USISEME HAKUNA WANAUME WA KUOA AU WANAWAKE WA KUOLEWA - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Sunday, May 26, 2019

USISEME HAKUNA WANAUME WA KUOA AU WANAWAKE WA KUOLEWA



Jamii tunayoishi imejaa watu tuliokata tamaa na mbaya zaidi tunawakatisha na wengine tamaa juu ya kupata mwenza wa ndoa na maisha kiujumla,,,,
Unakuta wanaume wanasema hakuna wanawake siku hizi wa kuolewa labda update wa kumpa mimba tu ILI akuletee watoto,,,wanadai wanawake wanapenda pesa tu,,,Wanawake nao wanataka wanaume wa kuwapa mimba tu,,wanadai maisha ya ndoa ni magumu na wanaume wote ni sawa,,
Nadhani wengi wana macho lakini hawaoni,,wengi wana masikio lakini wanasikia habari mbaya tu,,yaani ndoa zinazofungwa kila uchwao halafu wao wanasema hamna waoaji au waolewaji,,,wanaangalia ndoa zilizoharibika badala ya kuangalia ndoa zilizosimama,,
Swali la kujiuliza,,ukiangalia MABINTI,vijana/wanawake ama wanaume unaona nini?unaona mtu anayefaa kuwa mume au mke?au unaona watu kama miti tu?wakati wengine wakiona fursa ya wake wema na wanaume wenye akili katikati ya mazingira yaleyale unayoishi wewe,,kwako wewe ni tofauti kwasababu una mawazo hasi,,
Kama huwezi kubadilisha msimamo na mtazamo wako utaishia kuwaona wengine wakifunga ndoa na kufurahia maisha yao,,kumbi kibao za sherehe zimejaa booking za watu wanaotaka kufunga ndoa kila leo halafu wewe unasema hakuna wa kuoa au kuolewa nae,,,unasema hata wakioana hawawezi kudumu,,hao ni kwa wale wasiojua kusudi la ndoa na wamechagua kushindwa,,
Mungu atupe ndoa yenye amani na upendo kwa wale ambao hatujaingia kwenye ndoa
Ndoa ni muhimu ukimpata mtu sahihi,,omba uliye nae asibadilike,,
Tunatamani kuoa au kuolewa lakini ugumu unakuja kwenye kumjua mtu sahihi na mwenye hitaji la kuishi na wewe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa