WADADA HII NI YEENU - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Monday, May 27, 2019

WADADA HII NI YEENU



Umepata bwana umempenda  kweli kweli na umemlalamikia sana eti kwanini hakupeleki kwa wazazi wake kukutambulisha,,jamaa akagoma sana mwishowe akaona isiwe kesi akakupeleka,,,
Wewe badala utake hiyo advantage unafika ukweni umeshinda kutwa nzima unachati,,siku ya pili unachati,,tena ndio unajisifia kwenye magroup,,upo ukweni kumbe wao wanakutazama tu na kukupima na wala hawakwambii kitu,,
Siku ya tatu wanakwambia leo ni zamu yako kupika,,unaingia jikoni unaona kila kitu kigeni,,vya huku unaweka kule(yaani hujui kupika chochote)sufuria umeshika kama umeshika power bank,,unapika na lipstick,,mdomo mwekundu utafikiri mtoto wa jini katoka kufundishwa kunyonya damu,,tena huku umevaa saa na culture zimejaa nusu ya mkono,,umevaa miniskirt kama wafanyakazi wa emirates,,,,,
Msosi wa wakwe hauwezi kupika,,ukiambiwa hufai kuolewa unavuta mdomo utafikiri umenyimwa USB cable ubust smartphone yako,,unaanza kulalamika wakwe hawakupendii,,unalalamika wee,,unashindwa kuelewa kuwa wewe ndo tatizo,,,,,,
Usitake kuolewa ukidhani mume atakuwa anakula chips NA wewe utakuwa unakula pizza kila siku,,jifunze hata kuchemsha chai basi,,au unadhani google wataleta App ambayo unaweka USB kwenye simu yako halafu unaielekezea kwenye sahani inaproduce msosi,,,,,,
JIPANGE DADA USIDHANI NDOA NI KAMA KUPIGA SELFIE,,UTAISHIA KUSEMA UMELOGWA KUMBE MCHAWI NI WEWE MWENYEWE.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa