Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU
___sehemu ya 8____
Tulipo ishia jana,Gafla wale vibaka walipiga kabati la chipsi puuuu likapasuka paaaaa ,mmoja akarusha kisu ili amchome adinani .
Gafla walinzi waeneo lile walifika ndipo wale vijana wakakimbia
Mdada akiwa amechoka hoi anahema akaangalia ni nani kamsaidai?
Alikuta adinani ameshika pochi yake na viatu vyake ambavo vilitoka baada ya kupigwa teke,lakin adinani alivyoangalia kwenye sehemu ya maegesho ya magari ,palikuwa na mtaro mkubwa ,ambao huo mtaro waliuziba na mbao mbao,
Adinani alivyoangalia vizur alimwona mdada amedondoka chali ,huku analia jaman mguuu wangu nimeumia jaman.adinani alitizama nani mwingine akaumia alivyotizama kwa uzuri ndipo aliona kibaka mmoja alimwendea yule dada aliyedondoka chini alikuwa kalewa ,yule kibaka alichukua simu.
Ile anataka kuondoka adinani aliinyukaua ile simu kisha akamwambia we broo sepa,adinani ki mwili ni mdogo ila alikuwa mwepesi na mjanja sana wa kukwepa ngumi.
Yule kibaka alirusha ngumi mbili tatu adinani alizikwepa kisha alipiga kelele za kuomba msaada ,ndipo walevi walitoka kwenye baa na kuuliza nani analeta fujo,yule kibaka aliona akizubaa ataweza kupigwa ,adinani alimwinua yule mdada ambae nae alikuwa amelala chali.
Dada umeumia ?adinani aliuliza
Ooooh mguu wangu umeteguka,yule dada alijibu kwa sauti yake iliyojaa maumivu,adinani alimwita yule dada mwingine ambae ana mkoba wake ,alimwita dada njoo mkoba wako upo salama.
Yule dada ambae alikuwa analia amesalitiwa na mpenzi wake ,alifika na kumwambia adinani "kaka asante kwa kunisaidia kwa wale vibaka sijui pochi yangu ingeibiwa nawaza tungeendaje nyumbani,
Yule dada aliita zumra umeumia ? ,zumra alimjibu rafiki yake naomba umulike taa ya simu kwenye mguu wangu nione njinsi nilivyoumia ,
Rafiki yake alianza kutafuta simu kwenye mkoba ndipo zumra aliongea we suhaila mlika basi panauma ujue.
Suhaila aliwasha taa ya simu alimlika zumra usoni ,ndipo adinani alivyomtizama ni yule msichana ambae alikuwa abiria wake wa boda boda na alimlipa laki moja.
Adinani alishangaa na kujisemea moyoni " huyu dada nimekutana nae tena ,kumbe anaitwa zumra,
Basi suhaila alimlika mguu na kuona ameteguka basi ,suhaila alimwambia rafiki yake"zumra twende nyumbani maana huyu mpenzi wangu kanitibua ona nimesababisha umeumia,
Alimkokota zumra hadi kwenye gari ,ndipo alimpandisha suhaila alipanda upande wa dereva ili aendeshe gari ,lakin kabla hajawasha gari akakumbuka kijana amemsaidia na hajamshukuru.
Suhaila alimwambia zumra ,sio vizuri kuondoka pasina kumshukuru huyu kijana ambae ametusaidia laasivyo tungeporwa, basi suhaila alienda moja kwa moja hadi kwenye banda la chipsi ambalo anafanya kazi adinani.
Kufika tu alimkuta adinani akitukanwa matusi makubwa na bosi aliyemwajiri alikiwa ni mwanamke,we adinani akili zako zinakutosha kweli?,utaingilIaje ugomvi wa walevi ,we kazi yako kuwauzia chipsi walevi na si kuamua ugomvi je wewe umekuwa askar ama mgambo ,sitaki kuelewa nataka kabati langu mpya ,
Suhaila aliangalia kweli yeye alikuwa chanzo na amesababisha kabati la chipsi limepasuliwa ,suhaila alivyomwangalia adinani aliona anatiririsha machozi ,suhaila hakumwambia chochote adinani aliondoka na kuingia kwenye gari kisha akawasha gari wakaondoka na rafiki yake zumra,hawa mabinti wanaishi pamoja ,
Adinani aligombezwa mno na bosi wake kisha akaambiwa atoe vipande vya kabati lililovunjwa kisha kesho saa mbili bosi amkute ashafika kazini na ashanunua kabati jipya ,bosi aliondoka.
Adinani alilia alihisi anamkosi ,rafiki yake miki nae alimlaumu ,we adinani umezingua tu wewe haya huyo dada uliyemsaidia hata hajakuambia hasante kaondoka kimya kimya ,nini maana yake kutoa msaada?
Adinani alishusha pumzi alimwangalia rafiki yake kisha akamshika bega,adinani alipangusa machozi na kusema "ukimsaidia mtu ,si lazima usubiri asante yake ,ukimsaidia unakuwa umesaidia na siii kusubiri shukrani,mungu ndo anajua nimefanya vizuri kumsaidia au nimefanya makosa naimani mungu ndio mwenye majibu.
Mick alimwambia haya utalipa na nini kabati la watu maana jipya linauzwa laki tatu ,haya kituo cha polisi unadaiwa milion tatu ,rafiki yangu mbona hufikirii?
Adinani alicheka kicheko kilichojaa shida " aliita mick ,matatizo yakiamua kukuandama hata ushinde kwenye chumba kitupu kisichokuwa na chochote unaweza ukapata tena shida ,hivyo matatizo yangu nimeamini haya kwepeki.
Basi walizoa vipisi vya kabati walivyo maliza waliingiza vyombo kisha wakaondoka ,adinani alienda kulala kwake kisha mick nae alirudi kwao ,ilikuwa ni saa saba usiku ndipo adinani alifika nyumbani na kufungua mlango aliwasha taa na kukuta nyau wawili wamekufa wapo juu ya meza.
Adinani aliwasogelea kisha akafunua hotpot aliangalia wali ambao aliwawekea akina mudrick ulikuwa umebadilika rangi na kuwa wa kahawia ,,adinani alinusa ndipo aligundua harufu ya sumu.
Adinani aliwaza ni nani aliweka sumu kwenye chakula cha watoto ,ndipo adinani aliamin si yeye anaye andamwa hadi wadogo zake wanataka kuuliwa .aliwatoa wale nyau na kuwatupa nje,alitandika chini kisha alilala.
Kabla hajapitiwa na usingizi aliwaza "maneno ambayo aliyasikia kwa juma" nimewamaliza wazazi wake kinachotakiwa ni kuchukua nyumba,vile vile akakumbuka anadaiwa milion tatu ya piki piki iliyopotea ,na kesho ndio siku ya mwisho ,
Adianani alikumbuka mama mick alimwambia amekopa milion mbili na nusu kesho wanaenda kulipa kituo cha polisi kisha waombe siku tatu ili watafute pesa nyingine ya kumalizia.
Adinani alisoma duwa wakati wa kulala ili kujilinda na vitu vyoye vibaya ,lakin alikumbuka maneno ya mama amina ambae ni bosi wake wa kwenye banda la chipsi.
"Kesho nikukute hapa saa mbili na kabati mpya,adinani aliwaza nitapata wapi kabati?,aliwaza sana na kuvuta shuka kisha akapitiwa na usingizi.
Saa tisa usiku ,juma,kelvin na daniel walikutana mahali kisha walianza kupanga mbinu za kumdhibiti mama mick ili asiweze kumsaidia adinani ,kelvin aliatoa wazo
" jamani mnaumiza vichwa bure mie na wazo moja ,kesho tumuwindi huyo Mama mick akitoka tu nyumbani najua atabeba hizo pesa ambazo wanataka kuja kukulipa ,
Hizo pesa tuzipore ,kisha tunazigawana yaani tunakula faida mara mbil ,najua tukizipora hizo pesa , hataweza kulipa piki piki ,hapo nyumba watakuachia na pesa tumekula au mnaonaje.
Ha ha juma akacheka kisha akasema mna akili sana ,tufanye hivyo basi kelvini hakikisha kesho unaukwapua mkoba kabla hajafika kituo cha polis ,kelvini alikubali.
Walitawanyika ndipo kelvin alienda kwake ,juma pamoja na daniel nao walitawanyika.
Asubuhi ,na mapema ,adinani aliamka kisha akaenda kazini ili akutane na mama amina amweleze ukweli yeye hana uwezo wa kununua kabati ambalo limevunjwa, adinani anafika anakofanyia kazi alimkuta mama amina amefika mapema amekaa kwenye kiti huku amekunja sura.
Adinani alifika na kusalimia "shikamoo mama amina"
Mama amina alimwangalia kisha akasonya "hakuitikia alimwambia mbona unaleta tumbo na matendegu yako ya miguu kabati lipo wapi?,
Adinani alisema " mama samahani ,mimi sina hela ila nakiri nimefanya makosa kuingilia ugomvi ,mama nitatafuta kazi nyingine nitakuwa nakulipa kidogo kidogo hadi deni litakapo isha,
Mama alimwangalia na kumwambia ,hapana si kubali nataka kabati sasa hivi laa sivyo nakuweka ndani kituo cha polisi ukasote ,adinani alipiga magoti na kumwamba mama amina
"Mama amina nakuomba unisamehe usinipe hio adhabu nina wadogo zangu wadogo mno wananitegemea mimi ,
Mama alicheka na kusema sasa leo utaenda kuchimbua kaburi la mama yako uite miizimu yote ya kwenu wakupe laki tatu leo leo nikanunue kabati jipya.
Adinani aliomba msamaha ,alilia kwa huruma lakin mama amina wala hana habari anachotaka kabat yake.mara mudrick na nusra waliweza kufika mahali adinani aliko
Kaka mbona unalia?kuna mtu amekupiga?,ni swali ambalo nusra aliuliza "adinani aligeuka na kuwaona wadogo zake alifuta machozi upesi kisha " akawaambia mudrick mmefuata nini huku?.
Mudrick akamwangalia kaka yake na kumwambia "kaka toka jana hatujakuona hivyo tumekuwa na wasi wasi na wewe
Mara mama amina alisimama na kusema " hili banda langu la kuuzia chipsi si sehemu ya kulea yatima ,lipa kabati upesi kama hutaki nipige simu polisi nikakuweke ndani ,unataka kuleta ujeuri ,unajifanya masikin sana ,hata mimi nina machozi naweza kulia .
Adinani akiwa amepiga magoti akiomba msaada ,basi mama mick alimfuata akiwa na mkoba wenye pesa ili waende kituo cha polisi aakamlipe juma.
Mama mick ile anafika mahali aliko adinani,kuna watu ambao walitumwa na juma ,ili kukwamisha adinani asiweze kulipa ile piki piki ,mama aliporwa mkoba na kijana mmoja kisha akapanda piki piki na kuondoka.
Mama mick alipiga makelele ,jamani mwiziii jamani mwiziiiii ameiba pesaaa
Mama alishidwa hadi kuongea ndipo adinani aliinuka na kuangalia alikuta mama mick ndio kaibiwa,adinani aliinuka na kumuita mama mick kulikoni?
Mama mick hata kuongea hawezi ,alichanganyikiwa yaani milion mbili ambazo amekopa kwa ajili ya kumsaidia adinani kulipa piki piki ,tayari imekwapuliwa,
Mama alijibu he hee heela aambyo tulikuwa tunaenda kulipa piki piki imeibiwa"adinani alilia sana na kumwambia "mama sina namna twende nikampe juma hati ya nyumba ,adinani akiwaangalia wadogo zake ambao yuko nao wanamwangalia alijisikia uchungu na kulia.
Mama amina ,alipiga polisi adinani akamatwe ili aweze kumlipa kabati lake,lakin kabla polisi hawajafika,kuna gari aina ya suff iliingia ilifika eneo lile na kufunga breki wakati huo adinani analia huku amejiinamia chini.
Mdada mmoja alishuka kwenye gari ,pia na mdada mwingine nae akashuka walikuwa ni zumra na suhaila.
Zumra alikuwa anachechemea alimuuliza mwenzake,ni kijana yupi ambae jana tulisababisha kabati lake la chipsi kupasuliwa?
Suhali alinyoosha mkono na kusema yule pale analia huku amejiinamia?,wakati huo adinani analia hata mlio wa gari hajausikia ,alikuwa analia na kujutia baba na mama wamemwachia mzigo mzito kwenye dunia
Mama amina,mama mick na watu waliokuwa eneo lile waliwaangalia wale wasichana ambao walionekana maisha yao ni mazuri ,zumra alimgusa adinani shingon na kuita kaka amka acha kulia.
Wakati huo suhaila alifungua buti ya gari waliokuja nayo ,kulikuwa na kabati la chipsi kubwa na mpyaaaa ...
Je nini kitaendelea?
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments:
Post a Comment