Safari ya Mapenzi 6A - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, December 7, 2019

Safari ya Mapenzi 6A




ILIPOISHIA…….

” Ninawaza mambo mengi sana isack Ninawaza ni jinsi gani nitakavyoweza kuyatengeneza tena maisha yangu yaliyoharibiwa na yule muhuni.Ninawaza ni kwa namna gani nitaweza kuifuta aibu yote aliyonitia yule kijana.Sikufichi nimepata aibu kubwa sana kwa kuishi na kijana yule.Sikuwa nikifahamu hata kidogo kwamba heshima yangu ilikuwa imeshuka na kupotea kwa kuishi na kijana yule.Najutia sana kupoteza muda mwingi, Najuta sana” akasema mage
” mage ,maisha ni kama darasa ambalo sisi sote tuko ndani yake na tunaendelea kujifunza kila uchao.Kila siku tunajifunza kutokana na makosa tunayoyafanya.Binadamu kukosea ni jambo la kawaida na sote tunakosea lakini kurudia kosa mara ya pili ndilo tatizo kubwa.Tunapogundua kwamba tumefanya kosa tunajitahidi kujirekebisha ili tusije rejea tena makosa.Usiumize sana kichwa kwa sababu tayari umekwisha ligundua kosa ulilolifanya ,kitu cha msingi ni kujitahidi kuyapanga tena maisha yako .Bado unayo nafasi kubwa ya kuweza kuyapanga tena maisha yako.Bado umri unaruhusu na zaidi ya yote bado ni msichana mrembo mno na kwa usiku huu ouh my Gosh ! You are amazing..You are the queen of the night” akasema isack huku akiusogeza mkono wake na kuuweka juu ya mkono wa mage uliokuwa juu meza. Mage akastuka kama vile amemwagiwa maji ya baridi.isack mwili ukamsisimka alipoyakutanisha macho yake na macho ya mage
………………….SONGA…….NAYOOOO……………….

Macho ya mage na isack yakakutana na kila mmoja akajikuta akisisimka.Hakuna aliyekuwa ametegema hali ile kutokea.Waliangaliana kwa sekunde kadhaa isack akafungua mdomo wake na kutaka kusema neno lakini kabla hajasema neno lolote lile akatokea muhudumu akiwa na sinia lililokuwa limejaa matunda.
” Samahani jamani tulisahau kuweka matunda..” akaomba radhi mhudumu yule kisha akaweka sahani ya matunda katika meza na kuondoka.Hakuna aliyetaka kukiongelea tena kitendo kile kilichokuwa kimetokea muda mfupi uliopita ambacho kilionyesha wazi kwamba zilikuwa na hisia kubwa ndani yao.Wakaendelea na kupata chakula kimya kimya.
” Sielewi ni kwa nini hali ile ilinitokea..Hapana ! natakiwa niende taratibu vinginevyo ninaweza nikaharibu kila kitu.mage ni msichana mjanja sana na mwenye akili nyingi.Ili kumpata sitakiwi kwenda haraka.Ameumwa na nyoka muda mfupi uliopita na hivyo yuko makini sana na hataki tena kufanya kosa lingine ….” akawaza isack huku akimtazama mage kwa kuibia.
” Kuna hali ambayo ilimtokea mage wakati nimemshika mkono.Alistuka sana na akashindwa aseme nini.Kwa jinsi alivyoniangalia machoni nina hakika hakuwa amechukizwa na kitendo kile.Sielewi ni kwa nini nilisisimka sana mara baada ya kuushika mkono wa mage. Kadiri muda unavyozidi kwenda ndivyo ninavyozidi kumjua mage na kumpenda zaidi.Ni msichana ambaye anavutia na mwenye kila sifa ya mwanamke mzuri.Laiti angefahamu jinsi ninavyosikia furaha moyoni kwa kuwa naye usiku huu….” akawaza isack akachukua glasi yake ya maji akanywa na kuendelea kula kimya kimya.
Mage alikuwa akila taratibu huku akimtazama isack kwa kuibia ibia.Alitaka kumfahamu vizuri kijana huyu ambaye moyo wake ulimwambia kwamba ndiye anayemfaa katika maisha yake.
” Nilisisimka sana isack aliponishika mkono.Nilihisi kama vile nimemwagiwa maji ya baridi.Nilitamani aendelee kunishika mkono wangu kwani nilijisikia raha ya ajabu sana.Sidhani kama moyo wangu unanidanganya kwamba isack ndiye mtu sahihi kwangu.Nimetokea kumpenda sana na ninaamini kwamba ndiye kijana mwenye sifa za mwanaume ninayemuhitaji katika maisha yangu.”Akawaza mage akiendelea kula huku akiendelea kumchunguza isack kiujanja bila ya isack kugunda kwamba anachunguzwa.
Kwa isack moyo wangu umekubali kuongozwa na akili yangu na kukubal”i kwamba isack ananifaa.Pamoja na moyo kumkubali kwa asilimia mia moja lakini bado ninahitaji kumfahamu zaidi tabia zake za ndani na nje.” akawaza mage na kujikuta akiacha kula na kumtazama isack kwa makini.isack akainua uso wake na kukutana na sura ya mage akimuangalia.
” mage unawaza nini? akauliza isack
” Siwazi kitu isack.Nimekifurahia chakula.You’ve made my night kwa kunileta mahala hapa” akasema mage na kumfanya isack atabasamu.
” mage furaha yako ni furaha yangu .Kama umeridhika na kupafurahia mahala hapa hata mimi nimefurahi pia.” akasema isack
” isack nimepafurahia sana mahala hapa.Kila kitu kilich…………..” mara simu yake ikaita.
” Excuse me isack …akasema mage kisha akaitoa simu yake na kuizima.
” Samahani nilisahau kuizima simu” akasema mage
” Usijali mage….hakuna kilichoharibika” akajibu isack
” Hakuna kilichoharibika lakini si jambo zuri kutoizima simu hasa kwa muda kama huu ambao umetoka na rafiki yako kwa matembezi au chakula cha usiku.Unajua ghasia za simu.Unaweza ukapokea simu ukaambiwa jambo ambalo likaifanya furaha yako yote kutoweka” mage akasema na wote wakacheka.
Walipomaliza kula wahudumu wakafika na kutoa vyombo .isack na mage wakaendelea kupata vinywaji.;;;;;;;;;;;;;;;;; 


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa