NASEMA NA WEWE - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Tuesday, May 21, 2019

NASEMA NA WEWE



NASEMA NA WEWE
Usiyejua maana ya upendo,,kutwa kucha kumfanya mwenzio kama kinanda,,anakulilia wewe una wala hujali thamani ya machozi yame,,siku zako zinahesabika ipo siku na wewe utalia zaidi yake.
NASEMA NA WEWE
Dada usiyejielewa kuwa wewe ni mke wa mtu,,yaani mumeo akitoka na wewe unatoka,,mwanamke kiguu na njia kwa mashoga zako kwenda kuzungumza umbea wa mitandaoni,,chunga sana ndoa yako ipo mbioni kuvunjika,,hao watafuta kiki kwa mitandao hawalijui hilo,,unaivunja ndoa yako kwa mikono yako.
NASEMA NA WEWE
Unaejiita mume wa mtu,,kila siku wewe na Mpira,,umekariri majina ya wachezaji kama kocha wa timu yako,Huna muda na mkeo yaani ukitoka kwenye utafutaji wa riziki moja kwa moja unaenda mpirani,,jiandae kumuona mkeo akichepuka na mtu anayejua thamani ya muda kwenye mapenzi.
NASEMA NA WEWE
Dada unayepoteza muda wako kwenye mahusiano na mume wa mtu,, tambua kuwa kila lenye mwanzo lina mwisho,,sasa wewe jiachie na mume wa mtu ukidhani utakuwa nae daima,,la hasha!unachezewa bure mwisho wa siku anarudi kwa mkewe,,ila tambua machozi ya mwanamke mwenzio hayaendi bure,,utaachiwa laana itakayodumu katika maisha yako yote,,hautapata mwanaume mwaminifu maisha yako yote.
NASEMA NA WEWE
Dada uliyekolea kwenye penzi lisilo na ndoto wala tija na brother man,,sharobaro,,mramba lips,,mwenye kuvaa buti kubwa na jinsi ya kuchanika chanika,,mnyoa viduku,,mvaa vipuri,,muda wote anatembea na self stick na mbaya zaidi anakaa kwao,,nakupa pole sana dada yangu huyo bado mtoto wa nyumba,,hapo halipo hana mbele wa nyuma,,pesa tu ya kununua vocha kuongea na wewe mpaka ampige vizinga dady,,halafu bado unajisifia una mchumba pole sana,,kama anakupenda kwanini asikupeleke kwa wazazi wake,,kila anapokuhitaji mnatumia lodge au aazime ghetto kwa mshikaji,,unajipotezea muda dada yangu achana na huyo mtoto.
NASEMA NA WEWE
Mwanaume unayepachika mimba watoto wa watu halafu unakimbia au kuwatelekeza watoto wa watu,,hiyo damu unayoitupa haipotei bure,,tambua kuwalaghai mabinti na kuwatia mimba halafu unakimbia Mungu anakuona.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa