Hapa siongelei miwani ya jua “Sun glasses” naongelea wanaume wanaovaa miwani hasa wale wanaovaa kwa kuwa na matatizo ya macho,wengine husema ni wanaume wanao onekana kuwa na aibu sana, au wengine huficha makucha yao nyuma ya miwani ile ili waonekane wapole na wenye aibu.
Lakini kuna tetesi kuwa wanaume wanaovaa miwani hii huwa na mvuto wa kipekee mbele ya wanawake na hizi ndizo sababu
Muonekano wa kisomi
Wanawake wengi wanapenda kutoka na mwanaume kaenda shule, elimu ipo kichwani, kuna baadhi ya watu huamini mwanaume au mwanamke anaevaa miwani ni msomi sana, na mara nyingi muonekana wao na miwani huonekana kisomi na wa kuvutia, wapo wanawake wanavutiwa sana na wanaume wanaovaa miwani. Wengine husema wanakuwa na muonekanao wa kiume
Wako Makini na Mambo Yao
Kitu kingine wanaume wa aina hii, huonekana ni watu wasio na michezo na maisha wanapenda maendeleo na wako makini na kazi zao au Biashara, hii humvutia sana mwanamke. Wakiwa kwenye vazi la suti ni kama wanafunga mkataba wa mamilioni, muonekano wao unauza sana.
Wanapendeza (smart)
Wanaume wengi wanaovaa miwani huonekana wako smart mda wote, hasa katika mavazi yao, namuonekano wao mbele za watu, wanawake wengi wanapenda mwanaume anaejua kuvaa vizuri ili asimuaibishe mbele ya watu wake wa karibu.
Ni aina ya Mwanaume Unaeweza Mpeleka Nyumbani
Muonekano wa wanaume wa aina hii, ni rahisi kutambulishwa , wanawake hupenda mwanaume atakaeleta muonekano wa heshima na adabu mbele zawatu na ndugu zake, mara nyingi wanaume wavaa miwani huonekana watulivu na wenye heshima kwahiyo ni raisi kukubalika mbele za watu.
Hawachukizi kwenye Staili yoyote ya Mavazi
Wanaume wa aina hii, wanapendeza na staili yoyote ya mavazi kama ni kuvaa kiofisi, au kawaida kuvaa pensi au jinsi, mtoko wa aina yoyote ni sawa kwao.
No comments:
Post a Comment