Maumivu ya Mgongo kwa Mjamzito - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, February 8, 2020

Maumivu ya Mgongo kwa Mjamzito


WAJA-WAZITO wengi huumwa mgongo bila kujua sababu, leo nitaeleza kwa kina nini husababisha tatizo hilo kwa mjamzito.  Uongezekaji wa uzito wa mtoto tumboni, uongezekaji wa maziwa na uzito sehemu mbalimbali za mwili wa mjamzito, kubadilika kwa mwenendo wa mwili, kubadilika kwa mhimili wa mwili, uzito na stress kwenye figo na ugumu wa kuamka na kukaa katika viti na vitanda, husababisha mjamzito kupata maumivu ya mara kwa mara kwenye mgongo.
Hakuna dawa ambayo mama anashauriwa kunywa ili kukabiliana na maumivu yatokanayo na hali hiyo. Hata dawa za kupunguza maumivu kama aspirin na panadol, hazishauriwi kwa mjamzito kutumia. Badala yake maumivu ya mgongo yanaweza kuponywa kwa mazoezi, ulaji wa chakula bora na ushauri mwingine wa kitaalamu. Kuimarisha misuli ya tumbo kwa mazoezi, kukaa na kulala kwenye viti na vitanda vyenye sapoti ya kutosha, inaweza ikasaidia sana kuzuia uzito wa mtoto kuweka presha kwenye mgongo.
Kufanya mazoezi mara kwa mara bila kukosa, kutasaidia misuli iimarike na kuweka mhimili wa mwili sawasawa. Kuna mazoezi maalum kwa wajawazito ambayo hupunguza maumivu ya mgongo kama vile yaitwayo cat/cow. Hili zoezi unaweza kulifanya kila siku au pale unaposikia maumivu kwenye mgongo.
Kaa chini na inama ukiweka mikono chini na magoti chini kwenye sakafu. Vuta pumzi kwa ndani, shusha kichwa chini na weka mgongo juu kama paka wafanyavyo. Achia pumzi na weka kichwa chini kisha inua, endelea kurudia zoezi huku ukivuta na kuachia pumzi. Hili zoezi linaweza kufanywa pia ukiwa umesimama. Zoezi la kutwist magoti na kifua (Knee/Chest Twist):
Mara moja kwa siku au pale usikiapo maumivu, lala chali kwenye sakafu na vuta magoti kuelekea kwenye kifua. Nyoosha mikono pembeni, halafu taratibu elekeza magoti upande wa kushoto huku kichwa kikielekea kulia, kaa hivyo kwa nusu dakika huku ukirelax halafu badilisha mwelekeo wa magoti kulia na kichwa kushoto. Fanya hivyo mara moja au mbili. Maumivu yakizidi unaweza kwenda kwa mtaalamu wa massage au chiropractor ambaye anaweza kunyoosha misuli mbalimbali ya mgongo.
VITU VYA KUZINGATIA
Ukilala jaribu kuweka mito ili iweze kutoa sapoti maeneo ya miguu, mgongo na tumbo. Usisimame kwa muda mrefu, kula vyakula vyenye calcium kwa wingi na pata zoezi la kutembea kila siku.
Unaweza kukaa kwenye maji ya uvuguvugu na fanya mazoezi maalum ya ujauzito kuimarisha misuli na kusaidia kuunyoosha mgongo. Vaa viatu ambavyo ni vya flat kwani vitasaidia kukupa balansi na kutoa sapoti kwenye miguu na mgongo vizuri. Kaa vizuri na kutembea kwa kunyoosha mgongo yaani usiegemeze uzito wako sehemu moja.
Vyakula vyenye virutubisho vya calcium na magnesium kama tulivyoongelea kwenye mada zilizopita, vinaweza kuzuia au pia kupunguza maumivu ya mgongo. Magnesium inaweza kupatikana kwenye vyakula kama vile mboga za majani, matunda kama epo, na mbegu za jamii za karanga hasa hasa almonds. Maumivu yakizidi muone daktari au mtaalamu wa afya aliye karibu nawe.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa