STORY:PENZI LA MJEDA EP 2 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Monday, February 10, 2020

STORY:PENZI LA MJEDA EP 2




Asubuhi nimeamka nimechelewa sana nikaanza kujiandaa haraka haraka ili nisizidi kuchelewa..  Nimemaliza kuvaa nikachukua mkoba wangu yulee mbio kuelekea kazini.. Nikapishana njiani na mjeda kavaa gwanda mm sijamjua yaani nilimpamia maana nlikua nakimbia akasema "angalia unako enda" mm nikiwa nakimbia nikajibu "Polee" nikakimbia mpaka standa yani nahema hatari pumzi kama inataka kukata hivi..

Nimekaa stand karibu nusu saa gari hakuna nikasema leo sijui tasema nini kazini..mda kidogo gari ikaja ilikua ya kugombania nikawahi nikawa napambana wakati wa kusukumana pale nikawa nasukumana na mkaka amevaa gwanda mimi nasukuma ya yeye anasukuma akanizidi nguvu akapenya na mimi nikapenya nyuma yake nikapata siti pembeni yake.. Nikamsalimia akawa amekaa kimya nikasema kwa sauti ya chini kama hutaki kugombania gari raia panda uber..
Paaaaap mtu kanigeukia hivi alafu akasogeza kofia yake juu kidogo namuangalia vizuri.. yule mjeda wa kule nyumbaniii..  akasema "Nimesha kwambia acha kunifata fata" nikajisemea kimoyoni balaa gani tena hili asubuhi asubuhi..

Nikamwambia "kaka umenielewa vibaya mm siko ivo na hutakiwi kumfikiria mtu vibaya bila uthibitisho" akasema "Sihitaji uthibitisho mimi nimekaa kwenye mafunzo miaka mingi kuliko unavyo fikiri na nimefundishwa kila njia ambazo huwa mnazitumia kuwa seduce wanajeshi kama kuna mtu anakutumia mwambie haiwezekani mbinu zenu za kishamba" nikamwambia kwa hasira "Kaka chunga mdomo wako hata kama ni mwanajeshi huna haki ya kunidhalilisha" akasema "Kwanzia kwenye chakula jana usiku kunifata nyuma nyuma ukidhani takukaribisha ndani kunigonga leo asbuhi ukidhani takuwekea umakini na mpaka kwenye gari? Unalipwa kiasi gani?"

Nilishikwa na hasira sana nika kaa kimya maana niliogopa nnaweza kumtukana alafu nikapata matatizo bola nifunge mdomo wangu. Akasem tena "Unaona umekaa kimya huna cha kujibu nyie wasichana Mungu kawapa vi sura vizuri mnavitumia kufanya ulaghai" Nikasema "Konda naomba nishushe kituo kinachofata" hapo nna hasira nna ongea mpaka sauti inatetemeka nikatamani angekua hana izo gwanda nimsuuze mpaka akili zimkae sawa..nikasimama kuelekea mlangoni ila nikaona huyu atajiona ameshinda nikamfata nikasimama nikamwambia "Ukipewa cheo au mamlaka flani unatakiwa uwe na akili pana akili ya kuchanganua mambo ila nakuskitikia tena nahisi hata huko jeshini umeingia kwa connection maana ungekua ume sota mpaka kufika hapo kwa jitihada zako ungekua humble" Nilivo ongea hivo nikahisi moyo mwepesi kama nimetua mzigo japo nilitaka nimpe mitusi ya maana  akacheka akasema "Binti mdomo wako utakuponza" nikimwangalia yani mtu wa rika langu alafu anavo niita binti utadhani ananiziiiidi nikasema "Sawa kijana tajitahidi mdomo wangu usiniponze ndo mana sijakutukana kijana" nikamkazia macho hatari..konda akasema "Dada unashuka au?" Nikasema "Sishuki kwanini nishuke wakati sijafika safari yangu" Abilia wengi wakacheka

Nikiwa nimesimama nikawa nataka nichukue pesa kwenye mkoba ili niandae nauli kabisa..naona mbona helaa siiyoni tena akili inanambia nimeicha kwenye suruali niliyo ivaa jana wakati naenda kusuka nikahisi kama naishiwa nguvu kabisaa konda tamwambia nini na huyu mjeda mpuuzi atanionaje sasa..😯

Nikawa najipapasa yule mjeda akasema "Vipi umepoteza nauli?" Nikamkata jicho nikakaa kimya akasema tena "Sijui utafanyaje mm sina hela ya kukulipia usizoee vibaya" nikamwambia nikatabasamu nikasema "kaka shughuli zangu hazikuhusu mbona mm sikushobokei?" Akasema "kwa wakati huu unatakiwa uwe mpole na uombe well ukisema kaka naomba unilipie labda takufkria" nikakaa kimya ni kweli lakini sasa yeye yanamhusu nini? Mbona ananiabisha kama kuna kitu nimewahi kumkosea??

Mda huo huo konda ndo ana anza kupita kwa abiria kudai nauli dooooh...






No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa