ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA TISA : maana nikweli mama mkwe alikuwa kitika hali mbaya “ina maana wewe ni nani?, kuwadi au mpambe au mshakunaku?” Edgar alijikuta akiongea maneno ambayo alijuwa fika kuwa yange mchafua Para, ni kweli Para alichukizwa na maneno ya Edgar, akapiga atua za haraka kumfwata Edgar pale alipo kuwa amekaa na Malaika, huku bastora mkononi, hapo Edgar akajuwa kuwa kinachofwata ni mkong’oto wangu, aka tazama chini, akaona kisu ambacho Malaika aliuwa amekidondosha, mala baada ya mlango kubamizwa, hapo aka mwesabia para atuwa zake, ENDELEA.......
Ile anamfikia tu!, kitendo bila kuchelewa Para alistuka mkono wake wenye bastora ukipigwa teke na bastora ika mtoka mkononi nakuruka juu, wakati anaangaika kuidaka alistukia ngumi kali tatu toka kwa Edgar, ambae sasa alikuwa amesha simama, bwana Para alipigwa ngumi mfurulizo zikatuwa kifuwani kwake bara bara! na kumrudisa nyuma atuwa tatu, lakini Para akusikilizia maumivu, akajitutumua nakurudi tena kwa kasi ya hajabu, akimfwata Edgar, wale vijana wawili walikuwa wakitazama mpambano, wakiamini kuwa Para ata mshida yule bwana mdogo, Para akaruka juu na kuachia teke, ambalo lilipita pahewa, baada ya Edgar kukwepa, kwa kubonyea chini, na kuokota kisu haraka, wakati huo Para akiruka tena na kuachia teke jingine, safari hii alishangaa teke lake lilikutana na mkono wa Edgar, ambao ulijikita kwa nguvu maeneo ya paja lake, hapo bwana Para alistuka kisu kikipenya na kuzama chote nakubakiza mpini, ukinig’inia kwenye paja lake, la mguu wa kulia, aliotumia kurusha teke, Para aka piga kelele za maumivu, wale wengine wawili waka juwa kimenuka, kitndo bila kuchelewa, wakamvamia Edgar wote wawili, wakiwa na visu mkononi, Edgar ali chukuwa pillow moja la kochi, na kumrushia mmoja kati ya wale wawili, na huyu mwingine akaangalia kule kwa mwenzake, alie rushiwa pillow, (mto wa kochi) lilikuwa kosa kubwa sana kwake, alistukia ngumi nzito ikituwa shavuni kwake, ile anageuka na kutaka kumchoma kisu, Edgar akamdaka mkono na kuu mpiga kiwiko (kipepsi/kisugudi) cha mbavu aka legea kutokana na muamivu makari, na kuachia kisu “Edgar mwangalie huyu ana…” hapo edgar akusubiri Malaika amalizie kuongea, alisha juwa kinachofwata alimtazama yule mwingine, ambae alikuwa amesha vuta mkono wake wenye kisu, na kukipeleka kwa Edgar kwanguvu zake zote, tayari kumchoma nacho, kitendo cha haraka sana Edgar alimgeuza yule aliemshika, na kumfanya kama kinga yake, na kisu kika zama kwenye ubavu wa yule jamaa, mwenzie aka duwaa, akishangaa kilicho tokea, hapo alikutana na mvua ya ngumi za shingoni na kifuani, akimaliziwa na teke lililo mrusha, na kwenda kujibamiza kwenye kabati la vyombo, lililopo pale sebuleni, hapo hapo akakata moto (kuzimia), Para alisha gunduwa kuwa ameingia choo cha kike, aikuwa rahisi kama alivyo zania, akaikumbuka bastora yake iliyodondoka dakika chache zilizo pita, akaanza kuangalia huku na huko, akaiona chini karibu na mama Malaika akaanza kutambaa kuisogelea, mama Malaika akamwona Para anamsogelea, akapiga kelele za uoga “Edgar ananifwataaaaaaaaa” alisema mama Malaika huku akipandisha miguu juu ya kochi, Malaika akuwa mbali akainua bakuli kubwa la udongo lililo jaa kachumbari, na kum’bamiza nalo Para kichwani, pala akakatamoto hapo hapo(akazimia), yule mmoja alikuwa anatokwa na damu nyingi sana sehemu aliyo choma kisu, hapo wakina Edgar wakawafunga kamba wageni wao Edgar, akiwa amesha iokota ile bastora ya Para, mama Malaika akapiga simu kwa mzee Haule akamwambia kwamba apitie kituo cha polisi akawachukuwe polisi, kisha wampitie Jastin pale sokoni awalete nyumbani kwa Edgar haraka, kuna tukio la ujambazi, kweli mzee Haule akuchelewa aka jiandaa haraka na kumfwata Jastin, alipo mpata akamweleza kama alivyo elekezwa na mama Malaika, kisha waaelekea kituo cha polisi, japo ilikuwa ni ngumu sana kwa Jastin kukubari haraka, lakini alipo elekezwa juu ya tukio lililotokea alikubari, muda mfupi walikuwa njiani pamoja na magari mawili ya polisi wakielekea seed farm, ***** wakati huo mzee komba na mwanae Martin walikuwa, wanaingia eneo la tukio wakiongozana na Queen dada jambazi, ambae alikuwa anawasubiri mita chache toka nyumba ya kina Edgar, wakiwa na uakika kuwa wakina Malaika wapo chini ya mikono ya mjomba Para, waliingia moja kwa moja ndani wakiwa na shauku ya kumtendea unyama Malaika, ile wana ingia tu! wakakutana na mtutu wa bastora, mpo chini ya ulinzi tulieni hapo mlipo msubiri police, mzee Komba alistuka kusikia maneno hayo yakitamkwa na mtu toka nyuma yao, aliganda huku akipepesa macho huku na huko, alichofanikiwa kuona ni wakina Para na vijana wake wawili, mmoja akiwa anavuja damu nyingi sana ubavuni kwake, pia mzee komba na Martin, waliwaona Malaika na mama yake, wakiwa tazama kwa macho ya kebehi na tabasamu likiwa limechanuwa kwenye nyuso zao, kitendo kilicho uchoma moyo wa Martin, akajawa na hasira “we!fala nini, unazani mimi naogopa polisi, wewe masikini ndiyo unaogopa polisi, nitaenda na kutoka, nikitoka ndio utanijuwa mimi nani, pamoja na huyo Malaya wako” yalikuwa maneno machafu sana toka kwa Martin, Malaika akajikuta ameinuka kwa hasira na kumsogele Martin kitendo bila kutegemea, Martin alistukia akipigwa kwa goti (kifuti) kupiga teke la kwenye kegere za kiume, (pumb...) Martin akainana na kushikilia sehemu hiyo nyeti, huku akiuguria maumivu, watu wote walikuwa wametazama tukio lile, kasoro dada jambazi, ambae toka awekwe chini ya ulinzi, alikuwa anawaza namna ya kujinasua, hapo akaona ndiyo nafasi ya pekee, aka ruka hewani na kuachia teke kifuani kwa Edgar, lika mpata sawa sawa, na kumymbisha Edgar na kaumfanya aihachie bastora aliyo kuwa ameishika mkononi mwake ika dondoka chini, na kabla hajakaa sawa aliongezewa teke jingine la mbavuni, Edgar alishikilia mbavu, Queeen akaona wakatihuo ndio wa kumaliza kabisa, Edgar, akamsogelea na kurusha ngumi kuelekea eneo la shingo ya Edgar, Queen dada jambazi akastuka kuona ngumi yake imedakwa na Edgar, nikitu ambacho hakukitegemea, ilifwatiwa na kunyongwa kwamkono mzima kisha uka vutwa juu nakurudishwa chini kwa nguvu na kukutana na goti la Edgar, mkono uka lia kama kipande cha mti mkavu ukikatika, kikafwatia kilio kikubwa toka kwa Queen, kilio kilicho tulizwa na gumi nzito ya mdomo, iliyosababisha mwanamke huyo adondoshe meno yaliyo changanyika na damu, kisha Queen aka jibwaga chini kama kiloba, Martin naye akaona huu ndio muda wakuiwai bastora iliyo dondoka chini, lakini haikuwa rahisi, wakati anainama kuokota bastora hiyo, alikutana na teke zito la usoni lililo mrusha na kumbwaga chini, akifwatiwa na teke jingine la mbavuni “mama nakufaaa” ilimtoka Martin huku akishuhudia mguu wa Edgar ukimfwata usoni, na kutuwa vyema kabisa na kupasua pua yake, mpaka hapo mzee Komba alikata tamaha ya kujinasua, “lakini mama... ha!.. shemeji tuna weza kuyaongea” aliongea mzee Komba kwa sauti ya kubembeleza, “tutayaongelea mahakamani” alisema mama Malaika akiiendea simu na kupiga nyumbani kwa mzee Komba, simu ilipokelewa na wifi yake Sonia, yani shangazi yake Malaika, “samahani mwenyewe yupo nje kidogo ulikuwa una semaje” mama Malaika aliitambua sauti ya wifi yake “mimi wifi yako, mama Malaika, mwambie huyo shoga yako kuwa mume wake amekamatwa kwenye ujambazi pamoja na mwanae, wakijaribu kututeka nyala, na wewe wifi fungasha kila kilicho chako utoke kwenye nyumba yangu, utapo kwenda utajuwa mwenyewe” aliongea mama Malaika kisha akakata simu “lakini shemeji hukupaswa kumwambia mama martin” aliongea mzee Komba akimsogelea mama Malaika, akakutana na kofi nzito la usoni lililo mfanya aone nyota, akapepesuka na kutaka kumdondokea, Malaika akakutana na kofi jingine lililo m’badilishia uelekeo na kwenda kujigonga kwenye meza ambayo ilimchana paji la uso, Martin alishuhudia yote hasiweze kumteta baba yake, wakati huo wakina Para wakiwa wame lala kwenye sakafu awajiwezi, dada jambazi alipiga mahesabu ya haraka ya kukimbilia nje maana mlango ulikuwa wazi, akahesabu kimoyo moyo, “ moja...mbili.... tatu...”, itaendelea.....
No comments:
Post a Comment