Nawashwa Chini 20 (Mwishoooo) - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, January 30, 2020

Nawashwa Chini 20 (Mwishoooo)






SEHEMU________ 20

wakati mwingine mapenzi hayapangiwi uchague wapi wapi uache, chagua kile unachoona kinakufaa kulingana na moyo wako unavyohitaji, pengine ukachaguliwa kitu kisichofaa ukabaki ukilaumu kwanini nilikubari kuchaguliwa, nilichogundua katika mapenzi kuwa kuwa na wapenzi wengi au michepuko sio suruhisho la uhusiano wako bali ni uharibifu wa uhusiano wako, moyo wenye hisia ni mmoja utapendaje watu wengi, penda mmoja akikumwaga basi huenda haikuwa riziki yako, naimani utalia sana ukilaani mapenzi nakusema hutopenda tena lakini utakuwa unaidanganya nafsi yako mwenyewe, moyo huumia lakini pia moyo huifadhi hayo hayo mapenzi, mapenzi ni jambo kubwa ndani ya moyo na ndio imezunguka kwenye mioyo ya watu wote duniani usiamini kwamba moyo husukuma damu pekee, bali moyo husukuma hata mapenzi pia, kuumia ndani ya mapenzi ni jambo la kawaida ingawaje ni kitendo kinachokuacha na simanzi majonzi na kuyalaani mapenzi hasa kwa yule mtu uliempenda kwa dhati, pendo ni fumbo kumjua yupi mkweli yupi muongo haiwezekani na kwa dunia ya sasa hakuna mapenzi bila pesa yale maneno mazuri ya mahaba yaseme sana ila bila ya pochi nene ni bure, sawa mapenzi yapo ila sio yakweli, yote tisa ila kumi uamuzi mgumu unajitika sana na kaa nilivyosema sio kila kitu ukubali kupangiwa fata moyo wako vile unavyotaka alikuwa ni sehemu ya moyo wangu kila nilipojaribu kumuacha nilijikuta moyo wangu ukivuja damu na maumivu yake yalilitesa jicho kwa machozi yasio na kikomo, kweli nilimpenda sana maria boss susan licha yakufanya nae mapenzi lakini hakuwa na nafasi kabisa moyoni mwangu, nae jackrine vivyo hivyo.. siku hiyo nilionyesha ukweli wangu kuwa maria ndio chaguo la moyo wangu, maria ndio my only choise,
ni sauti ya jeff akimaliza kuwapa mkasa uliompata miaka ishirini iliopita, mtoto wake wa kiume aitwae bailon alimuuliza "lakini baba hujatwambia kuhusu jackrine siku hiyo ulipomkuta mama anataka kujiuwa" "aaah!! sorry nilisahau ngoja niikamilishe story" alijibu jeff, umri wake ukiwa umeenda sasa anamiaka arobaini na sita.. "mh! na nyie mnapenda kweli umbea?" alidakia maria mke wa jeff, "aaah!! mama tuhadithieni tu" watoto wote watatu waling'ang'ania, hivyo mama akaendelea kuwakangaia mayai huku baba nae akiendeleza story..
...jackrine aliuliza kwa dharau huku akinivimbishia kifua,sikutaka kumjibu nilizarau na kuingia ndani kumuokoa maria, nilikuta maria akiwa ameshaipiga sturi nakuanza kuning'inia. kwa kuwa kamba ilikuwa imeishika shingo yake vizuri ilinibidi nitoke haraka nakwenda jikoni nikachukua kisu nakurudi nacho chumbani kisha nikaikata ile kamba na maria alianguka chini huku shingoni akiwa ameumizwa vikari na ile kamba "kwanini unataka kujiua maria nambie kwanini??" nilimuuuliza maria huku nikimkumbatia "coz i love youuu" maria alijibu machozi yakimtoka "heeh!! jeff ndio nini sasa hicho unachofanya hapo??" aliuliza jackrine, niliamka kwa hasira huku maria akiwa amenikumbatia kwa nyuma nakumsogelea jackrine pale aliposimama. "unauliza ndio nini?? eeeh!! unauliza ndio nini??" nilimshika jackrine kwa hasira nikawa namtingisha tingisha huku nikimuuliza "Lakini mimi sinimpenzi wako jeff??" "toka lini??? mimi na wewe tumeanza mapenzi??" nilimuuliza "lakini jeff" "sio lakini wakwangu ni maria tu nimejitahidi kwa kila namna imeshindikana nampenda maria, kwa kile nilichokiongea asubuhi fanya kama hujasikia lolote" "kweli jeff??" "ndio nakwenye nyumba yenu naondoka kama ulifikrii nitaendelea kubaki hapa sahau naondoka na maria wangu" nilimjibu kisha nikamsukuma pembeni nakutoka muke chumbani, jackrine alikiona kile kisu pale chini alikiokota na kutoka nacho akiwa amekifich mgongoni nia yake afanye maamuzi magumu lakink bahati nzuri au mbaya mda huo nae boss wangu alifika akiwa na morine kisha akasema "umechagua njia nzuri mwanangu, kweli mapenzi hayalazimishwi hata kidogo licha ya kuwa mwanzo nilikuomba umuoe jackrine lakini nilifanya makosa makubwa, umegundua mapenzi yupi mwenye mapenzi ya kweli, mh! na leo ndio ilikuwa mwisho la lile shindano la mabinti wangu na maria umefanikiwa kuuteka moyo wa jeff hongera sana kwa moyo wako wa kujitolea muda wote," alisema boss lady kisha akamsogelea jackrine nakumpokonya kile kisu kisha akasema "asie na bahati milele habaatiki, n riziki y mwenzio usiilalie mlango wazi, maria amempta wake nawewe jackrinw subiria wako kwani subira yavuta kheri, jeff hakuwa chaguo lako, wewe chaguo lako litakuja siku moja" mama alisema. huku kila mmoja akilia kwa ujumbe wa mama "Nawabariki kwa moyo mmoja jeff na maria muishi mkikumbuka ujumbe wangu" alisema boss lady..
hio ndio siku ambayo niliweza kumpata mama yenu, niwapeni funzo wanangu hata kama utakuwa na wapenzi sita na wote ukawa unawapenda sio wote utawaoa yupo mmoja tu ambae ndio atakuwa chaguo lako la kweli. jifunzeni kupitia mkasa huu niliowasimulia ili na nyie yasije kuwapata yaliyonipata mimi enzi hizo. "aaah!! baba tumeinjoi sana na nimejifunza mengi pia, kwani baba hamna kastori kengine kazuri kama hako utusimulie??" mtoto mmoja aliuliza, "haahhah!! kaone kuleni mayai mkalale usiku umeenda sana" aliwajibu watoto wake,
Ahsanteni saaaana kwa wote mliokuwa nami tokea mwanzo hadi mwisho wa story hii kuisha kwa stori hii ndio mwanzo aa kuufungua ukurasa mwingine wa stori naimani utakuwa umepata funzo kupitia simulizi hii. ahsanteni sana tukutane katika simulizi nyingine nyingi zijazo  ..............



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa