ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA NANE : “nenda kamsikilize kaka kwani kuna ubaya” aliongea Jastin akijuwa fiki kuwa, Sophia akiingia ndani lazima azimie, mala tu! akimwona Malaika “ok! tangulia nakuja” aliongea Edgar na Sophia alitangulia kuingia bandani, ile kuingia tu! Sophia akakutana na Malaika, uso kwa uso, Malaika ambae alikuwa akimwona Sophia toka akiwa nje, alipokuwa amesimama na mpenzi wake Edgar, na alisha mtambua kuwa, ni yule mschana aliemkuta na Martin mala tatu, Sophia alipomwona Malaika alistuka na kutaka kutoka nje, lakini Malaika alimzuwia “hapana dada ingia tu!” Sophia akatulia na kwenda kukaa kwenye benchi pamoja na Malaika, walikaa pale kwa muda kidogo bila kuongea neno, ndipo Malaika akavunja ukimya “vipi bado unaendelea na Martin” Sophia ambae muda wote alikuwa amejiinamia akujibu kitu, adi Malaika alipo mwuliza kwa mala ya pili swali jingine, “eti dada, bado unampenda Edgar?” endelea ........
Hapo Sophia akainua uso na kumtazama Malaika, ambae aligunduwa kuwa, Malaika akuwa akiongea kwa kejeli, ila aliongea kwa upole na huruma, “nampenda sana Edgar, yani tamaha imeniponza, ninge juwa kama Martin ni shetani hivi, nisinge kubari kuwanae na kumwacha Edgar” aliongea Sophia kwa uchungu sana, huku sauti yake ikiashilia kilio cha chini chini, kwa hiyo unaitaji nini kutoka kwa Edgar” aliuliza Malaika, na Sophia akajuwa kabisa kwamba, nivigumu Malaika kumwacha Edgar iliamrudie yeye, japo ilo ndilo alilotaka, kiukweli Sophia akakosa jibu, “Sophia najuwa unafahamu ukweli, na mimi najuwa unacho mpendea Edgar, jinsi alivyokusaidia, na siyo kuwa unampenda, nikuombe kitu kimoja, niambie nikusaidie nini Katika maisha yako, kitakacho kufanya usimfwate tena Edgar” hapo Sophia akakosa tena jibu, wakati huo Edgar alikuwa anaingia kibandani, akawakuta Sophia na Malaika wakiwa wamekaa pamoja, “niambie Soph” aliongea Edgar akimtazama Sophia ambae alikuwa amejiinamia, kiukweli Sophia alishindwa kujibu, Edgar akamgeukia Malaika “mama mida ya chakula hii twende tuka jiachie nyumbani” aliongea Edgar, akimwambia Malaika, “ kweli wangu, twende tumpitie mama ofisini kwake, labda atatupa lift” aliongea Malaika kisha akamtazama Sophia, dada nakuomba kaa mbali na Edgar, kama unashida yoyote nitafute mimi nitakusaidia” baada ya hapo Malaika akisimama kisha kwapamoja yeye na Edgar, wakaondoka wakimwacha Sophia mle ndani ya kibanda, Edgar na Malaika wakaagana na Jastin kisha waka shika njia kuelekea ofisini kwa mama Malaika, njiani Malaika alijiahidi kujifunika na kofia kichwani ili watu wasi mtambue, lakini awa kujuwa kuwa kuna mtu anawa fwatilia, ni yule kijana wa Para, akawafwata kwa nyuma, kule walikokuwa wana elekea, Dakika chache baadae walikuwa ofisini kwa mama Malaika walimkuta bado anaangaika na kazi, Malaika akamsaidia, huku mama yake akiwasimulia ujio wa mama Martin, wakati wote yule kijana wa Para alikuwepo nje ya jengo, akiwa amesimama umbali wa mita chache, akiwasubiri kuona kama wata toka nakuelekea wapi, alitumia nusu saa akawaona wakitoka na kuingia wenye gari, wakiwa wote wa tatu, kisha gari likaondoka kuelekea upande wa mahenge, yule kijana akatoka mbio kule aliko wahacha wenzake, akawapa report, nao bila kuchelewa waka ondoa gari kwa mwendo mkari, kufwata barabara ya mahenge, ****** Wakiwa hawana taaarifa yoyote juu ya gari linalo wafuata nyuma yao, “nimepata wazo, ikiwezekana mkajifiche kwenye hotel yoyote, mpaka haya mambo yatakapo tulia” aliongea mama Malaika akiwa pamoja na Malaika na Edgar, wakiendelea na safari yao, ambapo walienda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Edgar, seed farm, wakasimamisha gari nje ya nyumba na kushuka, wakaingia ndani kila mmoja akionyesha uso wa furaha, awakujuwa kuwa kuna hatari nyuma yao, kwa hakiri za mama Malaika aliamini kuwa kitendo cha kumwambia mama Martin juu ya kuonekana kwama Martin na mzee Komba usiku, lazima mama Martin angewaambia watu wake nao wangeacha tabia hiyo, lakini kitu ndiyo kwanza aliwachochea, ***** shangazi naye tokea jumamosi akuwa na amani baada ya ndoa ya Martin kuvunjika na kushindwa kumuoa Malaika, alikaa kitafakari nini kimetokea, siku zote alishinda kwa kaka yake akinywa pombe, lakini kitu kilicho mshangaza ni furaha aliyonayo wifi yake mama Malaika, siku ya tatu leo, ashituki juu ya kupotea kwa Malaika zaidi ndiyo kwanza anaonyesha kuwa mwenye furaha, leo shangazi akaona bora akutane na mama Martin, amsimulie wasiwasi wake juu ya wifi yake kushiriki kwenye tukio hili la Martin kukataliwa kanisani, akajiandaa na kuelekea mfaranyaki kwa mama Martin ***** Nusu saa baadae tayari mama Malaika na vijana wake walikuwa ndani ya nyumba, wakati mama Malaika akiwa sebuleni amekaa kwenye lile kochi kubwa ambalo Edgar na Malaika wana penda sana kulitumia kwenye mambo yao, ya kupeana dudu, huku mezani amewekewa soup ya samaki, akipasha tumbo joto, sababu Malaika na Edgar walikuwa jikoni, wanapika chakula, wakati mwingine Malaika alikuwa akielekea sebuleni, na kumsemesha mama yake maneno mawili matatu, kisha anarudi jikoni, kuungana na Edgar, michezo midogo midogo ilikuwepo, japo Edgar alishindwa kujiachia mbele ya mama mkwe, dakika kumi baadae wote walikuwa sebuleni, chakula tayari kwenye ma hot port, kilichokuwa kina subiriwa ni kachumbari ambayo Malaika alikuwa anaitengeneza pale sebuleni, “yani hilo bakuri lote utalimaliza, kumbuka kuna minyoo” alitania mama Malaika kutokana na Malaika kujaza kachumbali kwenye bakuli kubwa sana la udongo, ambapo kwa sasa alikuwa anamalizia kukata vitunguu, ukaaji wao pale sebule, ulikuwa mzuri kidogo, mama Malaika alikaa juu ya kochi lile la watu wawili, wakati Malaika na Edgar walikaa kwenye kochi kubwa la watu watatu, ambapo malaika alikuwa aanaendelea na utengenezaji wa kachumbari, muda wote waliongea wakicheka kwa furaha, yote waliya fanya pasipo kujuwa kuwa nje kulikuwa na watu wanne, watatu wakiwa ni wanaume na mmoja wakike, ni para na vijana wake, muda wote walikuwa wame jibanza nje ya nyumba, wakifuatilia mwenendo mzima wa mawindo yao, wakisubiri amri toka kwa Para, iliwaingie wakavamie na kuwa kamata, kiukweli nyumba ya Edgar na ni kama nyumba nyingi za mtaa huu wa seed farm, zipo mbali mbali, kiasi kwamba linaweza kutokea lolote pasipo mtu yoyote wa jirani kusikia, kiukweli silaha kubwa waliyo kuwanayo wakina Para ni bastora moja, tena alikuwa nayo Para mwenyewe, zaidi ya hapo ni visu tu! mikononi mwao, para alichokuwa anasubiri ni kwamba wale watu wajikusanye sehemu moja, ambayo ni sebuleni, ili iwe rahisi kwao kuwa kamata, na muda pekee ni wakati watakapo kuwa wanakula, ni kweli sasa mama Malaika na wanae walikuwa sebuleni, maongezi ya kiendelea, huku wakisubiri Malaika amalize kutengeneza kanchumbari “mama mimi naombi moja” aliongea Malaika akimwambia mama yake, “ombi gani ilo mwanangu?” aliuliza mama Malaika akijiweka sawa, “tumshirikishe baba ili na sisi tuwe huru kutembelea nyumbani, pia niweze kwenda ofisini, maana itakushinda, si’umeona leo nilivyokuta viporo vingi” waliongea hayo, huku wana Endelea kumsubiri Malaika ambae alikuwa naendelea kukata ktungu cha mwisho, “swala hilo, atamimi nilisha lipanga, nilikuwa nangoja umalizie fungate kwanza” alijibu mama Malaika, wote wanacheka kwa maneno ya mama Malaika, kicheko chao kina katishwa na kishindo kikubwa cha mlango kubamiza kwa nguvu ukutani, baada ya kufungiliwa kimabavu, kwa teke la mmoja wa vijana wa Para, walipogeuka kutazama kilicho sabababisha, wanakutana na sura nne, zakuogofya, tatu zikiwa zime pinda kweli kweli, na kati ya watu hao mmoja anabastora mkononi na wanaume wengine wawili walikuwa na visu mikononi, huku mmoja akiwa ni mwanamke, “tulieni hapo hapo kama mlivyo,” aliongea yule mwenye bastora, ambaye alikuwa menyoa kipara na amefuga ndevi nyingi sana, huku akiwa ame wanyooshea ile bastora, kiukweli wote watatu walipatwa na mstuko mkubwa sana ulio sababisha ata Malaika adondoshe kisu alichokuwa anatengenezea kachumbali mezani, mama Malaika yeye alitulia pale juu ya kochi, mapigo ya moyo yakiongeza kasi kila sekunde, ata mkojo ulisha mbana, nakuwa tayari kutoka muda wowote, wakati Edgar uso wake ulionyesha wazi kustushwa na ule ugeni, “wakina baba, kwani tume wakosea nini jamani” aliuliza mama Malaika huku akitetemeka kwa uoga, wale jamaa wakacheka sana, tena kicheko cha kebei, “huyu ndie yule mama mjeuri, nilie ongea nae jana usiku” alisema Para huku akimwonyesha kwa bastola, kitendo kilicho sababisha mama Malaika ainue miguu akiipandisha kwenye kochi, na kuji kunyata kwa uoga, wale jamaa wakacheka sana, “wewe! simu hipo wapi?” Para alimwuliza Malaika akimgusa na bastora kichwani, Malaika akuwa nauwezo wakutowa sauti, akaonyesha kwa kidole, sehemu ilipo simu, Para akaifwata na kuanza kubonyeza namba flani, kisha akaweka sikioni mkonga wa ile simu, baada ya sekunde chache ikapokelewa, “Para hapa naongea… ndiyo … njoo moja kwa moja mpaka pale tulipo kuwepo jana usiku.... sawa tunakusubiri,” kisha Para akakata simu, ki ukweli mama Malaika alikuwa ana hali mbaya kuliko Malaika na Edgar, wakina Para nao wakiwa na uakika wa kwamba, wamesha maliza kazi yao, ya kuwateka wakina Malaika, ambao waliamini kuwa ni watu dhaifu kabisa, waliendelea kuwa kejeri na kuwa dhihaki, “we! Queen, nenda nje ukawasubiri wakina mzee Komba, pia uangalie kama kuna mtu yoyote anakuja huku” alisema Para, na hapo hapo yule mwanamke jambazi akatoka nje, na kuelekea waliko tokea, mwishoe akaenda kusimama walipo liacha gari lao, ni mita kama mia mbili hivi toka ilipo nyumba ya kina Edgar, Huku ndani Para alikuwa anaendelea kuwa kejeli, mateka wake, “wewe unaye jifanya kidume kuiba mchumba wa mtu, ona sasa una zalilika mbele ya mama mkwe” maneno ya Para yali uchoma moyo wa Edgar, maana nikweli mama mkwe alikuwa kitika hali mbaya “ina maana wewe ni nani?, kuwadi au mpambe au mshakunaku?” Edgar alijikuta akiongea maneno ambayo alijuwa fika kuwa yange mchafua Para, ni kweli Para alichukizwa na maneno ya Edgar, akapiga atua za haraka kumfwata Edgar pale alipo kuwa amekaa na Malaika, huku bastora mkononi, hapo Edgar akajuwa kuwa kinachofwata ni mkong’oto wangu, aka tazama chini, akaona kisu ambacho Malaika aliuwa amekidondosha, mala baada ya mlango kubamizwa, hapo aka mwesabia para atuwa zake, je? unazani Edgar atafanikiwa kuonyesha ujasiri mbele ya mama mkwe na mchumba wake Malaika, itaendelea.......
No comments:
Post a Comment