CHOMBEZO:MPANGAJI EPISODE: 13 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Friday, February 14, 2020

CHOMBEZO:MPANGAJI EPISODE: 13





Ilipoishia jumamosi…

“Ehee. Prince. Hawa ni wanangu,huyu mkubwa anaitwa Farida Donyo,huyu anaemfata anaitwa Sheila naye ni Donyo na huyu wa mwisho anaitwa Lilian.

Songa nayo sasa..

Wote naishi nao hapa na ninaomba uishi nao kwa amani sana. Uwalinde kwa kila kitu. Pia na nyie mfanye vivyo hivyo,mumuheshimu huyu kijana,sawaa?”.Mzee Donyo akatoa wosia huo mfupi kisha akawaruhusu wanawe waende kuendelea na shughuli huko nje.
“Najua utajiuliza kuhusu mke wangu. Sina mke,alishafariki miaka kumi iliyopita wakati anajifungua Lilian. Huyu Lilian nimempa jina la mama yake,yule pale”.Mzee Donyo aliongea huku akionesha picha moja ya ukutani kwa kusema yule ndiye mkewe.
“Pole sana mzee. Na nadhani tutakuwa pamoja sana”.Nilimfariji mtakatifu mimi.
“Sawa kijana. Wewe ukiwa na shida,ongea na hao watakusaidia. Kama unataka kwenda sokoni,kupika au jambo lolote la kike,waombe hao.Ila heshima muhimu,sitaki ujinga ujinga ufanyike,sawa kijana?”.Mzee Donyo aliendelea na ushauri wake.
“Nimekusikia mzee,na nimekuelewa. Ondoa shaka kuhusu mimi”.Nilimpa moyo Mzee Donyo japo nilijua ni lazima mwanae mmojawapo atafia kifuani kwangu. Watoto wazuri vile halafu unaleta habari za kuwaheshimu. Kanifanya mimi sina nanihii eeh,na baridi lile la Arusha,kama ni kesi na iwe,wakijirengesha natungua hata wote wawili.
“Sasa ngoja mimi niende huko kanisani,nadhani tutaonana baadae mida ya jioni,ukae salama”.Mzee Donyo aliniaga na mimi pia nikatoka mle ndani kwake na kuelekea kwangu ambapo moja kwa moja nikafikia kwenye TV na kuanza kucheki chaneli zilizopo kwenye king’amuzi kile cha DSTV.

Nilipata stesheni moja ambayo ilikuwa inapenda sana kuonesha mpira. Na siku hiyo,ilikuwa inaonesha mechi moja nzuri sana ya marudio kati ya Manchester United na Arsenal.
Enzi zile Arsenal alikuwa hajapoteza michezo karibu Arobaini na Tisa.Alikuwa yupo vizuri sana. Kule mbele alikuwa TH-14 au Thiery Henry,halafu kulikuwa na kapteni mmoja mkorofi sana anaitwa Viera,huyo alikuwa hana utani.
Aliwahi kumtandika vipepsi Rud Van Nistorooy au Rud Van Magoli,kisa Rud alijidondosha eneo la hatari na kupata penati ikiwa bado dakika kama mbili za nyongeza kuisha,kwa bahati mbaya penati ile United walikosa,hivyo ikawa suruhu.
Katika mechi ile niliyokuwa naiangalia,ndiyo ilikuwa ni mechi ya hamsini kwa Arsenal,yaani angeshinda ile,alikuwa anaweka historia ya kucheza mechi hamsini bila kufungwa.

Lakini enzi hizo unawakuta watu kama Roy Keane katikati,kwa mbele Paul Scholes,kuna Giggs pembeni,mbele kuna Ruud Van Nisterooy,thubutuuu. Utapita uende wapi,tuliwapiga kimoja cha afya. Mimi ni United damu, ile mechi tulipigiwa kandanda bwana.
Ila kweli Arsenal alikuwa wafalme wa soka kwa ligi ya Uingereza,lakini mimi sifa nazipeleka kwa Manchester United kwani alituvua ule ufalme wao.

Watajigamba wawezavyo kuwa walicheza mechi arobaini na tisa bila kufungwa,ila pia wasisahau kuwapa pongezi waliofanya historia yao kukatishwa. Kwani wasipofanya hivyo,ni sawa wanakuwa kama wanajisifia kuwa wao ni wakali na wakati wakali ni wale waliowagonga.
Hayo ni ya kimechezo zaidi. Ila Arsenal walinywea sana baada ya kukatishwa mbio zile na timu kama Manchester,timu ambayo sasa hivi inatishia sana amani hapa duniani. Ila na Arsenal wanakuja vizuri,wajipange wapinzani.
Baada ya mechi ile kuisha,nilielekea kwenye jokofu la mle ndani kama kawaida na kuchukua juisi moja ya box inaitwa Cares. Ile ilikuwa ni ya Zabibu.
Nikaanza kuinywa taratibu kijana mie,wala nilikuwa sina na wasiwasi na mtu,sijaua wala sina deni,basi acheni nienjoy maisha ya Arusha. Juisi ilikuwa ni nyingi na ni tamu sana.
Nikaamua utamu ule niende nao hadi nje kwenye kibaraza kimoja pale nyumbani. Nikaendelea kuburudika na kile kinywaji huku natumiana meseji na rafiki yangu mmoja niliyesoma naye Tabora Boys,wakati huo yeye alikuwa anaingia mwaka wa kwanza chuoni.
Aliniambia mengi sana,na alinisihi nirudi darasani kwaajili ya kujiendeleza kimasomo. Ila mimi kwa kuwa niliamini kaka na wazazi wangu wana uwezo,basi hata bila elimu, naweza kuishi kwa mgongo wao. Nikasahau kuwa mambo yanabadilika na kuna kipindi kila mtu hukaa pembeni na kujali maisha yake.

Hayo sikuyajua,ila nilikuja kuyajua na kuyapitia baada ya kutoka pale Arusha. Arusha hiyo hiyo iliyonifanya wanawake niwaone wachungu katika maisha yangu. Na ni Arusha hii,iliyonifanya nigundue mengi ambayo niliyaacha huko nyuma. Hii ndiyo Arusha iliyonifanya niuite mkasa huu mpangaji,na mwisho kabisa,Arusha ndiyo ilinifanya nikapige magoti kwa wazazi wa Maimuna. Utanielewa nachomaanisha,kuwa na subira.
Taratibu P wa watu nikawa najinywea Cares yangu huku nikijikita zaidi kwenye kutuma meseji nyingi kadiri niwezavyo. Mawazo yale niliyoyaweka kwenye simu,yakanifanya nisahau ya duniani kabisa.
“Wewe,khaa! Hata kusema upo bize,wewe too much pilipili”.Nilishtuliwa na sauti ya kike iliyoambatana na kofi moja dogo ambalo ni kama lilinitoa mawazoni.
“Ahaa,Farida. Samahani Bibie. Nilikuwa nachat na baba bwana,halafu alikuwa ananipa mikakati mizuri sana,na ndio maana akili yangu ikahamia hapa”.Nilijitetea kwa mtoto yule mzuri.
“Okey. Sisi tunataka kwenda sokoni mara moja”.Farida aliniambia huku pembeni akiwa na yule Lilian,mdogo wake wa mwisho.
“Poa. Mimi nipo hapa,naendelea kuchat”.Nilimjibu Farida na kuendelea kubofya-bofya simu yangu.
“Kwa hiyo hutaki kulijua jiji au?”.Farida aliniuliza na kunifanya nijione kama mjinga vile.Yaani mwanamke anakuja kwangu na kuniambia anaenda mahala,eti namwambia poa. Hanijui wala simjui,sikuweza hata kujiuliza kwa nini kaja kuniaga?
Hapa na maana kwamba,mwanamke asiyekujua akaja kwako na kukuaga au kukuuliza kama unaenda sehemu fulani,basi ujue anataka kitu. Eidha umsindikize au akuagize kitu fulani.
“Dah! Aisee kweli. Embu nichekie hiyo juisi,ngoja nikavae koti kwanza”.Nilimwambia Farida na kisha nikaingia ndani. Nilipotoka,nilikuwa nimevaa koti moja jeusi la leiza ambalo nililinunua Dar es Salaam pale Karume.
“Daah! Umendeza kweli mwenzetu”.Farida alinisifia baada ya kuniona nimevaa lile koti. Wakati huo,huku kwa ndani nilikuwa nimevaa tisheti moja iliyonikamata vizuri kama mwanamiereka. Halafu suruali nilipiga modo moja matata sana,ilikuwa ya buluu. Nyie niacheni mazee,mimi nilikuwa napiga pamba balaa. Hawa unaowaona sasa hivi,wanakurupuka tu!
“Mbona hata wewe umependeza tu! Tena umetoka ile mbaya. Kama Mary J Bridge au Keisha Cole”.Na yeye nilimsifia huku tukianza kutoka eneo lile la uzio wa nyumba ile na kuitafuta njia ya kutupeleka tutakapo.
“Ha ha haaa,sifa za kitoto hizo. Ila siriazi kaka umetoka”.Alisitiza kauli yake Farida.
“Haya bwana. Au nikupe umetishe na kofia nini?”.Nilimuuliza kwa kumtega kwa sababu na yeye alikuwa kavaa kofia ya leiza,ambayo ilikuwa imempendeza balaa. Wakati wote,yule mdogo wake alikuwa kimya tu!.
“Nitafurahi wewe,hayo makoyi nayapendaje?”.Hakuwa nyuma kuonesha hisia zake. Basi na mimi si mwajua navyopenda misifa,sikujali kama nimevaa kujikinga baridi lile la Arusha au vipi. Nikatoa lile koti na kumvisha mtoto yule mzuri,mzuri, mzuri,mzuri kupitiliza.
“Kumbe zito hivi?”.Aliuliza baada ya kulivaa.
“Ha haa,kwani hujui hilo?”.Na mimi nikauliza kama kumjibu.
“Mmh!Nilikuwa sijui mwaya”.Alijibu huku anarembua kiaina.
“Mmh”.Nikaguna kamanda.
“Nini tena?”.Akauliza.
“Kwani nini?”.
“Mbona umeguna?”.
“Ha haa. Hayo macho yako bwana. Eti sijui mwaya. Macho kama yanadondoka”.
“Ha haaa,kumbe na wewe wamo eeh”.
“Aaah wewe. Mimi nimesema tu!”.
Haya bwana. Palee ndiyo sokoni”.Farida alinioneshea sehemu moja kwa kuniambia ndiyo sokoni. Sisi hatukuenda huko,tukaingia chocho moja na baadae tukatokea sehemu moja haina maduka sana kwa pale mtaani.

*****Episode ya 13 inaendelea....*****



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa