SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial) - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, December 7, 2019

SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial)




MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 08



TULIPOISHIA: Ukimya ulitawala kwa sekunde kadhaa, ghafla akashangaa kuona fuvu la mtu likiwa lipo mbele yake, kuongea alishindwa vile vile na kupiga kelele alishindwa, akiwa anajiuliza afanye nini fuvu lile lili.......... 

SONGA NAYO! 

Latina akiwa anajiuliza afanye nini fuvu lile lili muingia ndani ya mwili wake ikampelekea kupiga kelele mara moja. 

Upande wangu sauti ya Latina niliiskia freshi moyo wangu ukalaluka nikadondosha kuni Chini na kusema: umeskia? 

Joseph: eeee Kwani Kulikoni? 

Nikamjibu: nimeskia sauti inatoka huku twende kwanza. 

Tuliacha kila kitu tukaanza kufuata sauti tulipoisikia muda ule, tulipofika eneo lile Latina alikuwepo hatukuweza kumuona Ila Joseph aliogota simu na kuniuliza: sio simu ya mdogo wako? 

Nilishtuka mno Baada ya kuona simu ile, kwa sauti ya Chini nikasema: Kumbe Hisia zangu zilikuwa zipo sahihi! 

Joseph: turudi kule kwa wenzetu kwanza. 

Kabla hatujachukuwa uamzi wowote Latina alitokea nyuma yetu, nilipogeuka kumuangalia baada ya kuskia mchakacho Sikuamini kumuona maana macho yake yalikuwa yamebadirika rangi, ukweli hali ya mdogo wangu kwa muda Huo ilikuwa tofauti mno. 

Moyo wa huruma uliniingia nikaanza kumsogelea huku nikisema: imekuwaje my dear! 

Joseph baada ya kugundua Latina ninaemjua Kama mdogo wangu sie kwa muda Huo alinifuata haraka na kunisukuma ili nisimshike, ile Hali ya mimi kudondokea Chini niligeuka kumtazama Joseph na kumuuliza: Ndo nini sasa! 

Joseph akiwa anamtazama Latina Akanijibu: huyu sie tukimbie! 

Kabla Joseph hajapiga hatua huwezi kuamini Latina alimuwahi na kumshika koo Jambo ambalo upande wangu lilinifanya nizidi kushangaa, vidole vya mdogo wangu vilikuwa na kucha ndefu mno. 

Latina akiwa anamnyoga Joseph damu zilianza kushirizika shingongo mwa Joseph maana aliingiza kucha Zile kwenye kolomeo, niliona atakuja kumuua nikanyanyuka ili kwenda kumzuwia, kabla sijamfikia Latina alinigeuzia macho akanitazama jicho mbaya Mpaka mwenyewe nikaogopa.

Muda Huo Huo Hamisa na Chande walifika, walipoona tukio lile walishtuka kwa mshangao mkubwa huku wakiwa wamekodoa macho,  haikuchukuwa muda wenzetu nao wakafika eneo lile, kila mmoja alishtuka mno Baada ya kuona macho ya Latina, tukiwa tunatafuta njia ya kumzuia ili asimuue, Latina alimrusha pembeni kwa nguvu zisizo za Kawaida ishara tayari Joseph hatupo nae tena kisha akasema kwa sauti nzito ambao kila mmoja hakuamini kuskia sauti ile: ntaua mmoja baada ya mwingine. 

Hapo hapo Latina akapotea, aisee ile Hali ya kuona mwenzetu anauwawa mbele yetu na Latina akapotea baada ya kutupa vitisho vikali sote tulikimbia huku tukipiga kelele. 

Baada ya dakika kadhaa Tulifika eneo lile tulipokuwa tunataka kuweka makazi yetu kwa Muda kila mmoja akiwa anahema vibaya. 

Moyo wangu haukuweza Kutulia, nilijiuliza mengi kuhusu mdogo wangu ila sikupata picha, wenzangu walianza kulijadiri swala lile Mpaka wakanisogelea ili kuniuliza. 

Patrick: Najma imekuwaje mbona hatuelewi?

Nilianza kulia huku nikisema: sijui nini kimemkuta mdogo wangu, Mimi mwenyewe sauti yake Ndo ilinishtua tukaongozana na Joseph maskini bila kujua kuwa mwenzangu nampeleka eneo hatari Sana. 

Amanda kwa presha Akaniambia: funga bakuli wewe na mdogo wako mnayajua haya, Haiwezekani umchague Joseph peke yake na watu hapa tulikuwa wengi, yeye tu ndo ukamchagua inaonekana ni plani zenu, Kwani Yule si ni mdogo wako?

Maneno ya Amanda yaliniumiza mno ukija kuangalia hata mimi sielewi ni kipi kimemkuta, nilikosa namna ya kujitetea nikaendelea kuwaangalia huku nikilia mno. 

Sofia akiwa Analia akasema: jamani mwenzenu naogopa, wallah Najma wewe na mdogo wako mnalijua hili. 

Kabla sijajieleza baadhi walianza kunilaumu wakimaanisha Mimi na mdogo wangu tumeamua kuwazunguka. 

Hasira ilinipanda kwa sauti ya Juu nikawanyamanzisha: basi!!!! 

Wote waliniangalia kwa umakini, ndipo nikasema huku nikiwa nalia: ndo nini kunilaumu? hivi niulize Kati Kati yenu Nani anamaumivu kunizidi mimi? Yule ni mdogo wangu na mtu aliefariki ni Rafiki yangu mnaponiambia niseme ukweli kuhusu hili je niseme nini? Moyo unaniuma mno sijui Kwanini kipenzi changu amebadirika kuwa namna ile. 

Amanda Akanijibu: usijitetee kila kitu wewe unajua. 

Professor mkuu alipoona nalaumiwa sana alimpiga kofi Amanda Mpaka kila mmoja akashangaa. 

Mimi sikujali wanachokifanya nilitupa simu Chini, nikavua koti  niliokuwa nimevaa, taratibu nikaanza kuvua viatu huku kila mmoja akiwa ananishangaa, Nilipomaliza nikasema: Ntaenda kumtafuta mwenyewe acha niwape amani.

Nilitoka hapo nikiwa nakimbia huku nikilia mno, Derick alipoona vile hakutaka kuniacha niende alinifuata mpaka akanifikia, alinishika mkono kisha akanivuta Na kunikumbatia kwa nguvu. 

Moyo ulizidi kuniuma mno, nikazidisha kilio Mara dufu, Derick kwa sauti ya Chini akaniambia: usijali mambo yatakuwa vizuri. 

Nikiwa nalia Nikamuuliza: mdogo wangu nini kimemkuta? 

Upande wa huku professor mkuu akiwa anatuangalia akawaambia wenzie: mkimgombeza namna ile mnataka afe au? Kwa hali alionayo mnaona kweli Yeye ndie kapenda iwe vile? msimulaumu tena hapa Kikubwa Nikujua namna ya kulihendo hili tatizo. 


Asubuhi na mapema wote walikuwa bado wamelala Ila Mimi Usingizi sikuweza kuupata, kila nikimfikiria mdogo wangu nilikuwa sipati picha, kilichonitesa zaidi nilipokumbuka alivyonikiss, nilihisi Labda ile tabasamu ndo Ilikuwa ya mwisho upande wake, kimoyo moyo nikawa najisemea huku machozi yakiwa yananibubujika mashavuni: mama na baba watanichukuliaje kama sintorudi na wewe? Labda huko uliko mdogo wangu baridi inakusumbua sana, I'm sorry my love nimeshindwa kukuwekea ulinzi wa kutosha. 

Nilijikumbata huku nikiendelea kulia,  muda mfupi professor ambae anajiita husband aliamka aliponiona Nipo kwenye dimbwi nzito la mawazo alisogea pale nilipo akanipa moyo akisema: hatuna muda tutakuwa tumefika, usijali mambo yatakuwa sawa. 

Nikamuuliza: mdogo wangu vipi? 

Professor: hata Yeye pia atapatikana. 

Watu wote waliamka wakaanza kujadili baadhi  tusonge Wengine turudi nyuma ndipo Dominic mwanajeshi akasema: hapa tupo kama uwanja wa vita, Hakuna kurudi nyuma tuendelee kusonga mbele lazma swala hili tulimalize kwasababu hata tukisema turudi nyuma Hakuna kitu cha kukomboa Ndo hivo tumewapoteza wenzetu na hapa tulipo tupo Kati Kati ya msitu nawaombeni tuendelee na safari. 

Professor mkuu akasema: Nikweli kila Jambo lenye kheri lazma changa moto zipatikane yawezekana kwenye hizi balaa ndo mafanikio yanatokea kwahio niwaombeni tutulize Nyoyo zetu na Tuzidi kuomba Dua. 

Upande wangu nilikuwa nilimelishikilia begi la Latina huku nikilitazama kwa umakini kama vile sintomuona tena. 

Hamisa akiwa Analia akasema: ukweli Mimi naogopa nisiwe muongo Huo Ndo ukweli wangu naombeni nirudi zangu nyuma. 

Professor Rodrigo akamjibu: hapa Hakuna maswala ya kurudi nyuma umeshaambiwa na Labda hauoni kama Hakuna mawasiliano yoyote! 

Joyce Rafiki yangu alipoona bado mimi hakili hazijakaa sawa Zidi ya mdogo wangu alinisogelea na kunipa maji ya kunywa, Nilichukua nikanywa na kumuuliza: atapatikana Latina? 

Joyce: usijali lazma apatikane.

Patrick alimsogelea Chilunga alipokuwa amesimama na kumuambia: nisaidie simu yako dakika mbili. 

Chilunga alimpa kisha Patrick akasogea sehemu yake huku akiwa anatafuta Miziki ya kikongi asikilize, alivaa headfone akaanza kusikiliza mziki taratibu huku macho akiwa ameyaelekeza kwenye simu. 

Muda Huo Huo Latina akiwa ametapakaa damu mwili mzima, uso wake ukiwa haugunduliki tena alitokea nyuma ya Patrick Ili kumuua na yeye pia, watu wote walipomuona aisee Hakuna aliekimbia na begi, baadhi walikimbia bila viatu, mimi ile kumuona mdogo wangu nilianza kumfuata taratibu huku nikisema: usifanye hivo ni mimi Najma dada yako. 

Joyce hakutaka nimfikia latina alianza kunivuta huku akiniomba nisifanye chochote ila Mimi nikang'ang'ana, Joyce alipoona namzingua alinipiga bonge la kofi na kuniambia kwa hasira: sio latina we mshenzi jitambue eee. 

Nilijitambua tukatoka hapo mbio, Patrick bila kujuwa hili wala lile kwasababu ya muziki kuwa mnene kwenye headfone aliendelea kuinjoi bila kujuwa kuwa wenzie wamekimbia Amebaki mwenyewe na kizaa zaa kipo nyuma yake. 



Unahisi nini kitatokea!
Usikose mkasa huu!


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa