpaka umtishe Chitemo" Alisema mtu huyo.
JE, NI NANI HUYO anayeongea kwa JEURI?
Naam mambo si mambo kijiji cha NDAULAIKE..
SHEA MARA NYINGI ILI USIPITWE NA KIGONGO HIKI CHA KUSISIMUA.. TRENI LEO IMETEMBEA PASIPO NA RELI 😂😂
No comments:
Post a Comment