PETE YA KIKE Sehemu Ya 27 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Sunday, February 2, 2020

PETE YA KIKE Sehemu Ya 27





Aliongea meneja huyo huku akiwa kama anakazia,.. Na anajua kabisa huyu ni mama yake asha hivyo anataka kufanya fitina kwasababu asha kamkataa kimahusiano....
"lakini boss ndio kaamua kumlipa hivyo,... Hivyo mi naona tumpe tu boss"
Shadya aliongea kumtetea mama surian, lakini sadiki akagoma huku akitoa simu na kusema..
"hapana... Wacha nimpigie,.. Huu uchumi umebana sana hatuwezi kulipa mfanya usafi wa vyoo mshahara wote huu.... Ngoja nimpigie huu mshahara tuupange upya"
Aliongea sadiki huku akilitafuta jina la boss surian.... Wakati huo mama surian analengwa lengwa na machozi kwasababu hana la kusema juu ya hilo, mana hakuingia kwa vyeti vyake, na mbaya zaidi umri wake ndio tatizo la kazi yake... Shadya haamini macho yake kwa kile sadiki anacho kwenda kukifanya...
"boss sadiki, tumlipe tu mwezi huu kisha mwezi ujao tutampunguzia"
"hapana... Afu wewe inaonekana unalijua hili swala... Ngoja boss apokee simu"

ENDELEA.......

Kiukweli familia hii imekumbwa na mitihani ya hapa na pale hususan katika upande wa kuyamudu maisha kwa kupata riziki,.. Mama surian aliokuja kuomba kazi katika kampuni ya mtoto wake ingali hajui kama mtoto wake surian ndie mmiliki wa kampuni hio,... Vigezo vya mama huyo viligonga mwamba kupata kazi katika kampuni hio, lakini alitokea dada mmoja alieweza kumsaidia kwa kumtengenezea vyeti feki ili mama huyo apate kazi katika kampuni hio,.... Jambo hilo liliwezekana na mama surian alipata kazi katika kampuni ya MICCO ambayo mmiliki wake ni mtoto wake wa kumzaa lakini hajui kama ni kampuni ya mtoto wake,...

Swala hilo la vyeti feki alilijua shadya pekee, hivyo hakuna alieweza kujua ufeki wa vyeti hivyo,... Sadiki alimtaka asha kimapenzi lakini asha alikataa na kumtolea nje meneja huyo, hivyo meneja alipokutana na utofauti wa mshahara na kazi ya mama huyu,.. Kutokana na meneja huyo kukataliwa na asha, sasa akaamua kufufua jipu kwa mama huyo,...

"boss sadiki, tumlipe tu mwezi huu kisha mwezi ujao tutampunguzia"
"hapana... Afu wewe inaonekana unalijua hili swala... Ngoja boss apokee simu"

Aliongea sadiki na wakati huo simu ya boss inaita, na sadiki anasubiri simu ipokelewe,...
"eeh hallo boss"
Aliongea sadiki baada ya boss kupokea simu,.. Mama surian alikuwa akitetemeka kwa woga kwani huenda asilipwe mshahara wake,..
"ndio sadiki kuna shida gani"
Aliuliza boss huyo kisha sadiki akaongea
"kuna mfanyakazi mmoja hapa ananipa mashaka boss,... Anafanya usafi wa vyoo na analipwa laki nne na nusu boss"
Aliongea sadiki huku boss akishangaa
"hapana, mfanya usafi w chooni analiwa kitu kama laki mbili hivi na nusu,.. Sasa huyo vipi analipwa hivyo"
"Kiukweli hata sielewi, na ndio mana nikakupa taarifa"
"anaitwa nani huyu mfanyakazi"
"aahhh anaitwa ZUWENA RASHIDI SURIA"
Aliongea sadiki lakini surian akamjibu
"ni kweli huyo mfanyakazi nilimpangia mshahara huo, lakini kitengo chake sio mfanya usafi bwana sadiki,.. Labda umechanganya tu, angalia vizuri"
Aliongea boss surian huku sadiki akiwa hakati tamaa katika maongezi
"sawa, lakini jina la huyu mama, lipo kwenye sekta ya usafi wa vyoo..."
"mbona unasema jina la huyu mama ina maana ni mwanamke mtu mzima"
Aliuliza surian huku sadiki akijibu
"ndio, ni mama mtu mzima... Ina maana boss umeajiri mfanyakazi humjui boss"
Aliongea sadiki kama kuchomekea fulani hivi ili tu mama huyo akose kazi,.. Na wakati huo mama surian analia lakini sadiki hata hana wazo la huruma kikubwa alipize kisasi cha kukataliwa na asha... Wakati huo asha yupo nje akisubiri foleni yake naye aje achukue mshahara wake,
"namjua ila hakuwa mama mtu mzima"
"hapana boss ni mama mtu mzima kabisa hakosi miaka 60 huyu"
"what???, miaka 60?"
"ndio boss"
"amekujaje na kapateje kazi hapo kiwandani na nani kampa kazi"
"boss, mi nadhani hili swala shadya analifahamu vyema mana ndio anawekea mkazo alipwe mshahara wake"
"hebu mpe simu huyo shadya"
Surian alikasirika mno kwa kuskia kuwa yupo mfanyakazi ambaye hajakizi vigezo vya kupata kazi,..
"halo boss"
"shadya, hivi huyu mfanyakazi kapataje kazi hapo"
Aliongea surian tena kwa hasira kidogo
"samahani boss, naomba nipate adhabu juu ya hili"
"hebu mpe simu huyo sadiki"
Shadya alimpa sadiki simu ili aongee na boss
"Hallow boss"
"sadiki"
"naam boss"
"mpe huyo mfanyakazi mshahara wake ila asirudi kazini tena... Sitaki kumuona mana nitachefukwa na kupiga mtu risasi,.. Sawa"
"sawa boss"
"mpe shadya simu"
Surian alipata hasira kali kwa mfanyakazi huyo kuajiriwa katika kampuni yake,.. Surian bila kujua anamfukuza mama yake mzazi,
"shadya?"
"abee boss"
"utawajibika kwa hilo, mishahara yote aliochukua huyo mfanyakazi utakatwa mpaka uishie... Na utaanza kukatwa mwezi huu"
"sawa boss, ila usinifukuze kazi boss"
"sitaki hili swala nilisikie tena... Shenzi taipu"
Aliongea surian kisha akakata simu kwa hasira,

"umeona sasa, unafanya vitu vyako vya ajabu ajabu tu... Haya jipigie mahesabu huyu mama kachukua mishahara mingapi"
Aliongea sadiki lakini hizo ni kusudi zake kisa kakataliwa,...
"lakini boss, ulichokifanya sio kizuri... Niliamua kumsaidia huyu mama aweze kuiisha familia yake,... Sawa nitailipa hio pesa"
Aliongea shadya tena kwa huruma huku akijuta kumsaidia mama huyo kwani ni miezi mitatu kama sio minne toka kampuni hio ianzishwe, hivyo ni mishahara takribani mitatu kama sio minne atakayo takiwa kuilipa shadya ili iwe onyo kwa wafanyakazi wengine.....
"mama, unapewa mshahara wako wote wa mwezi huu, lakini hutakiwi kuonekana tena hapa... Sawa mama"
"sawa baba"
"njoo usaini uchukue mshahara wako"
Aliongea sadiki huku mama akikubali kusaini ili achukue mshahara wake wa mwisho baada ya kubainika kuwa ni mfanyakazi hewa katika kampuni hio

