MBALI na tofauti ya kijinsia, mwanamke na mwanaume wametofautiana maeneo kadhaa. Utofauti huu una sura mbili muhimu.
Sura ya kwanza, huwa ndio chanzo cha furaha, raha na amani katika mahusiano. Ila sura ya pili, ndio huwa kisababishi cha migogoro na sintofahamu iliyopo katika mahusiano mengi.
Utofauti wa kufurahisha ni pamoja na ulaini wa umbile la mwanamke na ugumu umbile la mwanaume. Tofauti hii ndio huleta chachu na hamasa katika mapenzi.
Ila pia utofauti wa jinsi ya mwanamke na mwanaume ndio chanzo cha kuanzisha familia na kupata starehe ipasayo.
Leo nataka tuzungumze juu ya tofauti moja ya iliyopo kati ya mwanamke na mwanaume inayoleta hamasa ya migogoro na sintofahamu. Tofauti inayohusiana na namna ya kuhimili na kuwasilisha hisia.
Kiasili mwanamke ni kiumbe muwazi sana katika kuwasilisha hisia zake huku pia akiwa ni kiumbe mwepesi sana kujua hisia za mwanaume.
Mwanamke akiwa kakerwa atapenda kuongea ama kufanya jambo litakaloonesha namna alivyo na hasira. Mfano, mwanamke aliye katika mitandao ya kijamii akikerwa na mume wake ama mpenzi wake, angalia post zake.
Mara nyingi atapenda kukosoa juu ya tabia na mienendo ya wanaume ama ataongea jambo litakaloonesha yuko katika hali gani ya kihisia.Hii ni tofauti na wanaume.
Mara nyingi mwanaume akiwa katika hali inayofanana na hiyo, anaweza kwenda bar kunywa pombe kama ni mlevi ama ataamua kwenda kujichanganya na rafiki na jamaa zake ili kuweza kuipoteza hali hiyo.
Pia kutokana na mwanamke kuwa kiumbe mwenye uwazi katika kuonesha kilichopo katika nafsi yake, huwa hawezi kukaa kimya akihisi mume ama mpenzi wake anafanya au amefanya jambao linalomkera.
Na hapa ndio kunapoleta utata katika mahusiano mengi. Mfano, mwanaume anaweza kuwa kuna kitu jana alimkosea mwenzake na wakaongea na akamini yameisha.
Ila kama mwanamke husika hakupata muda wa kutosha wa kuzungumza ipasavyo ama kufanya jambo lililomsaidia kumtoa hisia zake, anaweza kutaka kuzungumza tena na leo kuhusiana na jambo hilo. Kitu ambacho wanaume mara nyingi hawapendi.
Hapa mwanamke anaweza kuwa anataka kuzungumza jambo husika ili kuonesha namna alivyoumizwa nalo kitu ambacho pia kitamsaidia kumuweka sawa kihisia, mwanaume naye kwa sababu ya kimaumbile anakuwa hataki kusikia akisemwa tena kwa sababu inamfanya ajione dhaifu na mkosaji.
Na katika kutekeleza hili, mwanaume husika unaweza kuta hayapi mazingatia maneno na lawama za mwenzake jambo ambalo mwanamke kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusoma hisia za mtu analigundua na linamuumiza zaidi kwa kuhisi ana dharaulika na hana thamani na maana katika maisha ya mwenzake.
Mwanamke anapenda kumsema aliyemkosea ila pia mwanaume hapendi kusemwa semwa akikosea. Utofauti huu umefanya wanaume wengi kusema wanawake wana gubu na wanawake wengi kusema wanaume ni viumbe visivyojali na kuthamini hisia za mwanamke.
Tofauti hii imesababisha watu wengi kuachana ama kuishi huku kila mmoja akimuona mwenzake ni wa ovyo huku kwa wengine ikiwa imeleta matatizo makubwa na kufanya waaamini uongo kuwa siku hizi hakuna mapeniz ya kweli.
Mwanamke na mwanaume wana tofauti nyingi sana za kimsingi ambazo wakati mwingine zinasababisha malumbano na gomvi katika mahusiano.
Unapopitia changamoto katika mahusiano acha kulaumu ama kudhani mwenzako hakuhitaji. Ebu fikiria tabia za jinsia ya mwenzako kwa kina. Je, ni tabia tu ya mwenzako ama hiyo ni tabia ya watu wa jinsia yake?
Wakati mwingine unaweza kutaka kuachana na mwenzako kwa sababu ya tabia fulani kumbe tabia hiyo ni tabia za jinsia yake. Badala ya kufikiria kuachana tafuta ushauri wa kitaalam ujue tatizo ni nini na njia gani zinaweza kutumika katika kuzikabili
WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments:
Post a Comment