_
Sherehe ya ndoa ni ya siku moja ila maisha ya ndoa yanaendelea kila siku.... Kila kijana anaetaka kuoa hupenda aonekane bingwa wa mapenzi kitandani lakini yuko zero kwenye mahaba,mapenzi ya kitandani ni ya mda mfupi sana ila mahaba yanataka yawepo masaa 24.
❤Mwanamke anaepata mahaba anakua na furaha sana na hayuko tayari kumpoteza mume huyo,unaweza kuona ni vitu vidogo vidogo sana ila ndivo vitavomfanya mke wako akupende kupita kiasi na atakua maridhia sana. ❤Hebu kua nae siku moja moja msaidie kufanya kazi za nyumbani huku mkiongea na kucheka.
_ ❤Weka siku maalum ya kumkogesha ,chukua taulo mfute maji ikisha mchagulie nguo unayopenda wewe ,anza kumvisha moja baada ya nyengine huku ukimsifu Kwa maneno matamu. ❤Mchukulie zawadi japo ya pipi unaporudi kisha ifungue pipi hio muifyonze Kwa pamoja mpaka imalizike. ❤Unapotoka kwenda kazini muage kwa kumbatio na mabusu huku ukiwa umemuachia ujumbe mzuuri wa mapenzi chini ya mto ama kwenye pochi yake.
_ ❤Mpigie simu ama mtumie ujumbe mzuri mwambie jinsi unavommiss na jinsi unavofurahia ukaribu wake. ❤Pendelea kumsifia kwa uzuri wake na mapishi yake na kila anapokufanyia zuri mpe shukrani.
No comments:
Post a Comment