SEH.69 Sasa Maurine kuna vile vyakula vya kuku kule nyumbani naomba uende na Chriss mkavichuke ili mpaka mimi namaliza kumremba mama yako mkubwa muwe mmesharudi alisema mama yake na Maurine.Jamani mama yaani mimi nirudi mpaka nyumbani sa hizi alilalamika Murine kwa sauti ya kudeka.Ebu acha kudeka kwani unaratiba gani mjini mama yake alimuuliza kwa ukali.Naenda kwa rafiki yangu kuna nguo nzuri amenambia ameninulia alisema Maurine kwa sauti ya upole.Sasa wewe mama mdogo si ndo vizuri maana Chriss ni dereva mzuri yupo na gari atakupeleka sehemu yoyote unayotaka alipendekeza mke wa mjomba.Ooooh kama hivyo sawa nikajua mpaka tuanza tena kuparangana na hice alijibu Maurine kwa furaha.
“Chriss naomba umpeleke huyu binti anapotaka alafu kwanza anzieni nyumbani mchukue kabisa hivyo vyakula vya kuku” alisema mke wa mjomba.Niliitikia oda hiyo kwa kutingisha kichwa.Tukaondoka na binti huyo na safari ya kwenda kwao ikaanza. “Naomba niendeshe mimi”alisema Maurine mara baada ya kutoka nje ya duka hilo.Sikuona haja ya kumbania nikampa funguo na safari ikaanza.Tukiwa kwenye gari baada ya ukimya wa mda mrefi binti huyo mrembo akaanzisha mazungumzo. “Nambaie Chriss mbona umepooza hivyo tofauti na nilivyokuwa nikisimuliwa habari zako” alivunja ukimya Maurine ambaye na yeye ni sawa tu na binamuyangu. “Habari zangu? Nani amekupa habari zangu” niliuuliza kwa mshangao.
Aaaaah usishituke sana na mimi na Lisa ni kitu kimoja na huwa tunatunziaana siri alisema Maurine huku akizidi kupunguza mwendo wa gari. Ooooooh kumbe Lisa vipi kwani alikuambia mimi ni mchangamfu? Nilimuuliza kiudadisi.Sio mchangamfu tu, na mengine mengi alisema binti huyo huku akiniangalia usoni.Jamani na mengine mengi kama niliuliza kwa mshangao.We acha tu jinsi alivyokusifia mpka na mimi nikapagawa alisema binti huyo na kuzidi kuniacha njia panda.Kabla sijaongea akanambia ila naomba usije ukamuuliza utaharibu undugu wetu alisema Maurine kama njia ya yeye kujihami.Usijali wewe nambiae tu mimi ni msiri sana nilijaribu kumuakikishia usalama
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments:
Post a Comment