Huku nje riki kafika na kakutana na asha pale kwenye foleni ta kwenda kupokea mshahara...
"hivi wewe, kwanini unidanganye kuwa yule ni mjomba wako kumbe ni kaka yako"
Aliongea riki, mana hasira zake ni kwamba kapewa namba akijua ni mjomba wa asha kumbe ni kaka yake na ni mchumba wa demu anaye mfukuzia, sasa anamlaumu asha kwa kuweka namba yake humo mpaka ikaenda kujulikana....
"wewe nani kakwambia ni kaka yangu"
aliuliza asha huku watu wakiwashangaa
"si nimekwenda kwa mpenzi wangu, akasema eti ni mchumba wake"
"aaahh bwana we niache nikachukue kibunda changu"
"mi nakulaumu kwanini uniletee linamba namba lako bwana... Umenifukuzia ndege wangu bwana... Nunueni simu sio kudandia simu za watu.. Si umwambie kaka yako boss akununulie simu"
Aliongea riki huku akiondoka,.. Lakini ghafla asha anamuona mama yake anakuja kwa huzuni sana...
"mama? Una nini"
Alimuuliza mama yake kuwa kapatwa na nini
"mwanangu, nimejulikana kuwa nimeingia kazini kwa vyeti hewa, kwani umri wangu haukustahili kufanya kazi hapa"
"jamani mama.... Boss hayupo sasa nani kajua hilo"
"meneja sadiki, ndio kampigia boss simu akaambiwa kuna mfanyakazi ana miaka 60"
"mama?? Sadiki huyu huyu anaye nitongoza au sadiki yupi mama"
"huyo huyo mwanangu... Wala sio mwanaume wa kukuoa mama... Bora hata ulivyo mkataa... Wacha nirudi nyumbani, ila asha mwanangu, fanya kazi kwa bidii... Mimi sipo kazini tena kuanzia leo"
Aliongea mama huyo huku asha naye akiangua kilio kwani haamini kiwa sadiki leo kamfukuzisha mama yake kazi,... Laiti wangelijua kuwa huyo ndio mama wa boss wao, sijui ingelikuwaje... Lakini wakati asha kamkumbatia mama yake kama kumfariji, ghafla alikumbuka maneno ya riki kuwa
"Si umwambie kaka yako boss akununulie simu"
Asha alizidi kupata mashaka juu ya hilo, mana riki kaambiwa na faima kuwa alisikia kuwa mtu huyo ndio mmiliki wa kampuni hio,...
"mama, we Usijali, mpaka sasa nina asilimia 60 kuwa hii kampuni ni ya kaka surian, mana kila jambo lazima likae kwenye msitari"
"mwangu, hizo ni ndoto za mchana... Mwanangu surian sijui yupo nchi gani, sijui amelufa au yupo hai... Japo nami nina asilimia 40 za kuhisi uwepo wake lakini sina uhakika"
"mama? Acha nikachukue mshahara wangu twende nyumbani"
"sawa, ila usiongee na huyo mbwa"
Aliongea mama huyo kumuonya asha asiongee na sadiki jambo lolote lile
"sawa mma, kwanza naanzaje kufanya hivyo"

Ikiwa ni nyakati za mchana kweupeee surian akiwa na mkewe ndani ya gari...
"mi naona tushuke twende pale restaurant tukapate lanchi"
Aliongea jini maimuna au maimati huku suria akikubali swala hilo,...

Huku ICC ambako faima Anauza nguo,.. Baada ya kupata namba ya suria amekuwa mtu wa furaha, lakini kila akitaka kuipiga anaogopa kufanya hivyo, mana amemmisi sana mchumba wake na haamini kama leo kamuona kwa picha,... Kila akitaka kupiga anaogopa, japo picha ni yeye lakini hana uhakika kuwa ni surian...
"wacha nikale Kwanza,.. Nikirudi nimeshiba ndio nitapata ujasiri wa kuipiga namba hii"
Aliongea faima huku akitoka kwenda kupata chakula cha mchana,.. Ikiwa ni eneo hilo hilo la mjini kati na hata akina surian pia hawapp mbali sana

"afu mbona unapenda kujificha sana, tokelezea watu wakuone"
Aliongea surian kuwa mkewe anapenda kuwa invisible (kuto onekana)
"surian mume wangu, siruhusiki kuonekana kabla mama mkwe hajaniona"
"duuuuuuu, kumbe ni masharti"
"ndio"
Alijibu maimuna huku safari ikiendelea, na wakati huo surian kavaa ile Bluetusi au Wayalesi (Bluetooth headset or Wireless).. Kile kifaa ambacho kinakaa upande mmoja wa sikio, ili ukipigiwa haina haja ya kutoa simu... Sasa surian kakivaa ili watu wajue anaongea na simu, mana hua watu wanamuona chizi kwasababu anaonekana anaongea mwenyewe, kumbe ana mtu kwa pembeni... Hivyo amekivaa ili aonekane anaongea na simu... Mana mke hataki kujionyesha kwa watu
"pale pana chakula kizuri sana hivyo tulie pale"
Aliongea maimuna huku wakielekea katika mgahawa huo... Lakini sasa mgahawa huo huo ndipo alipo faima akipata chakula cha mchana...

Faima akiwa hana hili wala lile, anakula wali samaki kama kawaida ya wasichana kula wali... Surian akapita hapo hapo mbele ya faima, afu faima hajamuona.... Surian waliketi mahali ambapo pana viti viwili viwili ikiwa na maana mtu na mpenzi wake au mke wake,... Walikaa lakini kiti kimoja kilionekan kutokuwa na mtu lakini kina mtu..
"samahani boss, nahitaji nikuhudumie lakini umekaa mahali pa V.I.P"
Aliongea mhudumu wa mgahawa huo
"una mana gani ukisema V.I.P"
"nina maana kwamba wanaotakiwa kukaa hapa ni mke na mume au mtu na mpenzi wake"
Surian na maimuna wakaangaliana kisha surian akamjibu
"hakuna shida, nipo na mke wangu anakuja muda sio mrefu"
Aliongea surian mana hakutaka kumwambia ana mke hapo alipo, kwasababu Muhudumu atashtuka kuskia kiti hicho kina mtu ingali anaona hakina mtu...
"ok sawa, nikuagizie nini"
"tuletee wali kuku"
"sawa boss"
Basi Muhudumu aliondoka kwenda kuleta chakula,... Punde si punde kafika na vyakula husika,... Basi mke na mume wakaanza kula tena surian analishwa na mkewe lakini hakuna anaye ona swala hilo zaidi ya kumwona surian akipanua tu mdomo na kutafuna...

Sasa huku meza ya pili ambako kakaa faima,... Kumbe alimuona surian kama dakika moja iliopita, lakini sasa haamini kama ni yeye, mana kakaa kibosi bosi sana, ingali kasikia kuwa anamiliki kampuni
"yule ni surian kweli"
Alijiuliza faima, lakini papo hapo akapata akili... Alishika simu yake kisha akapiga,.. Kweli alikuwa ni surian wake, kwani alimwona akishika simu na kuipokea...
"hallow"
Alianza surian,... Faima kwa furaha aliitupa ile simu chini na kumkimbilia surian
"suriaaaaaaaaaaaaaan"
Sasa surian nae kuangalia, waooo ni mchumba wake faima,... Sasa faima anakuka kwa lengo la kukumbatiana, lakini sasa surian anakosa nguvu mana yupo na mkewe hapo alipo... Lakini huezi amini surian aliamka na kumkumbatia faima..... Faima alishindwa kuzuia machozi yaliokuwa mengi katika macho yake,.. Wakati huo maimuna anaangalia tu huo mchezo wa hao binadamu...
"surian baba, ulikuwa wapi? Kwanini unataka kuniua baba"
Aliongea faima huku kumbatia likiwa zito kutoka... Surian alikumbuka kuna mkewe hapo na surian anamuona mkewe yeye peke yake na si mwingine,...
"nilikuwepo mbona"
"surian mume wangu... Kiukweli leo nina furaha mpaka nalia"
Aliongea faima, lakini surian alikuwa mpole kujibu kwani yupo jirani na mkewe,...
"usijali faima, naomba nikutafute kwa wakati mwingine"
Aliongea surian mana anajua pale hapafai kuongea mambo yao, ila sasa faima hajui....
"hapana surian, kwa sasa siwezi kukuacha a abadan mpaka kufa kwangu, nitalala kwako nitakula kwako, aitaki nikuache tena baba"
Aliongea faima kisha akakalia kile kiti ambacho maimuna au maimati kakalia... Surian alitoa macho mana yeye ndio anaona kuwa faima kakalia mtu, sasa atamtoaje pale...
"mwambie mtu wako kanikalia"
Aliongea maimuna baada ya faima kukalia kile kiti
"ok... Faima, chukua kiti kile pale ukalie, hicho kitakudondosha"
Surian aliongea hivyo ili faima asijue kitu
"hapana,... Huku ni V.I.P, lazima uwe na mweza wako... Nashukuru tumekutana"
Sasa kila neno analo ongea faima,.. Maimuna anaumia sana katika moyo na kujiona labda hana haki kwakua yeye ni jini...
"surian mwambie mtu wako kanikalia bwana alaaaa"
Aliongea jini maimati na hapo anaye sikia ni surian peke yake...
"faima vuta kiti ukae"
"mume wangu... Ina maana kwa sasa hutaki niwe karibu yako"
"sina maana hio faima..."
Sasa maimuna anazidi kuumia mana kakaliwa na mwanamke mwenzie afu ni lika lake, na vile faima ana umbo matata, basi na uzito umezidi...
"surian, narudi tena mwambie kanikalia... Na asipo amka nitamuadabisha mana kaingia anga zangu vibaya"
Aliongea jini maimuna kana kwamba kakasirika baada ya kujua huyo ni mke mwenzie ambaye ni binadamu kama surian.... Sasa surian naye anampenda sana faima, kuliko aumizwe ni bora amwambie ukweli
"faima? nimekwambia uchukue kiti kingine mana hapo ulipokalia umemkalia mtu"






No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa