JINSI YA KUMSINGA (KUMCHUA (massage) na KUMSUGUA (scrub) MWENZA WAKO KWA KUTUMIA BIDHAA ASILIA. - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, February 13, 2020

JINSI YA KUMSINGA (KUMCHUA (massage) na KUMSUGUA (scrub) MWENZA WAKO KWA KUTUMIA BIDHAA ASILIA.


_

Basi si kila siku tuwe tunakimbizana kwenye massage lounge,siku moja moja unatakiwa umsugue na kumchua mwenzio nyumba.
_

Oga vizuri kabla ya kuanza shughuli hii, inaweza fanywa kitandani, kwenye mkeka au chini palipo tandikwa vizuri. Unaanza kuusugua mwili wote kwanza kwa kutumia unga wa liwa na unga wa karafuu ulichanganywa na maji ya rose na mafuta ya miski. Sugua mwili mpaka uhisi uchafu na nongo zote zimeisha.Baada ya hapo unaoga nakurudi kwa ajili ya kuuchua mwili.
_

Unaweza chukua mafuta ya mzaituni,ya nazi,ya karafuu,ya ufuta au ya mchaichai unampaka mwili mzima na kuanza kumchua(kummassage) taratibu bila kutumia nguvu,tumia mda mwingi kuchua sehem za mgongoni na kiunoni.Utaendelea kumsinga mpaka utakaporidhika,baada ya hapo shughuli ya kusinga itakua imeisha.
_

Kusugua na kuchua mwili inasaidia kuondoa uchafu mwilini,kupunguza maumivu makali mwilini,inakufanya upate pumziko na kuondoa msongo wa mawazo , kutaiwezesha mishipa ya damu kuwa katika hali nzuri na hivyo kurahisisha msukumo wa damu katika mwili wako.Pia huleta furaha kwa wale wawili wapendanao.





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa