SMULIZI: HOUSEGIRL WA KITANGA
MTUNZI : KIZARO MWAKOBA
SEHEMU YA TISA (9)
ILIPOISHIA
Nilishukuru sana uwepo wa Baba na Fadhili katika sakata lile, sijui ingekuwaje kama siku hiyo ningekuwa pekeyangu nyumbani pale. Nilipokuwa naingiza mizigo ile ndani nikamtazama Fadhili kwa jicho la kuibia. Kumbe Fadhili naye alikuwa akinikodolea macho muda wote huo, hivyo nilipomtazama tu, macho yetu yakakutana. Fadhili alibonyeza jicho moja kunikonyeza na kuachia tabasamu kwa mbali ambalo lisingeweza kuonekana na mtu mwingine yoyote zaidi ya mimi. Namimi baada ya kuona mwanaume niliyekuwa nampenda akinikonyeza kimahaba nami nikamjibu kwa kuuma midomo yangu ya chini na kuunganisha na tabasamu huku macho nikiyazunguusha utafikiri nilikuwa nataka kukata roho.
Nilipokuwa nikiingia ndani na mizigo huku nikiwa nimejawa na furaha ya kuuteka moyo wa Fadhili nikakutana tena na Bi. Fatma amesimama kwenye korido akinisubiri. Kwa jinsi alivyokuwa amesimama kwa hasira nikapatwa na hofu tena.
“Hivi wewe unanitafuta nini?” mama lihoji kwa hasira.
ENDELEA
“Kuna ninitena mama?”
“Hivi unajua kilichokuleta hapa ndani?” alizungumza mama kwa hasira.
Mnh! Ukiwa na mkosi una mkosi tu, sasa nimemkosea nini tena Bi. Fatma jamani, au kazini kwake walikuwa wamemvuruga? Ah! Kusemakweli hata sikumuelewa. Maana yale ya nje tulikuwa tumeyamaliza.
“Si nakuuliza wewe, usinitumbulie macho kama mwizi” alifoka mama na kunifanya nishituke kidogo.
“Tangu asubuhi umefanya kazi gani?” mama aliendelea kuhoji na kunifanya nibaini kosa langu.
Ni kweli kabisa siku hiyo sikuwa nimefanya kazi yoyote ile zaidi ya kulala na kufanya mambo mengineyo ambayo sikupaswa kulaumiwa mimi. Hapa naomba nieleweke vizuri ndugu msomaji. Mtu wa kwanza kulaumiwa angekuwa ni kaka Imrani, kama asingeingia chumbani kwangu usiku, wala nisingechelewa kuamka na kusababisha watu wasinywe chai asubuhi, Lakini Baba naye pia alikuwa wa kulaumiwa bila ya kumsahau mwanaume kipenzi cha roho yangu Fadhili. Ndio wote hao walikuwa wamechangia kuharibika kwa siku yangu hiyo.
“Hivi ulimpikia Baba yako chai asubuhi?” Mama alihoji swali ambalo lilikuwa gumu sana kulijibu kwasababu sikuwa nimepika chai kama alivyokuwa amenisisitiza asubuhi wakatia anaondoka.
“Nakuuliza wewe kunguru, usiniangalie kama video”! Jamani nyie mwanamke yule aliendelea kuwaka kama kifuu. Sikuwahi kumuona Bi Fatma akiwa amekasirika kiasi kile hata siku moja tangu nilipokuwa nimeingia ndani mle. Nakwambia mwanamke yule alikuwa akitetemeka kwa hasira. Inawezekana kile kitendo cha Baba na Fadhili kule nje kunitetea ndicho kilichompandisha hasira zaidi.
Wakati nimezubaa nikiendelea kutafakari namna ya kujitetea, nikashitukia nimekamatwa na na Bi Fatma na kutikiswa kama vile dawa ya kifua ya maji. Mwanamke yule alikuwa amekusudia kunishikisha adabu siku hiyo. Alinyanyua mkono wake wa kuume juukwa lengo la kunitandika kofi maridhawa kwenye shavu langu la kushoto. Sasa nikahisi kifo kiliwa halali yangu siku hiyo, ikabidi niinamishe kichwa kusubiria maumivu makali.
“Mama unafanya nini?” nikasikia mtu akizungumza kwa sauti ya ukali.
Nilipoinua macho yangu, nikamkuta kaka Imran ameukamata mkono wa mama kuuzuia kutua kwenye shavu langu.
Sikuweza kuamini kwa kile kilichokuwa kimetokea. Hata sijui kaka Imran alikuwa ametokea wapikwasababu muda wote huo alikuwa hajarudi kutoka kazini. Nikamshukuru muumba kwa muujiza aliokuwa amenitendea kwa wakati mwingine.
“Imran niache nimfunze kidogo huyu mshenzi” alizungumza mama kwa hasira huku akiuvuta mkono wake kutoka kwa kaka Imran.
“Kwani ni kitu gani kinaendelea mamaangu?” Imranalihoji huku akiwa bado ameukamata mkono wa mama.
“Tena afadhali umerudi mwanangu, maana humu ndani naonekana wa hovyo kwaajili ya hiki kikunguni” Mama alizungumza huku akiwa ameachiliwa mkono na kaka Imran.
“Kumetokea nini?” Kaka Imran aliendelea kuhoji kwa umakini.
“Hivi leo umekunywa chai asubuhi?” mama alihoji.
“Sikunywa chai, lakini ni kwasababu nilikuwa na haraka sana” kaka Imrani alizungumza kwa kuongopa huku lengo lake lilikuwa ni kunitetea.
“Sawa lakini tangu asubuhi hakuna kazi yoyote ile ambayo ameifanya humu ndani. Vyombo vichafu, choo kichafu, sebule ndio kama unavyoiona vile hata kupangwa pia ameshindikana” mama alieleza.
“Lakini mama umemuuliza kama alikuwa anaumwa?”
“mgonjwa yuko wapi? Huyu mburumundu ndio mgonjwa? Mama alizungumza kwa mshangao kiasi cha kumfanya kaka Imrani kunigeukiamimi kwa hasira.
“Wewe unafanya utumbo gani?” Kaka Imranalihoji kwa hasira huku akiwa amenikazia macho. Tulipokutanisha macho yetu, kaka Imrani akanikonyeza kuashiria nisizungumze kitu hochote.
“Si umeona kalivyo kajeuri, yani unakauliza kamekaa kimyaaa kiburi kimejaa” alizungumza mama baada ya kuona kaka Imran alikuwa upande wake.
“Wewe si nakuuliza, kwanini unafanya hivi?” Kaka Imrani akajifanya kupandisha hasira.
“Nilikuwa naumwa” nikajaribu kujitetea
“Muongo! Wewe asubuhi si nimekuuliza ukaniambia mzima?” mama alidakia baada ya kuniona najaribu kujinasua kwa mara nyingine.
“Sikiliza wewe, naomba usimpigishe kelele Bimkubwa tena, na ukirudia utapata tabu sana” alizungumza kaka Imrani kwa msisitizo.
“Sawa kaka,siwezi kurudia tena” nikazungumza kwa sauti ya chini huku nimejikunyata kwa woga.
“Haya toka hapa!” kaka Imran aliniondoa kwa staili hiyo.
Kama vile nimeachiliwa kwa msamaha wa Rais kutoka kwenye kifungo cha maisha jinsi nilivyoondoka pale.
Baada ya mimi kuondoka kaka Imran akamgeukia mama yake na kumpoza.
“Basi mama naomba umsamehe, unajua foolish age inamsumbua yule” alizungumza kaka Imrani kwa sauti ya upendo.
“Unafikiri mimi nina shida naye, nilikuwa namkanya tu kama mwanangu” mama alizungumza huku akionekana wazi hakuwa na kinyongo tena juu yangu.
******
Asubuhi iliyofuata nakumbuka niliamka mapema sana na kufanya maandalizi ya watu kwenda kazini. Baada ya hapo niliendelea na shughuli za kufanya usafi. Pamoja na kwamba nilifanya kazi zote hizo mapema sana lakini akili yangu haikuwa ya kawaida kabisa. Nilihisikulikuwa na mzigomkubwa sana katika ubongo wangu uliokuwa unahitaji msaidizi wa kuubeba.
Nilipohakikisha nimemaliza kazi zangu zote ndanimle nikatoka kwenda mgahawani kwa dada Bupe. Kwakuwa haikuwa kawaida yangu kwenda mgahawani pale mida kama ile dada Bupe alinishangaa sana aliponiona. Akanitazama kwa sekunde kadhaa kama vile alikuwa akisikiliza shida ambayo ilikuwa imenipeleka.
“Shikamoo da Bupe” nilisalimia mara tu nilipomkaribia.
“Marahaba hujambo?”
“Sijambo, mbona wanitazama hivyo?” nilihoji.
“Nashangaa leo asubuhi sana” alisema dada Bupe.
“Kwani kuna ubaya wowote?”
“Mnh hakuna ubaya wowote lakini saa hizi! Saa moja na nusu upo hapa!”
“Dada Bupe na wewe mbona mie sioni hata kitu cha kushangaza” nilizungumza huku nikivuta kiti kilichokuwepo karibu na mlango wa jikoni na kuketi.
“Sawa, mgeni njoo mwenyeji apone” alizungumza dada Bupe huku akiingia jikoni.
“Ushaanza hivyo, mwenzako nimekuja kupumzika huku sio kufanya kazi” nikazungumza kwasababu nilikuwa naelewa kuwa mara zote ninapokuwa pale dada Bupe huwa ni lazima anipe kazi ya kufanya. Kama ambavyo nilikuwa nawaza ndivyo ilivyokuwa. Dada Bupe alipotoka jikoni alikuwa mkononi ameshika ndoo iliyokuwa na mchele.
“Haya mama kazi kwako” alizungumza dada Bupe huku akiweka chini ndoo ya mchele aliyokuwa amebeba.
“Haaa! Mi nitakuwa siji kwako dada Bupe, ukiniona tu lazima unipe kazi” nilizungumza huku nikiutazama ule mchele ndani ya ndoo.
“Hebu wacha uvivu wako mtoto wa kike, kesho tu unaolewa usije ukatutia aibu kwa mumeo” Dada Bupe alizungumza huku akiinama jikoni kugeuza maandazi yaliyokuwa yanachemka kwenye mafuta.
“Haa mie mwenzio siolewi leo wala kesho” nikasema kwa matani huku nikichukua ungo uliokuwepo umening’inizwa ukutani.
“Usiolewe una kasoro gani?”
“Mie mwenzio bado mtoto” nikasema huku nikichota mchele kidogo kutoka kwenye ndoo na kuuweka kwenye ungo.
“Kefuleee Mtoto nani!......Wewe au unazungumzia nani?” dada Bupe alizungumza pasipo kunitazama usoni huku akitoa maandazi kutoka kwenye karai na kuyamimina kwenye sufuria.
“Mimi ndio mtoto, hata maji naita mma” nikasema huku nikitabasamu na macho yangu yapo kwenye ungo kutafuta mawe na chuya.
“Una utoto gani wewe wakati unatakwa na hata mianaume mizee” dada Bupe alizungumza kauli yake hiyo na kunifanya nishtuke kidogo. Nilihisi mzee aliyekuwa anazungumziwa na dada yule hakuwa mwengine bali ni baba mzee Sekiza. Kumbe nilivyoshituka dada Bupe aliniona.
“Unashituka nini sasa? Au nimekugusa?” alihoji dada Bupe huku akiweka maandazi mabichi kwenye karai.
“Akaa hakuna chochote”
“Kwanza usijifanye mtoto hapo, kuna mkaka amekuja anasema anakupenda” alizungumza dada Bupe.
“Mkaka gani?”
“Anakaa hapo Hosteli”
“Mnh Mwanafunzi?”
“Vipi kwani we unataka walimu?”
“Mie sitaki yeyote yule” nilizungumza huku mkono wangu wa kulia ukichangua changua mchele kwenye ungo uliokuwa mapajani mwangu.
“Wacha ushamba wako wewe, wanafunzi wa chuo wanapesa kama nini”
“Mnh!....” niliguna huku nikihisi kushawishika na maneno ya dada Bupe.
“Unaguna nini?”
“Huyo kaka ni mzuri?”nilihoji.
“Aa we, kaka wawatu ni Handsome la nguvu”
“Lakini naogopa”
“Unogopa nini na wewe wacha mambo ya kijijini!”
➡️Itaendelea
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments:
Post a Comment