Tukiwa tumekaa tunamsubiri msusi amalize kumsuka mtu na sisi tusukwe si unajua foleni tena za kwa wasusi.. Akapita mkaka mmoja akasalimia "Wazima jamani?" Tukaitikia pamoja "Wazima" akaenda zake.. msusi akasema "Yule kaka kahamia nyumba ya pale juu ni mwanajeshi ana mwili mzuri na sura nzuri aiseeh kama siyo mjeda vile" tukacheka mm nikadakia "unadhani wanajeshi wote wamekomaa wengine wazuri bhn" rafiki angu martha akasema "Hee na unavopenda wanaume wazuri basi hiyo ndo mada yako" nikasema "anayependa mwanaume mbaya nani?" Tukacheka wote..zamu ya kusuka ilifika nikasukwa nikamsubiri martha naye kisha tukaondoka..
Nikaendelea na shughuli zangu kama kawaida. Nimepanga chumba na nna jitegemea. Basi jion imefika nawaza nipike au ninunue chakula naona uvivu kupika nikaamaua niende kununua chakula. Nikavaa kisuali changu na ki tishet nikatoka mpk kwenye kibanda cha chips nikaagiza chips kavu na mishkaki miwili nikawa nimekaa nasubiri.. Baada ya dakika chache akaja yule mkaka mjeda naye akaagiza chakula akawa amekaa anasubiri..akanisalimia nikamjibu mm nikawa busy na cm yangu nachat..
Viazi vikawa tayari nikaulizwa "unakula au unafunga?" Nikasema "Nafunga" nimefungiwa chips zangu bwana najisachi nilipe kumbe hela nimesahau nyumbani..😢 Loooh nikawaza hapa nfanyeje nikisema nimeghairi Tatukanwa hadi nijishangae nikisema nimesahau hela taonekana tapeli sijui nifanyeje..
"Dada vipi mbn umezubaa?" Akanambia yule muuza chips.. Nikamwambia "kaka samahani nlijua nna hela ila nimeisahau nyumbani" akaniuliza kwa hasira "Kwaiyo unatakaje sasa?" Nikasema "Kwangu sio mbali naenda kukuletea hela saiv kaka" akacheka kwa dharau akasema "We dada usini kunguzue unajua,nimeshaibiwa sana kwa style hiyo nataka pesa yangu kabla hujapasuka" Duuh nikaona hapa mambo yashakua mabaya.. nikapata wazo la haraka nikamsogelea yule mjeda alikua ameweka earphone maskion anakula zake chips.. Nikamgusa bega akatoa earphone akanigeukia nikamwambia "Kaka samahani nimesahau pesa nyumbani huyu muuzaji anadhani nataka kumuibia niazime elfu mbili mia tano ukimaliza kula tunaongozana naenda kukupa hela yako" Hakujibu akatoa elfu tano akanipa.. Nikasema Asante nikampa yule muuza chips akanipa chenchi nikamrudishia nika kaa ili nimsubiri amalize nikampe hela yake ila moyoni nasema _Yaani leo nimedhalilika kwa kias kikubwa sana sijui hii aibu taifanyaje_ akamaliza kula akalipa akawa anaondoka.. nikamfata nyuma maana kwanza tulikua tunaenda njia moja..
Nikaona anaelekea njia ya kwake maana si unajua mgeni akihamia mtaa mzima utajua kuna zile "Pale anakaa mwalimu,Pale anakaa Polisi,pale anakaa nani sijui" Sasa kwakua yeye alikua mwanajeshi tushajua mpaka anapo kaa.. kamfata alipo karibia kwake kasimama na mimi nika simama akaniuliza "Unaenda wapi?" Nikamwambia "Nyumbani" akanambia "Huku ndipo unapo kaa?" Nikasema "hapana ila nataka kukulipa hela yako" akasema "Iko wapi? Haya nilipe" nikasema "Huh..Hapa sipo nayo iko nyumbani" akasema "Kwaiyo una uhakika njia unayopita ndo ya kwenda kwako? Maana naona unanifata tu sikuelewi" nikakaa kimya.. Akasema "Michezo hiyo ya kizamani mwanamke hatakiwi kujirahisisha kwa mwanaume..Sina hakika hata kama iyo pesa umeisahau kweli au ilikua ni mmoja kati ya plan zako za kunitega naomba nikwambie tu imefeli.. Pale nimelipa mradi kelele zisiwepo kuwa na akili binti" Kudadeq niliskia moyo unapiga paaaah nikamwambia "Kaka umenilewa vibaya sina maana hiyo" Akaniangalia akatikisa kichwa kama ananisikitikia akaondoka..
Nikijiskia vibaya sana nawaza _Kwaiyo huyu kaka anawaza mimi nilikua namtega? Whoaa siwez kuamini maskio yangu yani ananitamkia maneno hayo wakati mm sikua na nia hiyo mbwa huyo.. Sina uhakika hata kama ni mwana jeshi mwanajeshi gani ana mjudge mtu kirahisi hivyo anauelewa mdogo sana.. kama wanawake wengine wanamshobokea asidhani kila mtu atamshobokea mpumbavu mkubwa huyo_ yaaani njia nzima nilikua naongea peke angu namtukana tu maana alinitia hasira sana na alinikera mno.. Nilishikwa na hasira mpaka machozi yananitoka maana mm sipendagi mtu anaufikirie vile ambavyo sivyo.. Nili mtukana sana..
Nikafika nyumbani nikala zangu nikalala ile kesho niwahi kazini sasa..
Itaendelea...
No comments:
Post a Comment