SMULIZI: HOUSEGIRL WA KITANGA
MTUNZI : KIZARO MWAKOBA
SEHEMU YA KUMI (10)
ILIPOISHIA
Kama ambavyo nilikuwa nawaza ndivyo ilivyokuwa. Dada Bupe alipotoka jikoni alikuwa mkononi ameshika ndoo iliyokuwa na mchele.
“Haya mama kazi kwako” alizungumza dada Bupe huku akiweka chini ndoo ya mchele aliyokuwa amebeba.
“Haaa! Mi nitakuwa siji kwako dada Bupe, ukiniona tu lazima unipe kazi” nilizungumza huku nikiutazama ule mchele ndani ya ndoo.
“Hebu wacha uvivu wako mtoto wa kike, kesho tu unaolewa usije ukatutia aibu kwa mumeo” Dada Bupe alizungumza huku akiinama jikoni kugeuza maandazi yaliyokuwa yanachemka kwenye mafuta.
“Haa mie mwenzio siolewi leo wala kesho” nikasema kwa matani huku nikichukua ungo uliokuwepo umening’inizwa ukutani.
“Usiolewe una kasoro gani?”
“Mie mwenzio bado mtoto” nikasema huku nikichota mchele kidogo kutoka kwenye ndoo na kuuweka kwenye ungo.
“Kefuleee Mtoto nani!......Wewe au unazungumzia nani?” dada Bupe alizungumza pasipo kunitazama usoni huku akitoa maandazi kutoka kwenye karai na kuyamimina kwenye sufuria.
“Mimi ndio mtoto, hata maji naita mma” nikasema huku nikitabasamu na macho yangu yapo kwenye ungo kutafuta mawe na chuya.
“Una utoto gani wewe wakati unatakwa na hata mianaume mizee” dada Bupe alizungumza kauli yake hiyo na kunifanya nishtuke kidogo. Nilihisi mzee aliyekuwa anazungumziwa na dada yule hakuwa mwengine bali ni baba mzee Sekiza. Kumbe nilivyoshituka dada Bupe aliniona.
“Unashituka nini sasa? Au nimekugusa?” alihoji dada Bupe huku akiweka maandazi mabichi kwenye karai.
“Akaa hakuna chochote”
“Kwanza usijifanye mtoto hapo, kuna mkaka amekuja anasema anakupenda” alizungumza dada Bupe.
“Mkaka gani?”
“Anakaa hapo Hosteli”
“Mnh Mwanafunzi?”
“Vipi kwani we unataka walimu?”
“Mie sitaki yeyote yule” nilizungumza huku mkono wangu wa kulia ukichangua changua mchele kwenye ungo uliokuwa mapajani mwangu.
“Wacha ushamba wako wewe, wanafunzi wa chuo wanapesa kama nini”
“Mnh!....” niliguna huku nikihisi kushawishika na maneno ya dada Bupe.
“Unaguna nini?”
“Huyo kaka ni mzuri?”nilihoji.
“Aa we, kaka wawatu ni Handsome la nguvu”
“Lakini naogopa”
“Unogopa nini na wewe wacha mambo ya kijijini!”
ENDELEA
“Sio hivyo dada Bupe, je nikipata ujauzito?”
“We yule msomi hawezi kukupa ujauzito, anaelewa afanye nini ili kuzuia mimba zisizo tarajiwa” dada Bupe alizunguza kwa kumsifia kaka huyo.
“Anaitwa nani?”
“Endru”
“Nani?”
“Endrus”
“Jina gumu” nilizungumza huku nikivuta taswira ya mwanaume huyo ndani ya ubongo wangu. Dada Bupe alinitazama akatoa tabasamu, namimi nikampokea kwa kumpatia lakwangu zito huku nimelegeza macho.
“Atakuja saa ngapi nataka nimuone kama tunaendana” Nilizungumza
“Anaweza kuja kunywa chai kama leo hana kipindi cha asubuhi” dada Bupe alieleza.
“Ngoja nimsubiri kwa hamu” nilizungumza huku nikimimina mchele kwenye ndoo nyingine iliyokuwa tupu pembeni kando yangu. Nilichota mchele mwingine kutoka kwenye ndoo kubwa na kuuweka kwenye ungo. Nikaanza kuusambaza kwa vidole vya mikono yangu kutafuta mawe na chuya.
Dada Bupe alijikohoza kidogo kuashiria kuwa alikuwa anataka kuzungumza kitu, niliinua shingo na kumtazama.
“Haya niambie jana ulivyoenda na zile nguo zako ulibabuka sehemu?” Dada Bupe aliuliza swali ambalo lilinishitua sana moyo wangu. Mwenyewe kwa kiasi fulani nilikuwa nimeshasahau mambo yaliyopita. Nikatulia kwa sekunde kadhaa nikawa kama vile nimepigwa na shoti ya umeme.
“Vipi mbona hivyo?” alihoji dada Bupe.
“Mnh! Umeniletea balaa dada wewe!”
“Umefokewa?”
“Si afadhali ningefokewa tu nikaachwa”
“Kumbe balaa gani sasa?”
“Mwenzangu kaka Imrani aliponiona nimevaa vile si akaanza kunitaka” nilizungumza kwa sauti ya chini kama vile kulikuwa na watu wengi nikawa naogopa wasitusikie, kumbe tulikuwa wenyewe wawili tu jikoni.
“Enhe usiniambie!” alihoji kwa shauku.
“Yaani dada wewe nimepata wakati mgumu mimi”
“Wakati mgumu! Kivipi sasa?”
“Unajua namheshimu sana kaka Imrani, sikutegemea kama angekuwa na mawazo kama yale” nikazungumza kwa msisitizo.
“Kwani anayeheshimiwa ndio hana moyo wa kupenda?”
“Mnh lakini sasa yule si ni kaka yangu?”
“Kaka yako umezaliwa naye?”
“Hata kama lakini mi namheshimu bwana”
“Unajua una bahati sana mdogo wangu!” alizungumza dada Bupe huku akiepua karai la maandazi na kuliweka chini. Alikuwa amekwisha maliza kukaanga maandazi.
“Bahati?” nikahoji kwa mshangao.
“Bahati ndio, we unadhani hapo ndani wamepita wadada wa kazi wangapi, lakini sikuwahi kusikia Imrani akimtongoza hata mmoja kati yao” dada Bupe alieleza.
“Kwahiyo dada unanishaurije juu ya hilo?” nilihoji huku nikimtazama kwa makini ili kuweza kupata ushauri kutoka kwa mtu ambaye alikuwa amenizidi sana umri.
“Sikiliza mdogo wangu, hiyo ni bahati ya kuokota embe dodo chini ya mnazi. Kama anakutaka we mkubalie tu, we mwenyewe si umeona mavazi aliyokuletea. Unafikiri ukimkubalia atakuletea vitu vingapi?” dada Bupe alizungumza kwa msisitizo.
“Je mama akigundua?”
“Hawezi kugundua bwana, kwani we mtoto mdogo!” alisema dada Bupe huku akifuta futa kopo la kuwekea sukari kwa kitambaa.
Nilivuta pumzi na kuzijaza kifuani kisha kwa mkupuo nikazimimina nje kupitia mdomoni. Nilitegemea dada Bupe angenipa ushauri wa namna ya kumuepuka kaka Imran, badala yake akazidi kunitumbukiza kwenye dimbwi la mahaba ya kaka yule niliyekuwa namheshimu kupita maelezo.
Nikatamani nimueleze shughuli na matukio yaliyonitokea siku iliyopita lakini moyo ulisita. Unajua ndugu msomaji sio kitu cha kawaida kwa watu wa tatu tena wa familia moja kutaka kukutia majaribuni ndani ya siku moja tena kwa masaa machache tu. Kwakweli katika maisha yangu sitokuja kuisahau siku ile.
“Vipi mbona kimya sana?” dada Bupe alihoji huku akipita na kuelekea mgahawani kuwasikiliza wateja. Nilitabasamu tu kisha nikaendelea kuchambua mchele huku shingo yangu nikiwa nimeipindisha upande kidogo.
“Enhe niambie dogo langu la kitanga” dada Bupe alizungumza huku akirejkea jikoni na kuchukua chenchi kwenye kopo alilokuwa anahifadhia pesa. Mimi pale nilipokuwa nimekaa niliendelea kutabasamu pasipo kutoa neno lolote.
Dada Bupe alitoka tena kwenda mgahawani, baada ya dakika chache alirejea na kikombe cha chai mkononi.
“He! Mteja wako anafriza mdomoni nini?”
“Kwanini?”
“Mara hii keshamaliza kunywa chai!”
“Hamna bwana huyu ni mteja mwengine, yule amekwisha ondoka” dada Bupe alizungumza huku akicheka.
“Anhaa nilifikiri ndo amebugia mara hii”
Dada Bupe aliweka kwenye beseni vyombo vile na kuanza kuviosha. Namimi pale kwenye kigoda nilikuwa anaendelea na shughuli yangu taratibu.
“Mdogo wangu kama Imran anakutaka wala usimkatalie” dada Bupe alizungumza huku akisugua vyombo kwa brashi na sabuni ya unga.
“Unajua nini dada Bupe?” niliamua kutoa dukududku langu kwa dada yule aliyekuwa ananipa ushauri wa kutembea na kaka Imran.
“Enhe niambie”
“Kusema kweli moyo wangu haupo kabisa kwa kaka Imran”
“Najua moyo wako unao wewe mwenyewe, lakini penzi lako mpe Imran”
“Simaanishi hivyo dada Bupe bwana”
“Kumbe?”
“Yaani, kaka Imran siye ninayempenda mimi” nilizungumza kwa umakini huku nikitabasamu.
“Ah! We achana na watu wa vijijini hao, umekuja mjii toka kimjini mjini”
“Wala kijijini kwetu sina mwanaume yoyote”
“Mnh! Kwahiyo mara hii hapa mjini umekwisha pata Bebe? Makubwa basi. Unafungiwa ndani tu hali hiyo, je ungekuwa huru si ndo ingekuwa balaa” Dada Bupe alizungumza kwa mshangao.
“Sio hivyo bwana dada Bupe” nilizungumza huku nikicheka.
“Kumbe vipi?”
“Yani mie moyo wangu ukiuchana hapa pyaaa! Utamkuta Fadhili amejaa” nilizungumza kwa hisia huku nikifumba macho kuonesha hisia zangu.
“Mnh basi makubwa”
“Yaani hilo ndio tatizo”
“kwahiyo wewe na Fadhili ni wapenzi?”
“Mnh….am…eeeh….hapana” nilizungumza kwa kigugumizi. Nilishindwa kuzungumza kama alikuwa ni mpenzi wangu kwasababu hakuwahi kunitongoza, lakini pia nilitaka kusema kuwa ni mpenzi wangu kwasababu ya shughuli ya jana pamoja na vituko vyake. Lakini kama jibu lingekuwa ni ndio basi hata kaka Imran pamoja na baba nao pia ningetakiwa kusema ni wapenzi wangu. Ndio kwasababu nao pia si walitaka kunifanyia kama Fadhili.
“Sasa mbona kigugumizi, kama ni mpenzi wako we nambie kwani mie si ni dada yako?” alihoji dada Bupe.
“Kweli nampenda sana Fadhili” nikasema.
“Wacha kujizunguusha jibu swali langu”
“Hajakuwa mpenzi wangu kabisakabisa lakini ananipenda pia” nilijikakamua na kuzungumza.
“Mapenzi yenu we na Fadhili yameanza lini?” dada Bupe alihoji swali ambalo lilikuwa gumu kidogo kulijibu ingawa jibu lake lilikuwa linafahamika. Nikatulia kidogo na kujifanya nakohoa.
“Haya kohoa useme” mnh dada alizidi kunisisitizia.
“Jana….” nikajikuta nikilitoa jibu hilo pasipo kutarajia mwenyewe.
“He! Kwahiyo jana hiyo Imrani amekutongoza, na jana hiyohiyo Fadhili amekutongoza” Dada Bupe alionekana kuzungumza kwa mshangao. Ndani ya moyo wangu nikajisemea, laiti ungetambua kuwa jana hiyohiyo unayoishangaa wewe na baba naye alikuwemo kwenye mkumbo huwo wa kunitaka kimapenzi, sijui ungeshangaaje. Nikatikisa kichwa kukubali swali lake lile.
“Na yote hayo ni kwasababu ya zile nguo ulizokuwa umezivaa, au uwongo?” alisema dada Bupe.
“Sivai tena!” nikazungumza huku nikiwa nimekauka uso na kuonesha kuchukia kitendo cha jana cha kuvaa vinguo vya nusu uchi. Ndio mimi nilikuwa naviita nusu uchi kwasababu havikuwa vya type yangu. Ebu fikiria ndugu msomaji, wewe mwenyewe unafahamu watoto wengi wa kitanga wanavyovaa mavazi yao. Sasa binti huyo umchukue na kumvisha vimini na viblauzi vya kifua wazi unafikiri atajisikiaje? Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa kwangu.
“Sio nusu uchi mdogo wangu” dada Bupe alieleza.
“Kumbe ni kilomoja?”
“Yaani zile ndio katalogi za mjini. We mwenyewe si umeona ulivyotupia tu ndani wote umewamaliza” alizungumza dada bupe maneno ambayo yalinitia wasiwasi kidogo. Nikahisi alikuwa analitambua sheshe lililonikuta jana jioni.
“Haa dada Bupe punguza chumvi bwana, sio nyumba nzima” nikajifanya kutetea ukweli ambao ulikuwa ni kweli.
“Kwani ndani mle vijana si wawili”
“Ahaa, nilifikiri unamuingiza na baba pia”
“Haaa! Naamini kwa jinsi ulivyokuwa umetokelezea jana, hata Mzee Sekiza naye angekuona asingekubakiza” dada Bupe alizidi kuzungumza maneno machachu ndani ya masikio yangu.
“Mnh dada na wewe! Baba anitake mimi, Sasa ndio nini?” nilijibaraguza.
“Ohoo kumbe hujui wanaume wa mjini wewe!”
“Mnh! Sasa kwamfano ndio imetokea mzee Sekiza ananitaka, Nitafanya nini?” nilizungumza baada ya kupata mwanya wa kuuliza swali ambalo nilikuwa sielewi namna ya kuanza kuliuliza.
“Mnh, hapo mdogo wangu ikitokea inabidi uwe makini sana. Tena omba sana isije ikatokea” dada Bupe alizungumza kwa msisitizo.
“Kwanini?”
“Mnh! Hapo sina la kuzungumza lakini unaweza ukajikuta unapoteza kibarua chako” alizungumza dada Bupe kwa umakini mkubwa.
Nilikaa vizuri na kumsikiliza kwa umakini baada ya kuhisi alichokuwa ananipatia kilikuwa ni kitu kizuri na chenye mafanikio kwangu mimi mwenyewe.
“Sasa nitapotezaje kibarua?” nikahoji.
“Kwamfano ukimkataa, anaweza kukuchonganishia hadi ufukuzwe kazi. Na ukimkubali, siku ukibainika na mke wake ujue litakuwa songombingo” alieleza dada Bupe na maneno yake yakaniingi vyema kwenye ubongo wangu.
“Duu! Kweli hilo balaa!” nikazungumza kwa suti ya kukata tamaa.
“Ndio hivyo mdogo wangu, ila ukifanikiwa kutoka na baba mwenye nyumba pasipo mtu mwingine kufahamu unaweza ukajikuta umeula” sasa dada Bupe akaanza kuzungumza maneno ambayo hayakuwa na busara tena. Mimi ndio niliyaona hivyo simaanishi kuwa hata wewe unayaona maneno yale kama niyaonavyo mimi.
“Lakini hata hivyo haipendezi kabisa kufanya kitu kama hicho cha hatari hivyo” nilizungumza kwa umakini.
“Ni hatari lakini kuna maslahi” dada Bupe alizungumza kwa kujiamini.
“Aisee mimi siwezi”
“Wewe huwezi si kwasababu ushachukua watoto wake!” dada Bupe alizungumza huku akicheka.
“Hapana, mimi nampenda Fadhili tu, hao wengine wananilazimisha tu” nilizungumza kwa sauti ya kudeka.
“Kina nani wanakulazimisha”
“Si huyo Fadhili”
“Mnh huna lolote”
“Kwanini unasema hivyo dada Bupe?”nikahoji kwa wasiwasi baada ya kumuona dada Bupe kama vile alikuwa na mashaka na mimi.
“Unajua mimi ni mtu mzima?”
“Sijui unakusudia nini dada Bupe?”
“Kuna kitu kinaendelea hapo ndani kwenu” dada Bupe alizungumza huku akitembea kuelekea mgahawani. Nikabaki na kigugumizi ndani ya nafsi yangu nikiwa sielewi alichokuwa anakimaanisha dada yule.
“Tumuuu” dada Bupe aliniita akiwa mgahawani.
“Abee” nikaitika huku nikimchungulia kwenye tundu ya mlango.
“Njoo maramoja”
Nilijiinua kutoka pale nilipokuwa nimeketi na kuelekea kule kwa dada Bupe. Tulipokutanisha macho yetu dada alinikonyeza kwa ncha ya jicho lake la kushoto. Nikahisi mapigo ya moyo wangu yakibadili muelekeo na kudunda kwa spidi kidogo. Nilihisi kulikuwa na kitu kilichokuwa kinaendelea kati yake, mimi na yule mteja.
“Abee” niliitika mara tu nilipomkaribia.
“Umemuona Endrus?” dada Bupe alihoji huku akinipisha nimuone mteja aliyekuwa ameketi akimhudumia. Maneno yale yanizidi kuushitua moyo wangu. Ghafla nikahisi aibu ikinivaa kwenye sura yangu. Nilipeleka mkono wa kulia mdomoni na kuuma kidole kidogo na kutoa tabasamu kwa aibu.
“Mambo mrembo?” mnh kijana yule alinisalimia.
“Poa” nikajibu huku nikijipindapinda kama jongoo.
“Haya kazi kwako we si ulisema unataka kumuona Endrus? Ndio huyo sasa!” dada Bupe alizungumza huku akiondoka na kutuacha mimi na Endrus mgahawani pale.
Itaedelea
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments:
Post a Comment