KITUMBUA CHA KIHINDI SEHEMU YA TANO (5) - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Wednesday, February 5, 2020

KITUMBUA CHA KIHINDI SEHEMU YA TANO (5)






ILIPOISHIA
Mama yule wa kihindi aligeuza shingo na kumtazama Magosho kwa jicho lililokuwa limelegea utafikiri alikuwa anataka kukata roho jambo ambalo lilizidi kumtisha Kijana wa watu. Kusema ukweli kilichomfanya kuwa na hali mbaya sio kwasababu heti alikuwa ameumizwa na Magosho, bali ni hisia zake za kimwili dhidi ya mtoto wa watu ndizo zilizokuwa zikimchanganya.
“Vipi mama mbona hivyo?” Magosho alihoji huku akisogelea kiti cha Bi.Fahreen. Pumzi yake ikamfikia mama yule wa kihindi na kuifanya hali ya mwanamke wawatu kuzidi kuwa mbaya.
ENDELEA..5
Laiti Magosho angeujua ugonjwa wa Bi.Fahreen wala asingemkaribia. Kwasababu akiwa mbali mama yule alikuwa anapata ahuweni, lakini akimsogelea tu anakuwa hoi taabani bin mahututi.
Magosho akainua mikono yake na kumshika Bi.Fahreen kwenye mashavu kwa viganja vyake. Lengo lake lilikuwa ni kumjulia hali kutokana na kuonekana kuishiwa nguvu. Wakati akimchunguza mama yake yule ghafla alitereza na kudondokea kifuani kwa Bi.Fahreen. Kitu cha ajabu ni kwamba Bi.Fahreen ambaye alikuwa mgonjwa mahututi aliinua mikono yake ghafla na kumkumbatia Magosho halafu akawa anampapasa mgongoni huku akilalamika kimahaba.
“Goso don’t leave I feel good now” alizungumza mama yule kwa lungha ambayo ilikuwa ngeni masikioni mwa Magosho.
Magosho aliitoa mikono ya Bi.Fahreen na kujinasua haraka huku akitetemeka kwa woga na wasiwasi mkubwa uliokuwa umejaa hofu. Akahisi pengine mama yule angemfikiria vibaya, kumbe vibaya hivyo ndivyo alivyokuwa akivitaka mama wa watu wa kihindi.
“Gosooo I need your hug, come close please” (Nahitaji kukumbatiwa Magosho. Tafadhali njoo) Bi.Fahreen alilalamika kwa lugha ya kiingereza pasipo kufikiri kama mtu aliyekuwa akimsemesha alikuwa haelewi kitu. Ingawa alisoma hadi kidato cha nne lakini lugha ile ya ughaibuni ilimpiga chenga, na ndiyo sababu iliyopelekea kufeli mtihani wake wa mwisho na kuambulia sifuri.
“Don’t late Goso, just do quik” (Usichelewe Magosho, fanya haraka) Bi.Fahreen aliendelea kulalamika huku akiwa amejilaza kwenye kiti cha gari.
“Bahati mbaya mama nimetereza” alisema Magosho huku akitoka nje ya gari na kuzunguuka upande wa pili. Alifungua mlango na kusimama nje wakati mama yule akiwa ndani ya gari. Moyo wa Magosho ulikuwa umejawa na wasiwasi kwa hali ya juu. Alijiona ni mkosaji mbele ya mke wa bosi wake. Akawa ameinamisha kichwa chini akifikiria cha kufanya, wazo lililokuwa karibu ni kupiga simu kwa dereva wa nyumbani ikiwezekana akamchukua mke wa bosi wao na kumuwahisha hospitali.
Wakati Magosho akitaka kutoa simu na kumpigia dereva, mawazo ya mtoto Vashal yalimjia Bi.Fahreen. Alikurupuka kama vile mtu aliyekuwa kwenye usingizi mzito. Alikwenda haraka kwenye usukani na kuwasha gari. Tukio lile lilimshangaza sana Magosho. Imekuwaje mgonjwa aliyekuwa mahututi apone ghafla na kutaka kuendesha gari. Akahisi pengine malaria ilikuwa imempanda kichwani mama yule wa kihindi. Akawa amesimama pale pale nje akimtazama alichokuwa anataka kukifanya mke wa bosi wake.
“Tende veve” Bi.Fahreen alitoa sauti kavu baada ya kumuona Magosho ameduwaa nje ya gari.
“Mama unaumwa lakini utaendeshaje geari?” alizungumza Magosho kwa umakini mkubwa.
“Bana Goso, toto yangu iko pekeyake kule suleni” alizungumza mwanamke yule kwa msisitizo.
“Lakini…” Magosho alitaka kuzingumza kitu lakini mwanamke yule alimkatisha.
“Lakini nini bhana Goso veve, iko fanya jeuri sasa enh?” alizungumza mwanamke yule kwa ukali kidogo.
Magosho akaingia ndani ya gari pasipo kuzungumza neno lolote linguine huku akiwa na wasiwasi juu ya hali ya mama yule wa kihindi. Aliamini kwa asilimia zote kuwa mama yule alikuwa mgonjwa na asingeweza kujifanyisha kwasababu haikuwahi kutokea hata siku moja kufanya vitu kama vile
* * *
Zilikuwa zimepita wiki mbili tangu mzee Nakeshiwar aliporudi kutoka safarini Bangladesh kibiashara. Bi.Fahreen hakuwa anafurahishwa na uwepo wa mume wake nyumbani. Alikuwa hivyo kwasababu alimuona ni kikwazo kikubwa cha yeye kupata penzi la mfanya kazi wao ambaye alitokea kuukonga moyo wake.
Usiku Bi.Fahreena akiwa amelala na mume wake bwana Nakeshiwar alijiwa na mawazo juu ya kijana wao wa kazi. Alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuweza kumtoa kwenye mawazo yake lakini alishindwa. Mume wake alikuwa kwenye usingizi mzito akikoroma. Laiti kama mawazo ya mtu yangekuwa yanapiga kelele sidhani kama Nakeshiwar siku ile angepata usingizi kutokana na mawazo aliyokuwa nayo mke wake.
Bi.Fahreen kila alipojaribu kufumba macho, sura ya Magosho ilimjia huku sura hiyo ikiwa imejawa na tabasamu la mapenzi. Kila alichofanya ili kupoteza hali ilikuwa vile vile. Akajishauri kuwa ni lazima aione sura ya Magosho usiku ule ili aweze kupata usingizi.
Mwanamke yule aliinua shingo yake na kumchungulia mume wake ambaye alionekana kuzama kwenye dimbwi la usingizi mzito. Baada ya kuhakikisha hilo Bi. Ahreen alifunua neti na kujichomoa mithili ya ndege aliyeekuwa anatoka kwenye kiota chake.
Alitembea kwa ncha ya vidole ili kuepuka mume wake asije akaamka kutoka usingizini. Ndugu msomaji hebu vuta picha mtu mzima akiwa ananyata kwa vidole kumtoroka mume wake. Sasa aliposhika kitasa tu cha mlango wa chumbani Mr. Nakeshiwar alishituka na kuanza kupapasa kitandani kwa lengo la kumkumbatia mke wake.
Mzee Nakeshwiwar alipopapasa mara kadhaa pasipo kumgusa mke wake, akabaini kuwa mke wake hakuwepo hivyo aliinuka ili kuhakikisha kwa macho yake. Alitupa macho mlangoni na kumuona mkewe amekamata kitasa cha mlango.
Lilikuwa ni jambo la kushangaza sana kwasababu chumba kile kilikuwa kimekamilika kwa kila kitu. Kulikuwa na choo na bafu chumbani mle. Sasa Bi.Fahreen amekutwa amekamata kitasa cha mlango anataka kutoka, Alikuwa anakwenda wapi? Mnh! Watu wana mambo jamani! Ngoja tuone pengine alikuwa anakwenda kufunga milango ya nje, au labda alikuwa anakwenda kufunga madirisha ya sitting room, ngoja tuone.
“Where are you going Darling?” (Unakwenda wapi mpenzi?) alihoji Mr. Nakeshiwar swali ambalo lilimfanya Bi.Fahreen kushituka kwa nguvu kwasababu hakuwa ametegemea kama mwanaume yule angeweza kuamka na kumsemesha.
“No my husband, I’m around” (Nipo mume wangu) alisema Bi.Fahreen. Alichofanya ni kutoa loki ya mlango ule na kuungua kisha akarudi kitandani huku akiwa na fundo la hasira kwenye moyo wake. Alijikuta akimchukia sana mwanaume yule kwa kitendo kile cha kuamka usingizini muda kama ule wa maangamizi. Yote hayo heti kwasababu ya mfanya kazi wao wa ndani. Mfanyakazi mwenyewe Magosho ambaye alikuwa hana lolote alilokuwa analijua juu ya yaliyomo moyoni mwa mama yule wa kihindi.
Bi.Fahreen aliporudi kitandani Mr. Nakeshiwar akamkumbatia ipasavyo mke wake. Ndio hivyo tena mtu chake, asiye na wake akumbatie mto. Kama mtu anataka kukumbatiwa au kukumbatia basi atafute wa kwake hakuna kuzengea zengea vya watu, tena Mungu na awalaani wale wote wanaozengea vya watu, Pumbavuu!
Kitendo kile cha Bwana Nakeshiwa kumkumbatia Bi. Fahreen, alikilaani sana mwanamke yule. Pumzi iliyokuwa ikitoka kwenye tundu za pua ya mume wake alihisi zikimletea joto kali lililomkera na kumsababishia kimuyemuye. Ni ajabu kwasababu siku zote mwanamke yule alikuwa akivutiwa sana na pumzi zile za mume wake. Ilikuwa akilala ni lazima wageuziane pua na mume wake ndipo apate usingizi vinginevyo angehangaita usiku kuha. Lakini siku ile ilikuwa kinyume nakwambia.
Baada ya dakika kadhaa Mr. Nakeshiwar alikuwa amekwisha pitiwa na usingizi. Mwanaume wa watu mwenyewe alikuwa hana tatizo katika suala la usingizi. Alikuwa akikoroma sana kiasi cha kuleta kero kwa mke wake. Siku zote ili Bi.Fahreen apate usingizi wa amani ilikuwa ni lazima asikie sauti ya mume wake ikikoroma. Lakini siku ile sauti ile ilikuwa ikimpigia kelele mama yule aliyekuwa amezama kwenye penzi la House boy wake kama vile alikuwa akisikia sauti ya mashine ya kukatia vyuma
Bi.Fahreen alihakikisha kuwa mzee yule wa kihindi alikuwa hajitambui, aliitoa mikono yake iliyokuwa imemkumbatia na kuiweka kitandani taratibu, kisha akalala kwa dakika kama mbili hivi ili kumsahaulisha mume wake kuwa alikuwa amemkumbatia. Kuna wanawake wabaya jamani yani wakiamua mambo yao wameamua hata ufanye nini hawazuiliki utafikiri majongoo. Sio wote lakini, wanawake wengine wanajielewa bwana.
Bi.Fahreen aliteremka kitandani na kuanza kunyata kama alivyofanya mwanzo, alifanikiwa kufungua mlango wa chumbani kwake na kutoka salama chumbani mle pasipo kumuamsha mume wake. Bi. Fahreen akaendelea kunyata hadi kwenye mlango wa Magosho na kusimama. Mapigo ya moyo wake yakaanza kwenda mbio. Aliinua mkono wake kutaka kushika kitasa cha mlango lakini moyo ulisita na kurudisha mkono chini. Akafanya zoezi lile mara kadhaa huku akijishauri aingie ama asiingie. Akapiga moyo konde na kuamua kufungua mlango ule.
Siku zote Magosho alizoea kufunga mlango wake kwa ndani kila alipolala, lakini siku hiyo alisahau kabisa kufunga mlango. Bi.Fahreen alipobaini kuwa mlango ulikuwa wazi akajikuta kijasho chembamba kikimtoka huku mapigo ya moyo wake yakiongezeka. Aliusukuma taratibu mlango ule na kuingiza kichwa kuchungulia ndani. Loo! Alijikuta akizidi kuchanganyikiwa baada ya kumuona mwanaume aliyekuwa akiutesa moyo wake akiwa kitandani huku amevaa boksa tu kutokana na hali ya hewa ya jijini Daressalaam.
“My God” alijikuta akitamka huku akiuma kucha ya kidole chake cha shahada mdomoni.
Masikini ya Mungu Magosho alikuwa amelala chali na mkono wake wa kushoto akiwa ameuchomeka kwenye nguo yake ya ndani na kukamata vyema mali zake. Kwa mara ya kwanza Bi.Fahreen aliweza kuliona tumbo la kijana yule likiwa wazi bila nguo. Lilikuwa limekaza tofauti na lile la mume wake ambalo halikuwa na mvuto hata kidogo, Bi.Fahreen aliweza kuiona misuli iliyokuwepo kwenye mapaja ya kijana yule ambaye alikuwa usingizini hasikii wala haoni.
Bi.Fahreen akaona hafaidi vizuri, akasogea hadi pale kitandani na kumuinamia Magosho. Hewa chafu iliyotoka kwenye mapafu ya Magosho ilipokelewa kwa furaha na kukaribishwa vyema kwenye pua za Bi.Fahreen.
Magosho alivuta pumzi kwa nguvu na kujinyoosha viungo vyake vya mwili na kuchomoa mkono wake kutoka kwenye hifadhi ya zana zake za kivita. Kisha akaendelea kuuchapa usingizi huku akiwa bado amelala chali. Kitendo cha kutoa mkono wake kiliweza kuruhusu umbo la silaha zake kuonekana kupitia kwenye kitambaa laini kilichotumika kuzisitiri.
Mwanamke yule akajikuta akitetemeka hasa baada ya kuona umbile la vile vitu vya watu ambavyo havikumhusu. Akameza funda kubwa la mate lililosababishwa na tamaa za kimwili. Kwa muda ule mama yule alikuwa amekwisha pagawa na alikuwa tayari kwa lolote ilimradi auridhishe moyo wake.
Bi.Fahreen aliuinua mkono wake wa kuume na kuutazama kwa sekunde chache halafu akawa anaupeleka taratiibu kushika ghala la watu bila ya ruhusa kutoka kwa mwenyewe. Wakati anatua mkono ule akashituliwa na sauti ya mlango wa chumbani kwake ukifunguliwa. Kitendo cha kushituka kilisababisha mkono wake kutua juu ya zana za Magosho kwa nguvu bila kutegemea na kusababisha kijana yule aamke kwa mshituko mkubwa.
ITAENDELEA



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa