KITUMBUA CHA KIHINDI SEHEMU YA 13 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Wednesday, February 5, 2020

KITUMBUA CHA KIHINDI SEHEMU YA 13






ILIPOISHIA
“Iko problem veve, sauti iko sikika mbaya sana” Nakeshwar aliposikia tu sauti ya Mansoor alihisi kijana yule alikuwa na tatizo.
“Mimi mzima mkuu ila nina jambo nataka kuzungumza na wewe” alisema Mansoor.
“Iko mutu chezea veve?” alihoji kwa umakini.
“Ah…ah..ni kwamba…Aah..” Mansoor alijikuta akipata kigugumizi kuzungumza kile alichokuwa anakikusudia.
“Kama iko mutu chezea veve sema bhana kubha, mimi kuje toa roho yake mara moya” alizungumza Mr. Nakeshwar kwa kujiamini na majigambo ya hali ya juu.

ENDELEA….13
“Naomba unisikilize kwa makini Mr.Nakesh” alizungumza Mansoor kwa msisitizo wa hali ya juu.
“Zungumuza tu bhana kubha hapana problem” Mr. Nakeshwar aliruhusu ma kusikiliza kwa makini ili kuweza
“Ni kuhusu……” Mansoor alishindwa kuendelea
“About what?”
“Ah! unajua mzee nadhani ingekuwa bora kama tungeonana” Mansoori alizungumza kwa upole.
“Ah bhana veve acha mineno yako mingi bhana kubha”
“Usiwaze Mr.Nakeshwar bwana wewe ni wangu” Mansoor alizungumza huku akijichekesha chekesha. Moyo wake ulishindwa kutoa kile kilichomfanya kumpigia simu tajiri yule wa kihindi.
“Sasa bhana Soor….”
“Ndio Nakesh”
“This week iko safari to South Africa” alisema Nakeshwar.
“Vipi mzigo upo tayari?”
“Yes, Zawadi sema Tumbua iko tayari”
“Aisee zawadi ni jembe hapendi utani na kazi, marahii KITUMBUA kipo tayari?”
“Thus why mimi iko penda sana ile toto” alizungumza Mr. Nakeshwar kwa kujitapa.
“Basi nitajitahidi niweze kufika ofisini kwako baadae” Mansoor alizungumza.
“Hapana shaka bhana kubhaa”
“Sawa Mr.Nakesh kazi njema” Mansoor alisema na kukata simu. Alirejesha mkono wa simu mahala pake na kujiegemeza kwenye kiti. Aliinua kiganja cha mkono wake wa kulia na kukipiga kwenye paji la uso huku akijisonya kwa kushindwa kumueleza ukweli rafiki yake. Alijiona ni mtendaji wa dhambi kubwa sana kwa kuto kuzungumza ukweli.
****
Magosho alikuwa amejilaza kitandani kwenye chumba chake huku macho yakiangalia juu ya dari. Kichwani mwake alikuwa akiwaza jinsi ya kuboresha maisha yake yeye na mdogowake Ashura. Ingawa kwa kiasi fulani maisha yao yalibadilika lakini hayakufikia malengo yake.
“Gosooo…” sauti ya Bi.Fahreen ilimgutusha kutoka kwenye lindi la mawazo. Kabla hajajiinua mama yule wa kihindi alikuwa amekwishaingia mle chumbani.
“Vipi Darling” Bi.Fahreen alimsabahi kwa sauti yake ya kubana.
“Shwari” Magosho alijibu kwa ufupi huku akiwa ameketi kitandani na Bi.Fahreen amesimama mbele yake.
“Iko problem?”
“Hapana”
“Mbona iko choka sana?” Bi.Fahareen alizungumza hukua akimsogelea na kwenda kuketi kitandani pamoja na Magosho.
“Hapana sina uchovu wowote?”
“Real?”
“Kweli kabisa”
“Nipe kidogo basi” alizungumza Bi.Fahreen huku akizungusha mkono wake wa kulia mgongoni mwa Magosho na mkono wake wa kushoto akimpapasa mapajani.
` “Lakini si unajua kuwa mzee yupo?” alisema Magosho kwa tahadhari.
“Mr.Nakesh hapana rudi sasa hivi” Bi.Fahreen alizungumza huku akimsukuma kumlaza kitandani Magosho ambaye hakutegemea tukio lile.
“Ngoja kwanza mama”
“What!!” Bi.Fahreen alishituka na kukunja uso kuonesha kukasirika.
“Subiri kidogo”Magosho alijitetea
“Naitaje mimi! Veve iko ita mimi mama?”
“Basi nisamehe” Magosho alijibu kwa upole
“Hapana ita tena mimi mama, sawa?”
“Sawa mpenzi”
“Good, haya nipe kidogo” alisema Bi.Fahreen huku akimpapasa Magosho sehemu za mapajani.
“Hapana mimi namuogopa Mr. Nakesh” Magosho alijaribu kujitetea lakini mama wa kihindi alionekana kutosikia maneno yake. Alichofanya ni kusaula blauzi kwa haraka kisha akarejea kifuani kwa magosho.
Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana kwa Bi.Fahreen, midomo yake myekundu ilikuwa imekwisha nata kwenye midomo ya Magosho. Kama ilivyokuwa kawaida ya kijana yule wa kibantu yaani Magosho, alipokea mashambulizi na punde watu wakawa wamehamia dunia nyingine tofauti na hii tunayoifahamu mimi na wewe ndugu msomaji.
“Oooh!” Magosho alishituka baada ya mama yule wa kihindi kugusa sehemu za magorofa ya Tandale.
“Tulia veve!” alizungumza Bi.Fahreen kwa sauti ndogo huku akiendelea kuchangamkia shughuli ile iliyokuwa imejitokeza kwa dharura.
“D a a a r l i n g…” Ilikuwa ni sauti ya Mr.Nakeshwar iliyosikika kwenye masikio ya Magosho na Bi.Fahreen. Watu wale wawili walitulia kusikiliza tena kwa makini kama masikio yao hayakuwa yakiwadanganya.
“B a b e e e” Sauti ya Mr.Nakeshwar ilisikika tena huku vishindo vya miguu yake vikisikika vikipita mlango wa chumba cha Magosho na kuelekea chumbani kwa Bi.Fahreen.
“Unaona mama!” Magosho alizungumza kwa lawama na wasiwasi mkubwa.
“Shiiiiiii” Bi.Fahreen alimnyamazisha Magosho kisha akateremka pale kitandani taratibu na kunyata kuuendea mlangoni.
Magosho alikuwa ametulia akimtazama mke wa bosi wake alivyokuwa akitetemeka kwa woga huku akijaribu kukwepa balaa lile. Ni mara nyingi sana kijana yule alinusurika kutoka mikononi mwa Nakeshwar. Lakini siku hiyo aliamini kuwa arubaini zake zilikuwa tayari zimekamilika.
Bi Fahreen alipofika mlangoni na kutaka kushika kitasa cha mlango, alishituka baada ya kusikia vishindo vya hatua za miguu ya Mr.Nakeshwar vikielekea usawa ule wa mlango wa chumbani kwa Magosho. Punde kitasa cha mlango ule kilinyongwa na baba wa kihindi akaingia chumbani mle pasipokubisha hodi.
Msomaji nakwambia ilikuwa ni pata shika nguo kuchanika mle chumbani. Kile kitendo cha kufunguliwa kwa mlango kilienda sambamba na tumbo la kuhara kwa Magosho. Ujanja wote na kujitia maufundi kwa wake wa watu ulimuishia. Nakwambia alishindwa kuhimili vishindo na kujikuta akichafua mazingira bila kutegemea.
Kwa spidi ya haraka sana Bi.Fahreen alirudi na kujibanza nyuma ya mlango huku mikono yake akiwa ameiweka mdomoni kuziba pumzi iliyokuwa ikitoka kwa sauti kubwa isisikike na kutiwa mikononi na Mwanaume yule wa kihindi.
Mr.Nakeshwar alipofungua mlango macho yake yakakutana na Magosho ambaye naye alikuwa akihaha pale kitandani huku akiwa amejifunika kwa shuka kuficha aibu ile.
“Vipi veve Goso iko gonjwa?” Mr. Nakeshwar alihoji baada ya kumkyta Magosho ameketi kitandani.
“Leo nimeshinda vibaya sana bosi” Magosho alizungumza kwa kujitetea huku sura ya aibu ikiwa imemtawala.
“Bi. Fahreen kupe veve dawa?”
“Ndio bosi, mama amenipa dawa”
“Hali iko vipi sasa?”
“Kwasasa sijambo kabisa Bosi, naweza kusema nimepona kabisa” alizungumza Magosho kwa sauti ya upole lakini iliyokuwa imejaa wasiwasi.
“Okay, where is mama?” alihoji Mr.Nakeshwar huku akiwa anazunguusha macho yake mle chumbani utafikiri alihisi uwepo wa mali yake katika chumba kile cha wazinzi.
“Mama alikuwa huko nje” alijibu Magosho kwa wasiwasi.
Mr.Nakeswar alituliza macho yake kwa magosho kwa sekunde kadhaa kama vile alikuwa akimsoma. Lakini Magosho naye alijitahidi kuficha hofu yake mbele ya mtu yule aliyekuwa hatari kwa maisha yake hasa kwa wakati ule.
“Leo toto yangu iko kwa njia from Bombay. Go na mama Airpot kupokea yeye” alisema Mr.Nakeshwar huku akiwa amemkazia macho Magosho kuashiria uzito wa maagizo yale.
“Nani Rachna?” Magosho alijitahidi kuficha wasiwasi wake kwa kuuliza swali
“Yes iko fika hapa jioni, mimi iko sehemu kwenda” alisema Mr.Nakeshwar huku akifunga mlango ule na kuondoka kwa haraka pasipo kubaini uwepo wa mke wake ndani ya chumba dereva wao.
******
Ashura alimeza funda la mate na kuitafuna midomo yake, alivuta pumzi na kuzitoa nje kisha akamkodolea macho Zawadi pasipo kuzungumza kitu.
"Ndio, hakuna cha zaidi. Kama upo tayari shoga yangu sema nikushirikishe kwenye biashara" alisema Zawadi huku mikono yake akiikumbatia kifuani na kuwa kama vile amefunga swala.
"Mie sikatai, ila ni kwamba hicho kitumbua unachokizungumzia wewe"
"Kimekufanya nini?"
"Sikijui"
"Inamaana wewe hujui vitumbua?"
"Najua, lakini hicho kitumbua cha kihindi ndicho sikifahamu"
"Na huwezi kukifahamu kama hautakuwa tayari kufanya biashara hiyo"
"Shoga na wewe, inamaana hujui kama biashara ya vitumbua ndiyo inayo niweka hapa mjini?" Ashura alizungumza.
"Wewe unafanya biashara ya vitumbua lakini sio kitumbua cha kihindi" Zawadi naye akazungumza kwa msisitizo kwa kujitapa.
"Na kwa nini mara unasema vitumbua, mara kitumbua?"
"Nasema hivyo kwasababu hicho kitumbua kimoja kinaweza kufanya maisha yako yabadilike kabisa" Zawadi aliendelea kuzungumza kwa msisitizo.
"Mnh!" Ashura aliguna huku akiamini rafiki yake yule alikuwa akizungumza kwa mafumbo mafumbo nab ado hakuwa amefahamu maana kamili ya hicho kitumbua cha kihindi.
"Usigune, unachotakiwa kuniambia ni kwamba upo tayari ama haupo tayari kwa biashara" Zawadi alihoji huku akijitingisha tingisha na mikono yake kifuani.
Ashura alijiinamia kwa muda akitafakari juu ya jambo lile. Moyo wake ulikuwa tayari kabisa kwa kufanya biashara lakini nafsi yake ilisita kwasababu hadi kufikia muda ule alikuwa hajaifahamu biashara yenyewe kiundani.
"Nasubiri jibu, mbona umeinama kama kobe?" Zawadi alimgutusha Ashura
"Hapana Zawadi mie naona sipo tayari kwa biashara hiyo" Ashura alijikuta akitoa jibu pasipo kujielewa.
“Kuzaliwa masikini ni bahati mbaya, lakini kufa masikini ni uzembe wako mwenyewe” alizungumza Zawadi kwa kebehi.
“Unamaanisha nini Zawadi?” Ashura akahoji baada ya kusikia maneno yale kutoka kwa shoga yake kipenzi.
"Utakufa na uimasikini wako mama" Zawadi alizungumza kwa msisitizo ulio mfanya Ashura kujutia jibu lake alilolitoa kwamba hakuwa tayari kufanya hiyo biashara ya kitumbua cha kihindi. Hata hivyo bado moyo wake haukuwa tayari kufanya hivyo biashara ambayo ilikosa maelezo ya kueleweka.
Sauti ya kengere ya mlango wa kuingilia ndani ndiyo iliyowagutusha na kuwatoa mle jikoni. Walipofika sebleni Ashura alikwenda kuketi kwenye kochi na Zawadi akaelekea mlangoni kufungua mlango.
"Woow! Karibu sana Mr. Nakeshwar" Alisema Zawadi baada ya kufungua mlango na kumuona mgeni wake.
"Thaks toto zuri" Mgongaji alijibu baada ya kukaribishwa na kuingia ndani.
Mgeni yule alikuwa ni mwanaume wa makamo mwenye umbo kubwa ambaye alikuwa na asili ya kihindi. Hakuwa mwingine bali kama alivyotajwa na Zawadi, alikuwa ni yule yule Mr. Nakeshwar mume wa Bi. Fahreen yule mama aliyekuwa anachepuka na Magosho kaka wa Ashura.
Mr. Nakeshwar aliingia ndani kwa Zawadi na kwenda moja kwa moja kuketi kwenye sofa pasipo kukaribishwa na mwenyeji wake. Zawadi naye alifunga mlango na kwenda kujiunga na mgeni wake.
"Your most welcome Boss" Zawadi alizungumza huku akijiweka kwenye kochi lililokuwa karibu na mgeni wake mpya.
"Sante sana toto zuri, vipi iko problem?" Mwanaume yule alizungumza kwa lafudhi ya kihindi huku macho yake yakiwa kwa Ashura.
ITAENDELEA



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa