Kwa nini baadhi ya wadada wanatafuta limbwata na madawa ya kuushika moyo Wa Mume wako na limbwata unayo wewe mwenyeo?
Limbwata ya kwanza:- _
JICHO LAKO
Unapomuangalia mumeo lainisha jicho liwe laini na mkiongea muangalie machoni na pa kurembua urembue.
_
SAUTI YAKO
Ongea na mumeo kwa sauti ya upole ya kubembeleza,sauti nyororo,usiwe mropokaji hakikisha kua unaweka sauti special kwa ajili yake.
_
MAVAZI YAKO
Unapokua na mumeo faragha Usivae madera na majuba , Vaa mavazi ya kimtego mtego , full kujiachia , Vimini ama jifunge kanga ama mtandio mwepesi au Vaa Nguo za Kulalia ( Night Dress ) - Inatosha sana Kumleta Karibu Kimahaba na akikubeep tu Mpigie.
_
UBUNIFU WAKO
Ubunifu kwenye mapenzi ni limbwata ya aina yake , Usifanye mazoea kwenye suala hili kila siku buni mbinu mpya, Usione tabu kusoma makala za wanasaikolojia ya mapenzi na Muda Mwingine hata kumuuliza Mwenzako anatakaje .
_
USAFI WAKO
Mara zote napenda kusisitiza juu ya hili - Usafi Wa chumba , Nyumba na mwili wako , hakikisha unakua msafi mda wote kwani huwezi kujua mda gani atakuhitaji.
_
MANUKATO NA MAPAMBO
Unaponukia unamfanya mumeo asogee karibu yako - Jihadhari Usinuke Maana manukato mengine yanakera Usimlazimishe Mwenzako hata kama wewe unayapenda na hakikisha kila kiungo kimevaliwa pambo lake stahiki.
_
MANENO MATAMU NA BASHASHA Wadada hakuna mwanaume anaependa gubu - acha tabia ya kununa nuna ovyo na Kuropoka ropoka mambo bila kupima uzito wake , neno NAKUPENDA MUME WANGU litamke kila Mara na mkumbatie bila sababu maalum - Kukumbatiana kunajenga mapenzi , Urafiki na kunaondosha hasira Usizozijuwa Pamoja na tofauti baina yenu .
_
MAPOKEZI MAZURI NA KUMUAGA VIZURI Jenga mazoea ya kumuaga kwa kukumbatiana na mabusu na uwe unamsindikiza , kumuombea dua na mpokee kwa bashasha na kumpa pole ya machofu anaporudi kutoka kazini.
No comments:
Post a Comment