JE HAYA NI MAPENZI!! 75: - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Wednesday, February 19, 2020

JE HAYA NI MAPENZI!! 75:





Sabrina alipanda kitandani huku mapigo yake ya
moyo yakienda kwa kasi sana.
Kabla dokta hajafanya chochote kwani ndio kwanza
alikuwa anavaa karatasi za mikononi akasikia mtu
akigonga kwa nguvu mlango wa kile chumba.
Naye dokta akashtuka kwani kile chumba
alichompeleka Sabrina huwa ni maalumu kwa kazi
hiyo na hakutegemea mtu kuja kumgongea vile kwa
usumbufu.
Akaenda kufungua, na moja kwa moja akaingia Sam.
Alienda moja kwa moja kwenye kitanda alicholala Sabrina ambapo Sabrina naye akashtuka kwa kumuona Sam kwani hakumtegemea.
Sam akamuangalia Sabrina kisha akamwambia neno moja tu,
"Endelea"
Halafu Sam akatoka na kuondoka.
Sabrina na dokta wakatazamana kwa uoga, kisha dokta akamuuliza Sabrina,
"Ni nani yako huyo jamaa?"
"Ni mume wangu"
"Anajua kama umekuja kutoa mimba?"
"Hajui"
"Sasa nani kamwambia?"
"Hata mimi mwenyewe sijui"
"Mmh! Hii ni kesi dada, naomba uondoke hapa sasa hivi kabla hayajazuka mengine"
Sabrina aliinuka na kutoka kisha akaondoka pale hospitali.

Wakati anatembea ili akachukue daladala aweze kurudi kwao, akashangaa kuna gari imesimama mbele yake na mlango wa gari kufunguliwa.
Ni Sam alikuwepo ndani, akamuuliza Sabrina,
"Umemaliza?"
Sabrina akatulia kimya tu kwa aibu na kuinamisha macho chini.
"Haya panda kwenye gari twende"
Sabrina alijikuta akisita kupanda kwani  hakujua ni kitu gani Sam anamuwazia kwa wakati huo.
Sam naye akamkazania kuwa apande ili amrudishe nyumbani.
Sabrina aliamua kupanda huku moyo wake ukiwa umejawa na mashaka ya kutosha kabisa.

Walienda hadi nyumbani kwa Sabrina kisha kabla ya kushuka Sam akamwambia Sabrina,
"Tunaenda kumchukua mtoto kisha tunarudi nyumbani sawa?"
Sabrina akaitikia kwa kutingisha kichwa.
Wakaingia ndani sasa, na moja kwa moja Sabrina akaenda kumsalimia shangazi yake ambaye ni majina wake.
Wakati Sabrina anamsalimia shangazi yake, huyo shangazi akamnong'oneza sikioni
"Mtoto una majanga wewe hadi unatia aibu"
Sabrina akainuka bila kujibu chochote bali alienda chumbani na kumchukua mtoto wake kisha kuwaaga, ambapo mama yake naye akamuuliza,
"Mbona mapema hivyo?"
Sam alidakia na kujibu,
"Kuna daktari alisema tumpeleke mtoto leo ila Sabrina alisahau ndiomana nikamfata"
Mama yao akawaitikia ila shangazi mtu alitikisa kichwa na kutaka kuongea jambo, ila kabla hajaongea Sabrina alishamvuta mkono Sam ili waondoke kwani alishayaelewa maneno ya shangazi yake siku hizi na akajua wazi atakachozungumza kama sio cha kumuharibia yeye basi kitakuwa chochote kibaya.
Kwahiyo Sam na Sabrina wakatoka nje na kuondoka.

Safari ikawa nyumbani moja kwa moja.
Walipofika walishuka na kuingia ndani, Sam alimuangalia Sabrina na kumuona yupo sawa na wasichana wengine ambao yeye aliwaona kuwa hawana akili ingawa mwanzoni alimuona kama mwanamke wa tofauti kabisa.
Akamwambia,
"Kamlaze mtoto Sabrina"
"Huyu ataamka muda sio mrefu sababu amelala sana"
"Una uhakika gani kama amelala sana? Umekaa nae muda wote leo?"
Sabrina akakaa kimya na kwenda kumlaza mtoto huku akijihoji kama arudi sebleni au la, lakini Sam alimuita na kumfanya arudi sebleni.
"Sabrina naomba leo nikuulize tena hili swali, hivi una akili kweli wewe?"
Sabrina akamuangalia Sam na kutikisa kichwa kama ishara ya kuitikia alichoulizwa.
"Umeona sasa, nakuuliza kwa mdomo unanijibu kwa kichwa. Hivi nikisema huna akili nitakuwa nakosea?"
Sabrina hakuweza kujibu na kukaa kimya, akampa Sam nafasi ya kuongea,
"Hivi nikupe nini wewe mwanamke utambue upendo wangu kwako? Nikupe uhai wangu au nikupe kitu gani Sabrina? Kwanini umekuwa ni mtu wa kutesa moyo wangu kiasi hiki?"
Sabrina aliinamisha kichwa chini kwa aibu,
"Niambie Sabrina, nikupe nini uridhike? Haya sasa mimba ya kwanza ulibakwa na hujui ya nani, ya sasa hivi je?"
Sabrina akatokwa na machozi kwani aibu na uoga vilimshika na kumfanya ashindwe kujibu chochote.
Muda kidogo mtoto alianza kulia ndani na kumfanya Sabrina aende kumchukua na kuanza kumnyonyesha.

Nyumbani kwakina Sabrina nako hali haikuwa nzuri kutokana na maneno ya shangazi yao,
"Kwakweli mimi kukaa kimya siku zote sitaweza, ipo siku nitasema ukweli tu"
Mama wa Sabrina alimuangalia wifi yake kwa jicho la chuki ya wazi wazi kwani yeye hakupenda mwanae aathirike kisaikolojia kabisa.
"Ila wifi yangu kwanini unakuwa hivyo jamani? Hayo mambo si yalishapita tayari ila wewe kutwa kucha kuyafufua sijui una matatizo gani wewe. Najuta hata kumpa mwanangu jina lako"
Muda huo James na mkewe Joy walikuwa wanajiandaa kuondoka, shangazi mtu akaona kachukizwa na kuwaambia,
"Nyie watoto kabla hamjaenda nina mazungumzo nanyi"
"Uzungumze nao nini sasa? Mbona unapenda kukuza mambo jamani? Ndiomana kipindi kile ukasumbuliwa na majini kwa umbea wako"
"Aaah mie mbea wifi? Leo umeamua kunitusi si ndio, sasa subiri nitakuonyesha umbea wangu vizuri ulivyo"
Shangazi akawa amechukia na kuchukua mkoba wake na kuondoka.
James na Joy walipotoka ndani wakashangaa kutokumkuta, James akamuuliza mama yake,
"Shangazi yuko wapi?"
"Achaneni nae yule, huwa ana matatizo kwenye akili yake"
James hakutaka kumuhoji zaidi mama yake kwani alimuona tayari akiwa amevimba kwa hasira.
Kwahiyo wakamuaga na kisha wao kuendelea na safari yao kwa wakati huo.

Sam naye aliingia chumbani na kumuangalia Sabrina akimnyonyesha yule mtoto.
Kisha Sam akawa kama anamchungulia mtoto na kusema,
"Mtoto ni mzuri sana, Mungu amsaidie asifate tabia yako"
Sabrina akamuangalia tu Sam, muda kidogo simu ya Sam ikaanza kuita, kuangalia mpigaji alikuwa ni mama yake.
Sam aliongea na ile simu huku akitabasamu ila kiuhalisia alikuwa akifikicha macho.
Alipomaliza kuongea nayo akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Mama anakusalimia sana"
"Nashukuru"
Simu ya Sabrina nayo ikaanza kuita na aliyekuwa anapiga kwake alikuwa ni mama yake, Sam akamwambia Sabrina aweke sauti kubwa ili naye amsikie.
Sabrina hakusita na kuweka,
"Sabrina, hivi bado unamnyonyesha huyo mtoto?"
"Ndio mama"
"Muachishe ziwa mwanangu, si u mjamzito wewe!"
"Kwani kuna tatizo mama?"
"Ndio ni  tatizo, utamuharibu mtoto. Nenda umtafutie maziwa ya kopo ya watoto au ya ng'ombe umpe ila usimnyonyeshe tena"
Kisha wakamaliza maongezi yao, Sam akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Starehe zako na tamaa yako vinakuponza sasa, vinafanya mtoto wako akose haki yake ya msingi. Hivi Sabrina ulijifikiria nini hadi kubeba mimba tena? Tena mimba isiyokuwa ya mumeo? Ulijifikiria nini Sabrina?"
Sabrina hakujibu ila alikazana kumnyonyesha mtoto,
"Hivi alichoongea mama yako hujakisikia au ni nini?"
Sabrina machozi yakamtoka,
"Nisamehe Sam"
"Sio nikusamehe, mtoto huyu kila siku anaharisha kumbe ni sababu ya maziwa yako machafu unayomnyonyesha. Muache nikamnunulie maziwa"
Sam aliinuka na kuondoka.
Sabrina alijifikiria sana, alishindwa kujielewa mambo anayoyafanya.
Alimuangalia mtoto wake, aliangalia tumbo lake kisha machozi yakamtoka.
Ila muda wote alijiuliza,
"Je haya ni mapenzi? Sielewi, huyu Sam simuelewi"
Alijiuliza tu na alikuwa ameshika tama hadi pale Sam aliporudi na maziwa ya kumkorogea mtoto.
Walimpa mtoto maziwa na kulala bila ya kuongezea neno lolote lile.

Kulipokucha, asubuhi na mapema kama kawaida Sam aliinuka na kujiandaa kisha kuondoka.
Sabrina hakuwe9a kuuliza ingawa alijua wazi kuwa ile ni siku ya mapumziko yani mwisho wa wiki ila anaanzaje kumuuliza ikiwa tayari anamajanga.
Sam alipoondoka, ndipo Sabrina nae alipoinuka na mtoto na kuanza kumsafisha.
Alipomaliza kazi zake za hapa na pale, akataka kutoka nje angalau akaone mwanga wa jua.
Ila alipojaribu kufungua mlango wa kutokea nje akaona mlango ni mgumu na kugundua kuwa umefungwa kwa nje.
Akajiuliza kuwa kwanini mlango ufungwe, akaenda dirishani na kufungua dirisha kisha kumuita mlinzi ambapo mlinzi alifika na kumsikiliza,
"Mbona mlango umefungwa kwa nje?"
"Sijui kwanini, ila mzee mwenyewe alisema kuwa umpigie simu na kumuuliza yeye"
  Sabrina alitulia kidogo na kurudi kukaa sebleni huku akijiuliza kuwa kwanini Sam amfungie nje? Na kumuuliza alishindwa na kujipa moyo tu ndani kuwa amsubirie arudi.

Dorry baada ya kuona kuwa hakuna chochote alichoulizwa na Sakina, akaamini kuwa Mungu amejibu maombi yake kwa kumfanya Sakina asijue chochote kuhusu ile mimba kuwa haihusiani na mtoto wake.
Muda kidogo Sakina mwenyewe akampigia simu,
"Nimekukumbuka sana Dorry, utakuja lini mwanangu?"
"Nitakuja mama, usijali"
"Vipi na mjukuu wangu tumboni huko anaendeleaje?"
Dorry akacheka kidogo na kujibu,
"Anaendelea vizuri tu"
"Uje jamani, mwenzenu nimewakumbuka huku. Napatwa na majanga peke yangu ila mkija nyie itakuwa kheri"
Dorry akafurahi na kumuahidi Sakina kuwa ataenda kwake hivi karibuni.

Sakina alipomaliza kuongea na Dorry, akampigia simu Sabrina.
Ila alimshangaa Sabrina kuwa mnyonge vile.
"Ila mdogo wangu ubishi utakuponza, mi nilikwambia kuhusu yule mtaalamu umekataa bure tu. Mwenzio toka siku ile mauzauza hayapo tena, watu wabaya sana duniani. Yule mtaalamu anasaidia mdogo wangu"
"Sawa dada nimekuelewa, basi acha nifikirie kwanza"
"Fikiria mdogo wangu na utakapokuwa tayari niambie nikupeleke, yani mwenzio hapa naishi kwa amani na furaha saivi, yale mauzauza hayapo tena"
Walipomaliza mazungumzo yao na kuagana, Sabrina akaikata ile simu na kuwaza kuwa huenda mtaalamu huyo anaweza kumsaidia,
"Hofu yangu ni moja tu, hawa wataalamu hawakawii kunipa masharti ambayo hayana maana yoyote kwangu. Mi nawaogopa jamani ila nitaangalia tu"
Alikuwa akingoja kuona pale atakapofika mwisho kabisa wa mawazo yake basi ndio akubali kwenda kwa huyo mtaalamu.

Mama wa Sabrina akiwa ametulia nyumbani kwake, muda kidogo akajiwa na ugeni na kumfanya ashangae.
"Kheee James!!"
"Ndio ni mimi, au unadhani umeona mzimu? Maana siku ya mahari ulizimia"
Mama wa Sabrina    alikaa kimya na kumkaribisha.
"Karibu sana"
"Asante nimeshakaribia"
Moja kwa moja James akaingia ndani na kukaa, kisha akamwambia mama wa Sabrina,
"Joy, nimekuja kwako leo. Naomba uniambie ukweli wa mambo yote"
"Unamaanisha nini? Mbona sikuelewi?"
"Hunielewi nini? Niambie ukweli kuhusu mtoto wangu Joy, mi sielewi yani sielewi kabisa ila nimeambiwa kuwa kuna mtoto wangu na ukweli wote unaujua ila ulinificha, tafadhari nakuomba Joy niambie ukweli"
"Hivi ni nani amekwambia hayo maneno James jamani? Nani huyo aliyekuletea hayo maneno ya uongo jamani?"
"Joy, mtu aliyeniambia ni wa kuaminika kabisa. Tafadhari niambie wewe mwenyewe ukweli kabla sijagundua kwa namna nyingine"
Joy akafikiria na kuona wazi kuwa kuna uwezekano wifi yake Sabrina atakuwa ameyapeleka yale maneno kwa James.
Hata hakujua ni kitu gani amwambie huyu James ili aweze kumuelewa ikiwa tu ameshaambiwa kila kitu.
James akamshtua tena kwa kumwambia,
" Nangoja ukweli Joy tafadhari niambie"
Muda kidogo akasikia mlio wa gari, kuangalia alikuwa ni mumewe amekuja yani baba yao na wakina Sabrina.

Sam alikuwa maeneo ya baa na mmoja wa rafiki zake, ambapo alimshangaa Sam kwa ule muonekano wake wa siku hiyo,
"Hivi Sam mbona leo upo hivyo? Unaonekana kuwa na mawazo"
"Ni kweli nina mawazo, zamani nilikuwa nashangaa sana kusikia mume kaua mke na watoto wake. Kumbe huwa kuna sababu nyuma ya pazia inayompelekea kufanya hivyo"
Rafiki wa Sam aliyashangaa maneno ya Sam na kumuuliza,
"Sijakuelewa Sam, unamaana gani?"
"Maana yangu ni hiyo hiyo unayoifikiria wewe"
"Nieleweshe tafadhari"
"Aaaah tuachane na hizo mada, hapa tunywe halafu kila mmoja akapumzike kwake"
Muda kidogo Sam akaonekana kama akifikiria kitu fulani kisha akainuka na kumuaga rafiki yake kuwa anarudi nyumbani kwake.

Sabrina akiwa amekaa sebleni kwa muda huu bila ya kuwa na habari yoyote   zaidi ya kufikiria matatizo yanayomkabili.
Muda kidogo akasikia mlango ukifunguliwa, kisha Sam akaingia ndani.
Akamsogelea Sabrina na kutoa bastora kisha akailengesha kwenye kichwa cha Sabrina na kumfanya Sabrina ashangae sana kuwa Sam amepatwa na nini.
Muda huo huo simu ya Sabrina ikaanza kuita, akamsikia Sam akisema kwa ukari
"Pokea hiyo simu Sabrina na uweke loudspeaker"
Sabrina alipoiangalia ile simu akaona ni namba ya nchi za nje, moja kwa moja akapatwa na hisia kuwa mpigaji atakuwa ni Jeff na kumfanya atetemeke zaidi.

Itaendelea



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa