Leo tutaiangazia khanga nyepesi namna inavyochangia kuleta hisia na hamasa baina ya mke na mume.
Hakika mwili wa mwanamke ni kivutio bora duniani na kila mume hupenda mkewe awe ndo kivutio murua,chonde chonde mwanamke atakikana ajue kubadilika kulingana nawakati pamoja na mazingira,kuna nguo mwanamke atakiwa aivae akiwa chumba na mumewe na kuna nguo mke avae kwajili ya kushindia. Sasa tuitazame khanga nyepesi,bila shaka khanga hii ni vazi bora zana kwa mwanamke wakiswahili akiwa karibu na mumewe huko chumbani,
Khanga ina namna yakuvaliwa na sio kujipachika nayo tu ili uonekanwe kua umevaa laa hasha!! Khanga nyepesi haivaliwi na kitu ndani labda chupi ya nyepesi ya cotton,na ukiivaa ili ilete kashda ni lazima ujue mwendo wa kutembelea dada!! Mwanamke hutakiwi viungo vyako kuvikaza mbele mumeo kama askari akiwa gwaride! Khanga yataka mwendo wa madaha na matao ili maungo yako yamtikise mume alipokaa,hakuna wakati mume hua makini kumtazama mkewe kama pindi mwanamke anapokua kavaa mavazi khafifu kwa stara,ndio maana ukiwa watoka kuoga na hali umevaa khanga basi basi lazima wanaume wakutupie macho,moja ya sifa ya khanga nyepesi ni kukamata mwili na kufanya maungo yako yatikisike kwa tikisiko la kuvutia,na hapo ndo mume hua kihisia a nakwenda mbali kiasi cha kujikuta jogoo anataka kukokorika,hakuna mwanume anaweza kustahamili pindi akiona mikato ya maungo ikipishana ndio maana kwa wajuzi huthamini sana khanga nyepesi maishani mwake, mwanamke hutakiwi kushinda na magauni ya kitenge mbele ya mume. Hata kumtega mume kitandani basi akukute umejilaza na khanga nyepesi kitandani na khanga imekushika vema hapo lazima utaona kijicho cha mume akikutupia.
Mke mshughulishe mume awe anakutazama kila wakati sio mume masaa 3 macho kwenye tv anaangalia sinema ya BENTEHA wala hana mda wa kukutazama hapo jua bibi kuna ulipojikwaa.
Nyumba zakupanga wanachukuliana sana wanaume mara nyingi sababu hua mitego ya khanga nyepesi
No comments:
Post a Comment