Je ni vema wanaume waende haha ndogo wakiwa wamesimama au wameketi? - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Tuesday, February 11, 2020

Je ni vema wanaume waende haha ndogo wakiwa wamesimama au wameketi?

Man at the urinals
Wengi wa wanaume katika nchi za magharibi wamekua wakifundishwa jinsi ya kwenda haja ndogo wakiwa wamesimama.
Katika tamaduni nyingi , watoto hufundishwa kwamba wavulana hukojoa wakiwa wamesimama, huku wasichana wakiwa wameketi msalani au kuchuchumaa.
Lakini hilo limeenea- lakini kwa sasa mtindo huu wa kwenda haja kwa sasa unahojiwa na maafisa wa afya katika nchi mbali mbali.

Wakati mwingine sababu zinazotolewa za kuangalia kuhusu ni vipi wanaume wanapaswa kwenda haja ndogo huzingatia sababu za kiafya na usafi, sababu zinazotolewa zikiwa ni jinsi wanaume wanavyopaswa kwenda kukojoa kwa kuzingatia afya na usafi, lakini sababu nyingine pia zikiwa ni suala la haki sawa.
Kwa hivyo, ni nani yuko sawa? Na la muhimu zaidi, ni njia ipi iliyo bora zaidi kwa wanaume?
Unaweza kuweka vyoo maalum vya wanaume vingi vya mkojo katika chumba kidogo, lakini huwezi kuweka vyoo vya kawaida vingi katika chumba kidogo
Kwa wanaume wengi, kujisaidia haja ndogo wakiwa wamesimama, ni jambo linaloweza kutokua rahisi sana.
Ni haraka pia na ni jambo linaloweza kufanyika kwa haraka: na katika vyoo vya umma kwa mfano huwa hakuna misururu mirefu sana . Wanaume huingia msalani na kutoka bila kuchelewa wakati wote.
Sababu ya kutokuwepo kwa misururu hii kweney vyoo vya haja ndogo za wanaume ni mbili:
  1. Wanaume wanaweza kukojoa haraka na hawalazimiki kutoa nguo nyingi kufanya hivyo, na...
  2. Kwasababu vyoo maalumu vya wanaume huchukua vyumba vidogo, unaweza kuweka vyoo zaidi kwenye eneo hilo hilo dogo.
Lakini maeneo wataalamu wa maeneo hayo maalum ya vyoovya wanaume wanasema jinsi wanaume wanavyosimama katika baadhi ya vyoo hivyo wakati mwingine inaweza kuathiri kiwango cha mkojo wanachokitoa.
Binadamu huhisi haja ya kuachilia mkojo kutoka kwenye kibofu wakati mkojo unapokua kiasi cha theluthi mbili ya kibofu cha mkojo , lakini usijilazimishe kukojoa
Hebu tuangalie jinsi tunavyokojoa. Mkojo wetu hutengenezwa katika figo, ambayo huchuja uchafu na kuutoa nje ya damu.
Hutunzwa katika kibofu cha mkojo, ambayo hutuwezesha kuendelea na shughuli za kila siku- na kulala nyakati za usiku- bila kuwa na wasiwasi sana kuhusu kwenda msalani.
Ingawa kibofu cha mkojo kina uwezo mkubwa wa kutunza kati ya milimita 300 na 600, huwa tunahisi kwenda msalani kuutua unapofikia theluthi mbili ya kibofu cha mkojo.
Kumaliza mkojo kabisa katika kibofu cha mkojo, tunahitaji kuwa na mfumo wenye afya njema katika ya neva, ambao hutupatia taarifa tunapohitaji kwenda msalani, na tunaweza kubana mkojo kama hatuwezi kuutoa mahala fulani.
Wakati tunapokua katika mahala pa kujistiri, mishipa ya kuta za kiuno na kibofu cha mkojo hulegea.
Hapo ndipo kibofu cha mkojo hujikamua na kutoa mkojo nje ya mwili.
Kusimama au kukaa?
Kwa wanaume wenye matatizo ya tezi dume (prostate)kuketi wanapokojoa hupunguza shinikizo la maumivu ya mfumo wa kutoa mkojo
Mtu mwenye afya hapaswi kuulazimisha mkojo kutoka.
Lakini wakati mwingine, wanaume hupata hali ambayo husababisha kupata ugumu wa muda au wa kudumu wa kukojoa.
Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida la Plos One, wanaume wenye majeraha kwenye tezidume - ambayo huvuruga utendaji wa mfumo wa kutoa mkojo- wanaweza kunufaika na kuketi wanapokojoa.
katika baadhi ya vyoo vya umma, kwenda haja ndogo ukiwa umesimama haikubaliki
Utafiti huo ulilinganisha wanaume wenye afya na wanaume wenye matatizo ya mfumo wa kutoa mkojo.
Ulibaini kuwa kwa wanaume wanaougua tezi dume hawapati maumivu makali wanapotoa mkojo huku wakiwa wameketi na kuufanya mchakato wa kukojoa kuwa wa haraka.
Lakini kwa wanaume wenye afya njema, matokeo hayakuonesha tofauti sawa kati ya kusimama na kuketi wanapokojoa.
Kufanya uamuzi unaofaa...
Baadhi ya vyoo vya mkojo vya wanaume hupambwa kwa kipepeo bandia kuwavutia wanaume kujisaidia haja ndogo
Nchini Uingereza, Huduma za taifa hilo za afya huwashauri wananaume wenye matatizo ya kukojoa kutafuta mahala tulivu na kiketi kwenye vyoo vya kawaida ili kupata urahisi wa kutoa mkojo.
Huenda umeishawahi kusikia hadithi zinazosema kuwa kukojoa huku ukiwa umeketi kunaweza kuzuwia mtu kupata saratani ya tezidume au kuboresha maisha ya kingono ya mwanaume - hata hivyo hakuna ushahidi au uchunguzi unaothibitisha taarifa hizi.

Vipi kuhusu vyoo vinavyotumiwa na watu wengi?

Tunachokifahamu ni kwamba taarifa kuhusu matumizi ya vyoo vya umma na usafi wake hasa vinapotumiwa ni wanaume ilijitokeza kuanzia mwaka 2012 nchini Sweden, wakati mwanasiasa nchini humo ambaye alichoshwa na hali ya vyoo vya umma na kuamua kutafuta mbinu mpya ya kuwaomba wanaume nchini mwake kuwafikiria watu wengine wanapotumia vyoo.
Alisema ushauri wake unachochewa na nia yake ya kuboresha usafi na kuhakikisha hakuna mtu anaingia katika vyoo vya umma akiwa na wasiwasi wa kuonwa na watu akiingia.
Mjadala ulipamba moto, na katika nchi za Ulaya- hususan Ujerumani -kuna vyoo vya umma ambapo kukojoa ukiwa umesimama ni marufuku.
Baadhi ya vyoo vina ishara nyekundu kama ya barabarani inayoashiria kumzuia mtumiaji kukojoa akiwa amesimama-lakini wale wanaochagua kuketi mara nyingi huwa huonekana kana kwamba sio wenye tabia za kiume wanaume.
Nyumba za kibinafsi pia zimeathiriwa, ambako wakati mwingine ishara za choo huwahimiza wageni wanaume kuketi wanapokwenda haja ndogo.
Mwaka 2015, kulikuwa na kesi maarufu nchini Ujerumani: ambapo mwenye nyumba alidai alipwe pesa kwa mpangaji ambaye alisema alimuharibia nyumba kwa mkojo wake.
Lakini hatimaye Jaji alitoa uamuzi kuwa njia aliyotumiwa inakubalika kwa utamaduni akisema "mtu kukojoa akiwa amesimama bado ni jambo la kawaida linalofanyika ".




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa