SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial) - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

Saturday, December 7, 2019

SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial)

20190326_124716



ushauri_saikolojia_mahusiano-20191207-0006


MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 11



TULIPOISHIA: Tuliangaliana usoni wenzangu ambao walikuwa wananilaumu muda wote wakatamani kuniomba msamaa. 

Patrick nae akamuuliza: kwanini akiskia mziki anacheza? 

SONGA NAYO!

Mkaka Yule mzungu akamjibu: Asili ya mtu wa Kongo ni muziki wa kwao, hio ndio dawa Tosha ya kumfanya asiwadhuru kama mnamiziki ya Kongo muwekeeni pale mtafanya kila mtakacho na mtarudi salama, huo ndo ubovu wake. 

Dominic: vipi kuhusu wewe umekuja kufanya nini? 

Akamjibu: Nilikuja ndani ya msitu huu mimi na baba yangu nikiwa na miaka 7 Ila kwasasa Nina miaka 30.

Tulishangaa ndipo Joyce akamuuliza: una maana gani? 

Akasema: tulipotelea huku, na Sisi pia tulikuwa tumekuja kwa ajili ya maswala hayo ya ebola. 

Rodrigo: ilikuwaje? 

Akasema: baba kuna makosa aliafanya kipindi hicho, muombeni Mungu msikutane na kabila la wambote (pygmy) ni binadamu wa Kali mno. 

Rodrigo akamgeukia Zakayo na kumuuliza: wewe si ulisomea Kidogo maswala ya Utafiti Enhe! tuambie wambote ni wakina nani? 

Zakayo: Nyinyi hamjui? 

Rodrigo: Sisi wana science bwana Ukitaka kuuliza mavairasi Njoo utaambiwa Mpaka wapi wanapatikana Mara nyingi. 

Tulicheka kisha Derick akasema: usijitetee! 

Rodrigo: Mwaya Zakayo tuambie. 

Zakayo: Nikabila la watu wa fupi mno hapa Kongo, Halafu wananguvu Sana na inasadikika wao ndio watu wa kwanza kuishi ndani ya nchi hii ya Kongo, wao wamejitenga Sana na binadamu wengine mara nyingi wanaishi mamistuni. 

Aliishia hapo sote tukamuelewa ndipo Rodrigo akamuambia yule mzungu: tumeelewa kuhusu hio kabila. 

Akasema: pygmy wanakula nyama za watu...

Tulishtuka mno huku tukiendelea kumuangalia kwa umakini ndipo akaendelea kusema: walitaka kunila mimi ila baba akamtwanga risasi mke wa mkuu wa kabila lile,  iliwauma sana ndipo wakatuambia kikwao hatutotokaga ndani ya msitu huu milele na milele, kwahio naweza kuondoka zangu? 

Nilimzuwia na kumuuliza: vipi baba yako yuko wapi? na je Kwanini Huyu fuvu Hawezi kuwazuru Nyinyi? 

Alitabasamu kisha akanisogelea akaninong'oneza maskioni: siraha ya pekee kumuangamiza huyu kiumbe ni Yale maji. 

Alipoongea hivo aliniachia kisha akanipiga piga begani na kuondoka zake, nilibaki hapo nimedubwaa huku nikijiuliza alimaanisha nini Ila sikupata jibu. 

Wenzangu baada ya kuona nimenong'onezwa kitu ambacho wao walihisi Labda ni muhimu kwetu walinisogelea Wakaanza kuniuliza nini kaniambia ndipo nikawajibu: ameniambia hivi siraha ya pekee ya kumuangamiza huyu kiumbe ni Yale maji, sasa sijui kama ni ule mto au ni Yale maji ya ajabu.

Walishangaa ndipo Zakayo akasema: Labda ni Yale maji ya ajabu. 

Profesa Rodrigo: nihisi! Ila Huyu mtu anaonekana baba yake ni Mtafiti Sana mambo ambayo wengi hawayajui Ila yeye anayajuwa kiundani.

Abdul akamuuliza: Kwanini wao Huyu fuvu hawazuru? 

Rodrigo: wazungu wakienda sehemu hawaendi kihorera horera kama Sisi wanajipanga kwanza ndo maana alievumbua maradhi haya ni mzungu. 

Nikauliza: hapa kila mmoja maji Yapo shingoni mnampango gani? je! turudi nyuma au tusonge mbele? 

Rodrigo: Goma tumelianzisha wenyewe sasa kila mmoja nikujuwa jinsi gani ya kulicheza, kurudi nyuma Haiwezekani hapa tupo Katikati ya msitu mi naona hivi tujitahidi twende kwenye huo mto ikiwezekana kama alivyosema tuweze kumteketeza kwanza huyo kiumbe mambo mengine yatafuata Baadae. 

Patrick: muongee hivo mkumbuke Ramani hatuna hapa. 

Nikamuuliza: tumeiacha wapi? 

Patrick: Muda ule tunakimbia profesa husband ndo alikuwa nayo. 

Ndo tukakumbuka muda ule alikuwa anaangalia Ramani ndipo Latina alitokea na kumuua. 

Derick alishtuka na kusema: lazma nirudi kule. 

Nilishtuka na kumuuliza: wapi? 

Derick: kule tulikokuwa mwanzo. 

Nikamuuliza: kufanya nini? 

Derick: begi yangu nimeiacha na Kuna vitu vyangu vya thamani vipo mle. 

Niliposkia hivo uzalendo ulinishinda nikamuwahi na kumshika mkono kisha nikamuambia: Nihatari sana wewe kwenda kule please Achana Navyo kwasasa kitu muhimu ni nafsi yako. 

Derick: lazma nirudi tu kwasababu bila Ramani tunaelekea wapi? 

Wote walimuunga mkono akaamua kuondoka, Nilikata tamaa ya kumuona tena maana nilihisi atafanyiwa Kibaya na Latina. 

Kwa sauti ya Juu nikamwambia: nisubiri. 

Derick alinisubili nilipomfikia nilichomoa kakisu kangu kadogo ka kutumia kulia matunda nikamkabidhi na kumuambia: hakikisha umerudi ukiwa upo Salama. 

Derick alinitabasamia kisha akaondoka.

Baada ya muda Tuliweka makazi hapo huku tukimsubiri arudi, baridi Muda wote ilikuwa inatupiga maana msitu wa equatorial Mvua haikati. 

Upande wa Derick alienda moja kwa moja mpaka ile eneo tulikuwa tumekaa muda si mrefu, alipofika aliukuta mwili wa profesa husband bado upo pale, alisikitika mno na kusema: lala mahali pema tuivumilie hatuwezi kukuzika. 

Alianza kutafuta Ramani kwa bahati nzuri akaiona ndipo Akachukuwa begi yake akavaa kisha akatoka eneo hilo. 

Upande wetu zakayo alianza kurusha mawe juu ya mti ambao Sisi tulikuwa tupo Chini yake huku tukizidi kumsisitiza aachane navyo atakuja kuumizana ndipo akasema: Muda wote nilikuwa siskii njaa sasa nimetulia njaa ya toka Juzi imeniingia. 

Amanda: sasa hapo unaona kuna matunda? 

Zakayo: Kama hauyaoni Sisi tunayaona. 

Patrick akasema: mimi hapa ngoma ya kikongo yenye ninayo ni ile ya Inno's Bella na diamond platnumpz sasa sijui Nyinyi huko. 

Nikamjibu: na Mimi ni hio hio. 

Wengi simu zao zilipotea tulikuwa wachache sana ambao tumebaki na simu ndipo Dominic Akachomoa kasimu kadogo kenye memory card akaomba arushiwe huyo mziki. 

Tukiwa tupo hapo huku Zakayo akiendelea kufanya yake ghafla alirusha kipande cha mti kikapiga nyoka Aliekuwa juu moja kwa moja nyoka yule akamdondokea Sofia, aisee alipige kelele huku akimkunguta nyoka yule ndipo akaenda Chini, haraka Dominic Akachomoa bastola yake akamtwanga nyoka yule risasi ya kichwa kisha akafa hapo hapo. 

Tulishusha pumzi huku Wengine wakimlaumu Zakayo ndipo Dominic akasema: risasi muda wowote zinakata. 

Upande wa Derick akiwa anazidi kusonga mbele huku akiwa anaangalia Ramani ile alishtuka kuskia mchakacho nyuma yake, akasimama huku akiwa anaangalia kona zote ila hakuweza kuona kitu, ile anaenda tena mchakacho ukazidi akaangalia tena nyuma ila hakuweza kuona chochote, ile anaangalia mbele alishangaa kuona Mbwa mwitu Kama thelathini wapo mbele yake huku wakiwa wanamvisia kimtindo flani, uzalendo ulimshinda akatoka hapo mbio huku akielekea sehemu tofauti na kule tulipo,  kizuri alikimbia huku akipiga kelele mno, Mbwa mwitu wale kwa kukimbia farasi wakasome. 

Upande wetu kelele za Derick tuliziskia maana haikuwa mbali sana na eneo lile, bila kupoteza muda tukamfuata huku tukikimbia mno. 

Derick alizidi kukimbia, ile Mbwa mwitu wale wanamfikia alifika eneo mbaya akajirusha ndani ya korongo flani kina chake kilikuwa cha Kawaida na Chini kulikuwa mto mkubwa ulikuwa unateremsha maji, alipaza sauti huku akizidi kuteremka. 

Mbwa mwitu wale Waliendelea kumtazama kwa uchungu maana wao kuingia ndani ya maji Haiwezekani, Tulipofika eneo lile tukawaona Mbwa mwitu wengi wakizunguka zunguka, ndipo Dominic alichomoa bastola yake akapiga lisasi Juu, ule mlio uliwafanya Mbwa mwitu wale wakimbie. 

Fasta tukasogea pale ambapo Mbwa mwitu wale walikuwa wamesimama aisee Sikuamini kumuona Derick akiwa ni mzima wa hafya, wenzangu wote walianza kucheka kwa furaha huku wakimtazama ndipo Abdul akamtania akisema: kurudi bila wewe Tanzania tunawekwa jela miaka yote. 

Derick akiwa yupo kati Kati ya mto ule, huku akiwa bado ameshikilia kile kisu mkononi alitabasamu kwa furaha na kusema: lazma niwe hai kwa muda. 

Derick Akiwa yupo hapo anatafuta njia ya kuweza kumtoa hapo, huwezi kuamini nyuma yake ilitokea nyoka kubwa mno ikajinyoosha kichwa kisha ikashuka fasta pale Derick alipokuwa amesimama na...... ..... Huku Sisi tukiwa tunashangaa shangaa. 



          Unahisi nini kitatokea! 
           Usikose mkasa huu!


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad