JE HAYA NI MAPENZI!! 96: - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, February 20, 2020

JE HAYA NI MAPENZI!! 96:





Jeff akainuka na kumfata pale kwenye kiti, Sabrina
alionekana kuwa na maumivu ya moyo kwani
alikuwa akilia kwa uchungu.
Jeff alipojaribu kumbembeleza, Sabrina alimtazama
Jeff na kumzaba kibao cha nguvu.
Jeff alijikuta akiwa kama ameganda huku akimtazama tu Sabrina ambapo Sabrina alimnasa tena kibao cha pili na kumuuliza kwa hasira,
"Nani kakutuma unilete huku tena Jeff? Nakuuliza wewe?"
Jeff akatabasamu kwani alijua tayari Sabrina amerudiwa na kumbukumbu zake.
Ila Sabrina alichukizwa zaidi na kile kitendo cha Jeff kutabasamu na kumfanya azidi kulia kwa hasira.
Jeff akamkumbatia sasa kama ishara ya kumbembeleza na kufurahi ile hali aliyonayo ya kurudiwa na kumbukumbu.
Jeff alimkumbatia tu ingawa Sabrina bado aliendelea kulalamika,
"Kwanini Jeff kwanini umenileta tena huku? Kwanini hutaki kuheshimu ndoa yangu?"
"Nisamehe Sabrina, sijakuleta huku kwa lengo lolote baya. Nakupenda sana na nilikuwa nataka urudiwe na kumbukumbu zako"
"Kwani nilipoteza kumbukumbu?"
"Ndio Sabrina, nisamehe kwanza na pia naomba utulie ili nikueleweshe kidogo"
Sabrina akamtazama kwa makini sasa Jeff na   kumuona ana mabadiliko tofauti na alivyokuwa awali.
"Ila saivi Jeff umekuwa mkubwa. Kwani ni kitu gani kinatokea hapa? Mbona sielewi?"
Jeff aliamua kumtuliza kwanza na kumwambia kwa kifupi kuwa alipoteza kumbukumbu kwa miezi kadhaa hata yeye alikuwa hamkumbuki.
"Kweli nilikuwa sikukumbuki wewe?"
"Ndio hukunikumbuka kabisa, na siku niliporudi na kukuona ndio siku hiyo ulishikwa uchungu na kwenda kujifungua"
"Kwahiyo nimeshajifungua?"
"Ndio mtoto wa kiume na amefanana na mimi balaa"
"Hapo ndio unapoanza kunikera sasa"
Akakaa na kufikiria kidogo, akaona kama mambo yamebadilika sana hakujielewa kwa muda huo.
"Naomba nipeleke kwa Sam, tafadhari Jeff"
Jeff alimuangalia kwa kumuhurumia na hakuweza kukataa lile swala ingawa hakuona kama ni vyema kwenda nae moja kwa moja kwa Sam.
"Kwanini tusirudi kwanza nyumbani halafu kwa Sam tukaenda hata kesho?"
"Hapana Jeff, nataka kumuona Sam nahitaji sana nimuone kwanza  hapa sielewi chochote. Tafadhari nipeleke kwanza kwa Sam, kuna kitu nakihitaji"
Jeff akaamua kutoka pale na Sabrina kisha kuianza safari ya kwenda kwa Sam.

Aisha naye alikubaliana na Neema kuwa siku hiyo aende mahali alipomuelekeza kuwa akaitoe ile dawa, na kama alivyokubali hakuona kama hilo ni jambo zito kiasi hicho mpaka kwa yeye kushindwa kulifanya.
Kwahiyo akawa ameondoka nyumbani kwa Neema huku akiwa na maelekezo ya kutosha.
Alienda mpaka alipoelekezwa na Neema huku wakiendelea kuwasiliana kwenye simu ili ikitokea kama atasahau basi amuulize kwenye simu na aweze kumuelekeza tena.

Aisha alifika mpaka kwenye mti ambao alihisi kuwa ndio alioelekezwa na Neema huku akiangalia uwepo wa wapita njia na kujaribu kufanya kile alichoelekezwa.
"Mmh dada Neema aliwezaje kufanya haya karibia na nyumba ya mtu kiasi hiki? Hivi kwa mfano wenyewe wakatoka na kuzunguka hapa na kunikuta nitajiteteaje mimi? Mungu   nisaidie kwa hili ninaloenda kufanya."
Aisha alikaa pale chini ya mti na kukaribu kufukua fukua ili aone kwani alipomuuliza Neema alimwambia ndio hapo hapo.

Sia alikuwa ndani kwa Sam akiendelea na harakati zake za kuchekecha hisia za Sam kwani alikuwa akicheza na kukatika haswa, alipoona kuwa inachukua muda mrefu kumteka Sam akaamua kuongeza sauti ya mziki huku akitoa nguo moja moja kwenye mwili wake.
Sam alikuwa akimtazama tu Sia anavyokatika, na kweli alikuwa akijua kucheza na kwa mwanaume yeyote rijali lazima mate yamtoke kwa kucheza kule tena bila nguo.
Sam akajikuta naye akiinuka na kuungana na Sia katika kucheza huku Sia akitumia nafasi hiyo kumtoa Sam nguo moja moja katika mwili wake.
Ila alipofikia kuitoa nguo ya ndani ya Sam, ni pale Sam akamzuia na kumfanya Sia ajiulize kuwa huyu mwanaume ni vipi kwanini agomee pale? Akahisi kuwa labda manjonjo yake hayakumvutia vizuri na kumfanya atafute pozi la kumvuta zaidi Sam.
Sia hakumvua tena Sam ile nguo ya ndani ila aliendelea kunengua na kucheza kitu ambacho kilimvutia zaidi Sam.
Kwavile Sia alikuwa na makalio makubwa, akaamua kutumia makalio yake hayo kumteka Sam ambapo aliinama huku anamkatikia Sam karibia na nguo yake ya ndani huku akimshawishi afanye kile anachokitaka.
Kwavile Sam naye ni mwanaume, hakuweza kustahimili zaidi hali ile na kumpa Sia anachostahili.

Kelele nyingine leo ilimshtua yule mlinzi wa Sam pale getini ila hakuielewa vizuri kwavile ilichanganyika na sauti za mziki.
Mlinzi wa Sam alijiuliza tu pale bila ya kupata majibu kwani kwa kelele ile ilikuwa ni kama mtu amekutana na kitu cha ajabu ila ni kelele ambayo aliisikia na kukatika gafla huku sauti ya mziki ikiendelea.
Hakutaka kufatilia kwani hayamuhusu na ukizingatia pale yupo kazini.

Aisha naye pale chini ya mti alibahatika kusikia ile kelele na kumfanya ashtuke sana ila hakuelewa chochote kinachoendelea huku akijaribu kuchimba haraka harana na aweze kuwahi kuondoka pale kwenye mti.
Muda kidogo akaona watu wawili wakiwa wameongozana na wanaelekea katika ile nyumba, alikuwa ni mdada na mkaka.
Aisha akaamua kujigeresha na kuacha kuchimba ili hata kama wakimuuliza aseme kuwa alikuwa amepumzika tu ila walipita bila ya kumuuliza chochote.
Aisha alipotazama kwenye kile kishimo anachokichimba kwa kisu, akaona kitu alichoelekezwa na Neema na kukivuta kwani kilikuwa kwenye mfuko ila kilikuwa kikipumua kama mtu na kumfanya Aisha atetemeke sana huku akikiweka kwenye mkoba wake.

Jeff na Sabrina walimkuta mlinzi wa Sam kama kawaida ambaye alikuwa tu akimshangaa Sabrina na kumuuliza,
"Unaendeleaje dada?"
"Naendelea vizuri, Sam yupo?"
Mlinzi alikuwa akiitikia kwa kusitasita na kumfanya Sabrina ampite pale getini na kuanza kufata nyumba huku Jeff akiwa nyuma yake.
Sabrina alishangazwa  na ule mziki mkubwa aliousikia kutoka ndani kwa Sam na kushangaa sana kwani si kawaida ya Sam kusikiliza mziki mkubwa kiasi kile.
"Yani kama disko"
Huku akiendelea kuufata mlango.

Sam alimuhurumia sana Sia ila tayari ilishatokea hapakuwa na jinsi tena zaidi ya kuvaa nguo zake na kumsitiri Sia kwa kumfunika shuka kwani alikuwa amekaa huku akilia sana yani Sia hakuamini kile kilichompata kwa siku hiyo na kumfanya ahisi kupagawa huku akiwa na maumivu makali kwenye sehemu zake za siri.
Alilia sana na hakutaka hata kumtazama Sam,
"Tafadhari Sia usimwambie mtu yeyote"
Sam alikuwa akimbembeleza Sia huku amemshika bega, ila Sia aliurusha ule mkono wa Sam pembeni na kusema kwa ukali,
"Niache shetani mkubwa wewe"
Sia alichukua blezia yake na kuvaa, alipoinuka pale alipokaa alishangaa kuona pametapakaa damu na kujigundua kuwa lazima ameumizwa kupita vile anavyofikiria.
Akachukua nguo yake ya ndani na kuvaa.
  Gafla wakashtuka mlango wa sebleni ukifunguliwa ndio Sam alipogundua kuwa hakuufunga mlango ule.
Macho ya Sia yakagongana na macho ya Sabrina ambapo Sabrina alimuangalia Sia kwa mshangao kwani Sia alikuwa na nguo ya ndani tu na ile blezia aliyovaa mwanzoni.
Sabrina akamwambia Sia kwa ukali,
"Sia!! Unafanya nini kwa mume wangu?"
Kisha akamuangalia Sam na kumwambia,
"Kumbe Sam nisipokuwepo ndio huwa unanifanyia hivi?"
Sam aliona aibu na kuinamisha macho chini, Sia naye aliona aibu ukizingatia kitendo alichofanyiwa na kumuona Sabrina mbele yake haikuwa rahisi kwake, alijikuta akijifunga lile shuka kwa aibu na kutoka mule ndani bila ya kuongea chochote.
Ila alipofika mlangoni, Sabrina akamvuta Sia na kumnasa kibao,
"Malaya mkubwa wewe, kuja hapa"
Sam akaona hii itakuwa khatari ukizingatia tayari Sia ameshapata pigo kama lile, ikabidi ainuke na kumshikiria Sabrina kisha kumwambia Sia achukue vitu vyake na kuondoka.
Alitoka nje na shuka huku akilia sana hata mlinzi wa Sam alimshangaa huku akiamini kuwa Sabrina atakuwa kamfanya kitu tu kwani ishakuwa kawaida yake ya kupambana na wadada wanaotembea na Sam.
Sia alishachanganyikiwa tayari, alitoka hadi nje na kukosa muelekeo kisha akarudi na kumuomba yule mlinzi wa Sam amuitie gari za kukodi.

Aisha aliyekuwa anakaribia kuondoka pale alishangaa kumuona Sia akiwa kajifunga shuka tena akionekana kuwa amechanganyikiwa na kupoteza muelekeo, kisha akamuona akirudi tena na kuamua kumfata na kumkuta akizungumza na yule mlinzi kisha akamshtua,
"Sia"
Sia akashtuka na kugeuka, akamuona Aisha na kumfata kisha akamkumbatia huku akilia sana.
Gari ya kukodi ilipofika, wakapanda na kuondoka.

Nyumbani kwakina Sabrina, alifika na Sakina kumuulizia Jeff.
"Maana leo kaondoka mapema na kudai anakuja huku"
"Ni kweli alikuja ila ameondoka na Sabrina hata nashangaa hawajarudi hadi muda huu."
Sakina alikaa kimya kwa muda akitafakari mahali ambako Jeff na Sabrina watakuwa wameenda bila ya kupata jibu huku moyo wake ukizidi kupata hofu juu yao.
"Tafadhari Mungu isiwe hivi ninavyofikiria"
Mama Sabrina akamuuliza Sakina kwa mshangao kuwa ni kitu gani anachofikiria.
"Kwakweli mama sielewi yani sielewi kabisa"
Mtoto mdogo wa Sabrina aliamka na kuanza kulia, ikabidi mama Sabrina na Sakina waingie ndani.
Kwavile mama Sabrina alikuwa kambeba Cherry mgongoni, ikabidi Sakina amchukue yule mtoto mdogo na kumbembeleza.
"Vipi mmeshampa jina huyu mama?"
"Ndio, kapewa jina na shangazi wa Sabrina kuwa aitwe Sam"
"Sam!"
"Ndio Sam mbona umeshangaa?"
"Kwahiyo ataitwa Sam Sam?"
"Ndio, hakuna ubaya kuitwa hivyo"
Sakina alikuwa akimtazama tu huyu mtoto kwani kulikuwa na kila sababu ya kumpa yeye jina kwavile alikuwa na hisia zote kuwa yule mtoto ni wa Jeff ingawa hakuwa na hakika na hisia zake.
Ila macho yake hayakubanduka kwenye sura ya mtoto huyu ukizingatia kuwa alimfananisha moja kwa moja na mwanae Jeff.

Sabrina alikuwa na hasira sana mule ndani ukizingatia kuwa yeye hajawahi kulala na Sam, kwahiyo kitendo cha kuona mwanamke vile kilimkera sana na wala hakutilia maanani kama kuna damu mule ndani kwani aliongea kwa mfululizo kisha kutoka nje.
Jeff naye alikuwepo katika kumfatilia nyuma nyuma ili kuhakikisha kwamba hawezi kupotea.
Sabrina na Jeff walipofika pale nje ndipo walipoona ile gari ya kukodi waliyopanda wakina Sia ikiishia, Sabrina akatamani kupata gari nyingine ya haraka ili wawafatilie ila Jeff akamzuia na kumsihi warudi nyumbani.
"Tafadhari twende nyumbani, kumbuka watoto tumewaacha. Kumbuka una mtoto mdogo sana anahitaji kunyonya, tafadhari twende nyumbani"
Kisha Jeff akatafuta usafiri wa kuwarudisha.

Sabrina alikuwa akilalamika tu kwenye gari mwanzo mwisho, mpaka Jeff aliamua  kumuuliza kwani aliona wazi kuwa kunauwezekano mkubwa wa Sabrina kuwa anafahamiana na yule dada.
"Kwani unamfahamu yule?"
"Namfahamu vizuri sana, alikuwa rafiki yangu hapo zamani ila alinitendea kitu cha ajabu. Alifanya niende mahabusu bila makosa, alifanya nione mji mbaya halafu leo hii ananiibia mume wangu? Mngeniacha nimfundishe adabu yule, yani leo ningemkumbushia machungu yote niliyoyapata kule mahabusu"
"Pole sana, kumbe ndio huyu alifanya uteseke kipindi kile dah pole sana"
Sabrina alikuwa akisema maneno yote mabaya dhidi ya Sia huku akikumbukia alikopitia yeye mpaka kufikia hapo.
Walifika nyumbani na kumkuta Sakina na mama yake wakiendelea na harakati za kubembeleza watoto.
Sabrina alipowaona alienda kuwakumbatia kanakwamba hakuwaona kwa muda mrefu sana na kufanya wamshangae.

Aisha aliamua kwenda na Sia moja kwa moja nyumbani kwa Neema kwani hakujua ni jambo gani lililompata.
Waliingia ndani huku Sia akionekana kuchechemea.
Moyo wa Sia uliamini kuwa kilichompata ni tego, na huku akiamini hilo tego limetegwa na yule mke wa Sam ambaye alikuwa rafiki yake hapo zamani.
Alikaa chini na kuanza kumueleza Aisha,
"Mume wa mtu sumu, ni sumu kweli Aisha ndicho kilichonikuta mimi leo"
Aisha alikuwa kwa makini kumsikiliza Sia aliyekuwa akieleza kwa uchungu,
"Yani mimi nisingekuwa na ujasiri basi ningezimia kwa yaliyonipata leo"
Sia aliendelea kueleza na kumfanya Neema ashtuke chumbani kwake kwani alikuwa amejilaza muda huo, Neema aliinuka na kujikongoja ili amuwahi Sia na kumzuia asizungumze.
Ila muda Neema anatokezea pale sebleni, ni muda huo huo Sia nae alianguka na kuwa kimya kabisa.

Itaendelea

JE HAYA NI MAPENZI!! 97:

Sia aliendelea kueleza na kumfanya Neema
ashtuke chumbani kwake kwani alikuwa amejilaza
muda huo, Neema aliinuka na kujikongoja ili amuwahi Sia na kumzuia asizungumze.
Ila muda Neema anatokezea pale sebleni, ni muda huo huo Sia nae alianguka na kuwa kimya kabisa.
Neema alimkimbilia Sia pale chini na kuanza kumtingisha huku akimuita kwa nguvu,
"Sia, Sia, Siaaaaaa"
Neema alitokwa na machozi mfululizo kwani alijua wazi Sia ameshakufa na kilichomuua ni tamaa aliyokuwa nayo kama yake, ni tamaa ya pesa tu. Neema aliumia sana pale chini.
Aisha alikuwa kama mtu aliyepigwa shoti kwani alijikuta ameduwaa kwa muda mrefu na kushangaa huku akimtazama Neema aliyekuwa akilia na Sia pale chini, kisha akajikuta akimuuliza Neema,
"Na wewe ndio ulifanyiwa hivi dada?"
Aisha alibubujikwa na machozi ila Neema hakujibu kwani alikuwa na mashaka kwakile ambacho kingemtokea ukizingatia alishawahi kumshuhudia rafiki yake Rose akifa mbele ya macho yake sababu ya kusema ukweli na sasa anamshuhudia Sia akikata roho pale.
Neema akamuomba Aisha waache kujadili na washughulike kumuwahisha Sia hospitali ingawa alijua wazi kuwa Sia ameshakufa pale.
Aisha alitoka nje kuomba msaada kisha kumuwahisha Sia hospitali na kukazana kuwapa taarifa baadhi ya ndugu zao na ndugu wa Sia.

Sam akiwa nyumbani kwake huku akili yake ikikosa muelekea, akahisi maumivu ya moyo na kujua wazi kuwa ni lazima Sia atakuwa amekufa.
Aliumia sana kuona amemuua msichana mwingine,
"Kwanini kipindi hiki jamani kwanini? Kwani hawa wanawake wanataka nini kwangu? Kwanini kunitia majaribuni kiasi hiki? Nimeishi miaka mingi na Sabrina na sijawahi kufanya nae chochote kwavile sikutaka kumuua. Mbona hakunilazimisha kiasi hiki kama hawa? Au kwavile aliwahi kubakwa? Hata kama ila jibu ni pale pale kuwa Sabrina ni mwanamke wa tofauti sana."
Sam alijiwazia sana na kujipanga kwenda msibani tu maana hapakuwa na namna nyingine.

Sabrina alikabidhiwa mtoto wake amnyonyeshe, akamuangalia sana na kuona alivyofanana na Jeff, alijikuta tu akijisemea moyoni kuwa kweli mficha maradhi kifo humuumbua kwani huyu mtoto wa sasa ilikuwa ni bora yule wa kwanza kwani huyu alifanana kila kitu na Jeff.
Sabrina hakusema kitu zaidi tu ya kumnyonyesha mwanae ambapo Sakina alikuwa akimuangalia sana Sabrina huku akimtafakari.
Jeff aliwaacha pale na kuondoka huku akimuaga mama yake kuwa anarudi nyumbani.

Sia alikufa akiwa na kunyongo dhidi ya Sabrina kwani hadi anaanguka pale licha ya kumsimulia Aisha yaliyomsibu ila bado alikuwa na kinyongo dhidi ya Sabrina.
Daktari aliwapa taarifa kuwa Sia alikuwa marehemu tayari na kufanya ndugu, jamaa na marafiki kuangua kilio pale hospitali.
Moyo wa Aisha pia uliamini kuwa huyo Sabrina ni mtu mbaya sana na hafai, alijikuta akimchukia huyo Sabrina bila hata ya kumfahamu yukoje.

Taratibu za mazishi ya Sia zikaendelea ila kuna baadhi ya ndugu wa Neema walijikuta wakihoji kuwa ndugu yao ana matatizo gani hadi Rose na Sia kufia ndani kwake? Na wote kutokuonekana na tatizo lolote zaidi ya damu.
Walijikuta wakimuhurumia Aisha aliyekuwa akiishi na Neema.
Ila Neema alielewa kila kitu kama ndugu zake wamemtenga, kwanza sababu ya harufu aliyokuwa akitoa na pia kifo cha Rose kiliwashtua sana na sasa ni kifo cha Sia.

Siku hiyo Sabrina alikaa kitandani huku akivuta kumbukumbu za matukio mbali mbali yaliyowahi kutokea katika maisha yake,
"Mara nyingine naona kama sinema vile kwa haya mambo katika maisha yangu. Sia alikuwa rafiki yangu sana, mwisho wa siku akaniunganisha na kaka yake Japhet tukawa wapenzi kisha akaungana na mpenzi wa zamani wa Japhet katika kuniangamiza mimi tena kwa kutumia njia ya uongo kuwa mimi nimempiga yule dada na kufanya mimba yake itoke wakati wao ndio walinipiga. Wakanifungulia kesi na kufanya nikalale rumande bila hatia, yani baba hasinge fahamiana na yule mkuu wa kituo hata sijui mimi ningekuwa wapi leo. Halafu leo hii anaenda kutembea na mume wangu ambaye mimi mkewe sijawahi kutembea nae kabisa mmh kweli kuna watu wapo kwaajili ya kuumiza wenzao"
Sabrina alifikiria na kulala.

Kulipokucha, Sabrina alikuwa wa kwanza kuamka na bado aliona maisha yake kuwa kama sinema.
"Eti nilipoteza kumbukumbu mmh! Maisha haya loh"
Akafanya usafi wa hapa na pale na kuwaandaa vizuri watoto wake kwani siku hiyo aling'ang'ania kulala nao wote wawili.
Mama yake alipoamka naye alimshangaa Sabrina kwa uchangamfu wake na kujua wazi kuwa kitendo cha kurudi kwa kumbukumbu zake kimesaidia sana na kumfanya arudi kwenye hali ya kawaida.
Alimfata mwanae na kumuangalia vizuri,
"Mbona unaniangalia hivyo mama?"
"Hapana mwanangu, namshukuru Mungu kwakweli maana sikujua kama ungerudi katika hali hii"
Sabrina akatabasamu tu.
Muda kidogo wakapatwa na ugeni, mgeni mwenyewe alikuwa ni Fredy na alishangaa kumuona Sabrina akitabasamu kwa kumuona,
"Karibu Fredy"
Kisha akainuka na kumkumbatia Fredy na kumkaribisha sana,
"Kheee Sabrina hongera kwa kurudiwa na kumbukumbu zako, hongera pia kwa kujifungua. Umepata mtoto gani?"
"Asante, ni mtoto wa kiume. Hivi Francis yupo?"
"Yupo ndio na hajajua tu kama umepona"
Wakaongea mambo mengi kisha Fredy akawapa taarifa kuwa anaenda msibani ndio akaamua kupitia hapo.
"Msiba wa nani tena?"
"Unamkumbuka yule dada yangu Neema?"
"Neemaaa, Neema"
Sabrina akawa kama anavuta kumbukumbu hivi,
"Yeah namkumbuka, si ndio yule aliyekuwa anamtaka mume wangu! Kafanyaje tena?"
"Kweli sasa hivi akili imekurudia"
"Ndio, kafanyaje basi?"
"Kuna mtu kafia ndani kwake na mtu huyo ni rafiki wa mtu anayeishi nae mule ndani"
"Maskini poleni, sasa huyo mtu chanzo nini hadi kufia ndani kwa Neema?"
"Chanzo hakijulikani ila ndio hivyo amekufa, Neema anatia huruma sana sababu huyu ni mtu wa pili kufia ndani kwake, kwakweli namuhurumia sana Neema"
Sabrina akampa pole pale kisha Fredy akaaga na kuondoka zake.
Mama Sabrina akamuangalia Sabrina na kumuuliza swali kulingana na yale maongezi aliyokuwa akiongea na Fredy,
"Unasema huyo dada alikuwa anatembea na Sam?"
"Ndio mama na nilimfumania mara mbili"
"Eeh niambie ilikuwaje kwani?"
Mtoto wa Sabrina akawa analia hivyo wakaanza kumbembeleza na Sabrina akamuahidi mama yake kuwa atamuelezea badae.

Jeff akiwa nyumbani kwao alijikuta akitafakari mambo mengi sana kwani aliona kuwa sasa akili yake imekua vya kutosha,
"Hivi mahusiano yangu na Sabrina nitaficha hadi lini? Hivi nitaendelea hadi lini kuficha kuhusu damu yangu mwenyewe? Watoto ni wangu ila wanapewa majina ya mtu mwingine na mimi naangalia tu. Ni kweli nilifanya kosa ila yote sababu nampenda Sabrina na kama nampenda sina budi kusimama na kutetea mapenzi yangu juu yake."
Jeff akapata wazo kwanza la kujitoa muhanga na kwenda kumueleza ukweli Sam.
Aliamua kujikaza kabisa, kisha akaondoka pale kwao na kumuaga mama yake.

Sakina alimuangalia sana mwanae huku akimuona kuwa ni kijana aliyepevuka na kujitambua, pia alimuona ni mtoto wa pekee mwenye kuaga mzazi pindi anapoenda katika safari zake ila kilichomuuma ni siri ya mwanae kwanini amfiche?
"Kwanini huyu mtoto ananificha? Kuna nini kati yake na Sabrina? Na kwanini Sabrina akubali kutembea na Jeff wakati na yeye ni kama mzazi wake tu? Miaka mingapi Sabrina kampita Jeff, hata kama si miaka ya kuweza kuzaa ila bado ni mkubwa sana kwake. Afadhari ingekuwa kampita mwaka mmoja au miwili, hivi Sabrina ana akili kweli? Kuweza kumvulia Jeff nguo mtoto aliyemlea mwenyewe? Hapana bado siamini na siwezi kuamini"
Sakina alijiuliza maswali na kujijibu mwenyewe kwa wakati huo huo, kwa kiuhalisia hakujielewa katika mustakabali mzima wa kilichotokea kati ya Jeff na Sabrina.

Jeff alifika nyumbani kwa Sam na kumkuta ndani ila zile damu za jana hazikuwepo tena kwani alishafanya usafi wote.
Na Jeff alipofika pale ndipo alipokumbuka kuhusiana na zile damu za jana ambapo ni yeye alizigundua ila Sabrina hakugundua kwavile alishapaniki tayari alipomuona Sia pale ndani ile jana.
Jeff alimsalimia Sam aliyeonekana kupooza sana, tena kabla Jeff hajaweka mazungumzo yoyote, Sam akamuomba kitu
"Afadhari umekuja, naomba nisindikize msibani"
"Msibani? Nani amekufa tena?"
"Kuna dada flani namfahamu ndio amekufa"
Jeff hakupinga, kisha Sam akainuka na kutoka nje kisha kuanza safari na Jeff ya kwenda huko msibani.

Neema alimuomba Aisha aende mwenyewe msibani kwani yeye hakuwa na nguvu ya kutembea, na ilikuwa ukimuangalia mwili wake ulivyodhoofu lazima umuonee huruma kwahiyo akakataa kabisa kwenda msibani hivyobasi Aisha akaamua kwenda mwenyewe msibani ili hata aweze kuwaelekeza watu wengine maeneo ya msiba ulipo.

Sam alizunguka zunguka na Jeff mpaka muda wa mazishi ulipofika ndipo walipoenda moja kwa moja makaburini na kama kawaida ya Sam alisimamisha gari yake mbali kabisa na pale wanapozika.
Jeff akamuuliza,
"Vipi mbona hatushuki kaka?"
"Kama unashuka we shuka tu ila mi nabaki humu humu kwenye gari"
"Sawa basi ngoja niangalie angalie"
Kisha Jeff akashuka na kwenda maeneo ya makaburi ambako watu wengine walikuwa wakipiga stori za wasifu wa marehemu huku wengine wakiomboleza.
Alijikuta akisogea sehemu waliyosimama vijana watatu na wakiongea kuhusu marehemu,
"Yani nilipoambiwa Sia amekufa sikuweza kuamini jamani mwenzenu, dah kweli kifo tunatembea nacho"
"Ndio hivyo jamani, mi Sia kaniuma sana. Huyu dada alikuwa mzuri jamani, sura nzuri, shepu nzuri, alikuwa na mvuto huyu ingawa alinikataa ila nilikuwa nampenda sana halafu hakuwa na makuu kwani alikuwa akinipa kampani, alikuwa hakatai kupiga picha na mimi dah kweli kizuri hakidumu"
Huku akibonyeza bonyeza simu yake na kufungua picha za Sia na zile alizopiga pamoja na Sia huku akiziangalia kwa masikitiko makubwa sana na kufanya wale wenzie kusogelea ile simu kuangalia picha za Sia.
Jeff nae akasogea karibu yao kuangalia picha za Sia, akashtuka kuona kuwa ni yule mdada wa jana na pia ndio yule yule aliyemkuta kwa Sam siku aliyoenda kwake.
Jeff alijikuta akiwauliza,
"Imekuwaje hadi kafa? Kapata ajali?"
"Bora hata angepata ajali masikini tungesema ni ajali, ila amekufa gafla kabisa yani unaambiwa ilikuwa gafla hata hospitali wamejaribu kuangalia kilichomuua bila ya kupata jibu. Yani kwakweli kifo hakina huruma"
Jeff akasikitika sana.
Wakati wakiendelea kubishana pale mvua ikaanza kunyesha na kufanya watu wote watawanyike kwanza.
Ilinyesha mvua kubwa ila kwa dakika tano tu.
Baada ya hapo ilibidi wafanye fasta kutoa maji kwenye kaburi kisha kuzika.
Jeff alisogea kwenye kundi karibu la wadada na kuwasikiliza,
"Namuonea huruma mchumba wa Sia jamani"
"Unamuonea huruma nani? Kama yule John hata usimuonee huruma walishaachana kitambo na kule alikofia Sia ndio kwa mwanamke aliyekuwa na mahusiano na John na hapo washaachana, na huyo John saivi nasikia kuwa bega moja limepinda eti aliwahi kupigwa risasi ya bega kwahiyo achana nae tu"
"Risasi ya bega alipigwa na nani?"
"Nasikia kuna tajiri mmoja alikuwa na mahusiano na Neema ndio aliyempiga John risasi ya bega. Ila kesi haikwenda popote si unajua tena pesa inaongea, tajiri na mali zake, maskini na watoto kwahiyo John yupo yupo tu"
"Ila nasikia huyo kaka ni tajiri haswa, anajulikana sana"
"Anaitwa nani kwani?"
"Kitu kama Sam ingawa sina uhakika kwani nasikia huwa hapendi kujionyesha utajiri wake. Ukimpata lazima ufurahie maisha ila usiwe na mchepuko ndio hivyo mchepuko anapigwa risasi"
Jeff alibaki kushangaa tu kwa yale mazungumzo hadi wanaondoka pale makaburini hakupata jibu la moja kwa moja kuhusu Sam.
Akarudi kwenye gari kisha Sam akaondoa gari bila ya kusema chochote.

Safari ilikuwa mpaka nyumbani kwa Sam, waliingia ndani ila Sam hakusema chochote cha ziada na alionekana kuwa na mawazo sana.
Jeff alimuangalia kwa kumshangaa huku akitamani kumwambia kinachomtatiza kuhusu yeye au kumweleza kuhusu Sabrina ila aliona ule sio wakati muafaka na kuamua kuinuka na kumuaga.
Sam alimuangalia na kumwambia,
"Tafadhari kabla hujaondoka naomba nifanye hili"
Jeff alisimama tu akimuangalia, Sam akaingia chumbani kwake na baada ya muda kidogo akatoka.
Alikuwa ameshika bastora mkononi na kumfanya Jeff ashtuke sana na kujikuta akimuita mlinzi wa Sam.
Mlinzi naye alishangaa kuitwa kwa nguvu na Jeff na muda huo huo kusikia mlio wa risasi ikipigwa na kuwa kimya gafla.   

Itaendelea

JE HAYA NI MAPENZI!! 98:

Mlinzi naye alishangaa kuitwa kwa nguvu na Jeff
na muda huo huo kusikia mlio wa risasi ikipigwa
na kuwa kimya gafla.
Mlinzi yule wasiwasi ukamjaa huku akihofia kuwa huenda kuna tatizo limetokea kati ya bosi wake mr. Sam na Jeff kwani alimjua bosi wake alivyo na hasira kiasi cha kumfanya muda mwingi aonekane kuwa hacheki.
Akataka kujisogeza ili akaangalie kilichotokea ila alisita kwani alihofia kuwa mambo yasije kumgeukia yeye.

Jeff alikuwa kama ameganda akimuangalia Sam kwani ilikuwa ni ngumu kuamini alichokifanya.
Hakuweza kumuuliza chochote zaidi ya kumuangalia tu, ila Sam akamsogelea Jeff na kumgonga gonga kwenye bega lake kisha akamwambia,
"Unatakiwa uwe ngangari, uwe imara. Wewe ni mtoto wa kiume, ukishtuka vitu vidogo kama hivi utaviweza vikubwa!"
Jeff hakujibu chochote kile zaidi ya kusema,
"Naenda"
Kisha akatoka na kuondoka.

Yule mlinzi pale alimuangalia tu Jeff akitoka, halafu akamuona Sam naye akitoka na kusimama mlangoni hadi pale Jeff alipotoka kabisa na wala yule mlinzi hakumuuliza chochote kile.

Jeff alipanda daladala huku akitafakari kuhusu Sam.
Akatafakari tukio lake la kutoka na bastora kisha kumuelekezea na kuipiga pembeni.
"Hivi alikuwa na maana gani mtu huyu?"
Alijiwazia sana moyoni hadi kuja kushtukia alijikuta ameshapitilizwa kituo na kuamua kushuka kisha kupanda gari ya kurudi tena.

Wakati yupo kwenye ile gari ya kurudi alishangazwa na baadhi ya maongezi ya wadada wawili aliokaa karibu nao,
"Unajua wadada wengi hatupo makini ila haya mambo yapo. Kuna wakaka sijui wana majini sijui ni nini yani inatakiwa kuwa nao makini sana. Ukilala nae tu unaenda na maji"
"Sasa utajuaje kuhusu wakaka wa namna hiyo?"
"Hapo ndio inatakiwa kuwa makini kuhusu mtu wake wa nyuma, watu wanakufa gafla sana ingawa sina uhakika na hizi stori ila najua zipo tu. Yani haya mambo haya huwa hayaeleweki kwakweli"
Jeff akashuka na kuwaacha na mazungumzo yao ila bado ilimfanya awe na mawazo  zaidi na kufanya akili yake izidi kuchanganyikiwa.

Ilikuwa ni jioni sana ambapo Fredy alipita tena kwakina Sabrina kama alivyoahidi.
"Tumeshazika tayari"
"Poleni sana"
"Alikuwa bado binti mdogo tu maskini, yani ni rika lako tu Sabrina tena amekufa gafla"
"Kifo tunatembea nacho Fredy, ngumu kutangulia"
"Ndio hivyo, Mungu amrehemu marehemu Sia jamani"
Sabrina alishtuka sana aliposikia jina la Sia na kuuliza kwa makini,
"Anaitwa Sia?"
"Ndio anaitwa Sia kwani vipi?"
"Aaah hamna kitu"
Roho ya Sabrina ilipatwa na maumivu ya gafla hadi pale Fredy alipoaga na kuondoka ila bado Sabrina alikuwa akijihoji kuhusu huyo Sia.
"Tafadhari Mungu asiwe yule Sia ninayemfikiria mimi"
Roho yake iliumia sana na kujiona kama kapungukiwa na kitu fulani vile.

Muda wa kulala ulipofika bado Sabrina alikuwa na mawazo kumuhusu Sia, yani ingawa alimtendea mengi mabaya ila bado aliumia kuhusu swala zima la kifo cha huyo Sia.
Sabrina alijizungusha pale kitandani na hatimaye akalala.
Akiwa katikati ya usingizi mzito, akajiwa na picha ya Sia akimtazama kwa jicho kali sana na muda ule ule Sabrina akashtuka huku jasho jingi likimtoka na kumfanya ainuke na kwenda kunywa maji ili kuiweka akili yake sawa.
Alikaa kitandani na kutafakari sana ila hakuweza kulala tena kwa muda huo hadi kulipokucha.

Jeff naye akatamani kwenda kuongea na Sabrina kile ambacho alikisikia makaburini watu walipokuwa wakiongea kwa vikundi vikundi.
Kwahiyo Jeff alitoka kwao ile asubuhi akielekea kwakina Sabrina na muda huo Sakina alikuwa akimuangalia tu mwanae akitokomea kwakina Sabrina na kumfanya na yeye apate wazo jipya.
"Hapa ni kumuhoji yule yule mtu mzima, na kama kweli mwanangu ndio muhusika kwa wale watoto yani hata sijui hii aibu tutaenda kuificha wapi jamani"
Alilalamika sana ila alishajipanga kumuuliza Sabrina na kumuwezesha kujua ukweli kuhusu mahusiano yake na Jeff, na kitu gani afanye kwa ile aibu inayojitokeza kati yao huku akimuomba Mungu kuwa mawazo yake yasiwe kweli.

Jeff alifika na kumkuta Sabrina alishaamka muda mwingi sana hata watoto walikuwa bado wamelala.
"Kheee vipi mbona asubuhi asubuhi?"
"Nimekuja kukusalimia, ila pia kuna khabari nataka kukupa"
"Khabari gani?"
Sabrina aliamua kutoa viti ili waweze kukaa ndipo amsikilize vizuri.
"Jana nilipita kwa Sam"
Sabrina akaanza kumsikiliza kwa makini ila huku moyo wake ukimzodoa Jeff na kumuona kuwa ni kijana asiye na aibu wala uoga, yani kuweza kuwasiliana na mume anayejua wazi anamuibia mkewe.
Ila aliendelea kumsikiliza ambapo Jeff alimueleza swala zima la yeye kwenda na Sam msibani,
"Tena msiba wenyewe ni wa mtu unayemfahamu kabisa"
Sabrina akashtuka na kuuliza kwa mshangao,
"Ni nani huyo mtu?"
"Ni yule Sia"
Sabrina akashtuka zaidi na kuuliza kwa makini ambapo Jeff alimueleza  kila kitu alichokutana nacho kule msibani na kumfanya Sabrina ashtuke zaidi,
"Na unajua kituko alichofanya mumeo wakati tumerudi toka msibani?"
"Alifanyaje tena?"
"Niliaga akaniambia nisiondoke, akaingia ndani si akatoka na bastora na kunilengeshea"
"Mungu wangu, ukafanyaje sasa"
"Nilimuita yule mlinzi wake, ila muda huo huo alifyatua risasi iliyopiga pembeni yangu. Yani ilibidi nitulie tu ila yeye alikuwa akitabasamu na kuja kunigonga gonga mgongoni kisha mi nikaondoka bila kuongea nae chochote"
"Yani akili ya huyu Sam huyu, sijui akili yake ikoje. Mi mwenyewe nishatishiwa ile bastora mara kibao, tena anazo mbili, moja inatoa sauti na nyingine ni kimya kimya yani huyu nilikuwa naishi nae kwa kubandika moyo wa chuma ndani yangu ila la sivyo hakuna anayeweza kuishi na kiumbe huyu"
Walimsikitikia Sam kwa pamoja, kisha Sabrina akamueleza Jeff kuhusu ndoto aliyoota usiku wa kuamkia leo kumuhusu huyo Sia na kuwafanya wajiulize kuwa mustakabali wa mambo yote yale ni kitu gani.
Walikosa jibu, Jeff akaingizia na utani pale,
"Angesikia mama hapa ungemsikia, twendeni kwa mtaalamu tu"
Na kumfanya Sabrina acheke.
Muda huo Sakina nae akawasili pale na kumfanya Sabrina acheke zaidi kuliko alivyocheka mwanzoni.
Sakina aliwauliza kwa mshangao,
"Jamani mwacheka nini? Au mnanicheka mimi?"
Sabrina akazidi kucheka hadi Sakina akaondoka kisha Jeff nae akaaga na kumfata mama yake.

Sam alikuwa akijiuliza maswali na akaona ni vyema akutane na Sabrina na aweze kumueleza ukweli huku akihisi kuwa huenda hiyo ndio njia pekee ya kumfanya yeye asahau kuhusu swala zima la kumsaliti na mwisho wa siku kuwa karibu nae.
"Yani wakati nipo na Sabrina sikuthubutu kufanya makosa, nilikuwa makini sana kupita maelezo ya kawaida ila toka yupo mbali nami kwa hii miezi michache tu nimejikuta nikimaliza hawa wadada. Nifanye nini kupunguza mawazo ikiwa hawa wadada ndio wenyewe wanaoniingiza katika vishawishi? Nifanyeje mie?"
Alijiwazia sana bila ya jibu na kuamua kwenda baa kwa asubuhi hiyo ili anywe hata supu aweze kuchangamsha akili yake.

Wakati Sam alipokuwa pale baa akinywa supu, alikuja mdada kumsalimia ambapo aligundua kuwa ni rafiki wa Sia,
"Shemeji, sijakuona kwenye mazishi jana"
"Mbona nilikuwepo, hili ni pigo letu sote"
"Yani mi hadi leo nashindwa kuamini, mara ya mwisho aliniaga kuwa anakuja kwako nikashangaa kupigiwa simu kuwa amekufa gafla akiwa kwakina Aisha yani hata sijui amepatwa na kitu gani kwakweli. Inasikitisha sana, hivi shemeji ulionana nae kweli marehemu Sia ile juzi?"
Sam akakaa kimya kidogo huku akitafakari cha kumjibu,
"Nilionana nae ndio ila aliniaga kuwa kuna mtu anamuwahi, maskini kumbe alikuwa anakiwahi kifo!"
Walijikuta wakisikitika kwa pamoja bila huyu rafiki wa Sia kujua siri iliyopo kwa Sam.
"Basi ndio hivyo  tulimpenda ila Mungu kampenda zaidi. Tumuachie Mungu tu haya mambo kwakweli. Hivi na wewe unaitwa nani vile?"
Sam alimuuliza jina huyu rafiki wa Sia,
"Kumbe umesahau jina langu, mi naitwa Ritha"
"Sawa Ritha, sitalisahau tena"
Kisha Sam akamuaga Ritha kuwa anaondoka ila Ritha akamuomba namba ya simu kwanza,
"Samahani shem, unaweza kunipatia namba yako"
Sam hakuwa na tatizo juu ya kutoa namba yake, alimtajia pale kisha yeye akaondoka zake.

Wazo kubwa lililokaa kwenye kichwa cha Ritha muda huo ni kuhusu kupata kazi kwani alikuwa na shida sana kuhusu swala zima la kazi kwahiyo alipoelezewa kuwa Sam ana ofisi yake ndipo wazo la kutafutiwa kazi lilipomkaa kwenye akili yake.
Aliona hapa sasa ni mahali pa matumaini.
"Ila Sia angekuwepo ndio ingekuwa rahisi kwakweli maana angenisaidia juu ya kumshawishi huyu shemeji. Maskini rafiki yangu, Mungu akupokee"
Alimaliza kuongea huku akiumizwa na swala zima la kufa kwa Sia.

Jeff alimfata mama yake nyumbani na kujaribu kumbembeleza kwani alijua wazi kuwa ni lazima mama yake atakuwa amechukia baada ya Sabrina kumcheka kwahiyo alikuwa nae kumbembeleza.
"Mama, mbona kuchukia vitu vidogo tu vile?"
"Vidogo wakati mlikuwa mnanicheka jamani"
"Sio hivyo mama, usipaniki ilikuwa ni katika hali ya utani tu"
"Utani wakati kuna mambo mnanificha"
"Jamani mama, tumekuficha nini tena?"
"Nakushangaa sana Jeff mwanangu, mamako nahangaika kulea watoto wa wengine wakati wajukuu wangu wa kiukweli wapo jamani! Mnachonifanyia sio sawa kabisa"
Jeff akajaribu kutafakari kwa haraka haraka na kugundua kuwa lazima kuna kitu ambacho mama yake anakihisia kuhusu yeye na Sabrina ila anawezaje kumwambia mama yake kuwa mawazo anayoyawaza ni ya kweli.
Alitamani kumwambia mama yake ukweli lakini aliona kuwa ni wazi atamchukiza Sabrina kama tu atasema ukweli kuhusu wao, ila bado Sakina alimtolea    macho mwanae akifikiria kama lipo jibu atakalopewa ila Jeff alikuwa kimya tu na kuelekea chumbani kwake.
Sakina alimuangalia mwanae bila ya kummaliza kwakweli.

Sabrina alibaki mwenyewe sasa na kwenda kuwasafisha wanae ambapo alikuta mama yake ameshafanya hivyo,
"Ila mama unanipenda sana"
"Lazima nikupende mwanangu, kwanza kabisa wewe ndio mtoto pekee wa kike kwenye tumbo langu"
Sabrina akapata upenyo wa kumuuliza mama yake swali,
"Hivi mama unaonaje mapenzi ya mdada mtu mzima na kijana mdogo wa kiume?"
"Ingawa sijakuelewa unataka nini, ila swala la mapenzi ni swala pana sana"
"Ndio nimekuuliza swali hilo, mapenzi ya kijana mdogo wa kiume na mdada mtu mzima. Je hayo ni mapenzi?"
"Kwanza kabisa utambue kwamba mapenzi yanamaanisha upendo, kama huyo kijana na huyo mdada wanapendana basi hayo ni mapenzi. Na kama ilivyo, mapenzi huwa hayachagui yani hutegemea tu na upendo uliopo baina ya hao watu wawili"
"Mmh mama, na mtu anayeolewa na mwanaume halafu hawafanyi chochote ndani kama mke na mume namaanisha lile tendo la ndoa, vipi hayo ni mapenzi?"
"Mmh Sabrina mwanangu kwani tatizo ni nini? Ningejua tatizo ingekuwa rahisi kukujibu, mume aishi na mke ndani na hawafanyi chochote mmh labda kama huyo mwanaume anatatizo ila bado sijaelewa mwanangu kwani kuna chochote kinachokutatiza?"
"Nitakueleza vizuri mama, upo muda nitakueleza vizuri tu na utanielewa mama yangu. Ni kweli kuna mambo mengi yanayonitatiza ila nitakwambia tu"
Mama Sabrina alimuangalia mwanae na kumsikitikia kwani aliumizwa sana na kitendo chake cha kufanya siri siku zote ila alishukuru hata kwa maswali aliyoulizwa na mwanae na kuona kuwa ni wazi ipo siku atamwambia siri zake.

Fredy alipigiwa simu na Neema na kwenda nyumbani kwake,
"Kaka yangu Fredy, nina ombi moja tu kwako"
"Niambie dada usiwe na wasiwasi"
Fredy alimsikiliza Neema huku akivumilia ile harufu mbaya iliyokuwa ikitoka kwa Neema.
"Nakuomba uniletee Sabrina hapa, nina shida nae nina maongezi nae"
"Mmh sidhani kama itakuwa rahisi dada, si unajua kama ana mtoto mdogo kwasasa?"
"Najua ndio, ila ningependa aje nizungumze nae tafadhari. Naomba ufanye njia yoyote uniletee Sabrina"
Fredy akajifikiria sana jinsi ya kumshawishi Sabrina ila mwisho wa siku ilibidi akubaliane na hali halisi tu kuwa Neema anashida na Sabrina kwa siku hizo na kumuahidi kulitekeleza swala lake.
Fredy alipoondoka, Aisha alimuuliza Neema kuhusu Sabrina aliyekuwa akiongelewa pale.
"Nasikia huyo Sabrina ni mtu mbaya sana"
"Hapana Sabrina si mtu mbaya ila sisi wenyewe ndio wabaya"
Kisha Neema akamuomba Sia ampatie karatasi na peni ambako alianza kuandika vitu alivyokuwa akivijua yeye mwenyewe kwani Aisha hakuelewa chochote ukizingatia hakupewa kuvisoma.

Kesho yake Fredy alifanikiwa kumshawishi Sabrina kisha kuondoka naye pale kwake hadi nyumbani kwa Neema, ambapo Aisha aliwakaribisha na wao kuingia ndani.
Sabrina alimuhurumia sana Neema kwa ile hali aliyomuona nayo, ila Neema hakusema chochote zaidi ya kuitoa ile barua aliyoiandaa na kumpa Sabrina, ambapo Sabrina alifungua ile barua na kuanza kuisoma taratibu.
Sabrina alishtushwa sana na kilichoandikwa na Neema, na alipojaribu kumtazama Neema alimuona kalala huku damu zikimtoka mdomoni.
Sabrina alishtuka na kuwashtua Fredy na Aisha.

Itaendelea

JE HAYA NI MAPENZI!! 99:

Sabrina alishtushwa sana na kilichoandikwa na
Neema, na alipojaribu kumtazama Neema alimuona
kalala huku damu zikimtoka mdomoni.
Sabrina alishtuka na kuwashtua Fredy na Aisha.
Wakamuangalia Neema vizuri sasa na alikuwa kimya kabisa, Sabrina alihisi kama kuchanganyikiwa ila kabla ya yote alikunja ile barua na kuweka kifuani pake kisha akainama alipo Neema akimtingisha na kumuamsha ila Neema alikuwa kimya kabisa na kuwafanya wote waumie.
Fredy alienda kufata gari kisha wakasaidiana kumbeba Neema na kumuwahisha hospitali huku wote wakiwa na hofu kuwa huenda Neema amepatwa na umauti na ndivyo walivyopewa jibu na daktari baada ya muda mchache tu kuwa Neema amefariki.
Sabrina alichanganyikiwa zaidi na hakujielewa kwa wakati huo kwani hata alisahau kama alienda na mkoba kwa Neema na kuuacha huko huko.

Fredy ndiye aliyekuwa mtu pekee wa kuweza kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki kuhusiana na kifo cha Neema kwani hata Aisha alikuwa kachanganyikiwa tayari kwa kifo hicho na kumfanya ashindwe hata kulia kwa mshtuko wa gafla uliompata, alijikuta tu akiongea peke yake kwa masikitiko,
"Dada Neema, ulikuwa badala ya dada yangu Rose. Nikakuthamini na kukujali, sikujali harufu mbaya iliyotoka kwako kwani nilikupenda na nilikuombea siku zote urudi katika hali yako ya kawaida dada. Jamani jana umeandika barua ndefu sana, hukutaka hata kuniambia inahusu nini ila kumbuka dada uliniahidi kunieleza mambo mengi sana. Ila mbona umekufa bila ya kuniambia chochote? Kwanini dada Neema umekufa? Kwanini lakini? Kwanini dada?"
Sabrina alijikuta akimuhurumia sana Aisha na kwenda kumkumbatia kwa uchungu, ni hapo ndipo machozi yakamtoka Aisha kwani alikumbuka maneno ya Neema kuwa Sabrina hana kosa lolote kwani Neema aliamini hivyo na kujiona kuwa yeye ndio mwenye makosa kwa kufosi penzi la mume wa mtu.
Sabrina alikumbatiana pale na Aisha huku machozi yakiwatoka.
Fredy alisogea na kumuomba Sabrina kuwa amrudishe nyumbani ila kwavile Sabrina alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa alijikuta akikataa kuondoka kabisa na kumfanya Fredy ashindwe la kufanya zaidi ya kuamua kumpigia simu mama wa Sabrina na kumwambia hali halisi ilivyo.

Muda Fredy anampigia simu mama Sabrina ni muda huo huo Jeff nae alikuwa nyumbani kwakina Sabrina kwa lengo la kumuona.
Akamshangaa mama Sabrina kuanza kulalamika simu ilipokatika,
"Yani huyu Sabrina huyu sijui vipi, eti amegoma kurudi nyumbani"
"Amegoma? Kwani yuko wapi?"
"Sijui hospitali sijui nani kafa huko na yeye kagoma, eti mimi nikambembeleze arudi na watoto hapa itakuwaje mbona huyu Sabrina ana matatizo jamani"
"Hebu nieleze vizuri nikamfate mie mama"
"Khee mie bibi yako wewe sio mama yako, ngoja tumpigie tena simu mtu huyu atuelekeze"
Mama Sabrina akampigia simu tena Fredy aliyewapa maelekezo na muda huo huo Jeff akaondoka kwenda kumfata.

Siku ya leo Sam alikuwa nyumbani kwake na kupatwa na maumivu ya moyo ya gafla sana, akajua kuwa lazima kuna  tukio limetokea, tena tukio sio la kawaida. Kengele ya khatari ikagonga kwenye akili yake,
"Ni kifo, Mungu wangu nani kafa tena?"
Hofu ikamjaa na kumuwazia Neema, akachukua simu yake na kumpigia Neema ambapo iliita tu bila ya kupokelewa.
Sam alitamani kujua kilichotokea kwani moyo wake ulikuwa na maumivu sana.
Aliamua kutoka kwenye nyumba yake na kuelekea hotelini ili tu aweze kujiliwaza japo kidogo.

Jeff alifika hospitali na kuwasiliana na Fredy aliyemuelekeza walipo.
Jeff aliwafata na kumuona Sabrina kajiinamia tu, Jeff akamsogelea Sabrina na kumfanya ainuke na kumkumbatia huku machozi yakimtoka kwa mfululizo,
"Tafadhari Sabrina, twende nyumbani"
"Sijisikii kwenda nyumbani Jeff, natamani nikae hapa hapa"
"Najua una uchungu sana, lakini fikiria kuhusu watoto wetu. Watoto wanakuhitaji mama yao, tafadhari twende mama"
Fredy alikuwa pembeni akimuangalia Jeff na harakati zake za kumbembeleza Sabrina, ila swala la kusema 'watoto wetu' hata yeye lilimshangaza kwakweli, ila baada ya maneno hayo alimuona Sabrina akikubali kuondoka kisha Jeff akamshika mkono na kumuaga Fredy pale.

Jeff alikodi gari ndogo ya kuwarudisha kwani kwajinsi Sabrina alivyoonekana kuchanganyikiwa akaona isingekuwa vyema kupanda nae daladala.
Alikaa nae karibu akimbembeleza na kumpa moyo huku akimwambia yote amwachie Mungu,
"Sabrina usichanganyikiwe, bali mshukuru Mungu kwa kila jambo mama angu. Kila kitu hutokea kwasababu fulani, usichanganyikiwe sana"
Sabrina alijiona kupata faraja ya kuwa karibu na Jeff kwani alionekana kumbembeleza sana na kumfanya hata ajisikie vizuri kiasi.
Walifika nyumbani na kushuka huku Jeff akiwa amemshika mkono na kuingia nae ndani.
Walipokuwa wanaingia, Sabrina akaona kuna nguo ya mwanae imeanguka na kuinama kuiokota, ila alipoinama na ile barua ikaanguka na kuokotwa na Jeff ambaye aliiweka mfukoni    mwake bila ya kuwmwambia chochote kile Sabrina ambaye aliingia ndani na kwenda kuoga kwanza kabla ya kuwashika wanae.

Sabrina alipotoka kuoga Jeff alikuwa ameondoka kitambo sana na mama Sabrina ndiye aliyekuwepo pale sebleni na watoto ambapo Sabrina alitakiwa kumnyonyesha kwanza mtoto kabla ya mambo mengine kuendelea ndiomana akaoga kwanza.
Muda kidogo mtoto alilala na kwenda kumlaza, Sabrina akakumbuka kuhusu ile barua na kukumbuka kabisa kama aliiweka kifuani ila alipekua kwenye nguo zake bila ya kuiona na kujiuliza kuwa barua ile iko wapi,
"Mmh sijui nimeiangusha?"
Alitaka kuimalizia kuisoma kwani anakumbuka wazi kuwa aliishia mahali palipoandikwa kuwa,
"Sijui kama utafanikiwa kuimaliza barua hii kabla ya mimi mauti kunikumba"
Ni mahali hapo palipofanya amtazame Neema na kumuona akitoa damu mdomoni na huo ukawa ndio mwisho wake.
Sabrina aliumia sana kuiangusha barua hiyo ingawa alitambua kuwa chanzo cha mambo yote ni Sam.

Jeff aliingia ndani kwao na kuitoa ile barua ili aisome ila kabla ya kufanya hivyo mama yake alimuita na kumfanya aiache kwanza ile barua.
"Dorry kanipigia simu leo na kusema kuwa ameoteshwa ndoto mbaya sana"
"Ndoto mbaya? Mmh huyo Dorry nae ameanzwa kuchanganyikiwa sasa, ndoto gani hiyo?"
"Tatizo mwanangu unapenda kupinga vitu sana, ila jaribu kuwasiliana nae anaweza kukueleza vizuri"
Jeff akaona isiwe tatizo na kukubaliana na mama yake pale kisha kuwasiliana na Dorry ambaye alimwambia kuwa asingeweza kumweleza kwenye simu ila labda aende na kumfanya Jeff afunge mlango wake kisha kumuaga mama yake na kutoka akielekea kwakina Dorry.
"Sasa si utachelewa sana kurudi?"
"Ndio mama, si unajua kama kule ni mbali mama"
"Sawa basi"
Jeff akaondoka zake.

Sam alikuwa vinywaji vyake pale na kutamani hata kulala pale pale hotelini.
Ila alipigiwa simu na Ritha na kumuelekeza alipo ambaye nae alienda pale hotelini kama kumpa kampani tu ila Sam alionekana kulewa tayari,
"Kwanini ulale hapa wakati una nyumbani kwako jamani"
"Sipapendi nyumbani kwangu, pamepooza sana. Mke wangu alinikimbia, mambo hayaeleweki kabisa"
"Pole sana, ila kwanini mkeo alikukimbia?"
"Historia ndefu ila mke wangu kanikimbia, kwangu kumepooza sana"
Halafu Sam alionekana kama kulengwa na machozi na kumfanya Ritha amuonee huruma sana,
"Basi mi nakuomba, nipo chini ya miguu yako twende nyumbani. Ni usiku huu tayari"
"Nimekwambia kwangu kumepooza"
"Usijali nitakupa kampani"
"Kweli? Utanipa kampani kama hivi?"
"Ndio, wee niamini tu. Twende nyumbani tafadhari"
Sam aliona ni jambo jema kuwa na kampani na kwavile Ritha alionekana ni mdada mpole na mstaharabu hakuhisi kama anaweza kufanya nae chochote kibaya.
Kwahiyo wakapanda gari na kuelekea nyumbani kwa Sam.

Jeff alifika kwakina Dorry na kumkuta Dorry ambaye alikwenda kumkumbatia.
Jeff nae akamkumbatia pia ili aweze kumsikiliza hoja zake, ila kabla ya yote alimuuliza kwanza kuhusu mtoto,
"Mtoto yuko wapi Dorry?"
"Yupo kalala"
"Eeh niambie hiyo ndoto mbaya uliyoota kuhusu mie"
"Mmh ndio kwa kusimama hivi, hebu tuingie ndani kwanza"
Jeff akakubali na kuwafanya waingie na kukaa sebleni ila leo nyumba yakina Dorry ilikuwa kimya sana na kumfanya Jeff aulizie na hili pia.
"Vipi mbona leo kimya sana hapa kwenu? Wengine wako wapi?"
"Wameenda kwenye sherehe, yani nimebaki mwenyewe hapa basi nyumba inaboa balaa"
"Pole kwa kubaki mwenyewe, ila nieleze kuhusu hiyo ndoto si unajua huku kwenu ni mbali na giza limeshaanza lakini!"
"Naelewa hilo, ila kabla sijakwambia naomba nikuulize kitu"
"Niulize tu"
"Hivi wewe yule Sabrina unampendea nini?"
Jeff akamshangaa Dorry kwa swali lake na kujikuta akimuangalia tu kisha akamuuliza,
"Kumpendaje pendaje yani sijakuelewa"
"Mmh Jeff umenielewa vizuri sana. Mi najiuliza siku zote wewe umempendea nini Sabrina? Kwanza yule mdada ni mtu mzima kwako, pili ni kama ndugu yako, tatu mabinti wa rika lako tupo tena tuna mvuto kuliko huyo bibi. Hebu nitazame vizuri mimi nilivyo Jeff"
Dorry aliinuka na kuanza kujinengulisha kwa Jeff kuwa amtazame vizuri ila Jeff alikuwa kimya tu bila ya kuongea chochote ambapo Dorry aliendelea kusema,
"Pia yule kakomaa, si mama yako mdogo yule? Hivi umempendea nini mwanamke mtu mzima kama yule Jeff, unajua kwamba unasikitisha wewe! Yule ni mtu mzima waachie watu wazima wenzie. Yule ni bibi kwako"
Jeff akachukizwa na kauli za Dorry dhidi ya Sabrina na kumuuliza,
"Umemaliza? Hiki ndicho ulichoniitia Dorry? Yani kunitoa kwetu hadi hapa nia yako ni kumuongelea Sabrina!"
Jeff aliinuka kwa hasira na kutaka kutoka, Dorry akamvuta shati ili asiondoke ila kwavile Jeff alishapandwa na hasira tayari alijikuta akimnasa kibao Dorry kisha akaondoka zake na kumuacha Dorry akiugulia kibao alichopigwa.

Jeff alirudi nyumbani kwao na kwenda kulala moja kwa moja kwani aliumizwa na kile kitendo cha kusemwa Sabrina wakati yeye ndio chanzo cha mambo yote.
Aliona ni bora mtu atokee na kumtukana yeye matusi yote ya duniani lakini sio kwa kumtukana Sabrina kwahiyo moyo wake uliumia sana.

Sam alifika nyumbani kwake akiwa na Ritha, ambaye alishangazwa na ukubwa na uzuri wa nyumba hiyo huku magari yake yakiwa vizuri yamejipanga na kujiuliza kama mke wa Sam ana akili timamu kweli kukimbia nyumba nzuri kiasi hicho na licha ya vyote ni kumkimbia mwanaume mwenye pesa kiasi cha Sam wakati ni wanawake wengi sana wanaopenda kuishi na wanaume wenye pesa kwani hakuna mtu anayependa maisha ya shida.
Sam alimkaribisha Ritha vizuri sana na kuongea mambo ya hapa na pale.
"Kwahiyo Sam mkeo kaondoka na watoto?"
"Ndio kaondoka nao, nimebaki mpweke tu hapa"
 "Pole sana"
"Asante, ila ukitaka kulala niambie kuna vyumba vingi tu vya kulala hapa"
"Kwahiyo wewe leo hutolala?"
"Kama nikipatwa na usingizi basi nitalala hapa hapa sebleni"
"Kwanini wakati chumbani kwako kupo? Kwani chumba unacholalaga kiko wapi?"
Sam akamuonyeshea tu Ritha kwa mkono kisha wakaendelea na maongezi mengine bila ya Ritha kudai kwenda kulala wala nini mpaka pale Sam aliposinzia pale pale sebleni.
Ritha akaamua kutumia uungawana na kuanza kumkongoja Sam mpaka chumbani kwake ambapo Sam alilala tu kisha Ritha kumfunika shuka na yeye kwenda sebleni kukaa.

Kwakweli nyumba ya Sam ilikuwa ni kubwa na kwa mtu muoga tena kama Ritha aliyefiwa na rafiki yake siku za karibuni ilikuwa ni ngumu kwa yeye kukaa mwenyewe pale sebleni na kugundua kuwa ni kwanini Sam hakutaka kurudi kwake.
Hivyo na yeye akaingia chumbani kwa Sam na kulala pembeni yake.

Sabrina aliwaza usiku kucha kuhusu Neema, maneno aliyoyaandika Neema kwenye ile barua yalimjia kichwani kwa mfululizo haswa neno la kusema kwamba,
"Sam ni muuaji"
Lilikuwa likijirudia kila mara kwenye akili yake na kupata wazo la kwenda kuonana tena na Sam ingawa ile barua ilikuwa imepotea.
Kwahiyo alipoamka tu alfajiri kabla ya watoto kuamka, yeye alidamka na kujiandaa ili amuwahi Sam kabla ya kwenda kazini ili hata badae apitie kwao waongee kwani kwa kipindi hiki Sabrina hakuwa na simu na hakuweza kuwasiliana na Sam kwa kupitia simu ya mama yake.

Sam naye kulipokucha akashangaa kuona Ritha kalala pembeni yake, alimuangalia tu bila ya kumuamsha huku akiinuka kutoka kitandani.
Akasikia mtu akigonga mlango, moja kwa moja akahisi ni mlinzi wake kuwa huenda ana tatizo.
Sam akaenda kumfungulia na Sabrina akaingia moja kwa moja ndani,
"Kheee mbona asubuhi asubuhi sana Sabrina?"
"Kwani mke anapangiwa muda wa kwenda nyumbani kwa mumewe?"
Sam hakusema cha zaidi ila alimkaribisha tu, muda huo Ritha nae akatoka chumbani kwa Sam na kumfanya Sabrina ashtuke na kusema kwa mshangao,
"Kheee Sam utaua wangapi?"
Ritha alibaki kuduwaa tu kwani hakujua kinachoongelewa, Sam naye alishangazwa na kauli ya Sabrina.

Itaendelea

JE HAYA NI MAPENZI!! 100:

Sam hakusema cha zaidi ila alimkaribisha tu,
muda huo Ritha nae akatoka chumbani kwa Sam
na kumfanya Sabrina ashtuke na kusema kwa
mshangao,
"Kheee Sam utaua wangapi?"
Ritha alibaki kuduwaa tu kwani hakujua
kinachoongelewa, Sam naye alishangazwa na kauli
ya Sabrina.
Sabrina aliendelea kuwatolea macho kama anahitaji jibu kutoka kwao.
Sam akaona hapa lazima Sabrina ataleta longolongo na kumuomba Ritha aondoke mahali pale, Ritha naye hakubisha zaidi ya kuchukua mkoba wake kisha Sam akamsaidia kumtoa nje ila alimshangaa Sabrina leo bila ya kufanya vurugu zozote zaidi ya yale maneno ya kwanza tu.
Sam alirudi ndani na kumtazama Sabrina kwa lengo la kutambua tatizo lake.
"Haya niambie Sabrina"
"Hivi unajua wewe Sam hujielewi, hivi unajua kama Neema amekufa?"
"Sasa kama amekufa mimi nifanyaje?"
"Hivi Sam unathubutu kweli kusema maneno hayo? Si unajua kama amekufa kwaajili yako?"
Sam akajua moja kwa moja kuna maneno ambayo Neema alimwambia Sabrina hivyobasi akaamua kujigelesha tu kwani Sabrina alishaujua ukweli.
Sam akaanza kwa kucheka,
"Amekufa kwaajili yangu? Hebu acha kunichekesha Sabrina, mtu anakufaje kwaajili yangu bhana!"
"Kwahiyo unaniona  mimi kama nimekuja kukutania vile. Au huyu mtu ametania kwa kusema wewe ni muuaji?"
"Kama mimi ni muuaji mbona sijakuua wewe? Au huyo Neema alipokuwa anakufa uliniona mimi nimekuja na kumpiga risasi au ni nini?"
Sabrina alimuona Sam akijaribu kukwepa tu ukweli wa mambo ila kwavile hata yeye hakuimalizia ile barua ya Neema ikawa ngumu kwake kujua kila kitu kilichomkabili Neema.
Alijikuta akimuangalia Sam kwa jicho la hasira sana kwani hakuona kama Sam ni mtu mzuri kwake.
"Naondoka, ila Sam uende msibani"
"Hapa tutaondoka wote, na huko msibani tutaenda wote"
Kisha Sam akaenda kufunga mlango wake kwa funguo ili aweze kujiandaa halafu Sabrina asiweze kutoka.

Jeff naye alipoamka alikaa na kutafakari yale mambo yanavyoenda, alijiuliza kuwa ni nani alimpa ujasiri Dorry na kumfanya aweze kuropoka kuhusu yeye na Sabrina.
"Huyu Dorry huyu sio bure, lazima kuna mtu anayempa ujasiri wa kufanya mambo ya kijinga kila mara. Ndiomana limezaa na mchina kisha kutelekezwa na kubaki kudandia tu wanaume wa kiswahili kuwa mtoto ni wao. Yani huyu mwanamke huyu na nitamkomesha"
Yani Jeff alikuwa amechukizwa sana na yale maneno aliyoambiwa na Dorry kuhusu Sabrina.
Alikaa sasa na kutafakari, kisha akakumbuka barua aliyoiokota toka kwa Sabrina, kisha akaitafuta ilipo na kuifungua kwa kuanza kuisoma na kushangaa barua iliyokuwa kama stori au risala.

"Kwako Sabrina, najua ni ngumu wewe kukubali kuja kwangu na kunisikiliza yale ninayotaka kukwambia ndiomana nimeamua kuandika hii barua ili angalau upate kwa kidogo kile ambacho nilitaka kukwambia.
Kwanza kabisa nisamehe sana kwani kuna mengi mabaya nimeyafanya kwako, tafadhari nisamehe sana.
Ila kabla ya yote napenda ujue kuwa Sam ni muuaji, tena ni muuaji kabisa. Ametumaliza wengi sana ingawa hadi nakufa sitaweza kujua kuwa uuaji wa Sam umesababishwa na nini ila Sam ni muuaji.
Nimeteseka sana mimi, nimeumia sana lakini chanzo cha yote ni Sam. Mauti itanifika ila ujue wazi kuwa Sam ndio chanzo cha mauti yangu. Wadada wengi wamekufa, tafadhari Sabrina kuwa mlinzi wa karibu kwa wadada wote wanaojisogeza kwa Sam kwani mauti itawakumba tu kama mimi.
Ila nakuomba utakapomaliza kuisoma barua hii uifiche, sitaki watu wajue aibu ambayo nakufa nayo.
Lakini sijui kama utafanikiwa kuimaliza barua hii kabla ya mimi mauti kunikumba.
Sabrina sina kinyongo chochote na wewe, na pia naomba tena na tena unisamehe.
Ni mimi niliyeenda kwa mganga na kushirikiana na rafiki yangu Rose ambaye naye ni marehemu kumvuta Sam kimapenzi. Na kweli tulifanikiwa kwani hata wewe ulisahaulika, pia tukakusababishia magonjwa mbali mbali. Leo nakiri kwako Sabrina kuwa ni sisi tuliokutupia jini na kukufanya upoteze kumbukumbu, mganga alitupa masharti mazito sana kuwa hairuhusiwi Sam kuja kukuona kwani akija tu inanifanya mimi kama muhusika mkuu kupatwa na magonjwa ya gafla, hivyobasi tukafanya juu chini ili Sam akusahau kabisa na tukafanikiwa kwa hilo.
Leo mimi nakufa kwani najiona kabisa mauti ikiniangalia, ila kinachoniua ni tamaa.
Tamaa ya pesa na mali, tamaa ya utajiri na maisha mazuri. Nakuomba Sabrina uwasihi sana wadada wenye tamaa kama mimi, tamaa ni mbaya Sabrina.
Mwanzoni nilijua ni wewe umefanya dawa kwa mumeo kuwa tukilala nae tuangamie ila jibu likaja kuwa ni kila mwanamke anayethubutu kulala na Sam basi anaenda na maji. Najua unajiuliza kuwa hilo jibu nimelipataje ila hata mimi nakufa huku nikijiuliza kuwa wewe umewezaje kuzaa na Sam ikiwa tu kila mwanamke anayelala nae lazima afe? Najua jibu unalo mwenyewe kuwa umewezaje ila walinde wadada waliobaki Sabrina.
Nilianza mimi ila nikakaa kimya kutunza siri hii kwa maumivu makali sana na mwisho wa siku nakufa, akafatia Rose ambaye hakuweza kukaa na siri hata masaa ishirini na nne tu naye akafa, amekuja Sia naye uzalendo ukamshinda na ameenda na maji. Nami sasa uzalendo umenishinda ila ikitokea nimepona basi nitakuwa ushuhuda katika jamaa na hata kama nikifa basi jambo hili ulishuhudie wewe.
Naumwa Sabrina, ugonjwa wangu ni toka siku ya kwanza kuingiliwa kimwili na Sam, kwakweli Sam si mwanaume wa kawaida hata nashangaa wfwe umewezaje kulala nae? Ilikuwaje hadi mkapata watoto? Ila jibu langu ni kuwa Sam sio mwanaume wa kawaida. Ningeandika mengi zaidi ila nimechoka Sabrina, nimechoka sana. Muulize Sam mwenyewe akueleze vizuri ila weka akilini kwamba kila msichana atakayethubutu kulala na Sam basi ataenda na maji kwani Sam ni zaidi ya ugonjwa wa ukimwi maana hapa nilipo ni kheri ningepata ukimwi saivi ningetumia dozi na kuendelea vizuri kuliko hali ambayo Sam anatuacha nayo.
Kwaheri Sabrina, pole kwa kukufanya uteseke na watoto, nisamehe sana.
 Najutia makosa yangu kwakweli, najutia kwenda kwa mganga nipendwe badala yake nimejitesa.
Asante kwa kuisoma barua yangu hii ambayo kuna baadhi ya sehemu utakuwa na maswali ya kuniuliza ila sitaweza kukujibu kwavile nitakuwa marehemu, nenda kamuulize vizuri Sam na umwambie ukweli kuwa nilimpa dawa ya kukusahau, nilimwekea kwenye chakula ila yeye amenifanya kikubwa kuliko dawa niliyompa.
Kwaheri tena Sabrina.
Ni mimi Neema."

Jeff alipumua kwa nguvu sana baada ya kumaliza barua hii, akamfikiria Sabrina.
Akakumbuka maneno aliyowahi kuambiwa na Sabrina kwenye barua pia kuwa hajawahi kufanya tendo la ndoa na Sam, ni hapo akapata jibu kuwa kwanini alimkuta Sabrina akiwa bikra, akatambua kuwa Sabrina hakufata mkondo wa wenzie kwavile hajawahi kulala na Sam,
"Hivi inakuwaje watu waishi kama wapenzi, halafu kama wachumba na kumalizia na ndoa kabisa kama mke na mume kwa miaka hii yani walale wote na kuamka wote bila ya kufanya chochote? Mmh inawezekanaje hii? Mwanzoni niliposoma barua ya Sabrina nilijua kuwa Sam si mwanaume kamili sasa kama si mwanaume kamili amewezaje kulala na hawa? Amewezaje?"
Jeff akajifikiria sana bila ya kupata jibu la aina yoyote.
Aliikunja ile barua na kuiweka kisha akainuka na kujipanga kwenda kwakina Sabrina ili aone kama kweli ameisoma ile barua.

Sam alipomaliza kujiandaa alitoka ndani na kumwambia Sabrina,
"Haya twende sasa"
"Twende wapi na wewe?"
"Twende nyumbani tukachukue watoto wetu tulee"
"Eti tukachukue watoto wetu tulee, watoto wako na nani wale? Mwanaume wa ajabu sana wewe unajua kulala na wanawake wengine wakati mkeo hata kumgusa hujawahi ila watoto ndio useme wako"
"Hivi Sabrina hayo maneno yanakutoka wewe au? Hivi ni mwanaume gani anayekubali kulea watoto wa mwanaume mwingine?"
"Mwanaume gani anayekubali kulea watoto wa mwanaume mwingine? Inamaana hujijui au?"
Sabrina  alikuwa akiongea kwa hasira na kupaniki tu bila hata ya kufikiria mara mbili kile anachoongea au madhara yake.
Sam naye alimuangalia kwa kumsikitikia tu,
"Shukuru Mungu nakupenda, shukuru Mungu sipendi kuumiza wewe wala kizazi chako. Sina kawaida ya kupenda kwani chuki niliwekewa toka nilipokuwa mtoto mdogo ila wewe nakupenda na kukuthamini shukuru sana hilo. Na usifikiri sijui kama wale watoto umezaa na mtoto mwenzao Jeff, mimi ni mtu mzima Sabrina na ninatambua kila kitu"
Sabrina alikuwa kimya gafla kama kamwagiwa maji baada ya kusikia kuwa Sam anajua kila kitu kuhusu yeye na watoto wake.
Kwahiyo ilikuwa kama mtu aliyeumbuliwa vile, Sam akamuangalia na kutabasamu kisha akasema
"Wapo watu wa kuwaficha ila sio mimi Sabrina, huwezi kunificha mimi. Nilijua kitambo sana ila sikuchukua hatua yoyote sababu nakupenda na sitaki uumie kwani najua ningemdhuru Jeff basi ningekuumiza wewe. Najua ni jinsi gani  unampenda Jeff ila huweki wazi kwavile unaogopa jamii itakuchukuliaje. Sabrina, huna la kunificha mama. Haya twende sasa"
Sabrina aliinamisha kichwa chini na kuamua tu kutoka na Sam pale ndani.

Jeff alifika kwakina Sabrina na kumkuta mama wa Sabrina,
"Mmh Sabrina hata mimi namshangaa, yani kaondoka hapa asubuhi asubuhi ila hajarudi hadi muda huu. Kama unavyoniona hapa nahangaika na hawa watoto."
"Kwani ameenda wapi?"
"Alipoenda sijui kwakweli, na kama ujuavyo sasa hivi hana simu kwahiyo hata mawasiliano naye sina"
Jeff akatafakari kidogo juu ya alipoenda Sabrina bila ya kupata jibu, ila wazo likamjia kuwa huenda ameenda kwenye ule msiba wa Neema kisha akapata wazo la kwenda kumfata huko.

Jeff akiwa anatoka kwakina Sabrina, akapigiwa honi na kuangalia gari akagundua ni moja wapo kati ya magari ya Sam.
Akasimama akiangalia linapoelekea, na lilikuja na kusimama karibu yake kisha Sam na Sabrina kushuka.
 Jeff aliwatazama na kuwasalimia huku akijiuliza kuwa imekuwaje kuwaje hadi waamue kuongozana vile.
Sam aliitikia salamu ya Jeff kisha wote kuingia ndani ila Sabrina alikuwa kimya tu.
Mama Sabrina nae alimshangaa mwanae kwenda pale na Sam,
"Sabrina mwanangu, si unajua baba yako hamtaki huyo mtu"
"Naelewa mama, ila kumbukeni kwamba huyu ni mume wangu. Nimefunga nae ndoa takatifu na halali iweje sasa nimfukuze jamani? Mama si jambo jema kwakweli, ni mimi mwenyewe niliyeamua kumleta"
Mama Sabrina alimuangalia Sam na kumwambia,
"Tafadhari baba naomba uende, sitapenda Baba Sabrina akukute mahali hapa"
Sam hakutaka kubisha, ila alimvuta mkono Jeff na kutoka naye nje.
Wakati huo Sabrina alitamani hata kuwafata ili ajue mbivu na mbichi ila mama yake alimzuia na kumsisitiza abembeleze watoto,
"Hivi wewe hujijui kama umeshakuwa mama? Ulivyokuwa unawabebanisha hawa watoto ulikuwa na maana gani? Haya tulia hapo ubembeleze wanao maana mimi kazi yangu ilishaisha"
Sabrina alitulia ila alitamani kujua kinachoongelewa huko nje.

Sam alienda na Jeff hadi mahali pale alipopaki gari yake, kisha akamuuliza,
"Unajisikiaje mimi kufukuzwa hapo kwakina Sabrina?"
"Kwakweli najisikia vibaya kwani hata mimi ningekuwa ni wewe ningeumia tu"
"Unauonaje upendo wangu kwa Sabrina?"
Jeff akatulia kimya kidogo kwani maswali haya ya Sam yalimpa mashaka na kumfanya ajiulize kuwa kwanini Sam amuulize maswali hayo ila alijikaza na kumjibu,
"Naona una upendo mkubwa sana juu ya Sabrina"
"Kushinda upendo uliokuwa nao wewe?"
Jeff akawa kimya akimtazama tu Sam na kumfanya Sam atabasamu,
"Ok, but sio tatizo ila ukweli utabaki pale pale"
"Ukweli gani?"
"Wewe ni mwizi"
Kisha Sam akafungua gari yake na kuingia halafu kuondoka eneo lile na kumuacha Jeff akitafakari yale maswali aliyoulizwa na Sam.

Sam alitaka kwenda moja kwa moja kwenye msiba wa Neema ila alihisi moyo wake kumuuma sana, hakuwa tayari kushuhudia Neema akizikwa au watu wakiomboleza kwa kuondokewa na Neema.
Hakuwa tayari kuona chochote na aliamua kwenda hotelini ambako alienda jana yake.
Na kwavile alikuwa mpweke sana, akaona ni vyema apate kampani kama aliyoipata jana yake, ile kampani ya Ritha na kuamua kumpigia simu.
Ritha hakusita na kuamua kwenda hotelini alipo Sam.
"Ila leo sitaenda nyumbani kwako maana ile asubuhi duh ningepigwa mie"
"Usijali, hata mimi leo sitarudi nyumbani. Leo nitalala hapa hapa hotelini"
Sam alizungumza mambo ya hapa na pale na Ritha huku wakila na kunywa.
Mwisho wa siku aliamua kwenda kwenye chumba alichokodi pale hotelini, Ritha hakuacha kumsindikiza kuelekea kwenye chumba hiko.

Wakiwa chumbani, Sam alimshukuru sana Ritha kwa moyo wake wa upendo na huruma.
Kwavile Ritha alikuwa anaaga kuwa anarudi kwao, Sam aliamua kutoa kiasi cha pesa na kumpatia kama shukrani tu.
Ritha alishukuru sana kwa hilo, kisha akainuka na kuondoka kwani muda nao ulikuwa umeenda sana.
Ila alipotoka nje Ritha alijifikiria kuwa ni zawadi gani ampatie Sam kwa pesa anazompa? Aliona kumpali kwa kumpa kampani si zawadi pekee, ukizingatia kikubwa anachokitaka toka kwa Sam ni kupata kazi katika kampuni yake.
Akajifikiria sana, kisha akajipatia jawabu na kurudi ndani.

Sam alienda maliwatoni kupunguza maji ya bia alizokunywa kwa usiku huo, na kurudi zake kwa lengo la kulala sasa.
Akashangaa kumuona Ritha akiwa kajilaza kitandani huku akiwa mtupu kabisa kwani nguo zote alitoa na alikuwa akitabasamu.

Itaendelea



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa