Safari Ya Mapenzi - sehemu ya sita 6C - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, December 7, 2019

Safari Ya Mapenzi - sehemu ya sita 6C




Safari Ya Mapenzi - sehemu ya sita 6C
” Sina hakika kama maamuzi haya niliyoyafanya ni sahihi lakini kitu kimoja ninachokifahamu ni kwamba ninaishi kwa furaha baada ya maamuzi hayo.Siumizwi tena na mapenzi na ndiyo maana ninaweza kumpa mtu aliyeumizwa na mapenzi ushauri wenye kufaa kwa sababu ninayafahamu na nimeyapitia mateso hayo…Lakini life is full of wonders.Who knows.. may be someday I’ll meet an angel who can change my mind and make me love again” akasema isack na kumfanya mage atabasamu.
” Natamani malaika huyo ningekuwa mimi.Kila dakika ninayokuwa karibu na isack najikuta nikimpenda zaidi.Hao wasichana waliomuumiza moyo wake waliipoteza bahati kubwa sana.Nitafanya kila niwezalo hadi isack anipende.Anastahili mtu ambaye atampenda kwa dhati na mtu huyo ni mimi.Ni kweli ninampenda sana isack” akawaza mage halafu akakumbuka jambo.
” isack kuna jambo ninataka kukuomba” akasema mage huku akivichezea vidole vyake
” Omba chochote mage niko tayari kukupatia.Hata ukitaka kichwa changu niko tayari kukikata sasa hivi na kukupa” akasema isack na wote wakaangua kicheko.
” isack Ijumaa ijayo kuna sherehe ya kumuaga bosi wetu wa zamani na kumkaribisha mpya kwa hiyo ninakuomba kama hutajali twende wote unisindikize katika sherehe hiyo.Sherehe zote zinazofanyika pale kazini kwetu ni mimi pekee ambaye huwa ninakuwa mwenyewe.Sikuwa tayari kuongozana na yule muhuni katika sherehe zilizojaa watu wa heshima” akasema mage kwa sauti yenye uoga ndani yake .isack akatabasamu na kusema
” Sitajali….mage na nitakusindikiza katika hiyo sherehe.Si katika sherehe tu hata sehemu yoyote ile ambayo ungependa nikusindikize kwako sintakuwa na neno hapana.Siku yoyote na muda wowote niombe chochote nitakuwa tayari kukufanyia.mage you deserve happiness kwa hiyo chochote ambacho kinakupa furaha niko tayari kukupa kama rafiki yako” Akasema isack
” isack nashukuru sana.Namshukuru Mungu kwa kunikutanisha na wewe kwa sababau kuwa nawe karibu kunayafanya maisha yangu yawe rahisi sana kwani nina furaha kubwa moyoni.”
Maongezi yaliyojaa vicheko na utani wa hapa na pale yakaendelea.mage alifurahi kupita kiasi.Hakuwahi kuipata furaha ya namna hii hapo kabla.Alitamani kila siku iwe ni kama usiku huu yaani awe karibu na isack .Saa tatu za usiku wakarejea nyumbani na kuagana kila mmoja akaelekea chumbani kwake.
Mpaka saa sita za usiku bado isack hakuwa ameupata usingizi.Alikuwa akikumbuka usiku huu wa kihistoria kwake.Ni usiku huu ambao aliweza kumsoma vizuri mage Na kugundua kwamba pamoja na uzuri alionao lakini pia ni mwanamke mwenye akili nyingi na uelewa mpana wa mambo.Alizidi kumpenda mage zaidi baada usiku ule.Picha ya mage akitabasamu ikamjia mara kwa mara nakumfanya atabasamu .Wakati bado akimuwaza mage mara ujumbe wa mfupi wa maandishi ukaingia katika simu yake.Ulitoka kwa mage
” isack ninashindwa kupata usingizi kutokana na furaha niliyo nayo leo .isack naomba nikushukuru tena kwa usiku wa leo..You real made my night.Thank you and good night” isack akatabasamu na kurudia kuusoma ujumbe ule tena na tena kisha akarejesha majibu
” Hata mimi nashukuru sana mage kwani nimefurahi mno na kilichonifurahisha zaidi ni kukuona ukiwa na furaha na amani ya moyo.Nafurahi kukuona ukitabasamu na kucheka tena.mage I’ll always be here anytime you need a friend…Sleep tight. Akaubusu ujumbe ule kisha akautuma………….ITAENDELEA……


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa