KITUMBUA CHA KIHINDI SEHEMU YA 14 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Wednesday, February 5, 2020

KITUMBUA CHA KIHINDI SEHEMU YA 14






ILIPOISHIA
Mr. Nakeshwar aliingia ndani kwa Zawadi na kwenda moja kwa moja kuketi kwenye sofa pasipo kukaribishwa na mwenyeji wake. Zawadi naye alifunga mlango na kwenda kujiunga na mgeni wake.
"Your most welcome Boss" Zawadi alizungumza huku akijiweka kwenye kochi lililokuwa karibu na mgeni wake mpya.
"Sante sana toto zuri, vipi iko problem?" Mwanaume yule alizungumza kwa lafudhi ya kihindi huku macho yake yakiwa kwa Ashura.

ENDELEA….
Mr. Nakeshwar alionekana kuwa na mashaka juu ya uwepo wa Ashura pale ndani. Nafikiri hakuwa ametegemea kumkuta binti yule ndani ya nyumba ile ya Zawadi. Aliketi kwenye kochi lakini ndani ya nafsi yake hakuwa na Amani kabisa.
"Hakuna tatizo, huyu ni rafiki yangu anaitwa Ashura" Zawadi alijaribu kumtoa wasiwasi Mr. Nakeshwar kwa kumtambulisha Ashura.
"Oh Sura!" Nakeshwar alisema kwa bashasha.
"Ashura, huyu ni bosi wangu anaitwa Nakeshwar. Ndio yule niliyekueleza kuwa nafanya naye biashara" Alisema Zawadi.
"Nashukuru kukufahamu boss" Ashura alijibu huku akimtazama kwa woga mzee yule wa kihindi.
"Mimi iko furahi zaidi, iko zima veve?"
"Ndio, mimi ni mzima kabisa"Ashura alijitahidi kuficha wasiwasi wake juu ya mzee yule wa kihindi.
“Ok, good”
“Vipi bosi unaniambiaje” Zawadi alihoji kukatisha zile salamu za Ashura na Mr.Nakeshwar ambazo zilionekana kukosa ukomo.
“Yeah, Lete tumbua bhanaaa” alisema Mr.Nakeshwar huku akiweka mezani brifkesi yake ambayo alikuwa ameketi nayo kwenye kochi kwa kumhofia Ashura.
Ashura aliinuka na kuelekea chumbani huku akiwa amewaacha sebleni Mr. Nakeshwar na Ashura.
“Your so beautiful girl” alizungumza Mr. Nakeshwar huku akiachia tabasamu lililozibwa na midevu.
“Abee” Ashura aliitika huku akionekana hakuwa ameelewa alichokizungumza mzee yule wa kihindi.
“I mean, veve iko zuri sana” Mr. Nakeshwar akafafanua.
“Asante” Ashura alijibu kwa aibu huku akitoa tabasamu la kujilazimisha.
Baada ya dakika kadhaa Zawadi alirejea na Brifkesi nyingine kutoka chumbani na kuiweka mezani ambako kulikuwa na briefcase ile aliyokuja nayo Mr. Nakeshwar.
“Good work” alisema Nakeshwar baada ya Zawadi kuweka brifkesi ile juu ya meza. Ashura alikuwa ametulia akiutazama mchezo ule. Alikuwa na hamu kubwa ya kupata kujua ukweli juu ya kitumbua cha kihindi alichokuwa anakiimba rafiki yake Zawadi pasipo kutoa ufafanuzi kamili.
Zawadi alifungua ile brifkesi na kuiwacha wazi. Ilikuwa imejaa vitumbua, kwa mahesabu ya haraka hara vilikuwa takribani vitumbua hamsini hivi. Mr.Nakeshwar aliokota kitumbua kimoja na kukimega kisha akakikodolea macho kwa makini na kukionja halafu akaachia tabasamu la matumaini.
“Vizuri Zawadi” alisema huku akifunga ile briefcase iliyokuwa imejaa vitumbua na kuvuta brifkesi yake ambayo ilikuwa mezani na kuifungua.
Noti za kitanzania zilizokuwa na thamani ya Elfu kumi zilikuwa zimefungwa kwenye maburungutu na kujaa ndani ya brifkesi ile aliyokuwa ameifungua Mr.Nakeshwar.
Ashura alihisi mapigo ya moyo wake yakidunda kwa kasi baada ya kuona ile minoti ndani ya briefcase ile. Akazidi kuchanganyikiwa na kuto kuelewakabisa juu ya biashara ile ya vitumbua. Akapiga moyo konde na kutulia kuendelea kuusoma mchezo ule.
“Poa bosi” Zawadi alisema na kuvuta ile brifkesi ya pesa, na Mr.Nakeshwar naye akavuta ile iliyokuwa na vitumbua. Walizifunga brifkesi zile kisha kila mmoja akawa amebaki ameshikilia ya kwake yaani wakawa wamebadilishana. Walitazamana kwa sekunde kadhaa kisha kila mmoja aliinua kidole cha mwisho juu kama ishara yao ya ushindi.
Pasipo kuzungumza neno lolote Mr.Nakeshwar alijiinua kutoka pale kwenye kochi na kutoka nje. Zawadi akawa amebakia na Brifkesi yake iliyokuwa imejaa maburungutu ya pesa.
Wakati wote huo Ashura alikuwa ametulia kwenye kiti akiutazama mchezo ule waliokuwa wakiucheza zawadi na mwanaume yule wa kihindi.
“Vipi shost” Zawadi alimgeukia Ashura baada ya kuondoka kwa Mr.Nakeshwar.
“Yaani ndio mmenichanganya kabisaaaa” alisema Ashura huku akikuna nywele zake.
“Kipi kilichokuchanganya sasa?” Zawadi akahoji kwa umakini.
“Hizo pesa ni za nini?” alihoji Ashura kwa umakini mkubwa.
“Ashura bwana maswali yako mwenzangu!”
“Nauliza kweli Zawadi namaanisha” Ashula akazungumza kwa msisitizo zaidi.
“Si umeona nimeuza vitumbua jamani au umeona kuna kitu gani kimetokea hapa?” Zawadi alijibu kwa kumalizia na swali.
“Vitumbua vile haviwezi kuwa na thamani ya pesa yote hiyo” alisema Ashura huku akioneshea kidole ile brifkesi iliyokuwa na pesa.
“Ulivipika wewe?” Zawadi akahoji kwa mkato baada ya kumuona rafiki yake yule hataki kukubaliana na ukweli.
“Mimi sio mgeni wa biashara ya vitumbua Zawadi” Ashura aliendelea kubishana na ukweli ule aliokuwa ameushuhudia.
“Lakini Ashura sijui kwanini umeng’ang’ania kuto kuelewa”
“Kwasababu sielewi!” Ashura akajibu kwa msisitizo.
“Unasema unajua biashara ya vitumbua, umeshawahi kupika vitumbua vya kihindi wewe?” alihoji Zawadi kwa msisitizo.
“Hata kama view vya kihindi au vya kisukuma, bado haujanishawishi”
“Shauri yako, mjini shule” alisema Zawadi na kuingia chumbani na Brifkesi yake iliyokuwa na pesa alizoziacha Mr.Nakeshwar.
*****
Taarifa za ujio wa Rachna binti wa kwanza wa Mr.Nakeshwar na Bi.Fahreen zilipokelewa kwa furaha sana na wazazi hao wawili. Walikuwa wakiwapenda sana watoto wao ambao walikuwa wawili tu kama mboni za macho yao. Watoto hao walikuwa ni Rachna na mdogo wake wa kiume Natal.
Kitendo cha Rachna kusoma mbali na nyumbani kilizidisha mapenzi kutoka kwa wazazi wake ingawa alikuwa binti mkubwa.
Macho ya Magosho hayakuweza kuamini pale alipomuona Rachna na Bi.Fahreen wakitembea maeneo ya Airport  kuelekea pale alipokuwa amepaki gari. Akiwa amesimama huku ameegemea gari na funguo amezining’iniza mkononi, alimkazia jicho Rachna binti wa kihindi aliyekuwa amevalia suruali ya jinzi ambayo ilikuwa imembana ipasavyo na kupelekea umbo lake kuonekana vizuri zaidi, na juu alikuwa amevalia T-shirt nyeupe iliyokuwa na michirizi myeusi kwenye ukosi na kwenye pindo za mikono.
“Mungu wangu!” Magosho alitamka kwa sauti ya chini kisha akazunguuka nyuma ya gari na kufungua buti kwaajili ya kuweka begi la msichana Rachna.
“Gosoo kuje pokea geni bhanaa!” Bi.Fahreen alipaza sauti kumwambia Magosho ambaye alikuwa amesimama nyuma ya gari akiwasubiri.
Magosho hakuwa na kipingamizi zaidi ya kufanya vile ambavyo mke wa bosi wake alimuamuru. Mzigo wenyewe ulikuwa ni begi dogo tu la nguo tena lilikuwa likiburuzwa na matairi yake. Magosho akatembea kwa haraka hadi pale walipofika Bi.Fahreen na binti yake.
“Karibu sana dada Rachna” Magosho alizungumza na kupokea begi lililokuwa likivutwa na Bi.Fahreen.
“Thank you brother, sante sana” Rachna alijibu kwa sauti ambayo ilipenya kwenye masikio ya Magosho na kumfanya ahisi hali fulani tofauti kwenye ubongo wake.
Magosho alipokuwa akiliweka sawa lile begi ili aweze kulivuta vizuri, Bi.Fahreen na Rachna walitangulia na kumuacha nyuma.
“M a m a y a n g u!” Magosho aliendelea kutaharuki baada ya kuona jinsi Rachna alivyokuwa amezawadiwa kamzigo ka uchokozi huko nyuma.
Magosho alivuta begi taratibu kwa kuwafuata nyuma huku macho yake yakiwa yameganda kwa mtoto wa bosi wake. Jamani nyie mwacheni tu Magosho wawatu apagawe, maana huyo Rachna jinsi alivyokuwa mnh!
“Mtoto nyonga!” alisema Magosho kwa sauti ndogo kusifia jinsi hipsi zilivyomfanya binti yule wa kihindi avutie zaidi. Na ukizingatia alikuwa amevaa suruali basi umbo lilikuwa limejichora sawia kiasi cha mtu yoyote yule kuweza kushuhudia baraka alizokuwa amependelewa binti yule wa kihindi, nakwambia utafikiri toto la kisukuma jinsi lilivyoumbika.
“We nimalize tu!” Magosho aliendelea kuzungumza pekeyake hasa alipoona jinsi kale kamzigo ka Rachna kalivyokuwa kakitikisika kwa midundo ya hatua zake. Jamani nyie loooh!
Magosho alisahau kabisa kuangalia lile zigo zito lililokuwa likimvutia siku zote kwa Bi. Fahreen. Pamoja na kwamba Bi. Fahreen alikuwa akidondosha kwa kuyachanganya manyanga lakini kijana Magosho hakuona kabisa siku hiyo. Macho yake yote yalikuwa kwa Rachna.
Bi.Fahreen na Rachna walifika pale kulipokuwa na parking na kufungua milango ya gari kisha wakaingia tayari kwa safari ya kuelekea nyumbani. Rachna aliketi siti ya nyuma na Bi.Fahreen akaketi siti ya mbele kama ilivyokuwa kawaida. Alikuwa akipenda sana kukaa siti ya mbele ili kuwa karibu na kiburudisho chake.
Magosho alipakia begi kwenye buti kisha akaelekea ndani ya gari ambapo aliyekuwa ameachiwa jukumu lake la kuendesha.
“Pole kwa safari mgeni wetu” alizungumza Magosho huku akikunja kona kuiweka gari sawa kwa safari ya kurejea nyumbani Kariakoo.
“Thanks my brother, am home now” alisema Rachna huku akitabasamu.
Magosho alimtupia jicho Rachna kwa kupitia kioo kidogo kilichokuwa pale mbele kwa juu. Tabasamu la binti yule lilizidi kummaliza kijana wawatu wa kibantu. Ulipita ukimya wa dakika kadhaa ndipo Bi.Fahreen akaamua kuvunja ukimya ule.
“Gosoo” aliita Bi.Fahreen pasipo kumuangalia Magosho
“Naam mama” Magosho aliitika kwa heshima na utulivu mkubwa huku akibadilisha gia kwa kupanga na kupangua.
“What! umeniitaje?” Bi.Fahreen alihoji kwa hamaki baada ya kusikia Magosho amemuita mama. Siku zote Bi. Fahreen alipendelea kuitwa majina ya kimahaba na sio mama. Sasa siku hiyo Magosho alimuita mama kutokana na uwepo wa Rachna mle ndani ya gari. Hata hivyo mwanamke yule mtu mzima alionekana kutokujali uwepo wa binti yake na kutaka kuleta masuala yao ya mahaba.
Magosho aligeuza shingo yake kumtazama Bi.Fahreen ambaye siku zote alikuwa anapenda amuite mpenzi, au baby hasa wawapo wenyewe wawili. Na alichukia sana kuitwa mama. Kosa hilo ndilo ambalo Magosho alikuwa amelifanya.
“Usinitazame, umeniitaje?” Bi.Fahreen alisisitiza swali lake huku ametoa macho.
ITAENDELEA



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa