SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial) - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, December 7, 2019

SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial)



MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 12



TULIPOISHIA: Derick Akiwa yupo hapo anatafuta njia ya kuweza kumtoa hapo, huwezi kuamini nyuma yake iliibuka nyoka kubwa mno kutoka ndani ya maji ikajinyoosha kichwa kisha ikashuka fasta pale Derick alipokuwa amesimama na...... ..... Huku Sisi tukiwa tunashangaa shangaa. 

SONGA NAYO! 

Nyoka yule alishuka fasta pale Derick alipokuwa amesimama na kummeza haraka huku Sisi tukiwa tunashangaa shangaa. 

Nyoka yule bila kupoteza muda akazama ndani ya maji.

 Nililia mno Baada ya kuona tukio lile, pia hata wenzangu walinisaidia kuomboleza.

Tukiwa tupo hapo bila kujuwa hili wala lile ghafla nyoka yule kwa Mara nyingine aliibuka katoka ndani ya maji akajinyoosha ajabu akamtapika Derick pembeni kisha akarusha damu ambao hata Sisi pia ilitufikia, baada ya hapo nyoka yule aliishiwa nguvu taratibu akaangukia ndani ya maji Kama vile kupoteza uhai, wote Tuliendelea kushangaa ndipo akapelekwa na maji. 

Mimi bila uoga wowote niliwaacha wenzangu pale nikajirusha ndani ya maji Yale huku wakizidi kunisisitiza niache tayari Derick hayupo tena duniani Ila sikutaka kuwapatia maskio bali nilitaka kuhakiki mwenyewe. 

Nilianza kupiga mbizi nikimfuata Derick, nilipomfikia nilianza kumvuta nikimtoa ndani ya mto ule, baada ya dakika kadhaa nilifanikiwa kumuweka pembeni Kidogo ambapo maji yalikuwa hayafiki. 

Mwili wa Derick ulikuwa umejaa vitu kama makamasi vilikuwa vinalenda kama mlenda lenda, Ila Mimi sikujali hayo nilianza kumtikisa. 

Nilipomuangalia kwenye mkono wa kulia niliona kashikilia kile kisu nilichompa Muda ule ndipo nikamuambia huku nikilia Kama mtu aliejikatia tamaa: Kwanini umeshindwa kujitetea hali ya kuwa kisu unacho mkononi! Usinifanyie hivo mwenzio nakupenda. 

Derick Muda Huo alikohoa akaanza kutema maji, nilifurahi mno nikawaita wenzangu waje Derick ni mzima. 

Baada ya muda tulikuwa tumemsafisha Derick huku tukiwa tumemlaza Chini ya mti.

Rodrigo: akipona lazma awe chizi. 

Patrick: Natamani sana kujua nikipi kimemfanya akawa hai!

Amanda Muda Huo alikuwa pembeni huku akimuangalia Derick. 

Tulikaa hapo mpaka Majira ya usiku Derick alikuwa bado hajazinduka, tukiwa tumetulia tulishtuka kumsikia akipiga chafla, kwa kuwa Mimi ndie nilikuwa karibu yake Nilimuwahi na kumshika Ila Amanda alikuja akanisukuma na kumshika yeye, wengi walimshangaa ila wakapotezea ndipo Zakayo akasema: ndugu zanguni kwa wale ambao wamebahatika kuwa na kasimu kumbukeni kale kamuziki ka diamond na inno's Bella mukaweke kwenye emergency. 

Sote Tulicheka maana alibadiri sauti. 

Derick alijitahidi akakaa kisha akatuuliza: hapa nipo wapi? 

Tulishtuka maana tulihisi Labda atakuwa amepoteza Kumbukumbu ndipo Nikamuuliza: mimi ni Nani? 

Derick: wewe ni mpenzi Wangu.

Wote waligeuka kunitazama kwa mshangao Mpaka Amanda mwenye ndipo nikasema ili kujitetea: atakuwa hayupo vizuri huyu Ndo maana neno linalokuja Ndo anaongea. 

Tulifurahi kumuona Derick ni mzima tena ndipo Rodrigo akamuuliza: muda ule ilikuwaje Baada ya wewe kumezwa na nyoka? 

Derick: aisee ni  Mungu pekee ndie kanipigania maana alivyonimeza ni kama vile niliingiwa na nguvu za ajabu kile kisu Najma alikuwa amenipa nilimchana kwenye mfumo mzima wa kupumulia sasa ukiniuliza baada ya hapo kilitokea nini sijui kweli. 

Profesa Rodrigo akasema: Duh! una bahati Sana, inaonekana ulivyomchana alikosa pumzi maana alikutema kisha akaturushia Sisi damu. 

Derick: najuta kuja huku.

Alinitazama na kuniuliza: Upo Salama wewe? 

Kabla sijamjibu Zakayo akasema: mbona unamjali Jali sana?

Joyce akadakia: Eee ni wapenzi Upo? kama Ndo ulitaka umtongoze Najma Utalamba lolo.

Zakayo: Mmmhhhh naanzaje kwamfano hata hayo mashahili ya kumtongoza nayatoa wapi kwenye balaa hili! Msione tunatembea Wengine Tukifika dar es salam tunapelekwa kwenye hospital ya vichaa. 

Wengi walicheka Muda Huo mimi nilikuwa namtazama Derick simshibi maana tumaini ya kumuona tena Ilikuwa imepotea, ndipo Rodrigo akamuuliza: Ramani umefanikiwa kuja nayo? 

Derick: muda ule Mbwa mwitu walipokuwa wananikimbiza sijui ilikuweje kuhusu Ramani maana nilikuwa nayo mkononi.

Wote tuliishiwa nguvu ndipo Amanda akasema: sasa tunafanyaje? 

Dominic: tusonge mbele tuufuate huu mto nahisi ndo mwenyewe. 

Tulishangaa na kumuuliza: huu mto Derick aliokuwemo? 

Dominic: Ndio, tupumzike mchaka mchaka kesho. 

Joyce alinyanyuka na kusema: Rodrigo twende kuzunguka kwanza. 

Nikamuuliza: bado mna moyo wa kuzunguka zunguka? 

Joyce: hatukawi. 

Joyce na profesa Rodrigo walitoka maeneo hayo wakatuacha hapo,  ukweli baridi iliopo ndani ya msitu Huo aisee sikuwahi kuskia, usiombe ikafika usiku,  watu wote walikuwa wanatetemeka mno kutokana na baridi kuwa nyingi. 

Nikiwa nimejikumbata imani yangu lazma mdogo wangu ntamuona tena akiwa yupo kwenye Hali yake nzuri.

Upande wa Joyce na mpenzi wake walikuwa wanapiga story za Kawaida kuhusu wakitoka hapo wataenda kuoana.

Wakiwa wapo hapo alitokea Latina nyuma ya Joyce Ila hawakuweza kumuona ndipo Joyce akasema: mpenzi Wangu naomba Usije kunisariti. 

Ukimya ulitawala maana Rodrigo alikuwa amejificha kwenye mti flani ili wacheze kombolewa ndipo Joyce akamuita kwa hofu: Rodrigo!!

Joyce alipogeuka nyuma aliona mtu akiwa amesimama akahisi Labda ni mpenzi wake bila kujuwa ni Latina maana giza ilikuwepo ndipo akashusha pumzi na kusema: usiwe unanitisha hivo twende mi nimeanza kuogopa. 

Rodrigo aliposkia mpenzi wake anaongea Kama vile kuna mtu anamuambia, alijitokeza na kusema: Kumbe muoga Sana? 

Joyce alishtuka huku akiwa anajiuliza huyu ambae kamshika begani ni Nani? Bila kupoteza muda akageuka kumtazama Rodrigo, kwa sauti ya juu akasema: tukimbie!!! 

Kabla Joyce hajapiga hatua yoyote latina aliingiza mkono wake wenye kucha ndefu ndani ya mgongo wa Joyce, ikampelekea Joyce kuganda huku akiangaliana na mpenzi wake kwa jicho la mwisho bila kujuwa.

Rodrigo aliendelea kushangaa ndipo Joyce kwa sauti ya Chini mno akamuambia: Kimbia. 

Damu zilianza kumtoka Joyce mdomoni, Rodrigo alipoona hivo aliamua kukimbia ili kuokoa maisha yake. 

Upande wetu tukiwa tumetulia profesa Rodrigo alifika huku akihema vibaya mno, bila kupoteza muda tuliamka fasta na kuanza kuulizana kuna nini kinaendelea, kabla hajaongea chochote Latina alitokea mbele yangu na......................................Huku nikiwa namuangalia machoni, vile vile na Yeye akiwa amenikazia macho. 



         Unahisi nini kitatokea! 
         Usikose mkasa huu!


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa