Ni muda mrefu sanaaa zaidi ya mwaka na sijapata nafasi ya kupitia jukwaa la Mapenzi labda kutokana na ubize au jukwaa la mapenzi kukosa mada za kushawishi na kujifunza kitu Kipya. Mara nyingi sanaaa mimi ni mpenzi wa jukwaa la Habari, siasa, Biashara na uchumi, pamoja na Jukwaa la Afya.
Usiku wa leo nikaona sio mbaya nikapita huku nikajifunza mawili matatu. Baada ya kufungua tu macho yangu yakavutiwa na wingi wa wachangiaji kwenye uzi wa ULISHAWA KULA TUNDA KIMASIHARA? Nimesoma mpaka page ya kumi naa, nikajiona Kweli mimi ni mshamba sanaaa, and I don't regret huu ushamba wangu.
Wanaume wengi wamejisifia jinsi walivyoweza kutembea na mwanamke for the first time tu walipokutana au kupata nafasi ya kukaa pamoja. Hapa ndio kumenifanya kuandika. Unawezaje kua mwanaume ( sio Mvulana) unayejitambua Ukaja mbele ya jamii kutangaza aibu ya mwenzio sababu tu yakuonekana ww mjanja?
Mwanamke aliyeweza kunivulia chupi namuoma ni mtu wa thamani sana kwangu sababu mimi sio mwanaume pekee niliyemtongoza, sio mwanaume pekee Duniani mwenye fedha, handsome au mwenyekujua mapenzi kushinda wengine. Tatunza aibu yake daima kama ishara ya shukrani na Asante sababu aibu yake ni aibu yangu pia.
Kutembea na mwanamke uliyemjua ndani ya siku moja au mbili sio sifa ila inaonesha jinsi gani Ulivyo cheap, aina ya wanawake wako unaotakiwa kuwa nao na ww ni mtu wa vipi.
Kutunza siri ya mwanamke uliyetembea nae ni kutunza Utu wako mbele ya jamii. Mwanaume mwenzio hatakiwi kujua chochote kuhusu mwanamke wako sababu huyo mwanamke hakutaka huyo mtu kujua hata kama hawafahamiani. Kigezo cha kutokufahamiana sio sifa ya kutaja aibu za mwenzio.
No comments:
Post a Comment