Haipiti Wiki Bila Kukwaruzana, Nikikaa Kimya Malalamiko - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Wednesday, March 4, 2020

Haipiti Wiki Bila Kukwaruzana, Nikikaa Kimya Malalamiko






Jamanii mi nna mama mtoto wangu ambaye tunaishi mbalimbali japo sio sana na tupo kwenye uhusiano almost 5 years now

Labda nielezee tabia zetu nikianza kwa upande wangu nna tabia zifuatazo

Sipendi kusikia/kuona mwanamke ananikoromea.
Ni mwepesi kukasirika Lakini ni mwepesi kurudi katika hali ya kawaida
Nina huruma na Nina jishusha pale ninapokumbuka wapi tumetoka na huyo mzazi mwenzangu/Mke wangu( hatujafunga ndoa)

Huyu mwenzangu ana tabia hizi:-

Mbishi sana sometimes hashauriki kwa yale ninayomshauri
Mkimya,ila sometimes ana majibu ya ovyo kwangu
Mgumu kupiga simu kutuma msg,hadi nimuanze Mimi

Sasa katika mawasiliano na kulingana na tabia zetu nlizozieleza hapo juu huwa tunakwaruzana kwaruzana Mara kwa Mara

Sometimes nikikaa kimya bila kumtafuta atapiga simu atatoa lawama nami najikuta nampandishia kwa hiyo tumekuwa watu wa migogoro ya Mara kwa Mara hadi najiuliza je huyu mwanamke hii kazi yake na mshahara wake unampa kiburi hadi awe na jeuri ya kunipandishia/kunijibu ovyo!?anajua nampenda ndo mana ananifanya mtumwa wa kuanza kumpigia simu kila siku!? , nashindwa kuelewa

N.B Nyie wanawake hata kama mna Mali na kuwapa waume zenu vitu mbalimbali ,kama umeshindwa kumpa heshima yake ni sawa sawa na bure,Mwanaume anahitaji KUHESHIMIWA





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa