MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 13
TULIPOISHIA: Upande wetu tukiwa tumetulia profesa Rodrigo alifika huku akihema vibaya mno, bila kupoteza muda tuliamka fasta na kuanza kuulizana kuna nini kinaendelea, kabla hajaongea chochote Latina alitokea mbele yangu na......................................Huku nikiwa namuangalia machoni, vile vile na Yeye akiwa amenikazia macho.
SONGA NAYO!
Kabla profesa Rodrigo hajaongea chochote Latina alitokea mbele yangu na kunishika shingoni Huku nikiwa namuangalia machoni, vile vile na Yeye akiwa amenikazia macho.
Watu wote walikimbia Ila Derick alijaribu akashindwa kukimbia maana nguvu alikuwa Hana tena, nilipoona latina muda wowote anaweza kuniua nilianza kujaribu kujitetea ila nguvu alizokuwa nazo zilikuwa sio za Kawaida, taratibu nikaanza kuona mawenge, wenzangu waliopoteza maisha ndani ya msitu Huo nikawa na kama vile nawaona ndo nikajua punde si punde nakata moyo, bila kupoteza muda huku mkono wangu wa kushoto ukiwa umemshika mkononi Latina ili Aache kuninyonga nilishusha taratibu mkono wangu wa kulia nikauingiza kwenye mfuko wa suluwali yangu taratibu nikatoa simu ile kuiwasha tu mziki wa inno's Bella na Diamond platnumpz ukajiliza maana tulikuwa tumeseti sehemu yenyewe kabisa.
Kama bahati latina aliniachia nikadondoka Chini na simu yangu ikaangukia pembeni, bila kupoteza muda akaanza kucheza nyimbo ile, sikutaka kupoteza muda nilimfuata derick nikamshika tukaanza kutoka eneo lile, tukiwa tupo njiani nikamuambia: jitahidi tuwahi.
Derick: kwahio ule mziki haujausave ujirudie rudie?
Nikamjibu: nilisevu Ila tatizo chaji inaisha bado asilimia tano simu izime.
Tuliongeza spidi.
Usiku wote kilituishia tukiwa tunatembea tembea tukiwatafuta wenzetu.
Alfajiri upande wa wenzetu walikuwa wamekata tamaa kuhusu Sisi ndipo Amanda akamuuliza Dominic: Mbona hukumpiga risasi Latina?
Zakayo akadakia: angekuwa wewe ungeweza?
Patrick akasema: pale wengi tunakimbia kwa mkumbo unaskia "huyo hapo" hujamuona unakimbia, sasa wewe Amanda upewe hio bastola ungefanyaje kwa Mfano?
Amanda akaanza kulia akisema: Naumia kuhusu Derick.
Sofia akiwa Analia akasema: Najma, Derick, Joyce tumewapoteza kwa siku moja jamani hata Sisi muda wowote tutakufa naogopa sana.
Upande wetu tuliamua kujipumzisha Chini ya mti ndipo Derick akaniambia: wewe ni wa thamani kwangu.
Nikamuuliza: kwa nini?
Derick: wote wamekimbia Hakuna alienikumbuka Ila wewe ukanikumbuka nakupenda sana Najma.
Nilitabasamu na kusema: Kikubwa sote turudi tukiwa hai Halafu mtu anaehitajika kurudi akiwa Salama ni wewe.
Derick: kwa nini?
Nikamjibu: wewe umeyasaidia maisha ya wabongo wengi, Istoshe nchi yetu inajivunia uwepo wako.
Derick: huu msitu una mengi.
Nikamuuliza: ulivyoingia ndani ya tumbo ya nyoka yule ilikuwaje?
Derick: ni marefu.
Nikasema: nimeyaona macho ya Latina, mdogo wangu kwa sasa atakuwa anahangaika sana.
Derick: una nini shingoni?
Nikamuuliza: kuna nini?
Nilipogusa nikaangalia damu zilikuwa zinavuja ndipo Nikamuuliza: kuna nini?
Derick: latina amekuumiza na inaweza kuleta Matatizo mbeleni.
Nikweli damu Muda wote zilikuwa zinatiririka ila nilikuwa sijaona wala kusikia kuwa Nimeumia ndipo Derick alivua begi lake akatoa dawa flani akaniwekea shingoni kisha akaniwekea bandeji na kusema: hii cheni uliitunza sana.
Nilitabasamu na kusema: kwahio ulikuja na vifaa vyako?
Derick: baadhi ya dawa.
Nilimshukuru.
Baada ya masaa kadhaa tulianza kuwatafuta wenzetu huku tukiwaita.
Mvua muda wote ilikuwa inanyesha mpaka tukazowea hali ile, tukiwa tunazidi kusonga huku Derick akiwa ameanza kupata nafuu Tukiskia sauti ya wenzetu Kama vile kuna kitu kimewatokea, fasta tukawafuata.
Tulipowafikia tulimkuta mwenzetu Zakayo akiwa amezama ndani ya tupe huku Dominic akiwa amemshika mkono ili asizame mzima mzima maana alikuwa anaonekana kuanzia kifua kupanda.
Profesa Rodrigo akasema: mtu asiingie kule atazama.
Zakayo akiwa Analia akasema: mnisaidiene jamani.
Dominic akasema: jitahidi sasa na wewe.
Nilipoona Dominic Hawezi kumtoa akiwa mwenyewe na kama vile ameanza kuchoka nilitoa Wazo bila kupoteza muda tukalitendea kazi, Chilunga alimshika kiunoni Dominic akafuatia Patrick, akafuatia Abdul kisha mimi tukaanza kumvuta huku Wengine wakiwa wanatuangalia Kama TV.
Kwa kuwa tulikuwa wengi tulishilikiana kwa Pamoja tukafanikiwa kumtoa Zakayo eneo lile.
Tulijipumzisha huku tukiwa tumelala ndipo Zakayo akiwa amelala akasema: huu msitu Miezi kumi na mbili kuna nyesha Mvua ndo maana kuna sehemu ardhi imeshakuwa laini kama uji sasa vihere here kama Sisi tunaenda bila kuangalia madhara yake Ndo haya.
Tulicheka Licha tulikuwa kwenye balaa ndipo Abdul akanipa mkono na kusema: umetoa Wazo nzuri maana muda wowote mwenzetu tungemkosa kiuzembe, Ndo maana nililia sana nilipokuacha kule.
Nilinyanyuka na kusema: jamani niliobaki na Masimu wallah ndio yatatusaidia.
Sofia: unataka useme na wewe ndo imekusaidia?
Nikamjibu: eeee!!!
Sofia simu yake Ilikuwa imezima kutokana na kunyeshewa sana na Mvua ndipo nikauliza: tumebaki na simu ngapi?
Watu waliokuwa wamebaki na simu ni Patrick na Dominic kasimu Kake kadogo ndipo Nikamuuliza Derick: simu yako vipi?
Derick: chaji imeisha.
Abdul akamuuliza: au Imeharibika kwasababu ya Mvua?
Derick: simu yangu hata niiweke ndani ya maji haiwezi kuharibika.
Nilipomtazama profesa wetu Rodrigo kwa Muda Huo alikuwa amejitenga na Sisi ndipo Nikamuuliza Sofia: Joyce yupo wapi?
Sofia: hatupo nae tena.
Alinipa mkasa wote, aisee moyo uliniuma sana maana Joyce alikuwa ni Rafiki yangu mkubwa, taratibu nilimfuata profesa Rodrigo nikamkuta akiwa anatiririkwa na machizi ndipo nikakaa karibu yake na kusema: yote ni matokeo, vipenzi vyetu, nafsi zetu vyote tutaviacha hapa, Hakuna atakaetoka akiwa ni mzima tafadhali jipe moyo kwa hizi dakika zilizobaki hata wewe utaenda kuonana nae punde si punde.
Profesa Rodrigo aligeuka kuniangalia kisha akaniuliza: una maana gani?
Nikamjibu: mimi Kifo kipo karibu yangu kila nikifumba macho wenzangu waliopoteza maisha nawaona na hio ni ishara mbaya Sana.
Rodrigo: Nisamee Sana, pia msamee Joyce tuliweza kukushawishi ukaja huku Labda angekuwa unamuuguza mama yako na mdogo wako angekuwa yupo vizuri.
Nilitabasamu na kusema: yote tunayoyafanya kwa hii dunia ni Allah pekee anaeyaelewa usijali wala usijilaumu.
Baada ya muda tulikuwa tupo njiani tunaufuata ule mto ile kusonga mbele tukaona kijiji flani ambacho nyumba zilikuwa Kidogo inashangaza ndipo nikasema: kwenye baridi hii kuna binadamu wanaishi huku?
Wenzangu waliomba tusongee tukaangalie ikiwezekana tukaombe msaada, Tulifika ajabu hatukuweza kuona hata mtu hata mmoja, kwa umakini wa hali ya juu tukaanza kuangaza angaza kona zote, ghafla niliskia sauti za watu Kama vile zitakuja tulipo ile kuangalia nyuma aisee kilikuja kikosi cha watu wa fupi aisee hatujapata kuona, wakiwa wameshikilia siraha zao za kiasiri (mkuki) ile kuangalia mbele Wengine wakatokea tukajikuta tunawekwa mtu Kati, aisee walikuwa ni wababa wenye Ndevu zao na vijana walioshiba ila wafupi mno.
Zakayo kwa sauti ya Chini akasema: Hawa ndo wale pygmy wanakula nyama za watu na Kumbukumbu tatizo wanaongea lugha yao hawajui kiswahili hata Kidogo sasa hapa muda wowote tunatengenezwa msosi.
Tuliposkia eti hio ni ile kabila ya ajabu tulishtuka mno huku kila mmoja akiwa anajiuliza tunawatoka vipi Hawa watu?
Unahisi nini kitatokea!
Usikose mkasa huu!
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments:
Post a Comment