Mume wangu alikuwa anaweza kutongoza wanawake mbele yangu - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Tuesday, February 4, 2020

Mume wangu alikuwa anaweza kutongoza wanawake mbele yangu


Kaka mimi najua utakua unanikumbuka kwani nilikusumbua sana mwaka jana, mimi ni yule ambaye kila siku nilikua nagombana na mume wangu tunaachana tunarudiana nakupigia, uliniambia kabisa kua mimi siwezi kuwa na amani na mume wangu hawezi kuacha kunisaliti na kuninyanyasa kama sina kazi. Mimi nilikua nakabiashara kadogo tu nyumani ukaniambia hiyo si biashara bali ni sehemu ya kuchukulia pesa ya mboga.
Kaka ulinipa hasira ya kutafuta, nilienda sokoni na kuanza kuuza mchele, nilikua nachagua mchele mzuri napeleka sample kwa majirani, wakiniagiza nawapeleke, nilienda hivyo hivyo nikidunudliza kwa kucheza mchezo mpaka nikapata mtaji wa milioni mbili, nilitafuta na kupata fremu sokoni, kuna mtu alikua na duka alikua anafunga nikainunua, niliwekeza milioni moja tu, nikaendelea kuuza mchele, lakini biashara haikua nzuri ukaniambia kua kwa eneo nililopo pale sokoni niweke M-Pesa.
Ukaniambia badala ya kukaa na pesa keshi basi zikae katika mzunguko. Mwanzoni mume wanngu alikua anona kama nacheza, hakunipa mtaji lakini M-pesa ilichanganya kwani pale sokoni kulikua hamna nikawa napata kamisheni mpaka laki tatu kwa mwezi, nilikua naongeza mtaji sana sasa hivi ninaduka langu nauza nafaka na M-Pesa imebidi kuajiri mtu kabisa. Kaka nina zawadi yako umenitoa mbali na kweli mume wangu ananiheshimu.
Sijui ksma anachepuka kwani nimeamua nisimfuatilie lakini kaka ananiheshimu kama mwanamke, unajua zamani alikua anaweza kuongea na mwanamke mwingine mbele yangu lakini siku hizi hata meseji sioni. Alijifanya hatoi matumizi kwakua eti nina biashara lakini aliisoma namba namimi nilijikausha, aisee kama umenipa ujasiri wa maisha na sasa najua thamani yangu siyumbishwi yumbiswi tena, Mungu akubariki uendelee hivyo hivyo nashukuru hukuchoka usumbufu wangu Mungu akubariki.
NB; Kama huna kazi ya kufanya kama unamtegemea mume wako kwa asilimia mia moja ni vingumu kuondoa au hata kumnunia kwa siku mbili tu kwani njaa ikizidi utanywea tu, kurudi kwenue hiyo si suluhu kwani watakuchoka na kukurudisha, kama unataka heshima tafuta kitu cha kufanya.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa