Watu wengi walikuwa wanatuangalia mimi na Farida wakati tunatembea. Tulikuwa tunaendana sana. Kuanzia urefu,mavazi na maumbile yetu. Wale wasiyonijua,wengi wao walishindwa hata kumsalimia Farida kwa kuhofia labda mimi ni mpenzi wake.
“Farida ndiyo Shem nini”.Dada mmoja alimuuliza Farida baada sisi kuanza kuondoka kwenye duka mojawapo la mtaa ule.
“Aaah,huyu kaka yangu tu!Kaja jana”.Farida alimjibu dada yule na hapohapo tukaanza kuondoka.
“Kwa hiyo ndo unasepa mwenyewe hata kunitambulisha? Tabia mbaya hiyo Farida”.Dada yule alimwambia Farida na kumfanya Farida arudi na mimi pale alipokuwepo dada yule.
“Kaka mimi naitwa Cindy au Cinderela.Farida ni best wangu tangu O-Level”.Dada yule mchangamfu alianza kujitambulisha.
“Na mimi naitwa Prince au kifupi,niite P yatosha. Nipo kwenu mara moja”.Nikamjibu huku nampa mkono wa salaam.
“Basi karibu handsome. Nadhani tutazidi onana”.Dada yule aliniambia huku akiniachia mkono wangu.
“Poa Cindy. Tutaonana”.Nilimjibu.
Baada ya salaam ile,tulianza kutokomea eneo lile huku tukiacha masharobalowa mtaa ule mimacho kodo kama wanacheki filamu ya ngono.
“Kaka P,naomba uninunulie ubuyu”.Lilian,yule mdogo wa mwisho wa Farida aliomba ubuyu baada ya kuuona unauzwa mitaa ile.
Nikajipekshina kutoa mia tano na kumpa akanunue.Akaipokea na akakimbia mara moja kwenda kununua ubuyu huo.
“P. Kuwa makini na midada ya huku,itaanza kuja kuja kwako halafu baadae itakuibia. Jichunge sana,usilete mazoea nao hata kidogo”.Farida alinikanya baada ya mdogo wake kuondoka.
“Zuga tu ile. Unadhani ataniona tena?Hapa ndio kaula,sitoki tena nyumbani. Nimekuja kupumzika na si kuzurura huku”.Nilimjibu huku tunaendelea kwenda kidogo kidogo kwa nia ya kutomuacha sana Lily.
‘Haya bwana.Ukiwa na shida utatuambia”Farida alimaliza maongezi na hapo,stori nyingine zikaanza kushika nafasi yake.
“Hivi juisi yako ipo wapi?”.Farida akaniuliza.
“Ishi! Halafu kweli,si niliwaachia pale?”.Na mimi nikamuuliza huku nikiwa nataka aniambie ukweli.
“Mimi sijui,labda umuulize huyu”.Farida alinijibu huku akicheka na kumuoneshea kidole mdogo wake ambaye tayari tulishaungana katika safari ile.
“Muongo dada. Wakati yeye mwenyewe alikunywa”.Dogo akajibuna kumsababishia kicheko kikubwa Farida hadi yale meno yake yaliyopangana kwa ustaarabu mdomoni mwake,yakaonekana.
Nilisimama huku namshangaa Farida ambaye alikuwa anaenda huku anazidi kucheka.Nikaanza kumfata kwa kasi kumuelekea. Alipoona hivyo,akaanza kukimbia huku anaendelea kucheka. Na mimi nikaanza kumkimbiza.
Yaani ungeona wewe tulivyokuwa,kama picha la kihindi,tena lile la mapenzi. Mtoto anakimbia na mimi namfuza kwa nyuma. Nilipomkaribia,nikashika lile koti lakini kwa bahati mbaya,Farida akadondoka,lakini si kivilee hadi labda aumie au achafuke.Kwanza alikuwa hakimbii kama Mrisho Ngasa bali kama kinyonga,na kile kisketi chake kifupi alichovaa na kumkaa vema,basi mtoto ni kama malaika. Kila kijungu kidogo kwa nyuma,daah! MUNGU anipe nini P?
Basi ile kudondoka,akachubuka kidogo sana kwenye goti. Akawa anadeka mwenyewe.
“P,umeniumizaa”.Hapo jicho lake lipo kama mrenda.
“Hamka bwana. Pole eeh”.Nilimjibu huku namnyanyua ambapo alinyanyuka na kuanza kutembea kama anachechemea.
“Umeniumiza kweli P”.Alizidi kudeka,hapo bado kama nyumba mbili ili tufike nyumbani.
“Ndani ipo spirit,ntakupa upake”.Nikampa moyo.
“Weee,spirit nini?Sipaki”.Alikuja juu hadi nikacheka.
“Sasa si kidonda hicho?”.Nikamwambia.
“Weweee,hata kama,ndio upake spirit”.
“Poa basi. Ntakupa bandeji”.
“Hapo sawa,hayo maspiriti yako,paka vitoto vyako vya ndevu”.Alinijibu na muda huo tulikuwa tayari tumefika nyumbani.
Wakati wote tunatembea baada ya kujidondosha,nilikuwa nimemshikilia vizuri kutokana na maumivu ambayo alisema anayasikia. Hivyo nilipofika nyumbani,nilimuachia na kuingia ndani kwa ajili ya kumletea bandeji. Sikujua nini kiliendelea kule nje,ila baada ya dakika mbili ya mimi kuingia mle ndani,Farida naye alisukuma mlango wangu na kisha akaingia kunikuta mimi nipo sebuleni napekua kutafuta zile bandeji.
Nilipogeuka kuangalia nani kaingia,ndipo macho yangu yalitua kwa mtoto Farida. Sikujua alibadili zile nguo saa ngapi,ila nachojua alibadili nguo na kuja kwangu. Na alifanikiwa kwa mavazi yale.
Alikuwa kavaa khanga ambayo aliivaa kiheshima sana tu!. Ila kwa huku juu sasa,dah! Nyie acheni tu! Wanaume tuna kazi kubwa sana ya kuepuka haya majaribu.
Alikuwa kavaa sijui niseme gauni au nini. Ila ni kama gauni,sema lenyewe lilikuwa lina vifungo kwa mbele. Yaani vifungo vyake vilianzia kifuani hadi lilipoishia lile gauni ambalo lilikuwa katika mtindo wa jinzi. Nashindwa kueleza jinsi lilivyokuwa lile vazi,lakini kwa kukusaidia tu,lipo kama ovaroli,sena lenyewe ni gauni.
****
:: Unavyodhani Prince atafanyaje hapo?
::Usikose Episode ya 14.....
No comments:
Post a Comment