SIMULIZI: NAITAFUTA FURAHA YANGU 10 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Wednesday, December 11, 2019

SIMULIZI: NAITAFUTA FURAHA YANGU 10






Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU

______sehemu ya 10_______
       Tulipo ishia jana,Juma alishusha pumzi kisha akawaza sana ,alimwambia daniel hama tu kwenye hio nyumba ,sasa inabidi hio familia tuue wote maana washatia nuksi ,
Nimesema huyo adinani tafuteni leo leo afe .

Juma aliongea na kutoa kiasi cha fedha alimkabidhi daniel na kumwambia kahamishe vitu vyako ,wakati unahamisha vitu ,daniel kawatie wale watoto kwenye roba katupe hata bagamoyo au kirungure.
Juma aliongea na kuingia ndani ,baada ya kuongea vile daniel na kelvin waliondoka na kwenda kuhamisha vitu kwenye nyumba ya akina adinani maana amelipwa pesa yake hivyo mpangaji atoke.

Mme wangu,ni nani huyo unataka auliwe leo leo?,mke wa juma alimuuliza mmewe,juma alimwangalia mke wake kwa jicho la ukali kisha akamjibu "hayakuhusu akasonya na kuingia chumbani.

Mke wa juma alikiwa ameshika fagio alikuwa anasafisha nyumba ,aliwaza sana ni nani amekosana na mme wake hadi aseme auliwe leo leo.mke anajua kazi ya mmewe ni uzulumaji na unyonyaji watu ,alitamani amjue huyo mtu ila ,hakufanikiwa ,mama aliendelea kufagia

Tukirudi tabata bima ,daniel alikuja na gari na kutoa vitu vyake ,wakati anahamisha adinani na wadogo zake walikuwa wanaangalia ,adinani aliwaza " tulikuwa na vitanda vitatu,tv,kabati friji magodoro mazuri ,yote yameibiwa ,ila namshukuru mungu nimefanikiwa kuirejesha nyumba ya baba yangu mikononi mwangu.

Basi danile alihama ,na kuwaachia nyumba,basi adinani alisafisha nyumba kisha akapanga kila kitu ,alienda kwa mama joy ,"alimwita mama mdogo joy kwa sasa nishairejesha nyumba mikononi mwangu mimi nitatoka kidogo kwenda kutafuta vibarua vya kazi naomba unisaidie kuwaangalia akina nusra na shangazi 

Mama joy alifurahi na kumwambia nitakuwa naenda kushinda huko wala usijali,basi adinani alitoka ili akatafute vibarua maeneo ya buguruni ,rozana ,karume hadi kariakoo ,hayo maeneo aliwaza ataulizia kazi kila mahali.

Adinani aliwafungia wadogo zake mlango na kuwaambia wacheze ndani tu wasitoke nje ,ila hakubana na kufuli,yeye akatoka na kwenda kutafuta vibarua.
Adinani mwenye mawazo aliondoka hadi sehemu moja wanatengeneza matofal ya block ,alifika na kukutana na mmiliki alimwomba kibarua,

Yule mmiliki wa hio sehemu alimwangalia adinani jinsi alivyo alimwambia "sikia kazi ipo ila kwa mwili. Wako huu sidhani kama utaweza kufanya hizi kazi ngumu ,maana umekaa kimayai mayai sana.adinani akiwa na shida ya kazi alimweleza naweza kufanya hivyo naomba uniamini.

Basi adinani alipatiwa kazi ya kutengeneza tofali maeneo ya matumbi.muda ule ule adinani alivua shati na kuanza kazi ,kulikuwa na kazi ya kusomba tofali na kuzipanga ,
Yule bosi alimwambia " we adinani kwakuwa leo unaanza kazi tofali moja kuhamishi ni shilingi 40 ,hivyo spidi yako ya kusomba ndio unajipatia pesa,
Adinani aliwaza ,nyumbani hamna chakula na wadogo zake wanamtegemea alisema haina haja ya kutafuta kazi nyingine hapa hapa nitakomaa kwakuwa nishaikomboa nyumba basi wacha nipambane.

Adinani alisomba tofali hadi jua likazama na alifanikiwa kupata shiling elfu nne ,kama mjuavyo matofali ya cement ni mazito mno ,adinani alihisi mwili unamuuma kila mahali ,lakin alipewa pesa aliyofanya kazi.adinani alivaa shati na kunawa kisha akaanza kurudi nyumbani.

Tayari giza lishaanza kuingia ,kumbe wakati adinani anafanya ile kazi kelvin hakuwa mbali na eneo lile alikuaa anamfuatilia adinani kisha juma alitoa pesa adinani auliwe leo leo .
Adinani kwa mwendo wa taratibu alitembea pole pole hadi stendi ili akapande dala dala arudi nyumbani alisimama barabarani kisha akaingiza mkono mfukoni ,adinani aligusa kama pesa zake bado sipo ,bahati nzuri alizikuta zipo .

Adinani akiwa anasubiria dala dala ,kuna binti alikuwa kati kati ya lami analia na kusema "jamani wenye magari naomba mnigonge nife ,sina thamani mimi ,mapenzi yananikosesha amani alilia kwa uchungu kisha alijilaza bara barank kati kati.

Lile tukio adinani aliliona mara kuna lori likawa ninakuja spidi adinani alimwangalia yule binti alikuwa analia mno huku akionesha kukata tamaa kabisa ya kuishi.

      Adinani aliona si vizuri kumwacha binti afe kisa mapenzi ,kwa mwendo wa haraka aliwahi na kumnyanyua yule binti kisha akaruka upande ambao kulikuwa na mtaro mdogo ,adinani alidondoka na yule binti ,adinani hakujali kama anaumia au laa

Adinani alitangulia chini kisha yule dada akamdondokea juu,yule dada alinyamaza gafla kulia aliangalia ni nani kamtoa barabarani ,alishangaa kuona ni adinani.

Yule dada aliinuka na kusema " wewe si ndio kijana ambae asubuhi tumekuta unalia kwa mama amina alikuwa anakudai kabati,wewe sindio zumra amekusaidia kulipa deni ambalo ulikuwa unadaiwa?
Adinani nae aliinuka na kujifuta vumbi kisha mikono yake ilikuwa imechubuka baada ya kudondoka mtatoni.

Yule binti alikuwa ni suhaila ,adinani nae alimwangalia jinsi alivyodondoka nae akakumbuka siku alivyomwokoa wakati anataka kuporwa mkoba wake na vibaka.

Adinani alimshika mkono na kumuuliza  ,kwanini unataka kujiua?,suhaila alisikia vyema swali la adinani ndipo alimkumbusha machungu yake ,yaani wanaume ninyi ni wauaji wakubwa ,mtu nampenda kwa moyo wangu wote bado ananisaliti  tena na wauza baa ,sina mama mimi ,sina baba yanini niendelee kuishi  niishi ili nifanyeje kila siku naumizwa,niliyempenda na kumjali hanitaki niishi nipate nini?
Suhaila aliongea kwa nguvu huku akilia ,adinani aliona ni kweli mapenzi yanamtesa sana huyu binti alimshika mkono kisha akamwambia nifuate ,suhaila alimwambia siendi popote nataka nijirushe barabarani halafu gari linipitie nigongwe nifee kuliko kukaa na hili jeraha moyoni.

Adinani aliona kweli huyu dada anamachungu na hasira imemjaa, alimshika mkono na kumwambia nifuate ,hakutaka suhaila ajiue maana kamsaidia kukomboa nyumba ,amemsaidia kulipa kabati adinani alijisemea moyoni suhaila  punguza hasira.

Alimchukua  kumtembeza kwa miguu adinani aliamua afanye hivyo sababu hakuwa na pesa ya dala dala , 
Pesa aliyoipata baada ya kusomba matofali tayari ameipigia kununua ,unga ,mafuta ,kitunguu na mkaa ,maana anatumia jiko la mkaa.

Adinani akiwa anatembea na suhaila aliona kama vile anachechemea ,adinani ilibidi asimame na kumwangalia kwanini anachechemea ,alivyotizama miguuni suhaila alikuwa peku.
Miguu yake ilionekana kuchunika .
Adinani aliuliza kwanini upo peku?
Suhaila alimwangalia adinani na kumwambia "sasa nitembelee viatu ili nipate nini sina hamu ya kuendelea kuutesa moyo wangu kwenye hii dunia iliyojaa usaliti. 

Adinani alivua raba zake kisha akamvalisha suhaila ,na kumwambia ,hautakiwi kuwa hivyo ,usiuchukie ulimwengu huu ulimwengu ndio unakufunza kuishi kutokana na makosa,
Adinani alimuuliza suhaila ,kwenu ni wapi?

Sipajui na wala sitaki hata kurudi sina thamani kwenye dunia nimekuambia,adinani aliwaza ,we si hutaki kurudi nyumbani kwakuwa nyumba nishaimiliki wacha tuende wote hasira zako zikiisha utarudi kwenu adinani alijiwazia moyon

Basi adinani alimchukua suhaila hadi nyumbani.walifika walikuta nusra na mudrick wana nawa chakula ili wale.
Adinani alifika aliwauliza hicho chakula mmekitoa wapi?
Nusra alishika paja la kuku ili ale ,mudriki alijibu " kaka kuna anko ameleta hapa alikuwa amevalia sweta lenye kofia ila alikuwa kavaa swete jeusi na suruali nyeusi .
Lakin huyo anko amesema amepewa hichi chakula na mama mick atuletee.
Kwa maelezo ya mudrick ,adinani aliyasikiliza na kuvuta kumbu kumbu ,alivyokuwa anasomba matofali kuna mtu alikatiza mbele yake akiwa amevaa sweta jeusi huku amevaa na kofia ,pia alivyokuwa amesubiri dala dala huyo mtu alimwona alikuwa anatembea nyuma yake kila akigeuka yule mtu alijifanya kama yupo bize na simu.

Wakati huo ,nusra ndio anataka kula paja la kuku"adinani aliuwahi mkono wa nusra na kumnyang'anya ile nyama ,msile subiri nimpigie simu mama mick kwanza.

Tukirudi upande wa piki ,kelvin alimpigia simu juma na kumweleza ,"jumaa sijafanikiwa kumuua huyu adinani maana alikuwa yupo mazingira ya barabarani ila nimewanunulia wadogo zake chakula kisha nikatia sumu hivyo nimewapa wale.

Juma alijibu "unahakika watakula ?
Ha ha nimewaambia kimetoka kwa mama mick ndio kaniagiza hivyo lazima wale " juma nae alicheka na kusema hapo umewapata kwahio kesho asubuhi tuwahi tukawazike hao watoto ee.
Ndio maana yake tukawazike ,halafu adinani najua atachelewa nyumbani alikuwa yupo na kimwanamke flani amekiokoa bara barani alikuaa anataka kujiua.

Basi simu ilikatwa pia tukirudi upande wa pili adinani alivyompigia mama  mick simu ilipokelewa 
"Shikamoo mama mick adinani alisalimia
Marhabaa adinani unaendeleaje?
Niko salama mama nilikuwa nauliza hivi " wewe ndio umewatumia akina nusra chakula?

Mama aliuliza chakula? ,mimi sijawatumia chakula hata "adinani alimwambia ,kuna mtu kaleta chakula kasema wewe umemwagiza " hapo adinani alipata shaka akawaambia wadogo zake "siku nyingine msipokee chakula kwa mtu yeyote wadogo zangu hichi chakula msile hata kidogo .adinani alichukua na kumwaga nje kwenye ndoo ambayo wanakusanyaga uchafu.

Adinani aliwaambia subiri nawasongea ugali sasa hivi.adinani alienda kununua unga na mazaga zaga yote alirudi na kupika kisha walikula lakin  suhailah aligoma kula 
Adinani alijaribu kumbembeleza lakin akakataa kata kata.
Basi adinani walikula chakula na wadogo zake ,aliamini suhaila ana hasira na maumivu ya kuumizwa na mpenzi wake ,wao walikula walivyoshiba.

Adinani aliwatandikia wadogo zake godoro chini kisha chumba kingine alimtandikia suhaila na kumwomba alale ili hasira zake zikiisha atamruhusu aende kwao.
Suhail aliuliza " wewe unaitwa nani maana umeniburuza hadi kwenu mtu hata sikujui jina.
Adinani alijibu mie naitwa adinani.

Suhailah aliuliza itakuweje mama yako akinikuta hapa?,lile swali lilimfanya adinani amkumbuke mama yake ,kisha akamwambia suhaila ,usijali ,hawez kurudi tena. Kisha adinani alitoka na kumwacha suhaila amekaa na kuegemea stuli.
Adinani alimkumbuka sana mama yake hivyo alitoka nje na kumpunga upepo  ,alikaa kwa muda mrefu ndipo alivyorudi ndani alikuta suhaila amelala huku kaegemea stuli.

Adinani alichukua shuka na kumfunika kisha nae akalala sebuleni maana chumba cha tatu hakikuwa na godoro wala kitanda
Hivyo alikaa na kuegemea ukuta ndipo usingizi ukampitia

Tukirudi kwa juma ,usiku wa manane alianza kuota yupo kwenye gari "alimwambia kelvin " unaona hio piki piki gonga pitia na gari huyo ni ally pamoja na mke wake.
Kelvin aliongeza gia za gari na kukanyaga mafuta aliigonga piki piki puuuu
Kitendo cha kugonga piki piki juma alishituka kwenye njozi yaani ameota jinsi walivyomgonga ally na mkewe hadi kupoteza maisha

Juma alianza kuhema kwa kasi kisha akachukua glass ya maji akapiga funda moja la maji alianza kuwaza "inakuwaje naota ndoto ya mtu ambaye tayari ashakufa.

Wakati juma anawaza vile bibie suhaila nae anaota ndoto ya tukio hilo " aliota gari jeusi limeigonga piki piki ambayo walikuwa wamepanda mme na mke ,baada ya kuwagonga likaridi nyuma na kuwapitia kwa juuu kisha likaondoka

Gafla suhailah aliamka kwenye ndoto kisha alikumbatia  masikio yake na kusema hapaaaaaaaaaaa kwa sauti ya juu jambo lililomfanya adinani ainuke ,kisha akawasha taa alikuta suhaila ameloa mwili mzima na jasho huku akitetemeka akisema sio mimi sio mimi 
Sijawaua mimi
Imekuwaje suhaila nae anaota ndoto ya tukio ambalo juma na kelvin waliwagonga ally na mke wake wakafariki pale pale

Je nini kitaendelea?


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa