Safari Ya Mapenzi - sehemu ya sita 6B - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, December 7, 2019

Safari Ya Mapenzi - sehemu ya sita 6B




Safari Ya Mapenzi - sehemu ya sita 6B
” isack nashukuru sana kwa chakula hiki kitamu.Nashukuru nimekaa na wewe hapa na kujikuta nikiyasahu matatizo yangu yote.Kama nisingekuwa hapa na wewe mida hii ningekuwa nimejifungia mwenyewe chumbani kwangu nikiwa na mawazo mengi sana lakini kwa kunileta hapa umenisaida kuniondolea mawazo mengi yanayokisumbua kichwa changu.” akasema mage
“Usjali mage, nafahahamu hali uliyonayo kwa sasa .Kuhama kutoka katika mfumo mmoja wa maisha kwenda mwingine si jambo rahisi na huwaumiza watu wengi.kama rafiki yako ninafahamu ni hali gani uliyonayo kwa sasa kwa hiyo ni wajibu wangu kuhakikisha kwamba ninakusaidia kwa kila niwezavyo..niasimama pamoja nawe hadi pale utakapokuwa na furaha kamili .”akasema isack
” isack unafanya kazi gani? Mage akauliza
” Mimi ni mtaalamu wa Kompyuta..nimeajiriwa katika kampuni moja inayouza vifaa vya elektroniki.”
” Usinielewe vibaya isack lakini unajua ni kwa nini nimekuuliza hivyo? akasema mage huku akitabasamu
” Kwa nini umeuliza hivyo mage?
” isack nafikiri ungebadilisha kazi”
” Nibadilishe kazi? akauliza isack huku akicheka kidogo
” Ndiyo ninakushauri ubadilishe kazi” akasema mage
” Unanishauri nifanye kazi gani mage? Pengine unaweza ukanishawshi nikajikuta kweli ninafanya maamuzi hapa hapa na kubadili kazi”
” isack ninakushauri ukafanye kazi ya unasihi..”
” hahahaa Unasihi? akasema isack akishangaa kidogo
” Ndiyo Isack.Kazi ile ingekufaa sana kwa sababu una uwezo wa kumshauri mtu akakusikia na kukuelewa.Una uwezo wa kumfanya mtu aliye kata tamaa ya maisha akapata tumaini tena na kurejea katika maisha yake ya kawaida” akasema mage huku sura yake ikionyesha kwamba hakuwa akitania.
” mage sina hakika kama kazi hiyo inaweza ikanifaa.Sijawahi hata mara moja kufikiria au hata kuota kwamba ninaweza kuwa mnasihi.Ninaipenda kazi ya kompyuta its an interesting job and I love it..Kila nikilala ninawaza kompyuta ,nikiamka ninawaza kompyuta.maisha yangu yote yametawaliwa na kompyuta.” akasema isack
” isack nina uhakika mkubwa kwamba unaweza kabisa ukaifanya kazi hiyo ninayokushauri uifanye.Naomba nikwambie kitu ambacho imekuwa ni siri yangu ili uamini kwamba ninayosema ni mambo ya kweli.Baada ya kuachana na yule jamaa yangu nilikuwa katika wakati mgumu sana.Nilikuwa nikijiuliza nitaanzaje maisha yangu mapya.Nilikuwa na mawazo mengi sana na kutokana na mambo aliyonifanyia yule jamaa niliwaogopa mno wanaume .Nilihisi heshima yangu mepormoka kwa kiasi kikubwa sana na sikujua nitairejesha vipi.Nilitamani hata kuhama na kwenda kuishi mbali ambako hakuna mtu yeyote anayenifahamu.Kuna wakati nilijichukia hata mimi mwenyewe na kujiona ni mtu mjinga sana kwa kuamua kumpa mwili wangu kijana muhuni kama yule .Nilikuwa nikitembea lakini hakuna mtu yeyote aliyekuwa akielewa nini ninakiwaza.Ninamshukuru MUngu kwa sababu aliyaona matatizo yangu na akakutuma kwangu na ukanipa maneno machache ya busara ambayo yalinifanya nisipate usingizi usiku ule nikitafakari.Asubuhi nilipoamka nilikuwa mtu mpya.Sikuwa tena yule mage ambaye alikuwa akitembea na
mzigo wa mawazo.Niliweza haya yote kwa sababu yako.Kama umeweza kunisaidia mimi na kunifanya nirejeshe tumaini katika maisha yangu ,basi unaweza ukaifanya kazi hii tena kwa ufanisi mkubwa na ukawasaidia watu wengi wenye matatizo,wenye misongo ya mawazo na waliokata tamaa.” akasema mage na kumfanya isack atabasamu na kusema
” mage nashukuru kwa ushuhuda huo..sasa ninaamini kwamba ninaweza kuifanyakazi hii ya unasihi.Sikujua kama maneno yale machache niliyokuwa nikikueleza kukutia moyo yalikurejeshea tena tumaini na kukufanya uyaanze upya maisha yako.” akasema isack
” isack unaweza ukaifanya kazi hii hata kama hujaisomea.Nakushauri ufungue ofisi na utatengeneza pesa nyingi” akasema mage na kwa sauti ndogo na ya taratibu isack akasema
” Nashukuru sana kwa ushauri wako mzuri mage lakini kumsaidia mtu si lazima akulipe.Kama ningekuwa na muda wa kutosha ningeweza kuifanya kazi hii bila hata kuhitaji malipo ya mtu .Sioni kama ni busara kutumia matatizo ya mtu kutengeneza pesa.Nitaangalia kama nikipata muda kwa siku za usoni ninaweza kufungua ofisi na kutoa bure msaada wa ushauri”
Mage akamuangalia isack usoni kwa sekunde kadhaa na kusema
” isack una roho nzuri sana.Sura yako inaendana kabisa na moyo wako ulivyo.Una moyo wa huruma ,moyo wa kusaida ,moyo wa kujitoa kwa ajili ya wengine.Mwanamke atakayebahatika kuolewa na wewe atakuwa ni mwenye furaha daima” akasema mage na kumfanya isack atabasamu
” Nashukuru isack lakini muonekano wa nje usikudanganye na kukufanya ufikiri kwamba hata ndani ya moyo mtu huyo ni safi.Wapo wanaume wengi ambao wana sura nzuri kwa nje lakini kwa ndani ni wachafu na wanatabia zinazokinaisha”
” isack wewe hauko hivyo..nina uhakika na ninachokisema kwamba wewe ni kijana wa tofauti sana na vijana wengi..Maisha yako,tabia zako na kila kitu chako vinaonyesha ni jinsi gani ulivyo mtu mwema na mwenye roho nzuri.Halafu isack kuna kitu ninaomba nikuulize ..samahani lakini” akasema mage.
” Uliza mage usiogope ”
” isack toka nimehamia katika ile nyumba nikakufahamu hata mara moja sijawahi kumuona mwanamke yeyote yule amekuja pale kwako..Wifi yangu unamficha wapi? Au hutaki tumfahamu? akauliza mage uso wake ukiwa na tabasamu
Isack akacheka kicheko kikubwa kwa swali lile la mage Akachukua kitambaa na kujifuta machozi yaliyomtoka kwa kucheka sana halafu akasema
” mage ni kweli unavyosema .Si wewe peke yako unayeniuliza swali kama hili.Nimekuwa nikiulizwa mara nyingi swali kama hili na watu wengi wakiwemo hata ndugu zangu wakitaka kufahamu kwamba ni lini nitawatangazia habari njema kwamba nina mchumba.mage kusema ukweli ni kwamba nimeamua tu kuishi mwenyewe na si vingnevyo”
” Kwa nini uishi mwenyewe isack.Kijana mzuri kama wewe,una sura nzuri,roho nzuri,una kila aina ya sifa zinazomvutia kila mwanamke na kumfanya akutamani kwa nini uamue kuishi mwenyewe?
” mage nilifanya maamuzi haya baada ya kugundua kwamba sina bahati katika mapenzi.Nimewahi kuwa katika mahusiano zaidi ya mara nne lakini mara zote hizo hakuna raha wala furaha yoyote ile niliyoipta zaidi ya karaha na kuishia kuumiza moyo wangu.Sikutaka tena kuendelea kuumiza moyo wangu kwa hiyo nikaamua kuishi maisha ya peke yangu.”
” Pole sana isack, Mapenzi ndivyo yalivyo.Mapenzi ni kama bahati nasibu kuna kupata na kukosa”
” Kama ni bahati nasibu basi mimi nilikosa.Mara zote niliangukia katika mikono ya wasichana ambao walichokitaka toka kwangu ni fedha na si mapenzi ya kweli hivyo nikaishia kuumia moyo .Baada ya kuumia mara nne nikagundua kwamba sina bahati katika mapenzi na suluhisho hapa ni mimi kujiweka mbali kabisa na masuala hayo ya kupenda.”
” Ouh isack pole sana. Lakini unavyofanya unaona ni sahihi? unautendea haki moyo wako? akauliza mage, isack….akanyamaza
akafikiri kidogo na kusema 


ITAENDELEA 


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa